Polisi kuua mlinzi wa bar Dar: Je, Chalamila anakwepaje kuwajibika?

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,606
29,754
Tumeshuhudia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akivalia njuga wanawake wanaojiuza almaarufu makahaba. Zoezi lilianzia kwenye kuvamia na kuvunja vibanda maarufu vijjlikanavyo kama Vibanda vya Wahaya na kuwatia mbaroni baadhi yao.

RC Chalamila anayesifika kwa tabia za ufyatu ambapo aliwahi kusikika akisema kuwa akimkuta kibaka nyumbani kwake anamuua na hata aliwahi kusema hivi karibuni kuwa akiliamsha dude hakuna wa kumfanya lolote (hata sheria), amenadi kuwa ataendelea kuwasaka wanaojiuza miili yao kila kona ya mkoa wa Dar.

Juzi tu kumetokea mauaji mjini Dar es salaam kwenye Bar moja iliyopo Sinza iitwayo Boardroom (mlinzi wa bar hiyo aliuawa kwa risasi kutoka bunduki ya askari wetu), chanzo cha mauaji hayo yaliyofanywa na Askari Mbumbumbu ni kwenda kuwasaka makahaba hapo Bar!

Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa chini ya mwenyekiti wake wanawajibika na tukio hili la kinyama. Serikali inaendaje kuwasaka wanawake wanaojiuza kwa kutumia mtutu?

Chalamila ni mteule wa Rais, na kama inavyozoeleka mama huwalinda wale anaowapenda. Tunaamini kuwa Chalamila akiendelea kuwepo ofisini inapelekea jamii kuamini kuwa mteuzi anaridhika na mwenendo na maadili ya RC Chalamila.

Tunataka uwajibikaji na sheria ichukue mkondo wake kwa sababu maagizo ya Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa yamepelekea mauaji ambayo yangeweza kuepukika endapo busara zingetumika. Kuanzia muuaji na wote wanaohusika na sakata hili wanapaswa kufikishwa mbele ya sheria ili haki ipatikanike.

Maadili ya viongozi wengi wa CCM imepelekea chama hiko kuwa kichaka cha wahalifu

Pia Soma Boniface Jacob: Polisi walioua Mlinzi wa Bar ya Boardroom Sinza wadaiwa kutumwa na RC Chalamila kukamata Wanaojiuza
 
Mungu wa mbinguni Uturehemu Sisi
Tuna viongozi wajinga sana.
Tuna teuzi za ajabu sana.

Kiufupi huyo marehemu ameuawa na serikali. Kuwashughulikia askari wawili pekee ni kutetea wauaji halisi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ajiuzulu au awajibishwe. Anaruhusuje polisi kutumika kwenye operesheni za kipumbavu. Watu hawana ajira wala uhakika wa kukidhi mahitaji yao, mikopo ya makundi maalumu inaliwa na viongozi, wakifanya biashara wanazuiwa kwa nguvu za dola.... haya sasa unawakatalia wanawake wasijiuze kwa mtutu wa bunduki badala ya kuweka mkakati kama kiongozi kuwaepusha binti zetu kudumbukia humo.

Chalamila ni muuaji. Ameshakiri mara kadhaa na bado ndiye turufu ya mama
 
Kama hao polisi walikuwa wamelewa, maana yake walikiuka miiko ya kazi yao, na kama mtu akifanya mauaji mahakama ikajiridhisha hakuwa sawa kiakili wakati wa kutekeleza mauaji husika, adhabu inaweza kupungua.

Tatizo linakuja, ni nani kati ya jeshi la polisi, au Chalamila mwenyewe, atakayekuwa na ujasiri wa kuwachukulia hatua polisi waliofanya mauaji, hawa polisi kawaida hulindana, na bahati mbaya hata Samia nae ni kama kuna watu wanamnyamazisha.

Nakumbuka mara ya mwisho tukio la polisi kufanya mauaji ya kijana kule Mtwara, mpaka leo hata sikumbuki wale washtakiwa walipotelea wapi, tena licha ya Samia kujua kila kitu kuhusu lile tukio na kuagiza uchunguzi ufanyike.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Kumbuk kulewa kazn n kosa na unawez fukuzwa kaz (PGO)

BADO amelew na kuua huyu ajiandae kwenda kulima kwao kjjn huko
 
Tumeshuhudia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akivalia njuga wanawake wanaojiuza almaarufu makahaba. Zoezi lilianzia kwenye kuvamia na kuvunja vibanda maarufu vijjlikanavyo kama Vibanda vya Wahaya na kuwatia mbaroni baadhi yao.

