Pay As You Earn (PAYE): Wafanyakazi mna maoni gani?

Wakuu PAYE ni kitu ambacho kinaumiza lakini hatuna budi kufahamu brackets zake ndipo kisha tuseme kuwa maumivu yake ni makali kiasi hicho ua tuna exagerate.

.Kama pato la mtu (Kwa maana ya Gross ukitoa nssf etc) halijazidi 100,000 Tshs hutakatwa PAYE

.Kama pato litazidi 360,000 lakini halizidi 540,000-Utakatwa 39,000Tshs jumlisha na 20%a kiasi kilichozidi kutoka 360,000

.Kama pato litazidi 540,000 lakini si zaidi ya 720,000-Utakatwa 75,000Tshs jumlisha na
25% ya kiasi kilichozidi kutoka 540,000 Tshs

.Kama pato litazidi 720,000 na kuendelea-Utakatwa 120,000 jumlisha na 30% ya kiasi kilichozidi kutoka 720,000 Tshs.

Huu ndio mgawanyiko wa kodi amabyo mafanyakazi hutakiwa kulipa kila pato lake la mwezi linapoingia....
Hapa ndipo wafanyakazi huuliza ni kwa kiasi gani wanaichangia serikali lakini serikali haitaki kuonyesha ni jinsi gani inavyothamini mchango huu kwa kuleta maendeleo thabiti..... Halafu mnashangaa kwa nini wafanyabiashara wanakwepa kodi.Kama wafanyakazi wangeambiwa wachague i bet 80% wangesema hawaoni faida ya wao kuwa deducted hii kodi.
 
Kandambili said:
Kuhusu suala la employer kushare na employee SAHAU KABISA TRA wanasheria zao ukifanya hivyo tu hata hiyo % uliyochangiwa na muajiri wana ADDBACK kama ni income kwako then wanakuchanja KODI.......

Haahahahaaaa....Kanda2 umenifurahisha sana hapo kny bold! Mkuu inaelekea PAYE ishakuumiza sana eeeeh!

Ni kweli anybenefit unayopata kutoka kwa employer inakuwa added back na ukuwa taxed accordly!

Regulation 4 of the Income tax act 2004, inasema ''Any expenditure by the employer for the benefit of employeee is not wholly and exclusively incurred for generation of incomes unless it is taxed in the hands of the beneficiary''

Kwa hiyo utaona hakuna sehemu ya kukumbilia zaidi ya kule kwenye mjengo!

Kwa hiyo hawa jamaa wa TRA wanamuogopa sana Employer, ndio maana huwa wanazungumza habari ya Corporate tax wanazolipa TBL, Vodacom etc
 
kama hiyo haitoshi serikali hiyo hiyo uliyo ipa income kwa wewe kuajiriwa na kulipwa mshahara mkubwa inakukata mkopo wa chuo kwa nini wasikate kwenye kodi wanayochukua
maisha ni magumu kwa ajiri ya upuuzi tu wakutotufikiria wenzao
 
Mkuu , mbona mishahara ya Wabunge haiko exempted ( only the gratuity is) mbona sasa mamlaka ya kodi inakuwa na kigugumizi kuwalipisha kodi?
hata hiyo gratuity kutokuikata kodi hakuna mantiki - anyway ndo sheria!

WoS siyo sheria bali hawa jamaa zetu wabunge wametumia fursa ya wao kuwa watunga sheria kujitungia sheria inayowapendelea. Na ndiyo hapa mimi huwa naunga mkono pia Wadaktari na Walimu kugoma kama nyenzo ya kudai haki na maslahi bora zaidi. Lakini utasikia wanasiasa wanawaambia kuwa si wazalendo na wengine kuwaita madaktari wauaji. Kama mwananchi anahamasishwa kulipa kodi kwa maendeleo ya taifa lake , Mbunge siyo raia?
 
Teheee usinivunje MBAVU kweli PAYE imeniumiza si tu mfuko bali na kichwa changu, especially ninopoona hakuna recognition sifa anapewa TBL, hela za kodi ZINAKWIBWA na MAFISADI... Basi tu natamani itokee muijiza watunga sheria iwaingie akilini mwao......

