Picha: Kasri a.k.a Nyumba Mpya ya Mh. Mchg. Dkt Rwakatare ktk ufukwe wa Bahari

mupenzi,
wenzio hawana sheria...
wako juu ya sheria..
kajenge wewe sasa...asubuhi unakuta bonge la X ukutani...BOMOA!

Hapo kwenye red Mkuu!

Wala siyo BOMOA tu! Huwa wanaandika BOMOWA!! Hili huwa naliona mara kwa mara huku kwetu, sijui huwa wanatumia watu gani kuweka hizo alama?
 
Kama hilo kasiri limejengwa kwa pesa za halali ,sioni tatizo lolote!
Tatizo langu kubwa na Mch.Dokta.Mhe.ni moja tu:anapenda kuabudiwa na kutukuzwa sana!
Sipendi kabisa hali hiyo.Anayeleta ubishi atembelee Kanisani kwake Mikocheni ''B''.
Akiwa anaingia kanisani eti waumini hutakiwa kusimama kama ishara ya heshima!!Hii ni halali wanajamvi?
Sasa sisi wengine tulioathirika na fikra za ''usawa wa binadamu'' na ''heshima kwa wote'' tunapata tabu sana kumuelewa!
Halafu kuna ''UCCM'' na ''userikali'' mwingi sana pale kanisani kwake.
 
Kwa hiyo na wewe umeanzisha dini ya ulokole na inakulipa???

Yeah nimeanzisha vile vile nimeoteshwa, naombea wenye ukimwi, wenye kansa, pumu na magonjwa yote sugu, vile vile nasaidia watu wafanikiwe kimaisha kama biashara na kazi. Karibu sana kanisa langu lipo Manzese Tip top utakuta bango kuuuubwa pale limeandikwa maneno ya kiroho.
 
Nyumba..nyumba!!. Nyumba ni ft. 6 chini ya ardhi.
Huu ni ufisadi, aturudishie chenchi inayozidi kwenye ada tunazolipia watoto wetu ktk shule zake hata kama tunalipa kwa hiari yetu. Uingereza wameweza, na yeye afanye hivyo...
Huko TANESCO ilikuwaje? amelipa faini? kiongozi wa dini anayeharibu mazingira na kujenga eneo lisilotakiwa halafu anakimbilia mahakamani. Nani atanusuru dunia hii?? Huyu ndio mbuge wa CCM. CCM juu, kasi zaidi..!!!!
 
rwakatare.JPG

NI KWANINI GETRUDE HAISHI NYUMBA MOJA NA HUYU MMEWAKE?
 
kila siku tukisema makanisa yamegeuzwa miradi watu wanabisha.i dont go to chuuuuuuurch.
God is everywhere kama alivyosema.
Tusipumbazwe akili na wachungajiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Yeah nimeanzisha vile vile nimeoteshwa, naombea wenye ukimwi, wenye kansa, pumu na magonjwa yote sugu, vile vile nasaidia watu wafanikiwe kimaisha kama biashara na kazi. Karibu sana kanisa langu lipo Manzese Tip top utakuta bango kuuuubwa pale limeandikwa maneno ya kiroho.
Tuletee mapichaya mahekalu yako na wewe tuone..
 
mtu anayejifanya mtu wa mungu na hizi anasa wapi na wapi?
ni rahisi ngamia kupenya kwenye tundu la ........................... kuliko tajiri kuuona ufalme wake.
wangapi wanalala chini hospitali,wangapi hawapati mlo,yatima wangapi wanahitaji msaada?

SHIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIT
 
Mkuu wakati mwingine tujaribu kupunguza kitu kinacHo onekana kama ni wivu vile! Kwani nani usiye juwa uwezo wa kifedha wa Mama huyu - ajenge shule lukuki hashindwe kijijengea kibanda cha ADHI YAKE - teh,teh,teh "Achana na shemeji yangu BWANA" ajinafsi.
 
haya bana
ni ile ya aliye nacho huongezwa.
nikatafute huko kibarua cha kufuta vioo.
 
Bagamoyo pole kwa kudhulumiwa na kujawa na chuki naye. Lakini huwezi kushitaki kwani ukithubutu nawe selo. Biashara hizo hatushitakiani bhanaaa ila tunapakaziana tu.
 
Back
Top Bottom