PICHA; Diamond afunika Dar- LIVE!

Kiganyi

JF-Expert Member
Apr 30, 2012
1,242
765

Mwanamuziki Diamond anayevuma kwa sasa hapa nchini kifanya onyesho zito na la kukata na shoka mbele ya mashabiki wake kwenye ukumbi wa Dar Live, onyesho hilo lililofanyika jana siku ya jumapili na kuvuta hisia za mashabiki wake lukuki waliojitokeza kumshuhudia akishuka na helikopta kama ilivyokuwa imetangazwa na waandaji wa onyesho hilo.

Mwanamuziki Diamond akijiandaa kwenda kupanda helikopta tayari kwa kuelekea katika ukumbi wa Dar Live

Mwanamuziki Diamond akiwa kwenye helikopta tayari kuelekea Dar Live.

Hapa akionyesha ishara ya kuwasalimia mashabiki wake kwa heshima.

Akiuangalia umati mkubwa uliojitokeza kwenye ukumbi wa Dar Live ili kushuhudia wakati akishuka na helikopta.

Wacheza shoo wake wakifanya vitu vyao jukwaani.

Wasanii wa Pah One, Watanzania wenye maskani yao Afrika Kusini wakifanya vitu vyao

Timbulo akifanya vitu na dancers wake

Katika shoo zote za Dar Live, Diamond amevunja rekodi ya idadi ya mashabiki​
 
Si walisema atashuka kwa kuning'inia kwenye kamba kama comando!! kumbe ameshuka kama abiria wa kawaida tuu!!
 
Naona ameanza kuvaa makofia na magwanda kama ya kina Wako J
 
Si walisema atashuka kwa kuning'inia kwenye kamba kama comando!! kumbe ameshuka kama abiria wa kawaida tuu!!

Inasemekana ni kwasababu viwanja husika vya Dar Live vilijaa sana hivyo waliona itakua si salama kwa Diamond na wananchi(wapenzi wake) walokua hapo.
 
Ajipange kushuka kwa helikopta atakumbuka akichokwa!!apige mambo ya maendeleo kuwekeza kwenye mambo ya maana!!mlio karibu nae mshaurini dogo awekeze!!
 
kuna kitu kimoja nimejifunza toka kwa watanzania wenzangu. Siku zote mtu akifanikiwa uwa watu wanakaa wakisubiri aanguke yani maombi yao na furaha yao ni pale atakapo anguka sijui nini uwa kinawauma.
Dogo hana shobo kivile na anajituma jukwaani so mimi naona poa tu anavyo shine anawapa challenge wasanii wengine wanaopga shoo kwa kushka sehemu nyeti na kutembea tembea toka kona moja ya stage mpaka nyinge yani show ya juzi leo na mwaka jana hazitofautiani.
I am sure ukiudhuria show ya diamond utakuwa unajiuliza leo atakuja vipi kwasababu anabadirika badirika.
La msingi na yeye awekeze asibweteke sana maana mziki hautabiliki.
Mtu mwingine ambaye nahisi atakuja fanya poa ni timbulo maana anaona naye kaamua kuwa na team yake ya madancer pia.
Helicopter ilitumika kama business technic ya kujaza watu wengi maana wabongo wengi wanapenda kushangaa helicopter si waona hata wanasiasa wanatumia hiyo technic kwenye kampeni zao.
 
elmagnifico...umeongea point!!!!nakazia!simtetei diamond ila kama ni mshkaji wako au mmekutana mkakaa dakika kadhaa!huwezi ukamkandia!ana heshima,hana kuvimbia wana kama wakali wengine!mistake yake ni kuweka mahusiano yake hadharani!hapi ndo raia wanamind kwani wanaona kama hastahiki kung'oa hao madem!kiufupi raia wengi roho inawauma ila wakichukulia kama ni weakness yake kujitangazia naamini hawatochukia!platinumz kung'oa hivi vifaa kama ndoto wamwache ajivunie!wangapi wanakumbuka FNL moja diamond hajatoka fresh kimziki halafu wema sepetu yupo juu wapo kipindi kimoja?diamond kapauka mbaya hapo hata hajui kama atakuja kutoka kimziki wala kuja kumpiga ndizi wema!diamond alikuwa anarap haimbi kama siku hizi!full mapowder anatia huruma
 
Last edited by a moderator:
Naomba nikupinge hawapendi ashuke, ila wanampa tahadhari mana Wengi hushuka na wanakuwa choka mbaya.

kuna kitu kimoja nimejifunza
toka kwa watanzania wenzangu. Siku zote mtu akifanikiwa uwa watu wanakaa wakisubiri aanguke yani maombi yao na furaha yao ni pale atakapo anguka sijui nini uwa kinawauma.
Dogo hana shobo kivile na anajituma jukwaani so mimi naona poa tu anavyo shine anawapa challenge wasanii wengine wanaopga shoo kwa kushka sehemu nyeti na kutembea tembea toka kona moja ya stage mpaka nyinge yani show ya juzi leo na mwaka jana hazitofautiani.
I am sure ukiudhuria show ya diamond utakuwa unajiuliza leo atakuja vipi kwasababu anabadirika badirika.
La msingi na yeye awekeze asibweteke sana maana mziki hautabiliki.
Mtu mwingine ambaye nahisi atakuja fanya poa ni timbulo maana anaona naye kaamua kuwa na team yake ya madancer pia.
Helicopter ilitumika kama business technic ya kujaza watu wengi maana wabongo wengi wanapenda kushangaa helicopter si waona hata wanasiasa wanatumia hiyo technic kwenye kampeni zao.
 
Wapi mr nice,prof j,mnyalu,crazy gk.Ferouz.Wacha dogo atumbue siku nyota ikishuka chini mabinti aliokuwa sasa hata waona tena piga mpaka no3 sijui ni nani.
 
nadhani dogo ni creative. anajaribu kubuni na kufanya vitu ambavyo siku za nyuma havikuwahi kufanyika. hii ina msaidia kutangaza biashara yake vizuri hivyo ku-make money zaidi. aendelee na ubunifu atafika mbali.
 
Tukubaliane kuwa hakuna aliyewahi kupata umaarufu kama Diamond. Na pia kijana anajituma, na show zake huwa anajipanga haswa. Yaani huwa anafanya maandalizi ikiwamo mazoezi na rehearsals.
Tunajua hao waliomtangulia walikuwa na tatizo la kuharibu kwenye live shows.
Diamond ni mkali kwa kila nyanja na hata live shows huwa anabamba sana.
Sidhani kama kuna msanii Tz aliyewahi kujaza watu kwa kiingilio cha 50,000TZS
Big up Diamond !
 
True Diamond ni moto wa kuotea mbali.
Ushauri wa bure kwa walio karibu yake wamwambie awekeze sasa hayo mafao kwenye assets ( fixed au hata kwenye mashares).Siju kama ana meneja wa kuangalia shughuli zake,mapato yake.ni vizuri akamwajiri atamsaidia sana.
 
Back
Top Bottom