Pay As You Earn (PAYE): Wafanyakazi mna maoni gani?

nadhani anamaanisha hapo........
Hapo nilikuwa najibu swali lako ulilouliza "Wote tukiwa wajasiriamali nani atakuwa mfanyakazi????".

Lengo langu ni kutanua wigo kwa namna ya kuliangalia tatizo uliloliainisha kwenye post yako ya mwanzo. Tunachotofautiana ni namna gani ya kufikia utatuzi.
 
Wote tukiwa wajasiriamali nani atakuwa mfanyakazi????

Tena mkuu??.........simple, that's what we are praying for? hapo ndipo serikali itambua umhimu wa kuwiden tax base na kuingia kutax effectively wajasiriamali ambao for now are not taxed effectively!
 
Practically sioni urahisi wake, kuacha ajira na kuwa mjasiriamali ni uamuzi mzito sana, lazima uwe umefanya uchambuzi wa kutosha nini utafanya ukiacha hiyo ajira, nakumbuka watu wengi waliacha kazi hasa NBC na kukimbili kwene biashara za usafirishaji wa abiria (Dala dala) bila hata kuwa na ABC ya biashara hiyo, achilia mbali kujua hata gari linatumia oil lita ngapi na service ni baada ya KM ngapi, kilichofuata hapo ni VILIO.

Je wangapi tuache hiyo kazi na nini tufanye? tukiacha wakaingia wengine tatizo la litakuwa limepatiwa ufumbuzi??
 
Wakuu nilikua napitia pitia sheria za kodi ya Mapato Tanzania na hasa kodi inayotozwa kwenye pato la mfanyakazi. Kwa ujumla kodi (PAYE) hii ni kubwa Mno kulinganishwa na kozi zinazotozwa biashara za ubia (partnership), binafsi (sole proprietorship), kampuni (Corporation). Nasema hii kwa sababu zifuatazo

1.0 Makampuni hutozwa kodi kwenye faida au kinachobaki baada ya kuchukua mauzo/mapato na kutoa matumizi yote. Kinachobaki kinatozwa kodi. Kama matumizi yatazidi mapato basi hamna kodi itakayotozwa hapo.

2.0 Wafanya biashara binafsi hutozwa kodi kwenye faida kama wanaweka rekodi vizuri au hukadiriwa kama hawaweki rekodi vizuri.

3.0 Mshahara kwa mfanyakazi ni sawa na mapato yaani sales. Lakini serikali badala ya kutoza kodi kwenye faida wanatoza kodi ya juu kwenye mapato moja kwa moja. Kama kampuni inatoa matumizi yanahusu biashara, kwa nini na mfanyakazi asiruhusiwe kutoa matumizi yanayohusiana na mshahara wake? Mfanyo Mfanyakazi anapokea Gross Salary ya TZS 1,000,000 kwa mwezi, hizi ni sawa na TZS 12,000,000 kwa mwaka. Kodi itatozwa kwenye 12,000,000 moja kwa moja na ni 30%. Lakini ingekua kampuni au mfanyabiashara angeruhusiwa kutoa matumizi yote yaliyomwezesha kupata hiyo 12M. Mfanyakazi analipa nauli au mafuta kwenda kazini, anajitibu ili kuhakikisha anakua na afya nzuri ya kufanya kazi, analipa kodi ya nyumba kwa usalama wake, ananunua nguo za kazini, yaani isingekua kazi asingenunua nguo hizo, inabidi ale diet ya ziada ili aweze kufanya kazi, umeme, maji. Hivi vyote havitolewi ili kupata kinachobaki kwaajili ya kutozwa kodi.

Je kwa hali hii tunaomba serikali itupunguzie mzigo wa kodi sisi wafanya kazi. Unakuta mtu unafanya kazi hauendelei hata siku moja lakini mfanyabiashara anaendelea sana. Hii ni kutokana na serekali kuwapunguzia mzigo wa kodi lakini sisi wafanyakazi unaumia kila mwezi kwa PAYE kubwa.

