Rais Jakaya Kikwete analipwa mshahara na posho kiasi gani? na analipa kodi kiasi gani?

Ukiuliza mambo haya utaambiwa unahatarisha AMANI NA MSHIKAMANO wa nchi. Utaanza kufuatwa akina Ramadhani Ighondu alias Abeid.

Mkapa wakati anaingia madarakani alitaja mali na peza alizonazo bank. Baada ya kutoka madarakani akakataa kata kutaja mali na pesa alizomiliki. Bado watanzania wanamuita mzee wa UWAZI NA UKWELI.

Nchi hii tumerogwa, amini usiamini!
 
Nadhani sio siri. Ila inategemea madhumuni ya anaetaka kuujua ni nini. Mshahara wa Raisi wa Marekani uliotajwa si wa ajabu hasa hasa ukizingatia kipato cha wastani cha watu wa Marekani na uwepo wa wingi wa watu wenye kipato cha juu. Kwakweli si haki kulinganisha na mshahara wa raisi wetu.

Isipokuwa shida nyingine, akina sisi ambao hatujashika hela nyingi nikikwambia raisi anapokea mamilioni kadhaa, tayari ushapata hoja ya kulalamika na kwa ufinyu wa kufukiri hatukawii kuulinganisha na wa mwalimu au daktari. Mwenye kuujua autaje, ila nimeshuhudia udhaifu wa hoja nyingi za namna hii na watu wanavyoweza kutafsiri vibaya.

Raisi Nyerere kipindi hicho alikuwa akitaja mshahara wake mara nyingi tu katika hotuba zake hasa pale anapotaka kutoa mfano wa maisha yake.
Mkuu hatulinganishi mshahara wa JK na BHO ila dhamira yetu ni kutaka kujua anlipwa kiasi gani ukilinganisha na umaskini wetu, Mbona mshahara hata wa PM wa Uingereza unajulikana, Hata Nyerere by then alitaja mshahara wake watu walipolalamika akapunguza
 
Bahati mbaya sisi wengi hatujui maana hatulipi kodi- tungelipa tungekutana huko huko
Mtanzania mwenzangu gulio hakuna mtu asiyelipi kodi! Umeshawahi kujiuliza kwa nini soda zinapanda kila mwaka? au hujawahi hata kununua sabuni??????????????????? KILA MTU ANALIPA KODI AIDHA DIRECT AU INDIRECT
 
Hakuna sababu ya mshahara wa Rais,VP,PM,Mawaziri kuwa siri. Ktk list hiyo niwajumuishe Jaji Mkuu,Spika wa Bunge,Gavana wa BOT na Viongozi Wastaafu,mfano marais,mawaziri waku,nk!
 
mada kama hii co mara ya kwanza kuletwa hapa jamiiforums ila bado jibu kamili halijapatikana.
labda nngu anaweza kutusaidia japo kwa approximation.
 
Tumpe hii assigment FaizaFoxy.
Waziri wa utumishi na ajira atwambie au waziri wa kazi.

Nchi yoyote ya kidemokrasia ni haki wananchi wake wajue mishahara na mapato ya viongozi wao maana ndio waajiri wao.
 
Tuanze kwanza na Nyerere kwasababu huu mfumo haukuanza kwa Jk mbona mnachuki mbona hamkuwahi kuuliza Mkapa analipwa shiling ngapi?
Jk hawezi kujiamulia msharaha wake analipwa kutokana na mfumo alioukuta na kama huo mfumo ni mbaya wakumlaumu sio Jk ni hao waliopita kabla yake.

Bahati mbaya, ubatili wa jana, hauhalishi ubatili wa leo, Ilikuwa ni mbaya hata nyakati za hao uliowataja, hivyo sioni mantiki au hoja yako sijaielewa, unataka tusihoji kwa kuwa Nyerere na Mkapa hawakuhojiwa? Nguvu iliyo nyuma yako ni chama au dini au njaa/maslahi binafsi? Chama sidhani kama ni kweli, nahisi itakuwa ni dini maana naona Mzee Mwinyi umemruka na kwa mbaali naona ni njaa!

Kwangu mimi wote, Nyerere, Mwinyi na Mkapa wote walifanya makosa kama mishara yao haikujulikana, ila naamini mshahara wa Nyerere ulifahamika ndo maana alikubali 20% ipunguzwe/itolewe -rejea mgomo wa wanafunzi wa chuo kikuu DSM(Sikumbuki mwaka)

Kwa mantiki hii, ni muda mwafaka kujua rais analipwa shillingi ngapi na analipa kodi kiasi gani, katiba itamke hili, sioni haja ya kufanya siri
 
Mmmmm!! Kapiti kamunyugi. Ccm vikeka lepi


Ndugu wana JF,

Ni jambo la kawaida kwa wananchi kujua mapato ya Viongozi wa nchi hususani the highest office in the land, Viongozi wengi ambao hawana nia ovu huweka hadharani mapato yao na kodi walizolipa na wananchi wao kujua na tena kuonyesha mfano wa kuigwa kwamba hata raisi wa nchi analipa kodi na hatumii nafasi yake ya uraisi kwa manufaa yake na familia yake, kujilimbikizia mali na kutolipa kodi kwa kipato anachopata.

Hapa chini ni mfano wa Raisi wa Marekani Barack Obama ambae alitoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya mapato yake kwa mwaka na kodi anayolipa bila kujali nafasi aliyonayo. mapato na kodi ya raisi obama na mkewe kwa mwaka ni:

Obama Taxes & Income: President & First Lady Paid $453,770 In Taxes On $1.7 Million Income
soma zaidi kwa kufuata link hii Obama Taxes & Income: President & First Lady Paid $453,770 In Taxes On $1.7 Million Income
Je ni kwa nini viongozi wa kiafrika wanakuwa na usiri sana kuhusu mapato yao na kodi wanazolipa, kwa nini viongozi wetu wasiwe wanatoa taarifa za mapato na malipo ya kodi kwa vyombo vya habari ili kuonyesha mfano? Na wananchi kujua vyanzo vya mapato ya raisi.

Je ni watanzania wangapi wanaojua mshahara wa raisi Jakaya Kikwete na marupurupu yote na posho ni kiasi gani? Je raisi JK na familiya yake wanalipa kodi kiasi gani kwa mwaka?

Lazima tujenge uwazi na kujua mambo muhimu kama mshahara wa raisi na kama raisi wetu analipa kodi au la! Ningependa kuwakilisha hoja yangu ili tuweze kudadisi na kujua mapato na malipo ya kodi kwa raisi wetu.

Natoa shukrani kwa Zitto Kabwe kwa kutufahamisha mapato ya wabunge na posho zote but tunataka kujua wabunge wetu pia wanalipa kodi kiasi gani kwa mwaka?
 
HII thread mwake mwake sanaaa hawa magamba watuambie walichonga sana walipoanzisha ya Dr.wa ukweli sasa leteni majibu hapa huyo rais wenu mshahara wake na posho na kodi mkishindwa mshirisheni gamba mwengine aliyeko Newyork kama ataweza, na ninyi vimagamba vidogo wa napi mliovamia hapa jf semeni,wala msikimbie mada.

Wewe ndiyo kilaza wa mwisho. Mshahara wa rais unapangwa ccm?
 
Back
Top Bottom