Kitu gani ulichonacho kilichokuhuzunisha zaidi maishani mwako?

The unpaid Seller

JF-Expert Member
Oct 27, 2019
1,876
5,443
" KITU GANI ULICHOKIONA MAISHANI MWAKO KILICHOKUHUZUNISHA ZAIDI ?!"

Peace be with you all,

Maisha yana mengi ya kufurahisha, kushangaza, kuchekesha lakini pia kuhuzunisha. Leo niwashirikishe jambo lililonihuzunisha zaidi maishani, pia wewe tuambie nini kilikuhuzunisha zaidi.

Mwaka 2009 nilipata kuona video ya mwandishi wa habari akichinjwa na watu wenye msimamo mkali wa dini fulani wakiwa wamevalia mavazi meusi waliwa na bendera nyeusi pia yenye maandishi ya kiarabu. Video ili ilikua ndefu, ya kikatili sana sana. Walimchinga kwa kisu butu ili kumzidishia mateso yule mwandishi, video ya zaidi ya dakika 13 jamaa anateseka. aise daa !!

Nakumbuka alivyokua akitikisa miguu iliyofungwa bara bara ni kama alikua akiwasihi wasimuue, lakini haikusaidia jambo, muuaji aliendelea na ukatili ule huku mara kadhaa akimgeuza huku na kule kukwepa damu iliyokua ikiruka kwa kasi isitue kwenye mavazi yake.

Cha kuuzunisha zaidi wakati mateka yule anachinjwa walikuwepo mateka wengine wawili (watalii na daktari waliokwenda kutembelea nchi hiyo) pembeni wamepigishwa magoti wakitazama mwenzao anavyochinjwa na kisha na wao kuchinjwa, hebu fikiria mateso ya kisaikolojia kwa wale wawili (sikuona wao wakifanyiwa ukatili baada ya kufuatilia taarifa zao nilikuja kujua nao waliuawa kwa mtindo ule ule)

Baada ya kuitazama nilipata mawenge kila nikilala kwa wiki mbili mfululizo, nilikua nikuona tukio lile kila nikifumba macho. Tukio lile lilinijaza huzuni sana moyoni, kila nilipowatizama watu mitaani nilitafakari jinsi binadamu tuna roho za kikatili kuliko hata wanyama. What a shame to humanity !!

Niliwaza mengi sana kwa mfululizo na hasa kujiuliza ni kosa gani walifanya mateka wale kustahili mateso makali kiasi kile ?! na kwa kiasi nilipata hasira. Ilinichukua miaka kadhaa kwa picha za tukio kunitoka kichwani na sitaki tena kupitia kipindi cha huzuni kama kile.

Screenshot_20230303-154527_Quora.jpg
 
Upotevu wa 1.5 Trillion na hela za plea bargain. Nalia sana
Pole sana mkuu, kuna jamaa alirekodiwa twitter mtoto wa wakubwa serikalini akidai kua wana off shore accounts huko Malaysia yamefichwa mabillion huenda zilipelejwa huko pia.
 
Pole
Peace be with you all,

Maisha yana mengi ya kufurahisha, kushangaza, kuchekesha lakini pia kuhuzunisha. Leo niwashirikishe jambo lililonihuzunisha zaidi maishani, pia wewe tuambie nini kilikuhuzunisha zaidi.

Mwaka 2009 nilipata kuona video ya mwandishi wa habari akichinjwa na watu wenye msimamo mkali wa dini fulani wakiwa wamevalia mavazi meusi waliwa na bendera nyeusi pia yenye maandishi ya kiarabu. Video ili ilikua ndefu, ya kikatili sana sana. Walimchinga kwa kisu butu ili kumzidishia mateso yule mwandishi, aise daa !!

Cha kuuzunisha zaidi wakati mateka yule anachinjwa walikuwepo mateka wengine wawili (watalii na daktari waliokwenda kutembelea nchi hiyo) pembeni wamepigishwa magoti wakitazama mwenzao anavyochinjwa na kisha na wao kuchinjwa, hebu fikiria mateso ya kisaikolojia kwa wale wawili (sikuona wao wakifanyiwa ukatili baada ya kufuatilia taarifa zao nilikuja kujua nao waliuawa kwa mtindo ule ule)

Baada ya kuitazama nilipata mawenge kila nikilala kwa wiki mbili mfululizo, nilikua nikuona tukio lile kila nikifumba macho. Tukio lile lilinijaza huzuni sana moyoni, kila nilipowatizama watu mitaani nilitafakari jinsi binadamu tuna roho za kikatili kuliko hata wanyama. What a shame to humanity !!

Niliwaza mengi sana kwa mfululizo na hasa kujiuliza ni kosa gani walifanya mateka wale kustahili mateso makali kiasi kile ?! na kwa kiasi nilipata hasira. Ilinichukua miaka kadhaa kwa picha za tukio kunitoka kichwani na sitaki tena kupitia kipindi cha huzuni kama kile.

View attachment 2535942
Pole kwa tukio hilo
Nje ya mada sio kila anaesema maneno ya kiarabu na kua kuua ni muislam, wengine wanalipwa kufanya hayo kuchafua uislam, kama ambavyo na mimi naweza kuvaa kanzue yenye misalaba na kuua yeyete kuuchafua ukristo mkifikiri mimi mkristo na mbaya kwa sababu mentality zenu zishaamini waislamu wauaji ni ngumj kukuelewesha.
Unajua kua uislam ni ni sdini ya amani, hata kwenye kuchinja mnyama tunatakiwa tutumie kisu kikali sana ili mnya huyo asipate maumivu makali, sasa imagin kama kwa mnyama tunakua wakarimu je kwa mwanadamu kweli kama anachinjwa angechinjwa kwa kitu kipi,
Hao waliomchinja huyo mtu Allah awaone
 
kuwa na hasira za karibu .....huwa najaribu kujichanganya na watu kupunguza misongo ya mawazo na kucheka kwa sana ila bado tu .....ukinivuruga kidogo tu....ugomvi usiyoisha
 
Pole

Pole kwa tukio hilo
Nje ya mada sio kila anaesema maneno ya kiarabu na kua kuua ni muislam, wengine wanalipwa kufanya hayo kuchafua uislam, kama ambavyo na mimi naweza kuvaa kanzue yenye misalaba na kuua yeyete kuuchafua ukristo mkifikiri mimi mkristo na mbaya kwa sababu mentality zenu zishaamini waislamu wauaji ni ngumj kukuelewesha.
Unajua kua uislam ni ni sdini ya amani, hata kwenye kuchinja mnyama tunatakiwa tutumie kisu kikali sana ili mnya huyo asipate maumivu makali, sasa imagin kama kwa mnyama tunakua wakarimu je kwa mwanadamu kweli kama anachinjwa angechinjwa kwa kitu kipi,
Hao waliomchinja huyo mtu Allah awaone
Nashukuru mkuu nilishapona. Tukijadili katika hali ya ubinadamu bila kuingiza maswala ya dini, ukatili na mamna ile unatutia doa binadamu hata kama mtu katenda makosa gani hamna namna kuhalalisha kifo kama cha yule mwandishi
 
Mods naomba uzi usomeki " KITU GANI ULICHOKIONA MAISHANI MWAKO KILICHOKUHUZUNISHA ZAIDI ?!"
 
Jihad John wa Islamic state ndio kazi zake hizo zilikuwa sema nae aliuliwa na marekani
 
Mi binafsi tabia yangu ya upole na huruma kwa kweli sipendi yaani naichukia vibaya ni vile nifanyeje natamani nibadilike
 
Back
Top Bottom