Jamani naomba tuchangie hii topic kwa hoja za nguvu kwa kuzingatia uzito wa swala hili.
 
Hiyo mkuu unayosema ni kweli kabisa, kodi ni kubwa (PAYE) na bado unalipa kodi nyigine! Ili kuinua kipato cha wafanyakazi, kodi iwe kidogo. Wafanyabiashara wanafaidi kwelikweli, ama kwa misamaha au kwa tozo kilingana na mapato.
Haya shine wafanyakazi, tupambane tupate kilicho bora.
 
Wakuu nilikua napitia pitia sheria za kodi ya Mapato Tanzania na hasa kodi inayotozwa kwenye pato la mfanyakazi. Kwa ujumla kodi (PAYE) hii ni kubwa Mno kulinganishwa na kozi zinazotozwa biashara za ubia (partnership), binafsi (sole proprietorship), kampuni (Corporation). Nasema hii kwa sababu zifuatazo

1.0 Makampuni hutozwa kodi kwenye faida au kinachobaki baada ya kuchukua mauzo/mapato na kutoa matumizi yote. Kinachobaki kinatozwa kodi. Kama matumizi yatazidi mapato basi hamna kodi itakayotozwa hapo.

2.0 Wafanya biashara binafsi hutozwa kodi kwenye faida kama wanaweka rekodi vizuri au hukadiriwa kama hawaweki rekodi vizuri.

3.0 Mshahara kwa mfanyakazi ni sawa na mapato yaani sales. Lakini serikali badala ya kutoza kodi kwenye faida wanatoza kodi ya juu kwenye mapato moja kwa moja. Kama kampuni inatoa matumizi yanahusu biashara, kwa nini na mfanyakazi asiruhusiwe kutoa matumizi yanayohusiana na mshahara wake? Mfanyo Mfanyakazi anapokea Gross Salary ya TZS 1,000,000 kwa mwezi, hizi ni sawa na TZS 12,000,000 kwa mwaka. Kodi itatozwa kwenye 12,000,000 moja kwa moja na ni 30%. Lakini ingekua kampuni au mfanyabiashara angeruhusiwa kutoa matumizi yote yaliyomwezesha kupata hiyo 12M. Mfanyakazi analipa nauli au mafuta kwenda kazini, anajitibu ili kuhakikisha anakua na afya nzuri ya kufanya kazi, analipa kodi ya nyumba kwa usalama wake, ananunua nguo za kazini, yaani isingekua kazi asingenunua nguo hizo, inabidi ale diet ya ziada ili aweze kufanya kazi, umeme, maji. Hivi vyote havitolewi ili kupata kinachobaki kwaajili ya kutozwa kodi.

Je kwa hali hii tunaomba serikali itupunguzie mzigo wa kodi sisi wafanya kazi. Unakuta mtu unafanya kazi hauendelei hata siku moja lakini mfanyabiashara anaendelea sana. Hii ni kutokana na serekali kuwapunguzia mzigo wa kodi lakini sisi wafanyakazi unaumia kila mwezi kwa PAYE kubwa.

Jamani naomba tuchangie hii topic kwa hoja za nguvu kwa kuzingatia uzito wa swala hili.

Hapo tu (red colour) nimeishiwa nguvu. Hakuna watu wajinga, labda niseme wapumbavu kama wafanyakazi wa Tanzania. Wanaona kama mshahara wanaopata ni hisani kutoka kwa mwajiri kwa hiyo hawana sababu ya kuuliza lolote. Serikali inaweza kukata kodi yoyote anavyotaka na waajiri (ikiwemo serikali) wanaweza kuingiza makato yoyote wanavyopenda bila kupata idhini ya mfanyakazi. Mfano vyama vya wafanyakazi vinakomba hela nyingi sana kwenye mishahara ila sijui kama kazi yao ina tija yoyote.

