Picha: Kasri a.k.a Nyumba Mpya ya Mh. Mchg. Dkt Rwakatare ktk ufukwe wa Bahari

Aiseee...kumbe biashara ya makanisa inalipa, ndiyo maana kila siku yanaongezeka.
Halafu uzuri ana uhakika wa kwenda mbinguni, kwahiyo kwake ni raha tu duniani mpaka mbinguni.
Hongera sana mama.
 
Hili jumba limejengwa ufukweni katika sehemu isiyoruhusiwa na sheria kujenga nyumba; ilikuwa ivunjwe wakati wa bomoa bomoa lakini wakakimbilia mahakamani kuomba injunction hivyo ikasalimika otherwise ingevunjwa!! Sasa haya mapicha ni kampeni ili wapate public sympathy kuwa serikali inavunja majengo ya gharama!! Let us wait and see kama serikali itakuwa na double standards kwani nyumba jirani na hii zimevunjwa pale ufukweni!
 
Mkuu umenichekesha mbaya! Sisi ndio hatuna makuu kila sheikh anakaa kwenye kamjengo kake na sadaka zote nikwa ajili ya msikiti sio tumbo la sheikh.

Hapo ndo Raha! Kuliko hawa wenzetu. Yaani kama ni Muumini presha inakupanda Mana huna hata baskeli na ulikuw unajitahidi kweli kutoa Sadaka

Yaani sisi RC ukimwona Padri/Sister anaendesha RAV 4 au Cruiser hupatwi na hasira Maana mlimchangia Wenyewe na Kumpa kwa Upendo wenu Kanisani na Inabaki ya Kanisa si Yake tena Masista/Mapadri wengine wataitumia pia
 
Kuanzisha kanisa ni biashara inayolipa kwani bongo vilaza ndio kwao; huoni hata watu wanaojulikana kufanya biashara ya madawa ya kulevya wanahusishwa na haya makanisa uchwara!
 
Kha, nimeipenda hii, sio unahubiria wenzio utajiri kumbe mwenyewe huna kitu!!! mie hata simo
 
Nimejifunza kitu kimoja, hakuna kitu mwandamu atafanya asipate Upinzani. Lakini ninasikitika sana mtu anyemtafuta Mungu akifanikiwa maswali yanakuwa mengi sana, hivyo wakati mwingine huwa najiuliza watu wanomuomba MUNGU iliwafanikiwe wakijua MUNGU atawasaidia au Wanajaribu tu liwalo naliwe nahata wakisaidiwa hawajui kuwa wamesaidiwa?.KwaniniMtu akumshukuru MUNGU kwa mafanikio watu wanoana shida? au ni imani kuwa MUNGU hawezi kumpa mtu Utajiri/mali na hivyo shetani ndiyo mwenye uweza wa kufanya hivyo.

Nimefuatlila mijadala mingi hata mtu akimwombea mtu akapona wazo la kwanza ni shetani kafanya, kanisa likiwa na waumini wengi mawazo ni kuwa nguvu zimetoka zinazo wavuta ni za kichawi, hivi ni mawazo sahihi au akiri za watu zimetekwa sana na mambo ya giza sisiamini nguvu ya MUNGU?. Au ndiyo silaha ya Uovu kuwatia watu giza wasiamini uweza Mtakatifu?.

Haya ni mawazo yangu naomba nifikiri na wewe, Kama kweli Unamwamini MUNGU, na kweli unaamini anauweza kufumfanya mtu aishi maisha bora kama yalivyo makusidi yake;je si kweli watumishi wake wangeishi maisha bora zaidi kuliko mtu yeyote kwa sababu wanfanya kazi yake?, mbona tumeona wanomtumikia shetani /freemason wanishi maisha bora na angali tuanamini MUNGU ana nguvu zaidi. sasa nini shida watumishi wa MUNGU wakimiliki mali inakuwa taabu wakati MUNGU wao ndiye mwenye Fedha na dhahabu.

