Rais Jakaya Kikwete analipwa mshahara na posho kiasi gani? na analipa kodi kiasi gani?

wamarekani wote wanajua ni wajibu wao kulipa kodi, je wabongo wangapi wanalipa kodi. Jifananishe na Kenya wewe sio kurukia America.
Kwa nini ujifananishe na udhaifu?Hivi wewe mwanao anayesoma Kinondoni muslim akipata zero utamwambia its ok mbona na wanafunzi wote wa Masjid Quba wamepata zero au utamwambia mbona wenzio wa Maua Seminary wamepata div one?
 
Huyu rais wetu wa kishikaji kishikaji hakuna kitu pale. Ridhi anamiliki kiasi gani kwani, chini ya CCM, za watanzania zitaendelea kuliwa kishikaji
 
am fed up with all they say that belongs to Riz1. Mungu yupo, yaani . . . . . . . . . !
 
Kwa nini ujifananishe na udhaifu?Hivi wewe mwanao anayesoma Kinondoni muslim akipata zero utamwambia its ok mbona na wanafunzi wote wa Masjid Quba wamepata zero au utamwambia mbona wenzio wa Maua Seminary wamepata div one?

hapo sasa kwenye huo mfano mimi sipo subiri vijana wa ustadhi ponda n co. Waje kukushikia na hoja za mfumo kristo
 
The president of Tanzania Kikwete salary per annum is Tsh 300,000,000/= three hundred million of which if convert to USD is $187,500/ the president gets many benefits free accomodations at resident all food and loundry and transportations is fully paid the president gets full medical including all his family members president also gets clothing allowance, travel and enteratiainment allowance

Basi ni kweli ndiyo maana serikali haiwezi kuwalipa madakatari Tshs 3,500,000. Wakati Nyerere alipokuwa akilipwa Tsh 2,500 kwa mwezi madaktari walikuwa wakilipwa Tsh 1,800 kwa mwezi. Kwa ratio hiyo ilitakiwa leo madakatari wawe wanalipwa Tsh 216,000,000 kwa mwaka: sawa na Tsh 18,000,000 kwa mwezi.
 
hapo sasa kwenye huo mfano mimi sipo subiri vijana wa ustadhi ponda n co. Waje kukushikia na hoja za mfumo kristo

yaani jamaa amelenga haswaa panapo. Kujisifu wewe ni shujaa kwakuwa umelala njaa tena kwa uzembe wa kufanya kazi, eti kwa sababu jirani yako naye kalala njaa wakati ungejituma ungekuwa kama mwingine ambaye hula mlo kamili basi unaupungufu wa ufikiriaji hapo.
 
Mshahara wa rais sio siri nakumbuka mara ya mwisho uliongezwa ukatangazwa magazetini ulikuwa kama around TZS 2,330,000 hivi.
 
Ndugu wana JF,

Ni jambo la kawaida kwa wananchi kujua mapato ya Viongozi wa nchi hususani the highest office in the land, Viongozi wengi ambao hawana nia ovu huweka hadharani mapato yao na kodi walizolipa na wananchi wao kujua na tena kuonyesha mfano wa kuigwa kwamba hata raisi wa nchi analipa kodi na hatumii nafasi yake ya uraisi kwa manufaa yake na familia yake, kujilimbikizia mali na kutolipa kodi kwa kipato anachopata.

Hapa chini ni mfano wa Raisi wa Marekani Barack Obama ambae alitoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya mapato yake kwa mwaka na kodi anayolipa bila kujali nafasi aliyonayo. mapato na kodi ya raisi obama na mkewe kwa mwaka ni:

Obama Taxes & Income: President & First Lady Paid $453,770 In Taxes On $1.7 Million Income
soma zaidi kwa kufuata link hii Obama Taxes & Income: President & First Lady Paid $453,770 In Taxes On $1.7 Million Income
Je ni kwa nini viongozi wa kiafrika wanakuwa na usiri sana kuhusu mapato yao na kodi wanazolipa, kwa nini viongozi wetu wasiwe wanatoa taarifa za mapato na malipo ya kodi kwa vyombo vya habari ili kuonyesha mfano? Na wananchi kujua vyanzo vya mapato ya raisi.

Je ni watanzania wangapi wanaojua mshahara wa raisi Jakaya Kikwete na marupurupu yote na posho ni kiasi gani? Je raisi JK na familiya yake wanalipa kodi kiasi gani kwa mwaka?

Lazima tujenge uwazi na kujua mambo muhimu kama mshahara wa raisi na kama raisi wetu analipa kodi au la! Ningependa kuwakilisha hoja yangu ili tuweze kudadisi na kujua mapato na malipo ya kodi kwa raisi wetu.

Natoa shukrani kwa Zitto Kabwe kwa kutufahamisha mapato ya wabunge na posho zote but tunataka kujua wabunge wetu pia wanalipa kodi kiasi gani kwa mwaka?
JK yuko juu ya sheria , na state inamhudumia kwa kila kitu , hivyo hakuna taxable income anayopata ila ni marupurupu tu anayoyopata katika kusaidia wa tz wapate wawekezaji ajira zipatikane .
 
Jamani ninaomba wanasheria watusaidie kwa hili. Mshahara wa Rais na marupurupu pamoja na anavyolipa kodi viingizwe kwenye katiba mpya. Katiba mpya iwe inamlazimisha Rais to put in public mshahara wake na marurupu yake na jinsi anavyolipa kodi.

Haya mambo ya KIFICHO ndiyo yanazaa UFISADI.
 
Aje hapa Salva atupe rate ya mshahara, marupurupu na posho zote ziwe convertrd into cash na TRA watupe takwimu za kodi inayotoka kwa Jk. Huu ndio uwazi. Hii itachochea wananchi kulipa kodi kwa kasi zaidi, nguvu zaidi na ari zaidi.
 
viongozo wengi wa tanzania awalipi kodi na pia president anavyosafiri sana hiyo posho na marurupu zikitajwa situnaweza pigwa na butwaa na kulalamika!
 
Back
Top Bottom