Kama haitawaingii akilini.......tutakimbilia huko kwenye ujasiriamali mkuu! Tumenyonywa vyakutosha!
 
Kila Mwananchi wa Tanzania analipa kodi, wengine wanalipa mara mbili.

Bidhaa zote mtu anayonunua imejumlishiwa VAT (20%) na VAT ya Tanzania ni kubwa hata kuliko kenya (VAT16%).

So Mfanyakazi yeyote awe wa Public,Private au Shirika analipa PAYE. Mie nafanya kazi private sekta na nalipa PAYE.

KWa hiyo Mfanyakazi yeyote anayelipa PAYE huwa pia analipa VAT. Tafadhali wafanyabiashara wao si walipaji kodi, wao ni wakusanyaji wa kodi kupitia biashara/bidhaa zao na kuwasilisha serikalini. Hivyo mfanyabiashara anapokwepa kodi ni Mwizi ana anapaswa kushitakiwa kama mwizi wa kuku,nguruwe, mbuzi, n.k

Sasa kwa sababu mfanyakazi analipa PAYE na VAT ninathibitisha kuwa mfanyakazi huyo anaonewa. Nadhani wafanyakazi hapa wananielewa, Hivyo Nashauri wafanyakazi wote wanaolipa PAYE wapewe 'privilege' unafuu huo.

Wafanyabiashara wao ni wakusanyaji wa kodi kwa niaba ya TRA na wabanwe sawa sawa. Vyanzo vyote vya kodi vikishughulikiwa vizuri Tanzania ni Tajiri Kabisa, kuanzia Madini, Utalii, Samaki, Bandari, Biashara za bidhaa, magari, maduka ya vyakula, supermarkets. tanzania ni tajiri ila tatizo ni UFISADI na UKWEPAJI KODI.

KAMA wafanyakazi wote wa sekta zote wakiungana wakadai haki zao inawezekana, kama ni kugoma wafanyakazi wote wagome na kuandamana mbona serikali itanywea!!!

Inawezekana ila cha maana ni kuwasiliana kati ya idara za serikali na vyama vya wafanyakazi.

"2gether we stand, divided we fall"

Kwa hiyo wafanyakazi wote wanaolipa PAYE wasilipe tena VAT na inatakiwa wanunue bidhaa DUTY FREE SHOPS.

NAtumaini mpaka hapo mmeshanifahamu ee
 
Teheee usinivunje MBAVU kweli PAYE imeniumiza si tu mfuko bali na kichwa changu, especially ninopoona hakuna recognition sifa anapewa TBL, hela za kodi ZINAKWIBWA na MAFISADI... Basi tu natamani itokee muijiza watunga sheria iwaingie akilini mwao......
Ukiwa na frustration za namna hii, ni ishara kwamba umepevuka kwenye hatua uliyopo. It is time to go to the next level.
Hiki kitabu hapa chini kina kurasa 40 tu - kisome!

Who Moved My Cheese?

https://www.jamiiforums.com/431747-post395.html
 
WoS siyo sheria bali hawa jamaa zetu wabunge wametumia fursa ya wao kuwa watunga sheria kujitungia sheria inayowapendelea. Na ndiyo hapa mimi huwa naunga mkono pia Wadaktari na Walimu kugoma kama nyenzo ya kudai haki na maslahi bora zaidi. Lakini utasikia wanasiasa wanawaambia kuwa si wazalendo na wengine kuwaita madaktari wauaji. Kama mwananchi anahamasishwa kulipa kodi kwa maendeleo ya taifa lake , Mbunge siyo raia?

Inavyoelekea mbunge kajiweka juu kuliko raia wengine.Kama kila mtu atakimbilia kuwa mbunge itakuwaje?

Wanasiasa wanatupeleka kubaya.Kila mtu anastahili kupata kipato cha kumtosheleza kujikimu.Kodi zinawabana zaidi wale wenye kidogo na kuwaacha wenye cha kuzidi kama hawa wabunge na wengine wenye kupokea per diems na allowances nyingi kwa kufanya kazi zilezile wanazotakiwa kuzifanya kwa mishahara wanayopokea! Ama kweli mwamba ngoma huvutia kwake.
 
