Orodha ya watu walio pona LOLIONDO HII HAPA

huyu babu lazima atakuwa, amewaroga watu yaani kati ya watu wote waliogida kikombe hakuna aliyepona? yet some people are still flooding to loliondo, this is very awkward.
 
Ushauri wa bure kwa Mods:
Jaribuni kupunguza uwingi wa hizi posts za Babu na Loliondo,

Ni hilo tu.

Ni kweli mkuu. Zinafanya tusiwaze Dowans,matatizo ya umeme,bei za vyakula kupanda,shida za maji matibabu elimu nk. Au hii issue imetengenezwa!?
 
Jana nilipata nafasi ya kuongea na mzee mmoja alieenda Loliondo wiki kama tatu zilizopita......Mzee huyu anasema kuwa aliwapeleka watu wanne ambao walikuwa wanaumwa magonjwa mbalimbali....Nilipokuwa nataka kumdadisi hali za hao wagonjwa alionekana ni mtu wa kukata tamaa kidogo...akaniambia namnukuu 'ah hile dawa ni imani tu' nikataka kujua zaidi,ndipo aliponiambia hali zao bado si nzuri na haoni mabadiliko.....

Sipingi kwenda Loliondo,ila kabla ujaenda ongea na Mungu wako,God is faithfull anatoa majibu ya hakika.

Tumwamini Mungu Kwanza
 
kipindi kinaendela wanaoweza wasilkilze, kuna wachungaji wawili, mmoja anapinga mwingine anaunga mkono tiba ya babu.
 
Bado huyo dada kanikata maini etí kapona lakini bado hajapima ila anahc kama kapona vle. Atokee mtu aliyethibitishwa na vpmo kwamba hana Hiv, Diabates, Cancer na mengineyo ili watu tumiminike kupata kikombe cha babu huko Loliondo..!?
 
Ishu za kwa babu-lolihondo kila siku ni kitendawili, serikali inatoa tamko leo, tusubiri labda tutapata mwelekeo.
 
Mmea anaotumia babu kutibu, umekuwepo kwa miaka mingi na unapatikana sehemu nyingi tu duniani hii ni kwa mujibu wa daktari
 
WanaJF Habari za Jumapili!
Nipo mirerani, nimekutana na mwalimu mmoja ananishuhudia kuhusu maajabu ya Dawa ya Loliondo.

Alikuwa loliondo tarehe 8/03/011 na kurudi 11/03/011 anasema ameshuhudia watu mbalimbali wakipona magonjwa zaidi ya yale 5 ambayo awali ndiyo nilijua kuwa dawa ya hy inatibu.

Naomba niwape shuhuda hzo:-
Kijana mmoja kutoka rombo amepona kichaa alichokuwa nacho kwa zaidi ya miaka 12. Kijana hyo alifka maeneo ya tiba akiwa amefungwa kamba mikono na miguu lakini baada ya dakika 12 baada ya kupata kikombe cha babu aliamka na kuanza kushangaa kama mtu aliyeznduka kutoka kwny ucngizi mzto! Dakika 5 baadae akaomba awasaidie wasaidiz wa babu kusafsha vikombe ili wagonjwa wengne wazdi kupata dawa.

Shuhuda nyingne ni kuwa mama mmoja ambaye alikuwa na kansa ya ini na kusababisha tumbo kuvimba kwa miaka 3 alipona dakika 20 baada ya kunywa kikombe cha babu.

Nyingine ni ile ya mtoto ambaye alikuwa hali kabisa nyama ya aina yoyote kupona na kuanza kula nyama ya mbuzi palepale samanga!

Kwa kifupi nimeona niwajuze ushuhuda huu ambao kwa kweli ulinifanya nibaki mdomo wazi na nikaona niwashirikishe wana-familia wenzangu.
 
Back
Top Bottom