RC Chalamila: Mkoa wa Dar es Salaam una ratiba iliyobanana ya siku kadhaa za mwezi January 2024

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,318
24,218
15 January 2024

Amesema siku hiyo kama kuna watu watajibadilisha kuwa takataka watabebwa.

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM ATANGAZA SHUGHULI NYINGI ZA WAZI ZA UMMA ZITAKAZO WATINGA WATENDAJI WOTE HADI MWISHO WA MWEZI

View: https://m.youtube.com/watch?v=i-7HQxxRbbQ
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam RC Albert Chalamila ametangaza mbele ya wakuu wa wilaya za mkoa wa Dar es Salaam jinsi mkoa ulivyojipanga huku diary / shajara imejaa matukio muhimu ambayo mkoa ilshajipangia
  1. Usafi wa jiji
  2. Tutakusanya kina mama wote waliozaliwa tarehe 27 kama mheshimiwa Rais
  3. Waalimu nao watakuwa na maadhimisho ya siku ya elimu
  4. Shughuli ya kupokea na kugawa vitendea vya kufanya usafi
  5. Clouds Media na Azam Media kuanza kushiriki katika shughuli hiyo ya kuhamasisha matukio hayo muhimu ndani ya mkoa
  6. N.k
Msururu wa shughuli hizo za watu wengi zitafanyika kuanzia asubuhi hadi jioni sana katika siku mbalimbali na wilaya pamoja na vitongoji vya mkoa wa DSM, mkuu wa mkoa RC Albert Chalamila akiwatangazia maDC wake wote pamoja na wakurugenzi wa wilaya na wakuu wa vitengo mbalimbali vya ofisi za mkoa na TAMISEMI waliopo mkoa wa DSM .

Alipoulizwa kuhusu maandamano, RC Chalamila asema yeye hana taarifa ya kuwepo maandamano maana mambo hayo yanamuhusu ACP Jumanne Muliro kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum mkoa wa Dar es Salaam na mpaka sasa yeye mkuu wa mkoa hajapewa taarifa hivyo hafahamu suala hilo.
 
Hao kina mama atakao wakusanya ni watoto wake au wake zetu? Hii shuruti ya kukusanywa inatoka wapi?
 
Kila mbinu inatafutwa na chama kongwe dola CCM kudhoofisha sauti na uhuru wa raia wa Tanzania
Wanaulinda utajiri waliokwisha upata wanajua katiba inaweza ikawadhibiti kwenye utajiri wao na jinsi walivyoweza kununua mijengo Dubai na Hong Kong.
 
24 January 2024
Dar es Salaam, Tanzania

ACP Jummane Muliro katikati ya maandamano leo eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam, wasalimiana na kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Tanzania Mh. Freeman Mbowe. Wateta na kusema naam, mambo yanakwenda vizuri kwa amani kabisa ..

View: https://m.youtube.com/watch?v=JJDeSc60Jww
 
Back
Top Bottom