Rafiki wa mume wangu ananitaka

Embu nisaidie ni vitu gani?,sooo kila anayetongozwa huonekana mrahisi kukubali na ikitokea hujakubali wanakuweka kundi gani?

wanaume wajanja hutongoza wake wa marafiki ambapo wanajua huyo ni rahisi kumpata angejua hawezi kukupata wala asingesumbuka.
 
.pole sana,ila nitabia chafu sana kupanga appointment na rafiki wa mmeo bila yye mmeo kuwa na taarifa,je angekukuta hilo eneo ungejitetea vp na anajua uko kazini?hala eneo ambalo lina vyumba vya kulala!!!!!!usipo mwambia mmeo atajua unainterest nae sema sikuyaku yakwanza umefanya pozi za kike,make things transparent.muwazi huishi huru zaidi.mtazamo wangu lkn

nilikokwenda kumwona ni restaurant ila kama hatua ishirini hivi kuna hiyo nyumba ya wageni. nilipanga kwenda na mr kumwona lakini aliinsist ni jambo la muda huo huo. na kwa vile namheshimu ndio maana nillikwenda.
 
Usimwambie mume wako alafu huyo rafiki akuchongee unamtaka ndo utajua kama ukweli ni mzuri au la!!Ila kama...narudia tena kama ungemjulisha mumeo shemejio anakuomba mkutane ingekua rahisi kumweleza yaliyojiri....kitendo tu cha kwenda kumwona rafikiye bila yeye kujua kinaweza mpa maswali mengi.So jifunge kibwebwe umwambie kabla rafiki hajaanza kumwambia “juzi nlikua na shemeji ujue...alikua anapita maeneo nikamwalika kinywaji.“
Ushauri mzuri kabisa!
 
Wewe ungekwenda naye kwenye hicho chumba cha gesti ili ukienda kushtaki kwa mume wako uwe na ushahidi kabisa, sasa hivi anaweza kukugeuzia kibao kuwa ulimtaka kakukataa ndio maana unamsingizia umbeya.
 
Jamani mi hata sielewielewi huyu kiumbe anataka nini. ni rafiki wa karibu sana na mume wangu. Amekua na tabia ya kutaka sana kunijulia khali.
nami kama shemeji namsabahi na namheshimu sana.
Mwenyewe kaoa, ana mtoto mmoja.
Sasa majuzi alinicall akasisitiza nimwone ana shida sana ya kuongea na mie. nikamwambia tungekwenda na Mr weekend, akakataa akadai shida yake ni siku hiyo hiyo. mi kwa heshima kabsaaa nkakubali nikijua ni shida ya kweli. nikajitoa job mapeema ili nikamwone.
Kufika alikosema nimkute nikakuta mwenzangu ashaanza kuutwika mtungi, kwa vile mi si mnywaji wa pombe nikaagiza maji yangu. Nkamuliza Shem kulikon? hakyanani mi sikuamini kama alimaanisha manake mshenzi yule eti na chumba alishalipia ili .... jamani jamani mi hata sijui nimwambie mume wangu au nifaneje manake nimekwazika sana kwa kweli. sina hata raha mie manake mtu bora hata angekua simjui au hana ukaribu na familia sasa huyu wako marafiki na ni mtu tunaemvalue kama rafiki kumbe ajenda zake mbovu.

kwa hali hii yani duuh sijui kwa kweli.

Kwani ukimpa hiyo kitu akague utaumwa? au yeye ataumwa?

Hiyo haudhuru ndo raha ya kula na nduguyo
 
Jamaa hata hajakutongoza keshalipia chumba? Lazima umewahi kumpa siku za nyuma,
 
unatakiwa kumwambia mumeo kwani huwezi jua kama ni mtego umewekewa....
Personally, huwa sipendi kabisa mke wangu anambie habari za nani amemtongoza au anamtaka. Maana kwanza inanipa mashaka kama kweli jamaa hajala. Maana anaweza kuwa ananambia kama sehemu ya kujilinda yeye binafsi, pili inaweza kuwa ni kinga, ili siku nyingine ukiona message mbaya kutoka kwa jamaa usiwe na la kusema, maana ukimuuliza atakwambia "si nilikwambia kwamba ananitongoza?" I hate it! Mke wangu ni mtu mzima, afanye maamuzi yake mwenyewe, wala asinihusishe mimi juu ya yale anayojibizana au wanayokubaliana na dume lake huko. Hata mimi nina madada wanaonitaka na simwambii yeye. So kama mme wake ni wa aina kama yangu, ni bora kutokusema kabisa. otherwise timbwili linaanza!!
 
Hujamaliza vizuri kwani hujasema ulifanya nini baada ya kuambiwa. Chumba mlikitumia? Isijekuwa ali-perform poorly ndo maana umemleta Jamvini
 
kuna watu wanapenda matatizo sana maishani mwao, y acngemjulisha cku waliyopanga appointment ya kuonana aje amwambie leo wameshatongozana huko, halafu ukishamwambia mumeo ndio afanyaje sasa, wakakti mwingine wanawake tuitumie ubongo wetu vizuri jamani, hana mcmamo na rafiki wa mume amejua kwamba hana mcmamo ndio mana hata akachukua na room kabisa, unamchekea huyo na atafanya kweli.

