Pay As You Earn (PAYE): Wafanyakazi mna maoni gani?

Nov 11, 2008
782
38
Juzi juzi wakati nikitafakari sherehe za mei mosi niliingia kwenye kabati yangu nikaanza KUPERUZI salary slips zangu nikiangalia namna ninavyotendewa na hao wanaojiita waajiri. Kitu kimoja nilichokigundua ni kuwa wafanyakazi tunalipa sana KODI kuliko mtu yeyeto Duniani.

Tunalipa indirect tax sawa sawa na watu wengine wote wanaopata huduma na bidhaa tofauti tofauti.

Tofauti na wafanyabiashara wanaolipa kodi kwenye faida, yaani NET PROFIT sisi tunachanjwa P.A.Y.E kwenye gross salary.

TATIZO LANGU HAPA ni kuwa hii PAYE ni kubwa sana kwanini badala ya kupigana eti tuongezwe mishahara huku tukijua na mzigo wa kodi utaongezeka kadiri mishahara inavyoongezeka tusijipange kwa pamoja tupiganie PAYE ipungue?

Najua serikali wanaipenda sana kwani inakusanywa kirahisi sana na garama POA kabisa, kama kweli JK wenu anataka Maisha bora kwa kila mtanganyika basi PAYE ipungue na kodi za kufidia zitafutwe mahali pengine kama kupunguza misamaha ya kodi, kupunguza matumizi MAKUBWA ya serikali, na Kuwa makini na wafuatiliaji wa maliasili zetu kama samaki na madini?

Vyama vya wafanyakazi mko wapi? hivi huwa mnachaguliwa kwakuwa mna CV zenu au uwezo wenu wa kuhamasisha migomo?

NAWASILISHA.

==========
KWA UNDANI:

Kuelewa dhana ya Kodi inayotokana na Ajira (Pay As You Earn)

Kodi inayotokana na Ajira inajulikana kama Lipa kadiri unavyopata (PAYE). Hii ni kodi ya zuio kwa waajiriwa wanaotozwa kodi. Chini ya mfumo huu, mwajiri anapaswa kisheria kukata kodi ya mapato kutoka katika mshahara au ujira wa mwajiriwa anayestahili kutozwa kodi. Sehemu ya 81 ya Sheria ya Kodi ya Mapato inamtaka mwajiri kukatalia kodi kutoka kwa malipo yaliyolipwa mfanyakazi. Mwajiri anahitajika na Sehemu ya 84 (1) kulipia kodi iliyozuia kwa TRA kati ya siku saba baada ya mwisho wa kila mwezi wa kalenda.

Screenshot 2019-12-27 at 10.14.33.png

Maana ya Mwajiriwa:

Mwajiriwa ni mtu anayehusika na ajira inayoendeshwa na mwajiri. Ajira inahusisha waajiriwa wa kudumu, waajiriwa wa muda, meneja, Mkurugenzi, na vibarua. Waajiriwa wanaweza kuajiriwa na mwajiri mmoja au zaidi (ajira ya msingi na ya ziada)

Maana ya mwajiri:

Mwajiri ni mtu anayeendesha, aliyeendesha au ana lengo la kuendesha ajira kwa watu.

Mkurugenzi wa ajira ya kudumu:

Maana yake ni mwajiriwa wa kudumu katika shirika anayefanya kazi ya kiutawala.

Usimamizi wa Kodi ya Mshahara

Mwajiri anapaswa kuzuia kodi ya mapato kutoka katika mishahara, ujira na malipo mengine yote yanayopaswa kukatwa kodi kutoka kwa waajiriwa.

==========

SASA: (Updated based on 2017 information available)

Kiwango cha kodi, ambacho mtu anatakiwa kukatwa kwa mujibu wa sheria ya kodi ya mapato, vinatofautiana kutoka mtu mmoja hadi mwingine, kulingana na kiwango cha kipato anachopata mtu kwa mwezi.

Kodi ya ajira, ambayo mwajiriwa anakatwa kwenye mapato au mafao yake, kiwango cha mshahara au kipato au ujira, kinachotakiwa kukatwa kodi ni kile kinachozidi Sh 170,000 kwa mwezi.

Kwa mujibu wa TRA, kwenye ajira kuna vyanzo tofauti tofauti vya mapato kwa mwajiriwa, kama vile motisha (bonus), kamisheni, ujira, mshahara, malipo ya likizo, posho na mengineyo, ambayo yote yakijumlishwa yanatengeneza kipato cha mwezi, hivyo kipato hicho kama hakizidi Sh 170,000 hakikatwi kodi.

Kipato cha Shilingi 170,000 kushuka chini hakina kodi, kimesamehewa kwa mujibu wa sheria ya kodi ya mapato Kifungu namba 10 ukisoma pamoja na jedwali la pili la kodi ya mapato ambalo linaonesha viwango vilivyosamehewa kodi kuwa ni pamoja na hiki cha Sh 170,000 kushuka chini.

Kwa mujibu wa TRA, kiwango kinachozidi Sh 170,000 lakini hakizidi Sh 360,000 kwa mwezi, kodi yake ni asilimia tisa (9%). Kwa mfano mtu analipwa Sh 360,000 au 240,000, kinachofanyika ni kwamba inatolewa Sh 170,000 kwenye kipato hicho na kiasi kinachobaki ndiyo kinakatwa kodi ya asilimia tisa.

TRA inasema kuwa kwa mwajiriwa anayepata kipato kinachozidi Sh 360,000 lakini hakizidi Sh 540,000 kwa mwezi, kodi yake ni Sh 17,100, lakini inajumlishwa na asilimia 20 ya kodi kwa kipato kinachozidi Sh 360,000.