Wafanyabiashara wako makini sana na ukicheza na wigo wa faida yao wako tayari kwa lolote. Wao hawaiombi serikali bali wanakaa nayo kukubaliana. Ila wafanyakazi wanaendelea kuomba kama hapo juu. Kwa mwendo huo hata Yesu ataikuta PAYE iko juu na bado itaendelea kuongezwa. Wajinga/mabwege ndio waliwao!
 
Achilia mbali ukubwa wa kodi bado ela unayokatwa haitumiki ipasavyo.
Ukienda hospital wakamuliwa,trafic nao zengwe on the road,police ndo usiseme wala hawajui kuwa kodi yangu inatumika kuwalipa mshahara na mengineyo mengi ambayo badala ya kutupunguzia ukali wa maisha inafanya maisha yawe magumu.
Kwa kweli inaoneka PAYE ndio uti wa mgongo wa TRA bse ata ukwepaji wake ni issue,mbaya zaidi uku kwetu mpaka allowance wanazilima kodi jamaniiiii.
 
Mramba ndo aliiongeza hiyo PAYE na akaintroduce hata ile ishu ya kukata kodi all the benefits. Inauma sana PAYE is so great. Wakati huo mbunge ambaye analipwa milion 7+ anakatwa kodi only kwenye 1.5mn. Hao hawawezi hata kutetea chochote.
Only solution ni kama tungekuwa na very strong labor union then wangeweza negotiate na hii serikali. On top of that kodi yenyewe hatuoni inafanya nini sana sana utakuta ni UFISADI in it. Ukifika hapo unachoka then unaconclude kwamba this is a stupid country ever.
 
Shapu,

Kama wewe ni mfanyakazi basi jina lako nimetoa hapo juu. Labour union za Tanzania hazifai na ndio maana inabidi kila mtu ahangaike kivyake vyake! Kuonesha wafanyakazi walivyo mabwege, angalia wahadhiri. Suala la pension wamelijua leo? Kwa vile wengi waliajiriwa kwa mkupuo kati ya 1980 na 1990, basi wakasahau kuwa siku moja watatakiwa kustaafu. Lilipokuja suala la serikali tutoajiri tena kwa utaratibu wa Tutorial assistants mwanzoni mwa miaka ya 90 wakaona ni poa tu. Pia hayo mambo ya pension hawakuona kuwa yanawahusu. Sasa wameanza kustaafu na kulipwa milioni 10 wakati mwalimu wa shule ya msingi anapata karibu milioni 50, ndio wanastuka na kukumbuka shuka wakati tayari kumekucha. Pia kwenye vyuo kama Muhimbili waliendekeza ujinga na kunyanyasa vijana ili wasiwasogelee (they thought youths were threat) sasa wanashangaa hawana walimu tena. Ningekuwa serikali ningeuchuna tu. Wafanyakazi wanavuna matunda ya ushenzi wao na hapatakiwi kuwa na mtu wa kuwahurumia!
 
Achilia mbali ukubwa wa kodi bado ela unayokatwa haitumiki ipasavyo.
Ukienda hospital wakamuliwa,trafic nao zengwe on the road,police ndo usiseme wala hawajui kuwa kodi yangu inatumika kuwalipa mshahara na mengineyo mengi ambayo badala ya kutupunguzia ukali wa maisha inafanya maisha yawe magumu.
Kwa kweli inaoneka PAYE ndio uti wa mgongo wa TRA bse ata ukwepaji wake ni issue,mbaya zaidi uku kwetu mpaka allowance wanazilima kodi jamaniiiii.

Kwa mwendo huu ningekuwa kamishina wa TRA ningebuni kodi ya watoto na wake au ndugu za wafanyakazi. Just to syphon them, kwa sababu mwisho wa siku wataniambia, "JAMANI TUHURUMIE"! Na hapo nasongea pembeni na glass ya ya champaign nachekelea kuwagida mabwege huku navuna 18m kwa mwezi!
 
