Pombe imekuletea madhara gani maishani mwako?

1472243652069.jpg

Kwa raha zangu...
 
Ni mbaya na ibilisi mbaya kabisa. Kwa yule ambaye hajaijaribu hasijaribu hata kidogo
Yaani kweli dunia imebadilika sana, Hivi inawezekanaje dhambi zako ukazi bebesha kwa pombe na kama ni huo uibilisi kwanini tusijitazame wapi tunakosea kuliko kuisingizia dear gambe
 
kila la heri mkuu. pombe ukishindwa kucontrol inaharibu quality ya maisha. mi imenishinda, nakunywaga hadi kunakucha. naona njia pekee ni kuacha. chukua na kitabu kukusaidie.

1. tafuta kinywaji mbadala wa pombe kama vile chai au kahawa.

2.tafuta vitu mbadala vya kufanya kwa wakati ambao unakuwa unakunywa pombe kama vile kusoma vitabu, kuangalia filamu, kushiriki katika michezo au mazoezi.
3.tumia pesa ambazo unaziokoa kutoka kwenye pombe kwa kujiburudisha kama vile kula vizuri au kununua vifaa vya nyumbani. Hii itakusaidia sana katika kuona umuhimu wa kuacha pombe.

4.jiwekee mkakati kabla ya kwenda kunywa kuhusu kiasi utakachoenda kunywa na pesa utakayotumia. Usibebe pesa zaidi ya uliyopanga kutumia.
5. tumia glasi ndogo wakati wa kunywa na tumia vinywaji vyenye nguvu ndogo. Utafiti unaonyesha watu hunywa zaidi wakitumia glasi kubwa kuliko wakitumia glasi ndogo.

6.kunywa maji kabla hujaanza kunywa pombe. na unavyokuwa unakunywa pombe hakikisha unakuwa na maji ya kunywa karibu na uyatumie mara kwa mara.
7.jaribu kuepuka vishawishi vya kunywa. Watu wengi huwa tunashawishika kunywa kwenye mazingira fulani au tukiwa na watu fulani. Unachotakiwa ni kugundua ni vishawishi vipi hukufanya unywe na uanze kuviepuka.

8.kuwa na msimamo. Watu wengi ambao hujaribu kuacha pombe hukutana na wakati mgumu wanapopata ofa toka kwa marafiki. Njia sahihi ni kukataa bila kusitasita. Kusitasita kunaweza kukufanya uteteleke katika msimamo wako. Ni vizuri ukatafuta sababu ya kukataa ofa mapema kabla hata ya

kukutana na ofa. Mfano, unaweza ukasema sinywi au siongezi pombe nyingine kwa sababu nataka kupunguza uzito au sababu nyingine ambayo utakuwa umeitengeneza kama ulinzi wako.

9.epuka kunywa pombe ukiwa na kiu au njaa. Hii inapunguza kiasi cha pombe ambacho kitaingia kwenye damu hivyo utapunguza madhara yake. Pia inasaidia kupunguza kasi ya mtu kuwa mraibu/teja wa pombe.

10.hakikisha ndugu na marafiki wanajua kwamba umedhamiria kuacha pombe. hii itasaidia kupata msaada kutoka kwao pia hawatakuwa wanakushawishi sana unywe. Pia hili linaweza kukusaidia kupata marafiki wapya kwani changamoto mojawapo ya kuacha pombe ni kupoteza marafiki.
11. kama unakunywa kwa kutumia glasi hakikisha kinywaji kimeisha kabisa ndo uongeze tena. Hii itakusaidia kujua ni kiasi gani cha pombe ulichotumia.

Kuna watu ambao mbinu hizo hapo juu zimeshindwa kabisa kuwasaidia kuacha pombe. msaada pekee ambao hubaki kwa watu hao ni kutumia dawa. Mara nyingi watu hawa ni wale ambao wanakuwa wametawaliwa sana na pombe na hupata madhara mara waachapo. Matibabu ya watu hawa hufuata hatua tatu muhimu.
Bwashe hili ni darasa mujarabu kabisaaaa
 
Pombe haifai. Kwa watumiaji ni vyema wakafanya jitihada za kupunguza na hata kuiacha kabisa.

pombe..jpg


Jana nilipanga kuanza rehab yangu. Leo nimeamka na hangover.... Eloi Eloi, lamasabakitan.
Mkuu badili mazoea uliyokuwa nayo awali.

Utafanikiwa tu
 
Wanasema kwamba huwezi kuacha pombe bila kukutwa na matukio,
Na Wanaume wengi walioacha basi ujue kuna siku walilewa mpaka wakazima kisha wakatatuliwa marinda,,,,
Yani wote wanaojifanya wameacha pombe tambua wamekumbwa na mkasa huo...
si kweli mkuu wengine waliumwa sana
 
kuna siku ukilewa vizuri unakumbuka list ya wanawake wote waliokukataa

Yote kunywa kistaarabu!
Mkuu umenifanya nicheke sababu ilishawahili nitokea baada ya kunywa pombe nilitembea barabara nzima nataja majina ya hao wanawake ila sasa nakunywa kiasi isije nivunjia ndoa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom