Pay As You Earn (PAYE): Wafanyakazi mna maoni gani?

Ndugu yangu Kandambili your observation is quite right!

Employees wanalipa kodi kubwa sana kulinganisha na makundi mengine ya kijamii relative to their income.

Ukifanikiwa kuwa mjasiliamali na business yako ikatake off vizuri, ukaiendesha informally, unauwezekano wakulipa kodi ndogo sana kuliko ukiwa umeajiriwa!

Ngoja nitoe mfano mmoja hapa;

Nimemwajiri mtu X kwa ajili ya kutoa huduma fulani kwenye yangu na namlipa kwa mwezi Tshs 400,000/= (Gross income), mwajiriwa huyu nitamkata kwa kila mwezi Tshs 54,500 kama PAYE so kwa mwaka atakatwa Tsh 654,000!

Scenerio ya pili, sitaki kuajiri na mcontract mjasiriamali Y awe ananifanyia kazi ambayo X angeifanya, tunakubaliana niwe namlipa labda baada ya miezi sita Tshs 2,400,000 so kwa mwaka Tshs 4,800,000 kama fees excluding disbursements. Huyu mambo ya kodi anatakiwa kuhandle mwenyewe, so labda ataenda kukata TIN na kujisajili kama mfanyabiashara mdogo.

Kwa kuwa mapato /mauzo yake hayazidi Tshs 7,000,000 kwa mwaka....anatakiwa alipe Tshs 95,000 tu kwa mwaka kama kodi

Now linganisha Tshs 654,000 PAYE anayolipa mwajiriwa na Tshs 95,000 kwa mapato sawa utaona jinsi waajiriwa wanavyoumizwa.

Mfano mwingine; niko na jamaa zangu pale k/koo wanafanya biashara mbalimbali na wanamiliki majengo kadhaa pale.....mauzo yao kwa mwaka ni kati ya Tshs 100,000,000 to 1,000,000,000! Lakini kodi wanayolipa.....utashangaa kweli, hata Tshs 500,000 kwa mwaka haifiki na hii wanakadiriwa na TRA. Wakati mfanyakazi anayepata say Gross ya 5,000,000 kwa mwezi, tayari analipa zaidi ya 1 mil kama kodi kila mwezi!

So ukiwa kwenye informal sector kodi unalipa kidogo sana relative to your income compared to employees!

TRA na serikali wanatakiwa kupanua wigo wa kodi (tax base) ili kuyanusuru maisha ya wafanyakazi waliobebeshwa mzigo wa kodi kama punda! Waache uvivu wa kufikiria vyanzo vingine vya kodi kama vile Kodi za pango (rental taxes), waongeze kodi kule kwenye informal sector, including income inayopotea kule kny masherehe, madalali, MCs, Usafirishaji etc na pia kupunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima kwa serikali!

Vinginevyo wote tutahamia huko kwenye informal sector, kwenye unafuu mkubwa sana wa kodi!
Hoja yako mkuu niliyoiangalia kwa haraka haraka,ni mbona mfanyakazi naye ana mtaji anaouingiza ili mwisho wa mwezi apate mshahara,lkn kodi haizingatii mtaji huo Kama Vile nauli ya kila siku,chakula etc,mfanyabiashara mtaji wake unalindwa na faida ndo inapigwa Kodi,
Pamoja na elimu nzuri iliyotolewa hapa bado nina swali kwa anayejua anielimishe ni kwanini mfanyakazi hatambulikani Kama mlipakodi kwa kupewa TIN namba? Hii inatuingiza hasara sisi wafanyakazi,inapotokea TRA wakafanya tax refund fedha hiyo inaenda Kwa mwajiri badala ya mfanyakazi aliyelipakodi.hii imekaaje?

Napendekeza mwajiri apeleke kodi zetu TRA kwa TIN namba zetu, Kama wanavyotupelekea kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.mh.mpango umesimamia Mambo mengi nakuomba fanikisha na hili.
 
Juzi juzi wakati nikitafakari sherehe za mei mosi niliingia kwenye kabati yangu nikaanza KUPERUZI salary slips zangu nikiangalia namna ninavyotendewa na hao wanaojiita waajiri. Kitu kimoja nilichokigundua ni kuwa wafanyakazi tunalipa sana KODI kuliko mtu yeyeto Duniani.

Tunalipa indirect tax sawa sawa na watu wengine wote wanaopata huduma na bidhaa tofauti tofauti.

Tofauti na wafanyabiashara wanaolipa kodi kwenye faida, yaani NET PROFIT sisi tunachanjwa P.A.Y.E kwenye gross salary.

TATIZO LANGU HAPA ni kuwa hii PAYE ni kubwa sana kwanini badala ya kupigana eti tuongezwe mishahara huku tukijua na mzigo wa kodi utaongezeka kadiri mishahara inavyoongezeka tusijipange kwa pamoja tupiganie PAYE ipungue?

Najua serikali wanaipenda sana kwani inakusanywa kirahisi sana na garama POA kabisa, kama kweli JK wenu anataka Maisha bora kwa kila mtanganyika basi PAYE ipungue na kodi za kufidia zitafutwe mahali pengine kama kupunguza misamaha ya kodi, kupunguza matumizi MAKUBWA ya serikali, na Kuwa makini na wafuatiliaji wa maliasili zetu kama samaki na madini?

Vyama vya wafanyakazi mko wapi? hivi huwa mnachaguliwa kwakuwa mna CV zenu au uwezo wenu wa kuhamasisha migomo?

NAWASILISHA.

==========
KWA UNDANI:

Kuelewa dhana ya Kodi inayotokana na Ajira (Pay As You Earn)

Kodi inayotokana na Ajira inajulikana kama Lipa kadiri unavyopata (PAYE). Hii ni kodi ya zuio kwa waajiriwa wanaotozwa kodi. Chini ya mfumo huu, mwajiri anapaswa kisheria kukata kodi ya mapato kutoka katika mshahara au ujira wa mwajiriwa anayestahili kutozwa kodi. Sehemu ya 81 ya Sheria ya Kodi ya Mapato inamtaka mwajiri kukatalia kodi kutoka kwa malipo yaliyolipwa mfanyakazi. Mwajiri anahitajika na Sehemu ya 84 (1) kulipia kodi iliyozuia kwa TRA kati ya siku saba baada ya mwisho wa kila mwezi wa kalenda.

View attachment 1304578

Maana ya Mwajiriwa:

Mwajiriwa ni mtu anayehusika na ajira inayoendeshwa na mwajiri. Ajira inahusisha waajiriwa wa kudumu, waajiriwa wa muda, meneja, Mkurugenzi, na vibarua. Waajiriwa wanaweza kuajiriwa na mwajiri mmoja au zaidi (ajira ya msingi na ya ziada)

Maana ya mwajiri:

Mwajiri ni mtu anayeendesha, aliyeendesha au ana lengo la kuendesha ajira kwa watu.

Mkurugenzi wa ajira ya kudumu:

Maana yake ni mwajiriwa wa kudumu katika shirika anayefanya kazi ya kiutawala.

Usimamizi wa Kodi ya Mshahara

Mwajiri anapaswa kuzuia kodi ya mapato kutoka katika mishahara, ujira na malipo mengine yote yanayopaswa kukatwa kodi kutoka kwa waajiriwa.

==========

SASA: (Updated based on 2017 information available)

Kiwango cha kodi, ambacho mtu anatakiwa kukatwa kwa mujibu wa sheria ya kodi ya mapato, vinatofautiana kutoka mtu mmoja hadi mwingine, kulingana na kiwango cha kipato anachopata mtu kwa mwezi.

Kodi ya ajira, ambayo mwajiriwa anakatwa kwenye mapato au mafao yake, kiwango cha mshahara au kipato au ujira, kinachotakiwa kukatwa kodi ni kile kinachozidi Sh 170,000 kwa mwezi.

Kwa mujibu wa TRA, kwenye ajira kuna vyanzo tofauti tofauti vya mapato kwa mwajiriwa, kama vile motisha (bonus), kamisheni, ujira, mshahara, malipo ya likizo, posho na mengineyo, ambayo yote yakijumlishwa yanatengeneza kipato cha mwezi, hivyo kipato hicho kama hakizidi Sh 170,000 hakikatwi kodi.

Kipato cha Shilingi 170,000 kushuka chini hakina kodi, kimesamehewa kwa mujibu wa sheria ya kodi ya mapato Kifungu namba 10 ukisoma pamoja na jedwali la pili la kodi ya mapato ambalo linaonesha viwango vilivyosamehewa kodi kuwa ni pamoja na hiki cha Sh 170,000 kushuka chini.

Kwa mujibu wa TRA, kiwango kinachozidi Sh 170,000 lakini hakizidi Sh 360,000 kwa mwezi, kodi yake ni asilimia tisa (9%). Kwa mfano mtu analipwa Sh 360,000 au 240,000, kinachofanyika ni kwamba inatolewa Sh 170,000 kwenye kipato hicho na kiasi kinachobaki ndiyo kinakatwa kodi ya asilimia tisa.

TRA inasema kuwa kwa mwajiriwa anayepata kipato kinachozidi Sh 360,000 lakini hakizidi Sh 540,000 kwa mwezi, kodi yake ni Sh 17,100, lakini inajumlishwa na asilimia 20 ya kodi kwa kipato kinachozidi Sh 360,000.

Vivyo hivyo kwa kipato kinachozidi Sh 540,000 lakini hakizidi Sh 720,000 kwa mwezi, kodi yake ni Sh 53,100, lakini itaongezwa na asilimia 25 ya kiwango kinachozidi Sh 540,000.

Kiwango chochote cha kipato cha kuanzia Sh 720,000 kwenda juu kwa mwezi, kodi yake ni Sh 98,100, lakini inajumlishwa na asilimia 30 ya kiwango kinachozidi Sh 720,000, hivyo kodi kwa mtu binafsi hata kama analipwa Sh milioni 20 au zaidi, anakatwa kodi kwa utaratibu huu.

Kiwango hicho cha kodi cha asilimia 30 kwa mujibu wa sheria za kodi ya mapato, ndiyo kiwango cha juu zaidi kuliko kiwango kingine chochote. Kwenye kodi kuna viwango vya asilimia tano, asilimia 10, asilimia 15, asilimia 20, asilimia 25 na asilimia 30 ambacho ndiyo kiwango cha mwisho kwenye kodi ya mapato.

Mfumo wa kodi ya ajira, unamtaka mwajiriwa alipe kodi kadri anavyopata kipato (PAYE). Mwajiriwa anayepata kipato kidogo, pia analipa kodi kidogo na anayepata kipato kikubwa na kodi pia huwa kubwa.

Punguzo la kodi kwa mujibu wa TRA, Serikali kila mara imekuwa ikirejea viwango vya kodi na kuendelea kuvipunguza ili kuongeza watu wengi zaidi kwenye wigo wa kodi.

Viwango vya kodi vinapokuwa juu sana, vinawafanya watu kukwepa kodi na ndiyo maana Serikali huvirejea viwango hivyo kila mara. Kwa zamani asilimia ya kodi ya ajira ilikuwa kubwa, kwa kuwa ilianzia asilimia 17 baadaye ikashushwa hadi asilimia 15, ikashushwa tena hadi asilimia 14, baadaye asilimia 12 na 11, na sasa ni asilimia tisa.

Matokeo ya punguzo la asilimia tisa la kodi ya ajira, alilolitoa Rais John Magufuli, linaonekana zaidi kwa watu wenye kipato cha chini, tofauti na wenye kipato kikubwa ambao kwa wengi bado kodi hii ni kubwa sana.

======
Baadhi ya mijadala:

2013: Punguzo la PAYE kwa asilimia 1 ni dhihaka kwa wafanyakazi!

2019: Rais Magufuli atashinda kwa kishindo 2020 ( 99.9) endapo ataigusa kodi ya Pay As You Earn ( PAYE) kwa wafanyakazi wa kada za chini!
NAOMBA MWENYE KUJUA KIASI GANI ANAPATA MTU MWENYE SCALE HII YA MSHAHARA PGSS2
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom