Elections 2010 PICHA: Kikwete alivyofunika jana huko Mwanza

n00b

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
1,006
2,667
umatiwawananchikatikamkutanowakampeniuwanjawasaharajijiniMwanza2.jpg

NyomiiliyomlakiJKuwanjawaSaharajijiniMwanzawakatiwamkutanowakampeni.jpg

MsaniiBushokeakitumbuizauwanjawaSaharajijiniMwanza.jpg

NyomiiliyomlakiJKuwanjawaSaharajijiniMwanzawakatiwamkutanowakampeni2.jpg

NyomiiliyomlakiJKuwanjawaSaharajijiniMwanzawakatiwamkutanowakampeni7.jpg
 
Uwe wazi ni wangapi ni wa hapo Mwanza na wangapi wameletwa kujaza hesabu kutoka nje ya Mwanza.............be honesty malori na mabasi ni ya nini?

Na wangapi wamekuja kuburudika na "show" ya bwererere................Ukizifanya hizi hesabu kwa makini utagundua kumbe JK alifunikwa na wala hakufunika hata chembe
 
Mzee Mwanakijiji;
"Tuseme kweli hata pamoja na malori bado JK anamvuto na yeye...."

Hilo halina ubishi.
 
Tuseme kweli hata pamoja na malori bado JK anamvuto na yeye....
akiwa kama mkuu wa nchi lazima awe na mvuto kaka. kila mtu hupenda kumwona mtawala na kujihisi ameona nyota njema.
But tutayaona haya kwenye ballot box jumapili
 
Tuseme kweli hata pamoja na malori bado JK anamvuto na yeye....

Mbona safari hii hajawapeleka CCM KILUMBA kama kweli bado ana mvuto???? Wanaanza kukimbia kivuli chao.Sasa wana tofauti gani na wapinzani wasio na viwanja??? Alijua akiwapeleka CCM kilumba watu wasingeenda. Hata hivyo nyomi haitoshi ukizingatia yeye ni Rais bado akisaidiwa na majeshi ya Lau Masha.Maji ya shingooooooooooooooo.Naona na mafungu ya kukodi malori yamekwisha.
 
Tuseme kweli hata pamoja na malori bado JK anamvuto na yeye....

MMKJ,
Mvuto wake ni Fiesta. Nani asiyependa Burudani. nani asiyependa kupata buku 5,000/- kwa usawa huu. Anayekubali kupanda kwenye lori ndo anapata T-shirt, Kofia na Buku 5.

Pili watu walitolewa mbali na malori. Huwezi amini watu walitolewa Misungwi, Magu, Ukerewe, Kwimba na sengerema. Hapo utasema wananchi wa jijini mwanza.

Acha wadanganyane kiama kinakuja
 
eeeh waliofunika mkutano huo ni WA CHADEMA na Vyama Vingine! Hawana ubaguzi kama wa JK kuzuia watu kutumia viwanja vya umma. Kilicho mfanya asifanyie mkutano wake CCm kirumba ni kutojiamini kuwa hawatapata watu wa kujaza uwanja kama alifanya last time kwa kusomba watu. Waache ubaguzi na unyanyasaji wao wa kuzuia watu kutotumia viwanja vya umma!!

CHAGUA CHADEMA CHAGUA CHADEMA
 
Watu wameandaliwa kutoka mikoa jirani hawa . Hata hivyo wengine wamekuja kumwangalia mara ya mwisho hapa ili historia isiwapite na siyo kwamba eti wamevutwa ili tarehe 31 October wampigie kura. Hapa wamehudhuria kutoa tu heshima za mwisho kwa Chama cha mapinduzi. Kama mi mwongo uulize ule umati waliohudhuria pale mnazi mmoja tare 9/12/1961 kama walikuja kum support mkoloni au kumuaga na kumkaribisha Nyerere
 
Tuseme kweli hata pamoja na malori bado JK anamvuto na yeye....

Mzee MK usidanganyike na huo umati hapo hao huwa wanakodiwa kutoka sehemu za karibu ikibidi hata mkoa wa karibu ili waje mkutanoni kuonekane kumejaa na anakubalika, hao ndio CCM wanafanya kila njia ili wakubalike but ukweli uko palepale watanzania wamewachoka
 
Ebu cheki umma ulivyo kubali yaani CHADEMA kuitoa CCM madarakani ni sawa na kuku kuzaa ndama na ng'ombe kutanga mayai....
 
Pamoja na hayo yote, urais kwaheri jk, mpeshe mkombozi wa kweli anayeaminika kwa Watanzania DR.Slaa na CHADEMA,:yield:
 
Back
Top Bottom