Umeona dada....Haya vijana wa dot com sijui wakajoe...Yaani aende akamwambie mumewe baada ya kuitikia wito? Mhhh....Sina hakika ila kama atatekeleza ma ushauri ya hawa ndugu basi ...tunaweza kuwa tunaongea mengine baada ya hapo...May be RIP can be the right word!!

Usijaribu kusema kwa mtu yeyote na huyo jamaa akizidi kumsumbua amrecord (akama alivyoshauri AD). Baada ya hapo anaweza kutumia hiyo clip kumshikisha adabu...Jamaa itabidi awe msukule kwa yule dada kwani atakuwa anajua kwamba dada anazo silaha za maangamizi zinazoweza kummalisa any time..!
 
Umechemsha kwenda kumuona, ila hujachelewa, mpotezee kabisa mpaka ajute kukufahamu
 
Kama alivyosema SMU hapo juu, inaelekea kuna shida/migogoro ya mara kwa mara ktk ndoa yako ambayo huyo shemeji yako anaijua na sasa anataka ku-take advantage. Pia inaonekana huyo shemeji yako anakujua kuwa wewe ni mrahisi (single click) ndo maana alichukua kabisa na chumba. Isitoshe inaonekana ulishawahi kuonyesha signs za kumpenda ndo maana ukakatisha mihadi na mr. wako ukaenda kumuona yeye bila kumjulisha mumeo.
 
"sikuamini kama alimaanisha manake mshenzi yule eti na chumba alishalipia ili .... jamani jamani mi hata sijui nimwambie mume wangu au nifaneje manake nimekwazika sana kwa kweli. sina hata raha mie manake mtu bora hata angekua simjui au hana ukaribu na familia sasa huyu wako marafiki na ni mtu tunaemvalue kama rafiki kumbe ajenda zake mbovu".
Pale uliposema bora ungekuwa humjui pana utata. Lakini ni vizuri kumuonya huyo jamaa ikishindikana muambie mumeo. Siku hizi wanaume wengi wakwale sana.
 
Duh hapa kuna shida kubwa. Inaelekea mmekuwa na mgongano wa 'mawasiliano' (ya alama) kwa muda mrefu na huyo shemejio. Most likely kuna signals kutoka kwao alikuwa anazitafsiri ndivyo sivyo au pengine hukuwa umemaanisha kuzituma signal hizo kwake. Kama mpaka aliandaa na chumba maana yake alikuwa amekusoma kama 'maji mara moja' au wengine wanasema 'maharage ya mbeya' (if you know what I mean!). Ni vema ukajitizama upya jinsi unavyo behave mbele yake au mbele za watu. Lakini inawezekana everything is fine with you isipokuwa huyo mwanaume ni mkware tu.
I feel you..had same feelings..haiwezekani hata kama mwanaume ni mkware vipi afanye hivyo alivyo fanya kama huyo mwanamke ajachangia kwa kiasi fulani...Fuata ushauri wa SMU jitizame unabehave vipi mbele za watu..haiwezekani kubehave anyhowUshauri wangu huyo dada aache ngono wakati ana stead relatioship..maelezo ya huyo dada yanaonyesha anatembea nje ya ndoa..anaposema afadhali angekuwa mtu wa mbali asiye na ukaribu na familia...my instinct inaniambia huyo rafiki wa mumewe anazo habari zake fulani kuhusu kutokuwa mwaminifu naye aliamua kutake chance..
 
kwanza mpotezee, futa ukaribu nae, futa number yake kama vp iblock ingawa cjui cmu yako ni ya aina gani. hata akija kwenu ucmpe nafasi ya kuongea nawe zaidi ya salamu tu. pia kama unatabia za ukicheche mpanulie tu mapaja maana itakuwa ndo kawaida yako.
 
Jamani mi hata sielewielewi huyu kiumbe anataka nini. ni rafiki wa karibu sana na mume wangu. Amekua na tabia ya kutaka sana kunijulia khali.
nami kama shemeji namsabahi na namheshimu sana.
Mwenyewe kaoa, ana mtoto mmoja.
Sasa majuzi alinicall akasisitiza nimwone ana shida sana ya kuongea na mie. nikamwambia tungekwenda na Mr weekend, akakataa akadai shida yake ni siku hiyo hiyo. mi kwa heshima kabsaaa nkakubali nikijua ni shida ya kweli. nikajitoa job mapeema ili nikamwone.
Kufika alikosema nimkute nikakuta mwenzangu ashaanza kuutwika mtungi, kwa vile mi si mnywaji wa pombe nikaagiza maji yangu. Nkamuliza Shem kulikon? hakyanani mi sikuamini kama alimaanisha manake mshenzi yule eti na chumba alishalipia ili .... jamani jamani mi hata sijui nimwambie mume wangu au nifaneje manake nimekwazika sana kwa kweli. sina hata raha mie manake mtu bora hata angekua simjui au hana ukaribu na familia sasa huyu wako marafiki na ni mtu tunaemvalue kama rafiki kumbe ajenda zake mbovu.

kwa hali hii yani duuh sijui kwa kweli.
kwahiyo ina maana angekuwa kama hapo kwenye bold ungempa, si ndiyo? Jichunguze utakuwa na matatizo
 
Kwani ukimpa hiyo kitu akague utaumwa? au yeye ataumwa?

Hiyo haudhuru ndo raha ya kula na nduguyo

loooh fidel80 angekua mkeo ungeruhusu? vya kula na ndugu si hivyo mwenzangu.... naona we ndo wale wale tu jamani khaa
 
Back
Top Bottom