Jigsaw
JF-Expert Member
- Jun 17, 2011
- 1,823
- 680
Sichochei wala sina mtimanyongo na mtu yeyote. Sipingi posho za vikao kuondolewa kwa wabunge na wafanyakazi wengine wa serikali. Ila sasa kusema kweli wafanyakazi wengi wa serikali wananufaika sana na hizi posho za vikao. Kuna viongozi (wakubwa), kuna wahudumu na kuna wataalamu (sekretariat) wote hawa kukiwa na vikao nao wanapata posho kusupliment mishahara yao. Pia kuna meal allowance na extra duty (siyo overtime) allowance; sijui kuna mtu anajua zinalipwalipwaje. Wafanyakazi kwa sasa wana chuki na mtu aliyeanzisha hili suala kabla ya kuhakikisha kuwa mishahara yao inapanda kabla ya kuondoa posho za vikao ambazo wanasema huenda zikafuatiwa na kuondolewa kwa posho zingine kama meal allowance na extra duty allowance.
Mkuu hao wanaolalamika ni wale wenye channeli zao. Nimefanya kazi mikoani huku zaidi ya miaka 19 . Kama kuhudhuria vikao vyenye kupeana posho nadhani haviwezi kuzidi vikao 6 au 7.
Fahamu kwamba hata hao wenye kulalamika si zaidi ya 1/10 ya wafanyakazi wote wenye kuhudhuria vikao. zaidi ni wakuu wa vitengo. Na ikitokea kasemina basi jua ni mara moja kwa mwaka tena fedha za misaada toka USAID , Danida, SIDA GTz na donars wengine. Na mpaka kikao chenye kutoa posho kikafika kule Nanyumbu vijijini tayari wizarani watu walisha chota sana. Nyie mnaambulia 5,000 au 10,000 kwa siku.
SASA ili wafanyakazi waweze kuongezewa mishahara ni lazima hivi vi mianya vyenye kuwafaidisha hawa 1/10 ya wafanyakazi pamoja na wabunge vikusanywe na kuwekwa kwenye kapu moja la mishahara. Na si hili la posho zawabunge tu bali hata hizi per diem za rais mawaziri na wengine wenye kufanana na hao lazima ziguswe na kufanyiwa tathmini kuona kama pia zinaweza kupunguza tabaka lililopo kati ya maskini na tajiri.