Ukiwa na frustration za namna hii, ni ishara kwamba umepevuka kwenye hatua uliyopo. It is time to go to the next level.
Hiki kitabu hapa chini kina kurasa 40 tu - kisome!

Who Moved My Cheese?

Lazy dog .....chukua 5!

Kanda 2.........solution hapa ni ujasiriamali!
....and your ID here on JF is Next Level
I didn't notice that

Ujasiriamali unanoga ukikumbana kwanza na kash-kash zinazomuumiza kichwa Kanda2;)
Kuna mahali nilisoma kuwa "It is only through challenge we become better" - only through challenge, I am afraid!
 
Lazy dog.....Asikudanganye mtu, ujasiriamali bongo ni mtamu na very simplem kuorganise...hasa informal one......ukitaka kuformalize...mmmh hailipi bongo!
 
Hivi majuu wafanyakazi hawakatwi mijikodi ya namna hii?
 
Hivi majuu wafanyakazi hawakatwi mijikodi ya namna hii?

hata wakiakatwa ina uwiano na ya mikodi ya wafanya biashra pia! tatizo bongo ni ka unyonyaji fulani kwa wafanyakazi kukatwa kodi kubwa, kisa eti ni rahisi kuikusanya kuliko wafanya biashara!
 
Lazy dog .....chukua 5!

Kanda 2.........solution hapa ni ujasiriamali!

Wote tukiwa wajasiriamali nani atakuwa mfanyakazi????
Swali lako lilishajibiwa.

So what does this tell us (employees)?
PAYEE itaendelea kuwepo maana wengi wataendelea kung'ang'ania kubaki kwenye comfort zone (being employed) - risk free area.

If you can't change others or the system....
...maybe you should start think about changing you!

Any government will favor those who create jobs for themselves or others.
Ikiwa nusu ya waajiriwa watahamia kwenye ujasiriamali, nafasi zao zitafidiwa na graduates. Kanda2 uking'ang'ania hiyo comfort zone, ajira zitazidi kuwa ngumu zaidi kwa vijana.
 
Swali lako lilishajibiwa.
Ikiwa nusu ya waajiriwa watahamia kwenye ujasiriamali, nafasi zao zitafidiwa na graduates. Kanda2 uking'ang'ania hiyo comfort zone, ajira zitazidi kuwa ngumu zaidi kwa vijana.

Mimi sio king'ang'anizi, kwa taarifa yako nimeajiriwa na kujiajiri pia. Vita vyangu sio PERSONAL naangalia kwa UJUMLA wake kwa kizazi hiki na kijacho, unadhani hao graduates ndio wanastahili KUKANDAMIZWA????? Sidhani ushauri wako kama mpiganaji natakiwa kuuchukuwa, mwisho wake utanishauri niikimbie nchi yangu eti kwa vile imejaa mapapa na manyangumii

NAOMBENI NAMBA YA DR. Slaa nimpelekee kilio changu............
 
That is very good. Uko kwenye level gani kati ya hizi:
a) Full time Employee & also run a part-time business
b) Run own Business (full time) & part-time employee

Ndiyo, graduates ni vyema wakakandamizwa kwanza! Soma hapa utaelewa nina maana gani :)
 
Hapo mdau umeongea jambo la maana sana. Mimi nafanya kazi kwenye kampuni moja ya mawasiliano yaani tunavyopigwa P.A.Y.E mpaka mtu unachanganyikiwa. Unaweza ukaangalia slip yako ina basic salary nzuri tu lakini take home ya mawazo kwa kuwa ukikaktwa P.A.Y.E karibu robo ya salary inapotea.

Yaani mimi mpaka nimefikia hatua ya kusema sitaki kusikia kiongozo ananiambia eti nitoe mchango sijui wa shule ya kata sijui madawati sijui mtaro sitaki kusikia kabisa. Kwa kuwa robo ya mshahara unaenda TRA bado gari nalipia kodi, nyumba nalipia kodi ya kiwanja kwa mwaka, mafuta kodi kila kitu nikinnunua kina VAT sasa nikiangalia nahisi nusu ya salary ni kodi. Hivi hii nchi sijui ina matatizo gani. Mi nahisi kuna tatizo la kufikiria na kuweka hoja mezani tukazijadili kwa umakini.