Last edited:
..tusisahau huko nyuma tuliambiwa nchii ni ya wakulima na wafanyakazi, sasa kilimo kinachechemea na kubaki wafanyakazi kubeba mzigo wote. Pengine ndiyo kisa ha serikali kuwa na mkono ktk uundaji wa vyama vya wafanyakazi..
 
Hivi ni kwa nini masurufu hayakatwi kodi?? Kama mbunge anapata 7m na masurufu ni 5m (tax free)..is it fair? kumbuka pia mmbunge anapata 105,000 kaama posho kwa siku akiwepo Dodoma nje ya mshahara!

Hivi posho ni % ngapi ya budget ya serikali??
 
Enzi za chama kimoja, serikali kupitia kwa chama tawala ilikuwa na mkono katika kila kitu. Vyama vya wafanyakazi, majeshi yote ya ulinzi na usalama n.k n.k...

Hata hivyo baada ya mfumo wa vyma vingi kuanza Julai 1992, watu walizugwa kuwa matawi ya chama (CCM) makazini na majeshini yalifungwa. Ukweli ni kwamba bado Tz ni nchi ya kiduma chama cha mapinduzi hadi leo. Ndio maana nasema wafanyakazi wa Tz ni mabwege. Wanashindwa hata kuunganisha dots kwa vitu vidogo kama hivyo pamoja na kwamba wameenda shule.
 
Hivi ni kwa nini masurufu hayakatwi kodi?? Kama mbunge anapata 7m na masurufu ni 5m (tax free)..is it fair? kumbuka pia mmbunge anapata 105,000 kaama posho kwa siku akiwepo Dodoma nje ya mshahara!

Hivi posho ni % ngapi ya budget ya serikali??

Ukipata hilo jibu ndipo utakapojua kwa nini serikali iliamua kuzuga wafanyakazi kuwa marupurupu yao yameunganishwa ni mishahara wakati yale ya wabunge na wakubwa wengine yanabaki pembeni! Wafanyakazi walalage tu!
 
Hata hivyo baada ya mfumo wa vyma vingi kuanza Julai 1992 said:
... kwa mantiki nyingine ukombozi wa wafanyakazi uko mbali kwani waliounda trade unions walikuwa na malengo yao ambayo yanatimia. Nadhani ukombozi wa kweli utakuja baada ya kuvikana vilivyopo vilivyo undwa kwa wenyenavyo kusema .. naviwe vyama vya wafanyakazi, .. nakiwe chama cha waalimu nk na kuunda vya kwao kwa matakwa yao/yetu.
 
Tujenge hoja yenye kueleweka.
Ni kweli nakubaliana na nyie PAYE ni kubwa nini chanzo mbadala km kodi ikipunguzwa? Nchi nyingine wanakata asilimia ngapi? Hiyo PAYE ni asilimia ngapi ya kodi yoote ya serikali?
 
Mramba ndo aliiongeza hiyo PAYE na akaintroduce hata ile ishu ya kukata kodi all the benefits. Inauma sana PAYE is so great. Wakati huo mbunge ambaye analipwa milion 7+ anakatwa kodi only kwenye 1.5mn. Hao hawawezi hata kutetea chochote.
Only solution ni kama tungekuwa na very strong labor union then wangeweza negotiate na hii serikali. On top of that kodi yenyewe hatuoni inafanya nini sana sana utakuta ni UFISADI in it. Ukifika hapo unachoka then unaconclude kwamba this is a stupid country ever.

Hakuna watu wabinafsi kama wabunge wetu. Hata siku moja hawatatetea kodi ya wafanyakazi kushuka maana wao tukikatwa nyingi ndipo wanapopatia point za kutaka waongezewe mishahara. Ni ubinafsi uliokithiri!
 
Hizi double taxation ni balaa, maraisi watakaofuata watarithi mambo ya ajabu sana.
Naona Kenya wanatoza 16% kwenye VAT. Hapa kwetu tunatozwa 21% kwenye nishati. I can't wait to leave the "employee" arena.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom