Njia 6 za kukabiliana na siku mbaya

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
9,506
14,369
Siku mbaya inaweza kuanza kwa kupokea taarifa ambayo mbaya kutoka sehemu yoyote kwa kutarajia au kutokutatajia na inaweza kuvuruga amani ya moyo wako kwa siku hiyo.

Katika makala hii inaelezea njia za kukabiliana na siku mbaya.

Kwanza kabisa kukabiliana na siku mbaya unatakiwa kujua siku mbaya imekuja na tukio gani ,kisha ujue mabadiliko ya mwili wako kwa kupokea taarifa mbaya kisha ujue ufumbuzi wake.

I.
HATUA YA KWANZA KUJUA CHANZO CHA TATIZO HUSIKA
Kama ukiweza kufahamu tatizo lako na chanzo chake utakuwa umefikia 50% ya kukabiliana na tatizo hilo.
Eneo hili kuna vyanzo vinne vya matatizo katika maisha ya kila siku.

A. MAHUSIANO /FAMILIA
Katika mahusiano na mwenza wako mnaweza kuingia kwenye migogoro au ugomvi kwa sababu zifuatazo

i. Kukosekana mawasiliano,mwenza wako kutumia pesa nyingi sana bila kukupa taarifa,

ii. Mwenza wako kugombana na wazazi wako,ugomvi wa wakwe zako na wewe,utovu wa nidhamu wa watoto, kumfumania mwenza wako, mwenza wako kuzaa na mtu mwingine kisha anataka kumleta mtoto wake ndani kwenu,

iii. Mwenza wako kuwa na wivu kupita kiasi,mwenza wako kupoteza hisia za mapenzi,mwenza wako kukosa shukurani,mwenza wako kukumbusha makosa ya zamani kila siku,mwenza wako kubadilika tabia ghafla bila maelezo,

iv. Mwenza wako kufanya mawasiliano na mwenza wake wa zamani.

B. MATATIZO YA KIFEDHA
Unaweza kupitia kipindi kigumu sana kifedha kwa sababu zifuatazo

i. Kuingiza fedha kidogo sana kwa mwezi vyanzo ni kufukuzwa kazi, kusimamishwa kazi ghafla,kukosa ajira au kazi ya uhakika, biashara kukosa wateja, kustaafu bila maandalizi,watu kukopa pesa zako lakini hawarudishi, kucheleweshewa mishahara,

ii. Dharura
Ajali yenye kusababisha ulemavu wa kudumu,ajali yenye kusababisha uharibifu wa samani na vifaa vya kielektroniki, kupata kesi, safari za dharura, kampuni kupunguza wafanyakazi, kuvamiwa na wahalifu, kuibiwa, kudhulumiwa, kutapeliwa, akaunti za benki kuzuiwa kutoa fedha n.k.

C. MATATIZO BINAFSI
Unaweza kupitia kipindi kigumu sana maishani mwako kwa sababu ya tishio la kufukuzwa kazi,tishio la usalama wako, tishio la kufungwa gerezani,kufanya kazi chini ya viwango,kukosa ushirikiano kutoka kwa wafanyakazi wenzako,kukosa maelewano na mwajiri wako au msimamizi wako wa kazi, kuzushiwa uongo kazini,umri kuongezeka bila kupiga hatua yoyote kiuchumi, kufumaniwa, kuhusishwa na ushirikina au biashara haramu, kushambuliwa kwa maneno makali sana mitandaoni au nyumbani.

D. MATATIZO YA KIAFYA
Unaweza kupitia kipindi kigumu sana maishani mwako kwa sababu ya kugundulika umeathirika na Ugonjwa usiokuwa na tiba, kupata ajali yenye kusababisha ulemavu wa kudumu, kuugua mara kwa mara,kuugua muda mrefu sana bila kupata nafuu, kupoteza uwezo wa kuona au kusikia,kushindwa kupata au kusababisha ujauzito kwa muda mrefu sana, kuathirika na kujichua (masterbation),maumivu makali sana ya kichwa na mgongo au mifupa.

HATUA YA PILI MABADILIKO YA MWILI BAADA YA KUPOKEA TAARIFA MBAYA
Kama umepokea taarifa mbaya iwe ya kifedha, kiafya, mahusiano, matatizo binafsi utaona mabadiliko yafuatayo mwilini mwako.