Vivyo hivyo kwa kipato kinachozidi Sh 540,000 lakini hakizidi Sh 720,000 kwa mwezi, kodi yake ni Sh 53,100, lakini itaongezwa na asilimia 25 ya kiwango kinachozidi Sh 540,000.

Kiwango chochote cha kipato cha kuanzia Sh 720,000 kwenda juu kwa mwezi, kodi yake ni Sh 98,100, lakini inajumlishwa na asilimia 30 ya kiwango kinachozidi Sh 720,000, hivyo kodi kwa mtu binafsi hata kama analipwa Sh milioni 20 au zaidi, anakatwa kodi kwa utaratibu huu.

Kiwango hicho cha kodi cha asilimia 30 kwa mujibu wa sheria za kodi ya mapato, ndiyo kiwango cha juu zaidi kuliko kiwango kingine chochote. Kwenye kodi kuna viwango vya asilimia tano, asilimia 10, asilimia 15, asilimia 20, asilimia 25 na asilimia 30 ambacho ndiyo kiwango cha mwisho kwenye kodi ya mapato.

Mfumo wa kodi ya ajira, unamtaka mwajiriwa alipe kodi kadri anavyopata kipato (PAYE). Mwajiriwa anayepata kipato kidogo, pia analipa kodi kidogo na anayepata kipato kikubwa na kodi pia huwa kubwa.

Punguzo la kodi kwa mujibu wa TRA, Serikali kila mara imekuwa ikirejea viwango vya kodi na kuendelea kuvipunguza ili kuongeza watu wengi zaidi kwenye wigo wa kodi.

Viwango vya kodi vinapokuwa juu sana, vinawafanya watu kukwepa kodi na ndiyo maana Serikali huvirejea viwango hivyo kila mara. Kwa zamani asilimia ya kodi ya ajira ilikuwa kubwa, kwa kuwa ilianzia asilimia 17 baadaye ikashushwa hadi asilimia 15, ikashushwa tena hadi asilimia 14, baadaye asilimia 12 na 11, na sasa ni asilimia tisa.

Matokeo ya punguzo la asilimia tisa la kodi ya ajira, alilolitoa Rais John Magufuli, linaonekana zaidi kwa watu wenye kipato cha chini, tofauti na wenye kipato kikubwa ambao kwa wengi bado kodi hii ni kubwa sana.

======
Baadhi ya mijadala:

2013: Punguzo la PAYE kwa asilimia 1 ni dhihaka kwa wafanyakazi!

2019: Rais Magufuli atashinda kwa kishindo 2020 ( 99.9) endapo ataigusa kodi ya Pay As You Earn ( PAYE) kwa wafanyakazi wa kada za chini!
 
Ndugu yangu Kandambili your observation is quite right!

Employees wanalipa kodi kubwa sana kulinganisha na makundi mengine ya kijamii relative to their income.

Ukifanikiwa kuwa mjasiliamali na business yako ikatake off vizuri, ukaiendesha informally, unauwezekano wakulipa kodi ndogo sana kuliko ukiwa umeajiriwa!

Ngoja nitoe mfano mmoja hapa;

Nimemwajiri mtu X kwa ajili ya kutoa huduma fulani kwenye yangu na namlipa kwa mwezi Tshs 400,000/= (Gross income), mwajiriwa huyu nitamkata kwa kila mwezi Tshs 54,500 kama PAYE so kwa mwaka atakatwa Tsh 654,000!

Scenerio ya pili, sitaki kuajiri na mcontract mjasiriamali Y awe ananifanyia kazi ambayo X angeifanya, tunakubaliana niwe namlipa labda baada ya miezi sita Tshs 2,400,000 so kwa mwaka Tshs 4,800,000 kama fees excluding disbursements. Huyu mambo ya kodi anatakiwa kuhandle mwenyewe, so labda ataenda kukata TIN na kujisajili kama mfanyabiashara mdogo.

Kwa kuwa mapato /mauzo yake hayazidi Tshs 7,000,000 kwa mwaka....anatakiwa alipe Tshs 95,000 tu kwa mwaka kama kodi

Now linganisha Tshs 654,000 PAYE anayolipa mwajiriwa na Tshs 95,000 kwa mapato sawa utaona jinsi waajiriwa wanavyoumizwa.

Mfano mwingine; niko na jamaa zangu pale k/koo wanafanya biashara mbalimbali na wanamiliki majengo kadhaa pale.....mauzo yao kwa mwaka ni kati ya Tshs 100,000,000 to 1,000,000,000! Lakini kodi wanayolipa.....utashangaa kweli, hata Tshs 500,000 kwa mwaka haifiki na hii wanakadiriwa na TRA. Wakati mfanyakazi anayepata say Gross ya 5,000,000 kwa mwezi, tayari analipa zaidi ya 1 mil kama kodi kila mwezi!

So ukiwa kwenye informal sector kodi unalipa kidogo sana relative to your income compared to employees!

TRA na serikali wanatakiwa kupanua wigo wa kodi (tax base) ili kuyanusuru maisha ya wafanyakazi waliobebeshwa mzigo wa kodi kama punda! Waache uvivu wa kufikiria vyanzo vingine vya kodi kama vile Kodi za pango (rental taxes), waongeze kodi kule kwenye informal sector, including income inayopotea kule kny masherehe, madalali, MCs, Usafirishaji etc na pia kupunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima kwa serikali!

