Only in Tanzania !

Eng Kimox Kimokole

JF-Expert Member
Jun 9, 2010
1,032
759
" ONLY IN TANZANIA!

Yapo Maajabu mengi sana...Ila Maajabu ya Wiki Hii yaliyo Tanzania ni kama Ifuatavyo

1. Mmoja wa Majaji Walioteuliwa kwa Mujibu wa Tundu Lissu Kumbe ndo kwanza anasoma shahada so darasani nae anasoma"What is Law of Torts" then anapata SUP...U can Only find in TZ..

2. Serikali Makini ambayo sio dhaifu ina Watumishi Hewa 9,949 wanaopata Mshahara ambao Jumla ya hela inayopotea ni kama Bil 70 ambazo zingetumika kulipa Madaktari na walimu, lakini Serikali inasema haina hela, hawana hela ya kulipa walimu na Madaktari ila wanazo za Watumishi hewa...Only u can find in TZ.

3. Serikali Ya Uingereza Ilirudisha Chenji ya RADA, Serikali ikasema hela inapeleka Kununulia Vitabu kwa Ajili ya Shule Nchi nzima, Kumbe Kampuni iliyopewa tenda ya Kusambaza Vitabu nchi nzima ilitoa rushwa ya dola 500,000 kupata tender Serikali ya Uingereza imeifungia miaka 7, You Can Only find in TZ.

4. Wanafunzi Waliofaulu Darasa la Saba (get me well waliofaulu darasa la 7) kwenda Sekondary Hawajui Kusoma wala Kuandika, Je waliofeli Watakuwa hawajui kufanya nini...You Can Only Find In Tanzania

5. Washiriki wa Michezo ya Kimataifa (sijataja Mchezo wala mashindano) wako watano (5) lakini wanaowasindikiza Washiriki wako 12, na kurudi bila medali hata moja. You can Only find in Tanzania......

6. Sehemu Pekee ambaye Mtu uliyetaka Kumdhuru kwa Kukusumbua then unaomba Umlinde (refer to Ulimboka's Case)..Yaani Mbwa Mwitu anaomba kazi ya Kulinda Mbuzi......You Can Only find in Tanzania.."

7. ......ongezeeni

1. Nchi inayojitapa kuwa ina serikali sikivu lakini serikali hiyo haitaki kusikia au kuongea na makundi yenye madai na kukimbilia kuwaziba sauti watu wake mahakamani ili isiwasikie.

2. Nchi yenye raisi asiye jua chanzo cha umasikini wa watu wake. Kumbuka ile kauli ya jk alipo hojiwa na mwandishi wa france.

3. Nchi yenye raisi ambaye amesha wahi kuwaomba wezi wa fedha kurudisha walichoiba huku wezi wa ndala na wakwapua simu wakipigwa ban (kuchomwa moto).

4. Nchi yenye usalama unaoruhusu ndege ya nchi nyingine kuingia kwenye anga yake kuja kubeba wanyama hai walio ibiwa na viongozi waandamizi wa serikali.

5. Nchi yenye bunge lenye spika ambae akitaka hoja iungwe mkono akiwahoji watu sauti za siooooo zikiwa kubwa kuliko ndio walio sema ndio hata kama ni wachache wanashinda. Kumbuka hoja ya wenje jana.

6. Nchi ambayo mnajimu mkuu ameshawahi kutangaza kumlinda raisi kwa ulinzi usio onekana. Achilia mbali ule wa vifaru na mizinga.

7. Nchi ambayo wakati wa uchaguzi viongozi wa chama tawala huwatishia watu kuhusu kuingizwa nchini makundi ya kigaidi huku wakijua kuna vyombo vya usalama.

Kuwa na serikali ya umoja wa kitaifa ktk upande mmoja wa nchi

Bunge linalopitisha sheria kama ile ya mafao ya kujitoa na baadae wanakuja kuishangaa.

can only happen in tanzania bana!

Nchi yenye mkulu asiyeweza kujibu maswali ya papo kwa papo, mpaka aandae majibu yake. only can be found in TZ

Kuwa na rais aneyeweza kwenda kushangaa mashamba ya mananasi nchi nyingine wakati geita,bagamoyo yamejaatele

kuwa na rais aneyeenda kushangaa kilimo cha nyanya brasili wakati nchini kwake zinaozea masokoni kwa kukosa soko.

Can only happen in tansania bana!

