Orodha ya watu walio pona LOLIONDO HII HAPA

WanaJF Habari za Jumapili!
Nipo mirerani, nimekutana na mwalimu mmoja ananishuhudia kuhusu maajabu ya Dawa ya Loliondo.

Alikuwa loliondo tarehe 8/04/011 na kurudi 11/04/011 anasema ameshuhudia watu mbalimbali wakipona magonjwa zaidi ya yale 5 ambayo awali ndiyo nilijua kuwa dawa ya hy inatibu.

Naomba niwape shuhuda hzo:-
Kijana mmoja kutoka rombo amepona kichaa alichokuwa nacho kwa zaidi ya miaka 12. Kijana hyo alifka maeneo ya tiba akiwa amefungwa kamba mikono na miguu lakini baada ya dakika 12 baada ya kupata kikombe cha babu aliamka na kuanza kushangaa kama mtu aliyeznduka kutoka kwny ucngizi mzto! Dakika 5 baadae akaomba awasaidie wasaidiz wa babu kusafsha vikombe ili wagonjwa wengne wazdi kupata dawa.

Shuhuda nyingne ni kuwa mama mmoja ambaye alikuwa na kansa ya ini na kusababisha tumbo kuvimba kwa miaka 3 alipona dakika 20 baada ya kunywa kikombe cha babu.

Nyingine ni ile ya mtoto ambaye alikuwa hali kabisa nyama ya aina yoyote kupona na kuanza kula nyama ya mbuzi palepale samanga!

Kwa kifupi nimeona niwajuze ushuhuda huu ambao kwa kweli ulinifanya nibaki mdomo wazi na nikaona niwashirikishe wana-familia wenzangu.

Asante kwa nia yako njema kutujuza, lakini hizo tarehe sizielewi kabisa, kwani naona bado ziko mbele. Weka sawa tafadhali
 
Alikuwa loliondo tarehe 8/04/11 na kurudi 11/04/11? Hizo tarehe tu zinatia uvivu kusoma
 
Alikuwa loliondo tarehe 8/04/011 na kurudi 11/04/011

hii inaonyesha ni jinsi gani usivyokuwa makini ,unaleta ushahidi wa kuambiwa halafu badala ya kuchunguza unakurupuka na kuleta habari za uzushi.

Kumbe ukitoka kunywa kikombe hata tarehe unasahau?
 
hii inaonyesha ni jinsi gani usivyokuwa makini ,unaleta ushahidi wa kuambiwa halafu badala ya kuchunguza unakurupuka na kuleta habari za uzushi.

Kumbe ukitoka kunywa kikombe hata tarehe unasahau?

sor ni mwezi march mkuu!!
 
Asante Babaubaya kwa kutuletea ushuhuda wa 3rd party ambao kitaalamu unaitwa ''hearsay' hivyo haukubaliki kama ushahidi. Ushuhuda wa kweli ni ule wa wewe kushuhudia kwa macho na masikio yako na sio wa kuambiwa.

Kama ni kweli huyo kichaa alipona baada ya dakika 12 na kuanza kushangaa shangaa na within 5 minutes akaanza kusaidia kazi ya kuosha vikombe akili yako haijakutuma kuwa jamaa ni bado anacho japo kimetulia tuu?!.
 
Ili kujiridhisha kwa sababu nipo bado hapa mirerani kuna dada mmoja aliyepona kansa ya kizazi miezi 3 iliyopita anakuja ili nisikie mwenyewe na kuondoa ushuhuda wa 3rd party (hearsay). Ntakujuza mkuu nimeomba aje ili niende sawa sawa na concern zako.
 
hii inaonyesha ni jinsi gani usivyokuwa makini ,unaleta ushahidi wa kuambiwa halafu badala ya kuchunguza unakurupuka na kuleta habari za uzushi.

Kumbe ukitoka kunywa kikombe hata tarehe unasahau?
...mkuu huyo nae ni mjasiriamali, huenda ana kausafiri kake ambako kanasafirisha wapiga kikombe! sasa mambo ya miezi hana shaka nayo yeye anajali ujumbe (ushuhuda) umefika maana anajua watanzania wanakwenda kwa fununu huwa hawasomi wala kutafakari.... hiyo stori ya jamaa imebidi nicheke maana inachekesha ni kama:
Kichaa mmoja alitulia tuli wodini wakati wenzake wakitetea kama kuku na kuwika kama jogoo, daktari akajua kuwa yule mmoja amepona alipomwendea yule kichaa akamuashiria asipige kelele na mwishowe akamwambia "sshhhhhh..........huoni kama nataga!!" daktari akapata jibu!
Hayo ndiyo ya Loliondo!!
 
na wewe ni walewale mabadiliko yapi?amezidiwa au amepona?vipimo vinasemaje?
..Hospitali ya mlima meru waahirika waliorudi pale kupimwa bado hali zao ni CHANYA! hakuna aliepata hasi!! na kanda ya ziwa ni vivyohivyo! lakini kwa maneno na matumaini, WAMEPONA, na VIRUSI VITAENDELEA KUPUKUTIKA BAADA YA MIEZI MITATU baada ya KIKOMBE!!

mbaya zaidi TUNAAMINI MNO MEDIA! ndio maana utasikia Redio imesema... TV Imesema....! Hkuna anaefuatilia kama ni kweli ama si kweli (matangazo ya biashara!)

ee Mungu wasaidie Watanzania!
 
Ishu za kwa babu-lolihondo kila siku ni kitendawili, serikali inatoa tamko leo, tusubiri labda tutapata mwelekeo.
Watawaambia dawa hiyo ni nzuri na inatibu!!!
Kenya hawajapasisha na wameanza kutafiti miaka takriban mitatu iliyopita na hata sasa wanaendelea...
SIASA ZA TANZANIA... duh!
 
Back
Top Bottom