Vinginevyo wote tutahamia huko kwenye informal sector, kwenye unafuu mkubwa sana wa kodi!
 
Kandambili kama ulivyosema PAYE ni rahisi kuikata, sasa unategemea kuwa itapunguzwa kweli. Na MAFISADI wataishije kodi ikipunguzwa??

Kinachotakiwa ni kutafuta mbinu za kuhakikisha kuwa kodi (PAYE) tunayolipa inatumika kausahihi. Kwanza unatakiwa kujua kuwa wafanyakazi wa kwenye private Sector ndio wanaolipa PAYE kubwa zaidi ya wale wa kwenye Public Sector.
 
Kwamba natakiwa kujua kuwa wafanyakazi wa kwenye private Sector ndio wanaolipa PAYE kubwa zaidi ya wale wa kwenye Public Sector!!!!!?????????? HIYO NAKATAAA KABISAAAAA (may be unipe mifano halisi na sio ya hear say) tena kwenye private wana malipo fulani fulani ambayo ni tax free kuna namna wanavyocheza nayo kwani wanajua kama mimi nataka NET 100,000 that means kama ni kodi wanatakiwa waiongeze na inakula kwao.

Tukiacha USHABIKI wa MAFISADI inaweza kupunguza kama hoja zikijengwa sawa sawa na public (wafanyakazi) ikaonyesha concern yake, mbona huwa inarekebishwa mathalani iliwahi kuchange kati ya minimum ya 18% na 15%
 
Kandambili hapa naona hujafanya utafiti vyakutosha, the Farmer yuko sahihi kabisa kwamba ukilinganisha wafanyakazi wa Private Sector na Public Sector wale wa Private sector wanalipa zaidi kuliko wa Public Sector kwa sababu zifuatazo;

1. Wafanyakazi wa Public sector wanaexemption nyingi zaidi kuliko wenzao wa private sector e.g benefit ya nyumba private workers ni taxable wakati huko public iko exempted, public workers wakiagiza magari wanaweza kupewa exemption wakati wale wa private sector hakuna kitu hicho.

2. Tax compliance huko public sector ni ndogo sana ukilinganisah na private sector kwa sababu TRA huwa hawana mkazi na hawafuatilii sana huko Public sector kama wafanyavyo private sector so utaona benefits nyingi sana haziwi taxed kabisa huko public wakati private sector every single coin anayopata employee iko taxed na TRA wanafanya audit za mara kwa mara kuhakikisha waajiri wanacomply

3. Mishahara ya public sector (Basic) iko chini sana na ukizingatia threshhold kwa sasa ni 100,000, unakuta mtu basic yake ni 150,000 which means anatakiwa akatwe kodi kwenye 50,000! But in reality unakuta kwa mwezi mtu huyu anatoka na like 1, 2,3mil kama gross income from sitting allowance, acting allowance, extra duty allowance, honorarioum, perdiem etc ambazo they don't tax kabisa! So wanaendup kuienjoy income kubwa but pay less tax, kumbe private mishahara ni mikubwa but hakuna eti malipo ya sitting allowance, acting sijui nini......! so mara nyingi utakuta gross income = basic income......maanake hakuna income inayokwepa machine ya PAYE.

Ofcourse kuna exceptions pia kwa wale wakwepaji kodi huko private sector ambao huandaa payroll mbili, moja iko na PAYE na nyingine haina..so hawa wanalipa kodi kidogo!

Kwa ujumla wafanyakazi wa private sector wanalipa kodi kubwa kuliko wale wa Public sector kama nilivyoeleza hapao juu!
 
Ndugu yangu Kandambili your observation is quite right!

Employees wanalipa kodi kubwa sana kulinganisha na makundi mengine ya kijamii relative to their income.

Ukifanikiwa kuwa mjasiliamali na business yako ikatake off vizuri, ukaiendesha informally, unauwezekano wakulipa kodi ndogo sana kuliko ukiwa umeajiriwa!

Ngoja nitoe mfano mmoja hapa;

Nimemwajiri mtu X kwa ajili ya kutoa huduma fulani kwenye yangu na namlipa kwa mwezi Tshs 400,000/= (Gross income), mwajiriwa huyu nitamkata kwa kila mwezi Tshs 54,500 kama PAYE so kwa mwaka atakatwa Tsh 654,000!

Scenerio ya pili, sitaki kuajiri na mcontract mjasiriamali Y awe ananifanyia kazi ambayo X angeifanya, tunakubaliana niwe namlipa labda baada ya miezi sita Tshs 2,400,000 so kwa mwaka Tshs 4,800,000 kama fees excluding disbursements. Huyu mambo ya kodi anatakiwa kuhandle mwenyewe, so labda ataenda kukata TIN na kujisajili kama mfanyabiashara mdogo.

Kwa kuwa mapato /mauzo yake hayazidi Tshs 7,000,000 kwa mwaka....anatakiwa alipe Tshs 95,000 tu kwa mwaka kama kodi

Now linganisha Tshs 654,000 PAYE anayolipa mwajiriwa na Tshs 95,000 kwa mapato sawa utaona jinsi waajiriwa wanavyoumizwa.

Mfano mwingine; niko na jamaa zangu pale k/koo wanafanya biashara mbalimbali na wanamiliki majengo kadhaa pale.....mauzo yao kwa mwaka ni kati ya Tshs 100,000,000 to 1,000,000,000! Lakini kodi wanayolipa.....utashangaa kweli, hata Tshs 500,000 kwa mwaka haifiki na hii wanakadiriwa na TRA. Wakati mfanyakazi anayepata say Gross ya 5,000,000 kwa mwezi, tayari analipa zaidi ya 1 mil kama kodi kila mwezi!