Swala la msingi ni kwamba kweli kodi zinakusanywa lakini zinafanya nini? Ni aibu kuzungumzia hilo. Nashangaa kuona mpaka leo eti hospitali ya taifa vitanda na neti ni ishu acha madawa yaani kitanda ni ishu. Wakati mabilioni ya fedha yanaingia mifukoni mwa wachache ambao mpaka katiba ya nchi inawatetea.

Mijadala ya wazi kama hii inahitajika ili kuweza kujadili maswala ya msingi yanayohusu maendeleo ya mwananchi wa kawaida na tuache kujadili uchumi kwa kusoma tu tarakimu na asilimia kwenye makaratasi.
 
Mimi sio king'ang'anizi, kwa taarifa yako nimeajiriwa na kujiajiri pia. Vita vyangu sio PERSONAL naangalia kwa UJUMLA wake kwa kizazi hiki na kijacho, unadhani hao graduates ndio wanastahili KUKANDAMIZWA????? Sidhani ushauri wako kama mpiganaji natakiwa kuuchukuwa, mwisho wake utanishauri niikimbie nchi yangu eti kwa vile imejaa mapapa na manyangumii

NAOMBENI NAMBA YA DR. Slaa nimpelekee kilio changu............

Kandambili!

Hoja yako ni ya msingi achana na huyo lazy dog hajui nyuma wala mbele!

Kwa taarifa ya wanajamiiforum PAYE ni mojawapo ya chimbuko la rushwa kwa watu wote walioajiriwa na wanalipwa mishahara mizuri! Haiingii akilini mtu kulipa 30% PAYE na INAYOBAKIA unalipa another 20% kama VAT simply because unafanyakazi! Kule UK wanokatwa kodi kiasi hicho ni wenye income inayozidi Sterling pounds laki moja na nusu 150,000 au say milioni 300 za Kitanzania na sio paundi elfu 5!!! Kalakabaho!!!!!
The CCM govt is corrupt using the taxation system!! In short ni incubator ya rushwa then to fight it ni ndoto ya mchana!!!

On top of that wanaambiwa wachangie na kulipia vitu lukuku apparently wakubwa ndio wenye uwezo wa kudai asilimia 10% (actually ni 90%) kutoka kwa washitiri na watoa huduma na ni mabingwa wa kuanzisha safari nje na ndani plus makongamano hewa ili kufidia kodi then that is when wana over do
na ndio mapapa wa ufisadi ambao Mengi hataki kuwataja!!

Kwa hiyo tunapojadili PAYE kila mtu akune kichwa!! Wafanyabiashara hawalipi kodi bali wanakusanya kutoka kwa walaji therefore THE gvt na TRA they should not talk of big tax payers!! Hiyo VAT is 80% returned through dubious calculations kwa hao VAT registered bastards!

The challenge is to revamp the taxation system ili kama tunasema 50%PAYE basi walipe watu wote!! Watu wote I mean kila mtu mwenye umri wa miaka 18 alipe kodi it could be graduated lakini we should all pay except makundi ya walemavu and senior Citizens (above 60years). or those on social benefit kama ikianzishwa !!

When it comes to property tax pia walipe wote!! Kila nyumba ya biashara na kupanga ilipiwe kodi this gvt inachefua inaleta politik kwenye kodi!!

Tuondoe double standards kwenye uchumi !! Ccm mmefuta kodi ya maendeleo halafu mnapelaka bakuli Japan kuomba msaada while your lazy people don't pay tax;;;;;stupid!! Changamoto ya maisha kwa hao mnaowadanganya mtawapa maisha bora iko wapi???? Nani kawaambia kodi ni kero!!! Bila kutafakari mkiendelea kuwakamua hao wafanyakazi wachache then you are dead and burried! Mitanzania bwana!!!!!! You could use the vipande vya kodi as ID's and later mprint kadi za uraia baada ya kupata kodi!!! Nyie!!! Waone!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom