...huyu si ndiye ambaye Shule zake (St. Mary`s) zinaiba umeme wa Tanesco!!
Ama kweli pesa haidanganyi kamwe
Nimejifunza kitu kimoja, hakuna kitu mwandamu atafanya asipate Upinzani. Lakini ninasikitika sana mtu anyemtafuta Mungu akifanikiwa maswali yanakuwa mengi sana, hivyo wakati mwingine huwa najiuliza watu wanomuomba MUNGU iliwafanikiwe wakijua MUNGU atawasaidia au Wanajaribu tu liwalo naliwe nahata wakisaidiwa hawajui kuwa wamesaidiwa?.KwaniniMtu akumshukuru MUNGU kwa mafanikio watu wanoana shida? au ni imani kuwa MUNGU hawezi kumpa mtu Utajiri/mali na hivyo shetani ndiyo mwenye uweza wa kufanya hivyo.
Nimefuatlila mijadala mingi hata mtu akimwombea mtu akapona wazo la kwanza ni shetani kafanya, kanisa likiwa na waumini wengi mawazo ni kuwa nguvu zimetoka zinazo wavuta ni za kichawi, hivi ni mawazo sahihi au akiri za watu zimetekwa sana na mambo ya giza sisiamini nguvu ya MUNGU?. Au ndiyo silaha ya Uovu kuwatia watu giza wasiamini uweza Mtakatifu?.
Haya ni mawazo yangu naomba nifikiri na wewe, Kama kweli Unamwamini MUNGU, na kweli unaamini anauweza kufumfanya mtu aishi maisha bora kama yalivyo makusidi yake;je si kweli watumishi wake wangeishi maisha bora zaidi kuliko mtu yeyote kwa sababu wanfanya kazi yake?, mbona tumeona wanomtumikia shetani /freemason wanishi maisha bora na angali tuanamini MUNGU ana nguvu zaidi. sasa nini shida watumishi wa MUNGU wakimiliki mali inakuwa taabu wakati MUNGU wao ndiye mwenye Fedha na dhahabu.
Naamini tunakosea mahali furani juu ya imani zetu, penginepo hatujui tuna mwamini mungu yupi(kwa wale wenye kuamini MUNGU) na pia hatujui uweza wake na mawazo yake juu ya watu wake, na ndiyo maana tumekuwa watu wakubebwa na yale tuno yasikia na kuyaona kila siku kutoka upande wa shetani.Mfano; tunafahamu kuwa watu wengi wanafanya kazi, biashara au kutoa huduma mbalimbali huku wakiwa wamekwenda kwa mafundi, waganga, wachawi na wengine hatakutoa kafara za damu za watu na wanyama na jambo hili limeene sana masikioni mwa watu hata kiasi kwambau ukiongea habari za mafanikio na MUNGU wanona ni jambo la uongo.
Ombi langu ni MUNGU ajionyeshe zaidi ili watu watambue uwepo wake na Waliofanikiwa wakiwa na uhakika kuwa ni MUNGU JEHOVA amefanya wajitangaze zaidi ili kushawishi watu, kwani shetani na watu wake wanajitangaza zaidi na kuufunika ulimwengu. Sisi sote tunahitaji kumili vitu vizuri hivyo ni rahisi kushawishika upande wowote ili upate, MUNGU awasidie wamwaminio kuangukia upande wake.
ubunge amepata kwa rushwa