So ukiwa kwenye informal sector kodi unalipa kidogo sana relative to your income compared to employees!

TRA na serikali wanatakiwa kupanua wigo wa kodi (tax base) ili kuyanusuru maisha ya wafanyakazi waliobebeshwa mzigo wa kodi kama punda! Waache uvivu wa kufikiria vyanzo vingine vya kodi kama vile Kodi za pango (rental taxes), waongeze kodi kule kwenye informal sector, including income inayopotea kule kny masherehe, madalali, MCs, Usafirishaji etc na pia kupunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima kwa serikali!

Vinginevyo wote tutahamia huko kwenye informal sector, kwenye unafuu mkubwa sana wa kodi!

Comprehensive analysis, jamani tuamke vita vya mafisadi viende sambasamba na kupigania haki zetu sio kila siku wanaongeza ongeza kodi kwenye mafuta, BIA wakati kuna sehemu kubwa tu wanaweza kupata kodi na kutunusuru na MZIGO HUU....
 
Kandambili hapa naona hujafanya utafiti vyakutosha, the Farmer yuko sahihi kabisa kwamba ukilinganisha wafanyakazi wa Private Sector na Public Sector wale wa Private sector wanalipa zaidi kuliko wa Public Sector kwa sababu zifuatazo;

1. Wafanyakazi wa Public sector wanaexemption nyingi zaidi kuliko wenzao wa private sector e.g benefit ya nyumba private workers ni taxable wakati huko public iko exempted, public workers wakiagiza magari wanaweza kupewa exemption wakati wale wa private sector hakuna kitu hicho.

Kwa taarifa yako HOUSE ALLOWANCE inakatiwa kodi in short ANY INCOME DERIVED FROM EMPLOYMENT IS TAXABLE, soma Income tax ACT utaelewa vizuri, kwenye magari naweza kukubaliana na wewe lakini jiulize pia hiyo incentive inawanufaisha wangapi na wenye kipato gani kuweza kununua gari? umefanya mchanganuo ujue huo msamaha una unafuu kiasi gani, najua VAT haipo kwenye msamaha.....

2. Tax compliance huko public sector ni ndogo sana ukilinganisah na private sector kwa sababu TRA huwa hawana mkazi na hawafuatilii sana huko Public sector kama wafanyavyo private sector so utaona benefits nyingi sana haziwi taxed kabisa huko public wakati private sector every single coin anayopata employee iko taxed na TRA wanafanya audit za mara kwa mara kuhakikisha waajiri wanacomply

Kwa taarifa yako siku hizi wanafanya Audit mpaka kwenye Public Sectors.....

3. Mishahara ya public sector (Basic) iko chini sana na ukizingatia threshhold kwa sasa ni 100,000, unakuta mtu basic yake ni 150,000 which means anatakiwa akatwe kodi kwenye 50,000! But in reality unakuta kwa mwezi mtu huyu anatoka na like 1, 2,3mil kama gross income from sitting allowance, acting allowance, extra duty allowance, honorarioum, perdiem etc ambazo they don't tax kabisa! So wanaendup kuienjoy income kubwa but pay less tax, kumbe private mishahara ni mikubwa but hakuna eti malipo ya sitting allowance, acting sijui nini......! so mara nyingi utakuta gross income = basic income......maanake hakuna income inayokwepa machine ya PAYE.

Hizo allowance zote ulizozitaja hapo ni TAXABLE

Ofcourse kuna exceptions pia kwa wale wakwepaji kodi huko private sector ambao huandaa payroll mbili, moja iko na PAYE na nyingine haina..so hawa wanalipa kodi kidogo!

nakubaliana na wewe 100%

Kwa ujumla wafanyakazi wa private sector wanalipa kodi kubwa kuliko wale wa Public sector kama nilivyoeleza hapao juu!

Nusu ya LIFE yangu kwenye AJIRA nimeitumia kwenye PRIVATE na PUBLIC nimeyaona mengi.............
 
Hoja ni ya kweli kabisa wala haihitaji kupepewa. Miaka yote kwa taarifa yenu PAYE ndio inayoongoza kwa kuliingizia Taifa mapato. That said inamaanisha nchi hii inaendeshwa na masikini ambao ni wafanyakazi. So hata hao mafisadi wanaowaibia ni wafanyakazi kwani wote tunajuwa namna ambavyo wafanyabiashara wakubwa wanavyoevade tax. So hii vita ya ufisadi haipaswi kuwekwa chini kwani itakuwa sawa na kujaza maji ndoo iliyotoboka. Ila pia of course tupigane hiyo PAYE ipunguzwe ni kubwa mno. Ninazo data ya rates za nchi ingine chache, yetu kama ilivyo VAT iko juu sana.
 
Kwamba natakiwa kujua kuwa wafanyakazi wa kwenye private Sector ndio wanaolipa PAYE kubwa zaidi ya wale wa kwenye Public Sector!!!!!?????????? HIYO NAKATAAA KABISAAAAA (may be unipe mifano halisi na sio ya hear say) tena kwenye private wana malipo fulani fulani ambayo ni tax free kuna namna wanavyocheza nayo kwani wanajua kama mimi nataka NET 100,000 that means kama ni kodi wanatakiwa waiongeze na inakula kwao.

Tukiacha USHABIKI wa MAFISADI inaweza kupunguza kama hoja zikijengwa sawa sawa na public (wafanyakazi) ikaonyesha concern yake, mbona huwa inarekebishwa mathalani iliwahi kuchange kati ya minimum ya 18% na 15%

Inawezekana sijakupata vyema, lakini sijaelewa concept ya '..malipo fulani ambayo ni tax free...' una maanisha nini. Ninavyoelewa mimi the tax bracket is the same which is guided by the Income Tax Act. Kwa hiyo kama kuna kitu ni tax free, kita-cut across kwa mtu yeyote anayeangukia kwenye bracket husika. Suala la mtu kuwa na mategemeo ya 'net' ya kiasi fulani, hapa sasa ni utundu wa mwajiriwa ambaye katike negotiation zake za kuingia kwenye ajira fulani, atakuwa ana mategemeo/matarajio yake. Mfano, yeye ataona kuwa ili hii kazi iweze kuwa na manufaa kwangu, basi nitataka mwajiri anipatie mshahara baada ya kodi (the so called net) wa shs 100,000. So it's up to the employee, to work out the gross salary ya huyo muomba kazi kuona kama itakuwa costfull kwake or not! Hapa ninakupa mbinu na wewe ndugu yangu, never negotiate a salary on gross figures, zitakuumiza mwenyewe. Cos, utashawishika na li-figure la ajabu, kumbe mwisho wa siku what goes into your pocket (the net) is peanut!

I support kuwa people from the private sector makato yao ya kodi yako juu sana, cos, as the the Income Tax Act, malipo yoyote anayolipwa mfanyakazi they are subjected to tax, whether in benefit or in kind. Mfanyakazi huyu atasalimika pale atakapolipwa per diem ambayo ndiyo itapita nje ya mshahara wake (payroll). Kama ana salary arrear yoyote, itapita kwenye payroll, and the amount will be taxed accordingly! Hii nimeiona ni tofauti kidogo kwenye public sector, ambako mtu ataishia kuwa taxed only on the BASIC SALARY, which I still have not recovered from the shock of realising that. Kwa hiyo hata akiingiziwa arrear, the line that will be taxed itakuwa ile ya basic salary tu. Marupurupu mengine kama subsistence allowance na wajukuu zake, yote yatapita on a separate voucher and they will get away from the tax!

All in all, siamini kama serikali itafikiria kupunguza PAYE, kwa sababu urahisi wake wa kuikusanya naona una mteremko kwao, so letting such 'easy' income slip away from their fingers...mmh yataka moyo. Labda kama alivyotoa maoni mchangiaji mwingine, kuwa tuanze kufikiria kuhamia kwenye 'informal sector' ndio salama yetu.
 
Ndugu yangu Kandambili your observation is quite right!

Employees wanalipa kodi kubwa sana kulinganisha na makundi mengine ya kijamii relative to their income.

Ukifanikiwa kuwa mjasiliamali na business yako ikatake off vizuri, ukaiendesha informally, unauwezekano wakulipa kodi ndogo sana kuliko ukiwa umeajiriwa!

Ngoja nitoe mfano mmoja hapa;

Nimemwajiri mtu X kwa ajili ya kutoa huduma fulani kwenye yangu na namlipa kwa mwezi Tshs 400,000/= (Gross income), mwajiriwa huyu nitamkata kwa kila mwezi Tshs 54,500 kama PAYE so kwa mwaka atakatwa Tsh 654,000!

Scenerio ya pili, sitaki kuajiri na mcontract mjasiriamali Y awe ananifanyia kazi ambayo X angeifanya, tunakubaliana niwe namlipa labda baada ya miezi sita Tshs 2,400,000 so kwa mwaka Tshs 4,800,000 kama fees excluding disbursements. Huyu mambo ya kodi anatakiwa kuhandle mwenyewe, so labda ataenda kukata TIN na kujisajili kama mfanyabiashara mdogo.

Kwa kuwa mapato /mauzo yake hayazidi Tshs 7,000,000 kwa mwaka....anatakiwa alipe Tshs 95,000 tu kwa mwaka kama kodi

Now linganisha Tshs 654,000 PAYE anayolipa mwajiriwa na Tshs 95,000 kwa mapato sawa utaona jinsi waajiriwa wanavyoumizwa.

Mfano mwingine; niko na jamaa zangu pale k/koo wanafanya biashara mbalimbali na wanamiliki majengo kadhaa pale.....mauzo yao kwa mwaka ni kati ya Tshs 100,000,000 to 1,000,000,000! Lakini kodi wanayolipa.....utashangaa kweli, hata Tshs 500,000 kwa mwaka haifiki na hii wanakadiriwa na TRA. Wakati mfanyakazi anayepata say Gross ya 5,000,000 kwa mwezi, tayari analipa zaidi ya 1 mil kama kodi kila mwezi!

So ukiwa kwenye informal sector kodi unalipa kidogo sana relative to your income compared to employees!

TRA na serikali wanatakiwa kupanua wigo wa kodi (tax base) ili kuyanusuru maisha ya wafanyakazi waliobebeshwa mzigo wa kodi kama punda! Waache uvivu wa kufikiria vyanzo vingine vya kodi kama vile Kodi za pango (rental taxes), waongeze kodi kule kwenye informal sector, including income inayopotea kule kny masherehe, madalali, MCs, Usafirishaji etc na pia kupunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima kwa serikali!

Vinginevyo wote tutahamia huko kwenye informal sector, kwenye unafuu mkubwa sana wa kodi!

That was a VERY VERY GOOD Analysis. Ni kweli kabisa PAYE wanaolipa wafanyakazi be it public or private ni kubwa SANA. And this was introduced during Mramba time as finance minister. It is very true kwamba inabidi tuangalie jinsi tunaweza kupambana PAYE ipungue. Yaani when you look at the tax we pay in your salary slip hailingani na kodi wanayolipa wafanya biashara.

Lakini nchi yetu iko so much influenced by bness men in terms of politics etc etc. So inaweza kuwa vigumu kupata support ya kutosha katika kuipunguza PAYE kwani ina athiri kundi ambalo si active sana katika kuinfluence decision of the BIG BOSS.

However any thing is possible, hata mleta mada hapa amejitahiti kwani tukianza kwa kulijadili na kujua ni tatizo is also a very good start.
 
Ndugu yangu Kandambili your observation is quite right!

Employees wanalipa kodi kubwa sana kulinganisha na makundi mengine ya kijamii relative to their income.

Ukifanikiwa kuwa mjasiliamali na business yako ikatake off vizuri, ukaiendesha informally, unauwezekano wakulipa kodi ndogo sana kuliko ukiwa umeajiriwa!

Ngoja nitoe mfano mmoja hapa;

Nimemwajiri mtu X kwa ajili ya kutoa huduma fulani kwenye yangu na namlipa kwa mwezi Tshs 400,000/= (Gross income), mwajiriwa huyu nitamkata kwa kila mwezi Tshs 54,500 kama PAYE so kwa mwaka atakatwa Tsh 654,000!

Scenerio ya pili, sitaki kuajiri na mcontract mjasiriamali Y awe ananifanyia kazi ambayo X angeifanya, tunakubaliana niwe namlipa labda baada ya miezi sita Tshs 2,400,000 so kwa mwaka Tshs 4,800,000 kama fees excluding disbursements. Huyu mambo ya kodi anatakiwa kuhandle mwenyewe, so labda ataenda kukata TIN na kujisajili kama mfanyabiashara mdogo.

Kwa kuwa mapato /mauzo yake hayazidi Tshs 7,000,000 kwa mwaka....anatakiwa alipe Tshs 95,000 tu kwa mwaka kama kodi

Now linganisha Tshs 654,000 PAYE anayolipa mwajiriwa na Tshs 95,000

Mfano mwingine; niko na jamaa zangu pale k/koo wanafanya biashara mbalimbali na wanamiliki majengo kadhaa pale.....mauzo yao kwa mwaka ni kati ya Tshs 100,000,000 to 1,000,000,000! Lakini kodi wanayolipa.....utashangaa kweli, hata Tshs 500,000 kwa mwaka haifiki na hii wanakadiriwa na TRA. Wakati mfanyakazi anayepata say Gross ya 5,000,000 kwa mwezi, tayari analipa zaidi ya 1 mil kama kodi kila mwezi!

So ukiwa kwenye informal sector kodi unalipa kidogo sana relative to your income compared to employees!

TRA na serikali wanatakiwa kupanua wigo wa kodi (tax base) ili kuyanusuru maisha ya wafanyakazi waliobebeshwa mzigo wa kodi kama punda! Waache uvivu wa kufikiria vyanzo vingine vya kodi kama vile Kodi za pango (rental taxes), waongeze kodi kule kwenye informal sector, including income inayopotea kule kny masherehe, madalali, MCs, Usafirishaji etc na pia kupunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima kwa serikali!

Vinginevyo wote tutahamia huko kwenye informal sector, kwenye unafuu mkubwa sana wa kodi!
So what does this tell us (employees)?
PAYEE itaendelea kuwepo maana wengi wataendelea kung'ang'ania kubaki kwenye comfort zone (being employed) - risk free area.

If you can't change others or the system....
...maybe you should start think about changing you!

Any government will favor those who create jobs for themselves or others.
 
Last edited:
Inawezekana sijakupata vyema, lakini sijaelewa concept ya '..malipo fulani ambayo ni tax free...' una maanisha nini. Ninavyoelewa mimi the tax bracket is the same which is guided by the Income Tax Act. Kwa hiyo kama kuna kitu ni tax free, kita-cut across kwa mtu yeyote anayeangukia kwenye bracket husika. Suala la mtu kuwa na mategemeo ya 'net' ya kiasi fulani, hapa sasa ni utundu wa mwajiriwa ambaye katike negotiation zake za kuingia kwenye ajira fulani, atakuwa ana mategemeo/matarajio yake. Mfano, yeye ataona kuwa ili hii kazi iweze kuwa na manufaa kwangu, basi nitataka mwajiri anipatie mshahara baada ya kodi (the so called net) wa shs 100,000. So it's up to the employee, to work out the gross salary ya huyo muomba kazi kuona kama itakuwa costfull kwake or not! Hapa ninakupa mbinu na wewe ndugu yangu, never negotiate a salary on gross figures, zitakuumiza mwenyewe. Cos, utashawishika na li-figure la ajabu, kumbe mwisho wa siku what goes into your pocket (the net) is peanut!

I support kuwa people from the private sector makato yao ya kodi yako juu sana, cos, as the the Income Tax Act, malipo yoyote anayolipwa mfanyakazi they are subjected to tax, whether in benefit or in kind. Mfanyakazi huyu atasalimika pale atakapolipwa per diem ambayo ndiyo itapita nje ya mshahara wake (payroll). Kama ana salary arrear yoyote, itapita kwenye payroll, and the amount will be taxed accordingly! Hii nimeiona ni tofauti kidogo kwenye public sector, ambako mtu ataishia kuwa taxed only on the BASIC SALARY, which I still have not recovered from the shock of realising that. Kwa hiyo hata akiingiziwa arrear, the line that will be taxed itakuwa ile ya basic salary tu. Marupurupu mengine kama subsistence allowance na wajukuu zake, yote yatapita on a separate voucher and they will get away from the tax!

All in all, siamini kama serikali itafikiria kupunguza PAYE, kwa sababu urahisi wake wa kuikusanya naona una mteremko kwao, so letting such 'easy' income slip away from their fingers...mmh yataka moyo. Labda kama alivyotoa maoni mchangiaji mwingine, kuwa tuanze kufikiria kuhamia kwenye 'informal sector' ndio salama yetu.

Inawezekana nimetumia neno TAX FREE vibaya lakini maana yangu ilkuwa ni some personal emoluments ambazo haziko mkwenye payroll, allowance hizo zote kwenye public sector zinatakiwa zikate kodi kama huko unakorefer hawakatwi siku KITILYA akiwatembelea WATAJIJU, mimi naamini hili likipigiwa kelele SANA watafungua masikio yao na kuliona, naamini hata hao watunga KODI ni VICTIM wa P.A.Y.E
 
Kimsingi kuna hoja hapa...But iam afraid if SUALA la kupunguza PAYE litaweza

kukubalika kirahisi na mamlaka. Viwanda vingi ambavyo vingesaidia serikali

kwa mapato ni vya wahindi, na hawa jamaa ni wataalam wa kukwepa kodi.

Wafanyabiashara wengi, kama ambavyo unaona huko madukani, wanakuuliza

kama unataka risiti ya kodi, ama la, na kisha bei za bidhaa hiyo..!!!

Sasa, katika hali kama hiyo tegemea kuwa huenda PAYE ikapanda zaidi ya

hapo, maana mfanyakazi tayari upo kwenye 18 zao!!.

Nasupport initiative zote zinazoweza kufanywa na vyama vya wafanyakazi na

pressure groups zinginezo, na kimsingi, mii ni mmoja kati ya wapenda

mabadiliko hayo

Lets join hands people!!
 
Muhimu kufanya study ya tax system yetu nakujua wapi zinaweza kupatikana fedha za kufidia hilo punguzo, tunaweza kupigania HAKI hii kwa kuangalia, kushauri na kutoa mapendekezo ni wapi kodi inapotea au haikusanywi vizuri.
Unajua mimi huwa nadhani ni bora kukosoa huku ukitoa suggested solution ndio inajenga zaidi...........
 
Kandambili hapa naona hujafanya utafiti vyakutosha, the Farmer yuko sahihi kabisa kwamba ukilinganisha wafanyakazi wa Private Sector na Public Sector wale wa Private sector wanalipa zaidi kuliko wa Public Sector kwa sababu zifuatazo;

1. Wafanyakazi wa Public sector wanaexemption nyingi zaidi kuliko wenzao wa private sector e.g benefit ya nyumba private workers ni taxable wakati huko public iko exempted, public workers wakiagiza magari wanaweza kupewa exemption wakati wale wa private sector hakuna kitu hicho.

2. Tax compliance huko public sector ni ndogo sana ukilinganisah na private sector kwa sababu TRA huwa hawana mkazi na hawafuatilii sana huko Public sector kama wafanyavyo private sector so utaona benefits nyingi sana haziwi taxed kabisa huko public wakati private sector every single coin anayopata employee iko taxed na TRA wanafanya audit za mara kwa mara kuhakikisha waajiri wanacomply

3. Mishahara ya public sector (Basic) iko chini sana na ukizingatia threshhold kwa sasa ni 100,000, unakuta mtu basic yake ni 150,000 which means anatakiwa akatwe kodi kwenye 50,000! But in reality unakuta kwa mwezi mtu huyu anatoka na like 1, 2,3mil kama gross income from sitting allowance, acting allowance, extra duty allowance, honorarioum, perdiem etc ambazo they don't tax kabisa! So wanaendup kuienjoy income kubwa but pay less tax, kumbe private mishahara ni mikubwa but hakuna eti malipo ya sitting allowance, acting sijui nini......! so mara nyingi utakuta gross income = basic income......maanake hakuna income inayokwepa machine ya PAYE.!

Wafanyakazi wengi wa Umma hawapatiwi nyumba, ukiacha Walimu, watumishi wengine ni mpaka uwe Mteule katika nafasi za Ukurugenzi ndo unaweza kupatiwa posho ya nyumba.

Kwa upande wa sitting, extra duty, acting na allowance nyingine ambazo umezitaja, huwa hazipatikani kiurahisi hivyo kama ulivyoandika. Mnaweza kuwa mnafanya ofisi moja lakini Mtumishi mmoja akawa anasafiri sana wakati mwingine anakalia kijiwe. Na hapa ndipo tunapokoseaga na kushindwa kudai nyongeza ya mapato ya msingi (Mshahara) kwa kuamini kuwa unaweza kupata safari na allowance nyinginezo
 
1. Ila kweli ni kwa nini personel emulments hazikatwi kodi??

Angalia Mbunge Basic salary ni 1.8 m ndo hukatwa kodi. Na marupurupu mengine ya 5.0 m ni tax free!! Katibu Mkuu wa Wizara ana Salary ya 3m na marupurupu 11.0 m ambayo ni tax free!

2. Kuna haya malipo wafanyakazi wanakatwa kwa nguvu bila ridhaa yao ya vyama vya wafanyakazi: ni pesa nyingi sana na hukatwa kwa nguvu toka ktk salary wakati hivi vyama havieleweki vinatetea nini!!! Hivi Tz ni nchi ya kidiktator? kwa nini kuwe na sheria ya kukata pesa za wafanyakazi kwa nguvu wakati sii kodi?