A. Kupata mshtuko, kuona aibu,macho kuona ukungu, kuona vitu ambavyo sio halisi, kupaniki ghafla, kuhisi unataka kudondoka ghafla, kuhisi unataka kurukwa akili, kuhisi unataka kufa ghafla

B. Moyo kwenda mbio, kizunguzungu, tumbo kuvurugika, kupoteza hamu ya kula, kupoteza hisia za mapenzi, kutamani kujiua, kuumia kooni, kutetemeka,kushindwa kumeza mate

C. Kushindwa kutuliza akili sehemu moja,kuanza kulia,kifua kubana, pumzi kuwa ngumu sana,mwili kuishiwa nguvu, kutokwa jasho bila joto,kukosa nguvu ya kutoka kitandani

D. kuacha kufanya usafi binafsi kama kufua na kuoga,miguu kuishiwa nguvu,kuanza kujitenga, kujichukia sana, kujiona huna thamani, kujiona mpweke sana, kugombana na watu wa karibu,kukata tamaa ya maisha.

E. Kujilaumu, kujuta, kujikosoa sana, kukosa uamuzi,kujiona umepoteza mvuto wa muonekano.

MADHARA YA MUDA MREFU UKIWA NA MAUMIVU

~ Kifedha- Utapoteza fedha nyingi sana kwa kutumia pesa bila mahesabu,kufanya makosa yenye kujirudia rudia,kununua vitu vingi sana kwa hasira,wengine hupoteza fedha nyingi kwa kunywa pombe kupindukia, kuvuta bangi au dawa za kulevya, au kucheza kamari, au kubadilisha wanawake au wanaume mfululizo

~ Mahusiano yanaweza kuvunjika au kuwa na ugomvi wa mara kwa mara

~ Afya - Utakuwa hatarini kupata matatizo ya kiafya kama vile tumbo kuvurugika, kuumwa kichwa na mgongo, kuchanganyikiwa, kisukari, madonda tumbo, uvimbe, shinikizo la damu, kupooza, kuugua mara kwa mara,kupata maambukizo ya magonjwa yenye bakteria na virusi haraka, ujauzito kuharibika, hedhi kuvurugika.

UFUMBUZI WAKE
1. PATA UTULIVU WA AKILI
vuta pumzi ndefu kisha hesabu 1 mpaka 5 kisha iache pumzi polepole itoke huku unahesabu 1 mpaka 5 kwa dakika 5 utaona mabadiliko ya mwili,fanya mazoezi ya viungo,kunywa maji ya kutosha,kaa kimya sehemu tulivu

2. ANGALIA MAKOSA YAKO
Ni vigumu sana kuona makosa yako ukiwa na maumivu makali sana moyoni,hisia za kisasi, kinyongo moyoni,chuki na wivu. Hata kama ni makosa ya wengine angalia wapi umeathirika na makosa yao.

Jiulize swali la kwanza tatizo ni nini?,chanzo cha tatizo lako?,Orodhesha njia zaidi 3 za ufumbuzi wake,chagua njia sahihi na salama kwako,kuwa tayari kufanya mabadiliko ya njia yako kwa sababu huenda njia yako isiwe sahihi hata kama unaona ni sahihi kwa wakati huo.

Tambua kwamba unafanya maamuzi kwa kuongozwa na hisia za wakati uliopo na hisia hizo zinaweza kubadilika baada ya muda mfupi kupita na kupata wazo tofauti hiyo ni kawaida.

3. HAKUNA CHENYE KUDUMU MILELE
Haijalishi utakuwa unapitia kipindi kigumu sana au kizuri sana hali yako haiwezi kudumu milele.Kuna afya na maradhi, kusifiwa na kukosolewa, kupewa pongezi na kuzomewa, kufaulu na kufeli, kupata na kukosa.

Hakuna chenye kudumu milele katika ulimwengu huu uongozi unakuja na kuondoka, fursa zinakuja na kuondoka, marafiki wanakuja na kuondoka, fedha zinakuja na kuondoka, mahusiano yanajengwa na kuvunjika, umaarufu unakuja na kuondoka,ajali zinatokea, umri unasogea, vitu vyenye thamani vinapoteza thamani kwa vitu vipya kuzalishwa, ujana unakuja na kuondoka.

