Natamani sana Dar es Salaam ingeweza kuzingatia sana kwenye usafi wa mazingira maana kwa mazingira yalivyo kwa sasa sio salama

MaylaGladson

Member
Jan 18, 2020
17
21
Habari wana Jamii Forum
Ningeomba niwasilishe hili swala kwa jamii ili tuliongelee.
Dar es Salaam ni Jiji zuri sana kwa hapa Tanzania ambalo linapendwa na wengi na huo ndio ukweli usiopingika,lakini pamoja na uzuri wake wote kuna kitu kimoja tu kinashusha thamani ya Jiji hili nacho ni MAZINGIRA MACHAFU TENA YASIYO SALAMA.

Ukitaka kuamini zaidi kama mazingira ya Dar es Salaam sio rafiki basi subiri kipindi cha mvua ndio utaelewa angalau kukiwa najua ni nafuu(Ushawahi kukutwa na mvua ukiwa maeneo yavKARIAKOO).Mvua zikinyesha unaweza ukatamani usitoke hasa ukijua maeneo utakayopita ni yatakua ni balaa maana unaweza ukapita eneo chemba zote zimefunguliwa kwahiyo mimaji michafu ya chooni yote inatiririka kuelekea mabarabarani na huko barabarani unakuta watu wanauza biashara na hazifuniki ila bado watu watanunua na hawajali lolote..Na unakutana na vitoto vinachezea hayo maji machafu bila kuelewa kuwa wanachokifanya ni hatari kwa afya yao.Aisee ni MUNGU tu hulinda watu wake.

Hapo hapo utakutana na takataka kibao zimezagaa kiholela holela tena za kutosha. Mazingira yananuka harufu mbaya sana na haya bariki. Kwanini kusiwe na utaratibu wa utunzaji wa mazingira na kuwekwe sheria kali kweli kwa wale ambao watakiuka?Kwa upande wangu naona itasaidia sana sana.

729923F1-21E6-4415-A287-35867A37599A.jpeg

Kwa nchi za Africa ni Rwanda(kigali)ndio nchi inayosifika zaidi kwa usafi Africa.Hivyo basi ingependeza basi na sisi tujifunze kutoka kwa wenzetu.Kibongo bongo ni MOSHI Pekee ndio inasifika kua na mazingira masafi sana na kweli ni masafi na yamekaa katika muonekano mzuri sana wa kuvutia.Uongozi wa mkoa wa Moshi nadhani uliamua kuweka msimamo wao, na watu wao wakaamua kutiii mpaka leo hii utaratibu ndio huo huo, kwanini DAR ES SALAAM kusiwekwe utaratibu huo? Mbona inawezekana japo kua itachukua muda ila inawezekana.

Mh Paul Makonda wakati ni Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam aliwahi kufanya huo utaratibu wa kuzingatia mazingira kwa hili jiji na kiukweli apewe maua yake kwa hilo.Lakini alipomaliza uongozi wake ni kama ule utaratibu uliishia alipomaliza yeye.Hivi inakuaje jambo la msingi kama hilo mwenzako alilianzisha halafu linaachwa kuendelezwa?Mi nadhani kama mwenzako ameanzisha jambo la maendeleo lenye faida na akamaliza uongozi wake,Wewe ukiingia endeleza alichokianzisha mwenzako ili kuhakikisha lile jambo linatimia,na hayo ndio maendeleo.Sio mwenzako kaanzisha hivi wewe ukija unalisahau kutilia mkazo lile swala na unakuja sera zako mpya. Ni vizuri ukaja na vya kwako na vizuri walivyoanzisha wenzako pia ukaendeleza ikiwa tu vitaleta matokeo chanya

Kwa Maoni na ushauri wangu,Ni kwamba Serikali isimamie kwa Kuweka sheria kali sana ambazo zitamtengenezea mtu utaratibu fulani wa kuyalinda mazingira bila kushurutishwa na akikiuka sheria ifate mkondo.Kama ni faini alipe na alichokosea pia ahakikishe anawajibika nacho.
Baadhi ni taratibu ambazo zikifatwa zitasaidia.

- Kuzuia kutupa Takataka hovyo,kuwe na utaratibu wa kutupa taka kwa kuweka mapipa ya kueka Takataka maeneo yote ya sokoni,vituo vya mabus,mashuleni, Bar, Migahawa, mahospitalin, viwandani na mazingira yote kuzunguka barabara zetu. Kwahiyo watu watajiongeza kua tunatakiwa kutupa mahala hapa na hizo taka zikijaa kuwe na watu maalum wa kuziondoa mapema wasisubiri mpaka zikamwagika watu wakakosa pakuweka taka,na hao wabeba taka walipwe vizuri ili kazi ifanyike kwa moyo.

-chemba zisifunguliwe wakati wa mvua…kama chemba yako imejaa kuna magari yale yanakuja kunyonya kila kitu na sidhani kama ni gharama kihivyo ni swala la mtu kuamua na kujipanga,tuache kujiendekeza kulea uchafu ambao utatuletea milipuko ya magonjwa.

-kwenye Mitaro sio sehemu ya kutupa taka ndio maana mvua ikinyesha inaziba na maji yanakosa sehemu za kupita yanahamia majumbani mwa watu.

-Kingine watu wa wenye magari ya taka wanatakiwa waheshimu siku za kuchukua taka,maana wanaweza kaa miezi hawapitii taka na hela za taka mtaani tunachangishwa kila mwezi.Msipopita ndio chanzo cha watu kutupa taka kwenye mitaro na chemba.Ningeomba serikali isimamie hili swala hawa watu wa magari ya taka wapewe magari mazima sio chakavu vile na wao wapewe mavazi maalum yenye muonekano wa kisasa hata kama wanabeba taka(wabeba taka wa nchi za wenzetu walivyo nadhani tunaona hata kwenye movie).Kingine walipwe vizuri ili waijali kazi yao na watu wasiwachukulie poa maana ndio wanaohakikisha jiji haliwi katika mazingira machafu,Kwahiyo waheshimike sana sana.

-Majalala yawe yanasafishwe vizuri yanachomwa vizurii.Ikiwezekana kuondolewa kabisa kama hayatumiki.

-Mazingira ya nyumbani watu wajiongeze wafyeke,walimie na serikali za mtaa ziwakazie watakao kiuka huo utaratibu.l

-Wauza biashara za barabarani kina Mama|Kaka|Dada|Baba wapewe elimu kuhusu Afya na mazingira.Wapewe elimu ya kuheshimu kazi zao hata kama wanaziona ni za kipato cha chini lakini wanapaswa kuuza bidhaa zao huku wenyewe wakiwa wasafi na mazingira yawe masafi na yamridhishe mteja kununua vitu.
Wafunike vyakula vyao hasa wauzaji wa vitu kama Ubuyu,Juice,Nyama|Mishkaki|Maandazi|Vitumbua|Mihigo nk wajitahidi sana kufunika hivyo vitu vyako na kutengeneza mazingira ya kumuonyesha mteja kama anaweza kupats huduma fulani .

Mazingira yanayotakiwa kutiliwa mkazo sana ni HOSPITALINI HASWA VYOONI NI HATARI,MASOKONI PIA HATA VYOONI NI HATARI,BARABARA KUU.MASHULENI.MIGAHAWANI.

Serikali ikiweza kufanikisha hili swala la usafi wa mazingira kwenye jiji la Dar Es salaam linakua safi basi itakua rahisi mikoa mengine kua misafi.Hata hivyo pia Kila mwananchi popote pale anajukumu la kulinda mazingira na kuhakikisha jirani yake analinda mazingira.Hivyo basi,ni jukumu la kila mtu kumlinda mwenzake maana yanayotokea huko mitaani ni mengi.

Ahsanteni
 
Ndio maana nasema DAR USUMBUFU...

Back
Top Bottom