Is this fair?
 
Kandambili hapa naona hujafanya utafiti vyakutosha, the Farmer yuko sahihi kabisa kwamba ukilinganisha wafanyakazi wa Private Sector na Public Sector wale wa Private sector wanalipa zaidi kuliko wa Public Sector kwa sababu zifuatazo;

3. Mishahara ya public sector (Basic) iko chini sana na ukizingatia threshhold kwa sasa ni 100,000, unakuta mtu basic yake ni 150,000 which means anatakiwa akatwe kodi kwenye 50,000! But in reality unakuta kwa mwezi mtu huyu anatoka na like 1, 2,3mil kama gross income from sitting allowance, acting allowance, extra duty allowance, honorarioum, perdiem etc ambazo they don't tax kabisa! So wanaendup kuienjoy income kubwa but pay less tax, kumbe private mishahara ni mikubwa but hakuna eti malipo ya sitting allowance, acting sijui nini......! so mara nyingi utakuta gross income = basic income......maanake hakuna income inayokwepa machine ya PAYE.

Kwa ujumla wafanyakazi wa private sector wanalipa kodi kubwa kuliko wale wa Public sector kama nilivyoeleza hapao juu!

  1. Kwa mujibu wa INCOME TAX - EMPLOYMENT INCOME allowance zote LAZIMA zikatwe kodi PER DIEM haikatwi kodi.
  2. Wanaolipwa acting allowance, sitting allowance ni wafanyakazi wa level za juu ambao ni wachache sana.
  3. Kama hazikatwi ni makosa kwa mujibu wa sheria.
  4. ALL IN ALL HOJA YANGU IKO PALE PALE, wafanyakazi tunaopokea mishahara tunakamuliwa sana regardless uko kwenye PRIVATE or PUBLIC SECTOR, nasimamia hapo hapo............................
 
Kwa taarifa yako HOUSE ALLOWANCE inakatiwa kodi in short ANY INCOME DERIVED FROM EMPLOYMENT IS TAXABLE, soma Income tax ACT utaelewa vizuri, kwenye magari naweza kukubaliana na wewe lakini jiulize pia hiyo incentive inawanufaisha wangapi na wenye kipato gani kuweza kununua gari? umefanya mchanganuo ujue huo msamaha una unafuu kiasi gani, najua VAT haipo kwenye msamaha.....
Nilimaanisha housing benefit, yaani kama wakipewa nyumba za kuishi....sheria inawalinda......

Section 7 (f): in calculating an individual's gains or profits from anemployment, the following shall be excluded;

a) - (f) benefit derived from the use of residential premises by an
employee of the Government or any institution whose budget
is fully or substantially out of Government budget subvention;

Pili exemption kwenye magari ya wafanyakazi wa serikali impact yake kwa mwaka wa fedha 2006/2007 ni loss of tax by Tshs 3.2bil......

Kwa taarifa yako siku hizi wanafanya Audit mpaka kwenye Public Sectors.....

Sina matatizo na hilo, ila ninacho sema umakini wake sio kama ule wa kwenye Public sector mkuu!
Hizo allowance zote ulizozitaja hapo ni TAXABLE

Si kweli mkuu, hata sheria tu ina exempt some income kwa baadhi ya wafanyakazi wa serikali.....see below;

Second Schedule to ITA 2004: Exempt amounts

The following amounts are exempt from income tax:-

(a) amounts derived by the President of the United Republic or the President of the Revolutionary Government of Zanzibar from salary, duty allowance and entertainment allowance paid or payable to the President from public funds in respect of or by virtue of the office as President; Act No.5 of 1986 Cap.245

(b) amounts derived by the Government (including Executive Agency established under the Executive Agencies Act,
1997) or any local authority of the United Republic or by the Revolutionary Government of Zanzibar or any local authority of Zanzibar except amounts derived from business activities that are unrelated to the functions of government;

(m) amounts derived by way of foreign living allowance by
any officer of the Government that are paid from public funds and in respect of performance of the office overseas;

(s) gratuity granted to a Member of Parliament at the end of each term;

Sasa wale wa private sector hawana cha baadhi wala nini, everyone is treated with equal foot!

nakubaliana na wewe 100%

Naam!

Nusu ya LIFE yangu kwenye AJIRA nimeitumia kwenye PRIVATE na PUBLIC nimeyaona mengi.....

Mimi ugali wangu wa kila siku unategemea maissues ya kodi mkuu, so I know very well the ITAs, TRA & Co!
 
PAYE haiwezi kupunguzwa kwa sababu ni kadi ambayo haina usumbufu wowote ule kwenye ukusanyaji. Yani Employer amebanwa kwa mujibu wa sheria kuikusanya hiyo kodi kila mwezi. Angalia tax brackets based on Basic salary http://www.tra.go.tz/documents/new tax rates.pdf Pia unaweza ukafanya calculations kwa kutumia hii calculator ya TRA http://www.tra.go.tz/Paye.html

ETI "PAYE haiwezi kupunguzwa kwa sababu ni kadi ambayo haina usumbufu wowote ule kwenye ukusanyaji......"

MUNGU WANGU, Kama kweli hii ndio sababu basi watanzania uvivu utatumaliza, hizo sheria zenu za kuwabana Employer kwanini msizitumie kubana kwenye vyanzo vingine?n HAINIINGII AKILINI HII kwakweli.......
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom