Mr.Professional
JF-Expert Member
- Oct 4, 2010
- 1,582
- 258
NI lazima kufikiri kwa makini sana kuhusu hili. Kinachopigiwa kelele siyo stahili za wafanyakazi bali ni posho za vikao ambao wanafaidika nazo wachache na sio wafanyakazi wote. Posho kama per diem ni lazima kwa wafanyakazi wote wanapotoka nje ya vituo vyao vya kazi hizi hata wao chadema wanazipokea mpaka sasa hivi bungeni na hawana tija ya kuziondoa. Imagine zikiondolew posho za vikao kwa watumishi wote wa serikali je tutaokoa mabilioni mangapi na tutakuwa tumeisaidia serikali kubana matumizi ya fedha zake kwani serikali zote ulimwenguni kwa sasa wanapunguza matumizi yasiyo ya lazima ili kuendana na hali ya uchumi wa kidunia. Pesa hizi tunaweza kuzielekeza katika kilimo na zikafanya mapinduzi makubwa ya kijani na tukasahau kabisa shida ya njaa hapa nchini.