Naamini tunakosea mahali furani juu ya imani zetu, penginepo hatujui tuna mwamini mungu yupi(kwa wale wenye kuamini MUNGU) na pia hatujui uweza wake na mawazo yake juu ya watu wake, na ndiyo maana tumekuwa watu wakubebwa na yale tuno yasikia na kuyaona kila siku kutoka upande wa shetani.Mfano; tunafahamu kuwa watu wengi wanafanya kazi, biashara au kutoa huduma mbalimbali huku wakiwa wamekwenda kwa mafundi, waganga, wachawi na wengine hatakutoa kafara za damu za watu na wanyama na jambo hili limeene sana masikioni mwa watu hata kiasi kwambau ukiongea habari za mafanikio na MUNGU wanona ni jambo la uongo.

Ombi langu ni MUNGU ajionyeshe zaidi ili watu watambue uwepo wake na Waliofanikiwa wakiwa na uhakika kuwa ni MUNGU JEHOVA amefanya wajitangaze zaidi ili kushawishi watu, kwani shetani na watu wake wanajitangaza zaidi na kuufunika ulimwengu. Sisi sote tunahitaji kumili vitu vizuri hivyo ni rahisi kushawishika upande wowote ili upate, MUNGU awasidie wamwaminio kuangukia upande wake.
 
Wachungaji wa sasa wanatuaonyesha jinsi ilivyo mbinguni hapahapa duniani, halafu sisi tutadanganywa eti tukifika mbinguni tutapata raha....mbona wao wanakula raha hapahapa? Narudia dini yangu ya asili!!!!!!!!!!!
 
Mie kitanda changu ni nne kwa sita na tunalala watatu, mimi, mke wangu, na mtoto, hivyo hata siku tukiwa tumepishana kiswahili ni lazima tupatane tu maana kila ukigeuka huyu hapa, huna jinsi ya kumkwepa, sasa jumba lote hili huku unalala kwene chumba kimoja!! ni lanini? au ndio mijusi na buibui watakaua wanakula gud time tu!!! Kweli nimekumbuka Mithali; Tazama Mijusi wamo kwenye nyumba za wafalme
 
Mch. Mh. Getrude Pangalile Rwakatare kabla ya kuhamia kwenye hekalu lake jipya alikuwa akiishi Mikocheni B katika nyumba ya kifahali pia. Alizidi kukaa katika uwepo wa Mungu na kufanya kazi yake kwa bidii na kujituma. Katika mahubiri yake kwa waumini wake amekuwa akiwatabiria watu mafanikio na watu wamefanikiwa kutokana na utabiri wake. Leo hii imekuwa zamu kwake ambapo Mungu hakutaka kumuabisha kma mtumishi wake, akamshangaza kwa muujiza wa kumuwezesha kujenga jumba la kifahari kwa gaharama kubwa sana,


Nisowachoshe kwa maneno mengi, naomba tuangalie kazi ya Mungu kwa wanadamu.


Source: habari imenukuliwa neno kwa neno na picha zaidi
RUMAFRICA: HEKALU JIPYA LA MCHUNGAJI DK. GETRUDE RWAKATARE KUFUNGULIWA RASMI

Sasa huyo mungu badala ya kutuletea Hospitali za kifahari anatuletea hekalu la mtumishi wake? Isije ikawa yeye na mtumishi wake wametumia sadaka zetu!
 
Biashara ya imani inalipa sana, kwa sababu wanaoamini wanakuwa vipofu!lol
 
Wachungaji wa sasa wanatuaonyesha jinsi ilivyo mbinguni hapahapa duniani, halafu sisi tutadanganywa eti tukifika mbinguni tutapata raha....mbona wao wanakula raha hapahapa? Narudia dini yangu ya asili!!!!!!!!!!!


Yeah_wewe ndio utakuwa mlokole wa kweli,...umeushtukia mapema huu utapeli wa mashariki ya kati.
 
Back
Top Bottom