ONLY IN TANZANIA....

Waziri Mkuu kila Alhamisi bungeni kwenye maswali ya papo kwa papo majibu yake huanzia na sentensi hizi:

Nadhani....

Nafikiri....

Tuliona tuliweke hivi...

Tumeliona hilo...

Sina hakika sana...

Tuliache kama lilivyo...

Hili jambo lipo mahakamani.....

Wagombea wanaomba kura kwa kupiga magoti wakifanikiwa wewe uliyepigiwa magoti unawaita WAHESHIMIWA na kuwasujudia
wacko.gif

kujivunia ni kisiwa cha Amani mpaka Rais kutabasam/kucheka kwenye misiba yenye majonzi .. only in TZ
 
Open Univ inasaidia sana. Rais Karume (mstaafu) alikuwa akisoma pale, sijui kama alimaliza au la. Shamuhuna naye aligraduate pale mwaka juzi nk. Wazee wanapiga miasainimenti, matesti, matekihome, mayuii, masaplimentari kama kawaida. Jaji naye anagonga msuli.
 
Na ajabu jingine wananchi kutotaka kuondoa serikali yao kwa maunafki ya amani na utulivu ambao aupatikani nchi yoyote duniani ajabu jinginge ni Rais wa nchi kuvunja rekodi mpaka yake mwenyewe ya kusafiri nje ya nchi kaka nchi inamaajabu ambayo nadhani ayajawahi tokea hapa duniani hata huko kwa mungu ambako atupajui na sidhani kama yatakuja tokea mpaka dunia iishe.
 
Kuwa na chama cha upinzani ambacho upande wa pili wa Muungano (Zanzibar) hakina hata sheha (mjumbe wa nyumba kumi), wala muwakilishi hata mmoja wala mbunge hata mmoja. Halafu kinaamini kabisa hicho ndio chama mbadala cha Watanzania...kwi kwi kwi teh teh teh!
 
Kuwa na chama cha upinzani ambacho upande wa pili wa Muungano (Zanzibar) hakina hata sheha (mjumbe wa nyumba kumi), wala muwakilishi hata mmoja wala mbunge hata mmoja. Halafu kinaamini kabisa hicho ndio chama mbadala cha Watanzania...kwi kwi kwi teh teh teh!

vipi pemba mnao wangapi?
 
Open Univ inasaidia sana. Rais Karume (mstaafu) alikuwa akisoma pale, sijui kama alimaliza au la. Shamuhuna naye aligraduate pale mwaka juzi nk. Wazee wanapiga miasainimenti, matesti, matekihome, mayuii, masaplimentari kama kawaida. Jaji naye anagonga msuli.

Kwenye red mzee, kama kuna siku nimecheka basi siku ya leo nayo imo kwenye zilizotia fola! Wonderful
 
Kuwa na chama cha upinzani ambacho upande wa pili wa Muungano (Zanzibar) hakina hata sheha (mjumbe wa nyumba kumi), wala muwakilishi hata mmoja wala mbunge hata mmoja. Halafu kinaamini kabisa hicho ndio chama mbadala cha Watanzania...kwi kwi kwi teh teh teh!
Hii ndio Tanzania bana!!! Kwi kwi kwi kwi!!!
 
5. Washiriki wa michezo ya kimataifa (sijataja mchezo wala mashindano) wako watano (5) lakini wanaowasindikiza washiriki wako 12, na kurudi bila medali hata moja.

yapo tanzania tu, hiyo point ya tano ukiwauliza wanajijitetea kati ya nchi 54 zilizoshiriki mashindano, only 10 ndo wamepata kitu wengine wote hatujaambulia kitu, hatuko peke yetu. Ha ha ha ha,....you can only find such answers in tz
 
Hii ndio Tanzania bana!!! Kwi kwi kwi kwi!!!

kweli only in tz:
1. Kubadilishana vyandarua+walimu 47 kwa dhahabu, almasi, tanzanite na wanyama pori. Only in tz.
2. Kupandisha twiga kwenye ndege,can only be done in Tanzania.
3. Rais, Waziri mkuu, Mwanasheria mkuu, na Waziri wa katiba kupingana hadharani wakati wanakaa meza moja ya baraza la mawaziri. This is definately in Tz n only in Tz...
3. Kuwa na wanachama uchwara wanaoendekeza siasa za majitaka za C C Mabwepande.. Can only b found in Tz.
 
Back
Top Bottom