Rafiki wa mume wangu ananitaka

kisasangwe

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
292
52
Jamani mi hata sielewielewi huyu kiumbe anataka nini. ni rafiki wa karibu sana na mume wangu. Amekua na tabia ya kutaka sana kunijulia khali.
nami kama shemeji namsabahi na namheshimu sana.
Mwenyewe kaoa, ana mtoto mmoja.
Sasa majuzi alinicall akasisitiza nimwone ana shida sana ya kuongea na mie. nikamwambia tungekwenda na Mr weekend, akakataa akadai shida yake ni siku hiyo hiyo. mi kwa heshima kabsaaa nkakubali nikijua ni shida ya kweli. nikajitoa job mapeema ili nikamwone.
Kufika alikosema nimkute nikakuta mwenzangu ashaanza kuutwika mtungi, kwa vile mi si mnywaji wa pombe nikaagiza maji yangu. Nkamuliza Shem kulikon? hakyanani mi sikuamini kama alimaanisha manake mshenzi yule eti na chumba alishalipia ili .... jamani jamani mi hata sijui nimwambie mume wangu au nifaneje manake nimekwazika sana kwa kweli. sina hata raha mie manake mtu bora hata angekua simjui au hana ukaribu na familia sasa huyu wako marafiki na ni mtu tunaemvalue kama rafiki kumbe ajenda zake mbovu.

kwa hali hii yani duuh sijui kwa kweli.
 
Mbona husemi wewe ulimjibu alivyokwambia hivyo? au ulimwambia utafikiria ndo umekuja kuomba ushauri hapa JF?
 
Umeshafanya kosa kumfuata bila kumjulisha rafiki yake. Ila mkanye na mwambie akirudia utamwambia rafiki yake.
 
Usimwambie mume wako alafu huyo rafiki akuchongee unamtaka ndo utajua kama ukweli ni mzuri au la!!Ila kama...narudia tena kama ungemjulisha mumeo shemejio anakuomba mkutane ingekua rahisi kumweleza yaliyojiri....kitendo tu cha kwenda kumwona rafikiye bila yeye kujua kinaweza mpa maswali mengi.

So jifunge kibwebwe umwambie kabla rafiki hajaanza kumwambia “juzi nlikua na shemeji ujue...alikua anapita maeneo nikamwalika kinywaji.“
 
.pole sana,ila nitabia chafu sana kupanga appointment na rafiki wa mmeo bila yye mmeo kuwa na taarifa,je angekukuta hilo eneo ungejitetea vp na anajua uko kazini?hala eneo ambalo lina vyumba vya kulala!!!!!!usipo mwambia mmeo atajua unainterest nae sema sikuyaku yakwanza umefanya pozi za kike,make things transparent.muwazi huishi huru zaidi.mtazamo wangu lkn
 
Dawa ya huyo nikumteka..
Beba ka voice recorder kwenye
Pocha la mkononi kutananae tena
Mrikodi halafu hapo ndio umkabidhi mumeo.

Maana kuna wanaume wengine huwaamin
marafiki zao kuliko wake zao. Sababu tu
Wamejuana kwa muda.
 
Wala usibabaike mkubalie halafu mweleze mumeo pahala na muda alopanga. Akakione cha mtema kuni, huna sababu ya kumsitiri mshenzi huyooo!! Siku ya siku atakuja kukubaka na mumeo asikuelewe???
 
Yaani hili hata sio la kushauriana wewe mwambie Mr halafu wao wawili watajuana huko huko wanapokutania ...........tupa huko shemeji najisikia vibaya.
 
du pole
ushauri namba 10 ni wa ukweli zaid

anza na km lizy alivyokuambia
 
Usimwambie mume wako alafu huyo rafiki akuchongee unamtaka ndo utajua kama ukweli ni mzuri au la!!Ila kama...narudia tena kama ungemjulisha mumeo shemejio anakuomba mkutane ingekua rahisi kumweleza yaliyojiri....kitendo tu cha kwenda kumwona rafikiye bila yeye kujua kinaweza mpa maswali mengi.

So jifunge kibwebwe umwambie kabla rafiki hajaanza kumwambia “juzi nlikua na shemeji ujue...alikua anapita maeneo nikamwalika kinywaji.“

kuna watu wanapenda matatizo sana maishani mwao, y acngemjulisha cku waliyopanga appointment ya kuonana aje amwambie leo wameshatongozana huko, halafu ukishamwambia mumeo ndio afanyaje sasa, wakakti mwingine wanawake tuitumie ubongo wetu vizuri jamani, hana mcmamo na rafiki wa mume amejua kwamba hana mcmamo ndio mana hata akachukua na room kabisa, unamchekea huyo na atafanya kweli.
 
....hakyanani mi sikuamini kama alimaanisha manake mshenzi yule eti na chumba alishalipia ili .... ...

Duh hapa kuna shida kubwa. Inaelekea mmekuwa na mgongano wa 'mawasiliano' (ya alama) kwa muda mrefu na huyo shemejio. Most likely kuna signals kutoka kwako alikuwa anazitafsiri ndivyo sivyo au pengine hukuwa umemaanisha kuzituma signal hizo kwake.

Kama mpaka aliandaa na chumba maana yake alikuwa amekusoma kama 'maji mara moja' au wengine wanasema 'maharage ya mbeya' (if you know what I mean!). Ni vema ukajitizama upya jinsi unavyo behave mbele yake au mbele za watu. Lakini inawezekana everything is fine with you isipokuwa huyo mwanaume ni mkware tu.
 
Back
Top Bottom