4. FURAHA NA HUZUNI
Kila kitu ambacho unakipenda sana utakuja kukipoteza na furaha kwako itarejea tena kwa njia tofauti.
Ukiwa na furaha sana muda huu na endapo utachunguza sana chanzo cha furaha yako utagundua kwamba sio furaha bali ni yale màumivu makali sana moyoni ambayo yamegeuka kuwa furaha sana.

Wingi wa màumivu moyoni huwa kiashiria cha wingi wa furaha katika nyakati za baadaye kama hutokata tamaa eneo hilo.

5. JIFUNZE TABIA ZA WATU
Elewa kwamba watu waliokuzunguka watakuwa kikwazo kikubwa kwa mafanikio yako na furaha yako.Baadhi ya watu watakusaliti, watavunja ahadi, watavunja uaminifu, wataongea uongo,watakusingizia kesi,watazusha uongo juu yako,watafanya makosa mengi sana kuliko matarajio yako,wapo watasema au kufanya vitu vyenye kukutoa machozi bila hata kutarajia na hali hiyo ikitokea kumbuka maneno haya hiyo ni hulka ya binadamu popote pale uendapo utakutana na watu wa aina hiyo.

IKiwa unatarajia kuishi na watu wasiofanya makosa utaishi maisha ya upweke siku zote.Hakuna binadamu mzuri kwa 100% wala mbaya kwa 100% kila mtu anaweza kuwa mwema au muovu muda wowote

6. KUWA NA MOYO WA SHUKURANI
Lolote lile kwenye kutokea maishani mwako tambua kwamba haiwezi kuwa mwisho wa ulimwengu.Epuka kujuta au kutamani urudi nyuma kuongea au kufanya kitu tofauti ili uwe na matokeo tofauti badala yake fikiria nini ufanye tofauti kwa wakati huu.

Wekeza nguvu zako sehemu unaweza kudhibiti tu kisha yale yapo nje ya uwezo wako acha .
Maamuzi ya wengine huwezi kuzuia,makosa ya wengine huwezi kuzuia,tabia za wengine zipo nje ya uwezo wako.

Kila mtu anaongea na kufanya maamuzi kulingana na akili yake mwenyewe sio matarajio yako kwake.

Epuka kufanya watu wengine wajute, wabadilike tabia,epuka kuwalaumu wengine,epuka kufanya watu wengine wajione wachoyo kwa sababu hawajatoa ushirikiano kwako ukiwa na maumivu kwa sababu haiwezi kukusaidia chochote.

Zingatia kwamba matatizo hayatazami malengo yako, matatizo hayatazami historia yako, matatizo hayatazami kama wewe ni mchamungu au mshirikina, matatizo hayatazami kama wewe unasaidia sana watu au ni mchoyo sana, matatizo hayatazami kama upo mlemavu au upo na viungo kamili, matatizo hayatazami kama huna fedha au upo nazo, matatizo hayatazami kama ni mgonjwa au mtu mwenye afya.
 
Haya Mambo yakiwa katika Maandiko unaweza sema unakosea mno kuishi.

Lakini katika Maisha halisi, hasa haya ya TZ ukiwa huna kazi Mkuu ni Disaster! Huwezi fuata kanuni zote hizo Mkuu..tunaishi kwa kuviziana
 
Haya Mambo yakiwa katika Maandiko unaweza sema unakosea mno kuishi.

Lakini katika Maisha halisi, hasa haya ya TZ ukiwa huna kazi Mkuu ni Disaster! Huwezi fuata kanuni zote hizo Mkuu..tunaishi kwa kuviziana
Kibongobongo ngumu unaweza kuta wazuia rushwa wamekula rushwa lazima ikuume ila utaona poa ona kwanza kwa mfano serikali tu yenyewe ukiifanyia zuri haikuona ila utakuja kuiona ukikosea hata kosa dogo..tunaviziana ndo system iliyopo kama unavyosema
 
haya maisha yanaapply USA, Europe. Dubai in short sio kwa nchi zetu hizi shitholes. We have a lot to deal with so ikitokea jambo moja likavuruga lazima uvurugike kweli.
 
Dawa yake ni kuvuta moshi wa bange.
Kichwa kinakaa sawa,
Siku inaenda poa kabisa.


🍁..........kush master..........🍁
 
Back
Top Bottom