RC Chalamila anayesifika kwa tabia za ufyatu ambapo aliwahi kusikika akisema kuwa akimkuta kibaka nyumbani kwake anamuua na hata aliwahi kusema hivi karibuni kuwa akiliamsha dude hakuna wa kumfanya lolote (hata sheria), amenadi kuwa ataendelea kuwasaka wanaojiuza miili yao kila kona ya mkoa wa Dar.

Juzi tu kumetokea mauaji mjini Dar es salaam kwenye Bar moja iliyopo Sinza iitwayo Boardroom (mlinzi wa bar hiyo aliuawa kwa risasi kutoka bunduki ya askari wetu), chanzo cha mauaji hayo yaliyofanywa na Askari Mbumbumbu ni kwenda kuwasaka makahaba hapo Bar!

Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa chini ya mwenyekiti wake wanawajibika na tukio hili la kinyama. Serikali inaendaje kuwasaka wanawake wanaojiuza kwa kutumia mtutu?

Chalamila ni mteule wa Rais, na kama inavyozoeleka mama huwalinda wale anaowapenda. Tunaamini kuwa Chalamila akiendelea kuwepo ofisini inapelekea jamii kuamini kuwa mteuzi anaridhika na mwenendo na maadili ya RC Chalamila.

Tunataka uwajibikaji na sheria ichukue mkondo wake kwa sababu maagizo ya Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa yamepelekea mauaji ambayo yangeweza kuepukika endapo busara zingetumika. Kuanzia muuaji na wote wanaohusika na sakata hili wanapaswa kufikishwa mbele ya sheria ili haki ipatikanike.

Maadili ya viongozi wengi wa CCM imepelekea chama hiko kuwa kichaka cha wahalifu
Ni kweli nakubaliana kwamba huyu RC pia ni mtuhumiwa kwenye sakata hili(Accessory to crime), lakini, Je, huyo Askari amri ya kufyatua risasi na kuua mtu alipewa na nani?

Je, Immediate Commander wake aliyeongozana naye kwenye doria hiyo alimuamuru kufyatua risasi?

Kama doria waliyofanya Askari Polisi hao hapakuwa na Immediate Commander, basi hilo litakuwa ni tatizo kubwa sana ktk Utendaji wa Jeshi la Polisi Tz, na watu/maafisa wengi wa Polisi ndani ya Jeshi hilo wanapaswa kuwajibishwa, ukianzia na Mkuu wa Kituo cha Polisi hapo Mabatini (OCS), Incharge aliyekuwa zamu siku hiyo ya tukio, n.k.,
 
WAkati Bi Samia anamrudisha kwenye uongozi alimwambia "ukue sasa".
Mwana hataki kukua, damu ya baunsa aliyepigwa inamlilia mikononi mwake
Dar imetamalaki kwa uchafu,
Miundombinu ya mchongo inashindwa kuhimili hata mvua ya nusu saa.

MKuu wa Mkoa badala ya kubuni mikakati ya kimaendeleo, yeye anaonesha ubabe wake na ukatili akitumia dhamana aliyopewa.

Usikute Gekul ni mwenye tabia njema kuliko hawa tunaowaona wakijichekesha kwenye kadamnasi
 
Bejamini Netanyahu huenda anakumbuka tukio la akwilina ambaye risasi ilitoka hewani bada ya kunguru kuiangusha na kumdondokea akwilina akiwa ndani ya daladala.
Tukio lile ni matokeo ya CCM kutumia dola kubaki madarakani.

Damu ya Akwilina, Mawazo, Ben Saanane, Azory, Mwangosi na wote waliouawa na dola zinawalilia CCM na ndiyo mafuta ya kuwachomea kila wanapoundei
 
Dar imetamalaki kwa uchafu,
Miundombinu ya mchongo inashindwa kuhimili hata mvua ya nusu saa.

MKuu wa Mkoa badala ya kubuni mikakati ya kimaendeleo, yeye anaonesha ubabe wake na ukatili akitumia dhamana aliyopewa.

Usikute Gekul ni mwenye tabia njema kuliko hawa tunaowaona wakijichekesha kwenye kadamnasi
Inashangaza kweli. Kuna mambo chungu mzima ya kudeal nayo kuliko kufuatilia watu wanaotumia miili yao kupata pesa.
 
Back
Top Bottom