mpita-njia
JF-Expert Member
- Dec 3, 2010
- 1,733
- 1,610
Very good point. Ila sasa inarudi ile ile hoja ya kuwa yeye ni Mwenyekiti wa Chama na hataki kuona Chama kina fail mikononi mwake.Very timely arranged....! Kinachotokea ni kumchosha na kumuanika jamaa udhaifu wake na watendaji wake....ni mbinu za kisiasa kupima weledi wake na hekima yake...hili wengi hawajaligundua
Mwisho akifanikiwa kutoharibu atakuwa amechoka mno...angalia sasa operation UKUTA imemlazimisha naye aanze kuzunguka mikoani kama kipindi cha kampeni wakati huku kuna majukumu ya urais yanamsubiri
Haya mambo ya kisiasa angekiachia chama chini ya katibu mkuu . katibu mwenezi na viongozi wengine waifanye ili binafsi apate wasaa mzuri wa kushughulika na ya kitaifa
Wenzake wana majukumu ya kichama tu anataka kushindana nao....ikifika 2018 kwa mwendo huu atakuwa hoi mno na hiki ndio upinzani wanachotafuta
Ukitaka kumshinda mpinzani wako mchoshe mwili na akili
Kwa maoni yangu Raisi asiwe Mwenyekiti wa chama awe member tu wa Kawaida mwenye special privileges ili awe na wasaa mzuri wa kufanya shughuli za Kimaendeleo kwa Raia wake.