Only in Tanzania !

Ni nchi ya pili kwa kuwa na vivutio vingi vya utalii duniani rudia duniani lakini haipo hata 100 bora kwa kuingiza watalii nchini eti tumezidiwa hata na kenya na burundi.chezea bongo wewe tupo tupo tu
 
Kuwa na chama cha upinzani ambacho upande wa pili wa Muungano (Zanzibar) hakina hata sheha (mjumbe wa nyumba kumi), wala muwakilishi hata mmoja wala mbunge hata mmoja. Halafu kinaamini kabisa hicho ndio chama mbadala cha Watanzania...kwi kwi kwi teh teh teh!
Wewe nawe ni ajabu lingine la dunia, kuona hilo ndilo jambo baya zaidi kuliko wizi wa rasilimali zetu, udhaifu wa M.k.w.e.r.e na serikali yake, rushwa na ufisadi, kupanda kwa gharama za maisha, hali tete ya amani, viongozi kutokuwa na sera na mikakati maalumu ya kushughulikia matatizo yanayowakabili wanachi, ujangili, etc. Hivi chama cha upinzani kikiwa na sheha huko Zanzibar ndio ugumu wa maisha na matatizo ya wanachi wa Tz yataisha? Ninyi mlio na hao viongozi huko mbona ndio chanzo cha matatizo yote ya nchi hii? Sasa tofauti ya wale ambao hawana viongozi Zanzibar na ninyi mlio na hadi mashehe achilia mbali masheha, ni nini? Unazi mwingine bwana, wewe Zomba ni mojawapo wa maajabu ya dunia hii! Itabidi tukupigie kura! Shwaini!
 
Spika wa Bunge kumpongeza Waziri kwa kufanya vizuri katika kazi yake(MAKINDA AKIMPOGEZA MWAKYEMBE) .nilijua uliposema treni itakuwa njiani yalikua ni mambo ya PWAGU na PWAGUZI,utayakuta TZ.
 
Haya ndio maajabu ya Tz
1.Watoto kufaulu hawajui kusoma wala kuandika.
2. Marehemu kupiga kura kwenye BMK
3. Rais Mzururaji kuliko wote duniani.
4. Mbunge awe na uwezo wa kusoma na kuandika tu,hata kama aliishia darasa la pili ilimradi anajua KKK
5.Uwajibikaji,uwazi,uzalendo na ukweli ni vitu visivyotufaa hivyo viondolewe.
6. Rais ambaye hata nukuu zake haziwezi kuwekwa katika vitabu vya kumbukumbu et unaweka nukuu kama hii" ukitaka kula lazima uliwe"
7. Rais,makamu na waziri mkuu wapo kama hawapo.
 
Yapo Maajabu mengi sana...Ila Maajabu ya Wiki Hii Yaliyo Tanzania ni kama Ifuatavyo

1. Mmoja wa Majaji Walioteuliwa kwa Mujibu wa Tundu Lissu Kumbe ndo kwanza anasoma shahada so darasani nae anasoma"What is Law of Torts" then anapata SUP...U can Only find in TZ..

2. Serikali Makini ambayo sio dhaifu ina Watumishi Hewa 9,949 wanaopata Mshahara ambao Jumla ya hela inayopotea ni kama Bil 70 ambazo zingetumika kulipa Madaktari na walimu, lakini Serikali inasema haina hela, hawana hela ya kulipa walimu na Madaktari ila wanazo za Watumishi hewa...Only u can find in TZ.

3. Serikali Ya Uingereza Ilirudisha Chenji ya RADA, Serikali ikasema hela inapeleka Kununulia Vitabu kwa Ajili ya Shule Nchi nzima, Kumbe Kampuni iliyopewa tenda ya Kusambaza Vitabu nchi nzima ilitoa rushwa ya dola 500,000 kupata tender Serikali ya Uingereza imeifungia miaka 7, You Can Only find in TZ.

4. Wanafunzi Waliofaulu Darasa la Saba get me well waliofaulu darasa la 7 kwenda Sekondary Hawajui Kusoma wala Kuandika, Je waliofeli Watakuwa hawajui kufanya nini...You Can Only Find In Tanzania

5. Washiriki wa Michezo ya Kimataifa (sijataja Mchezo wala mashindano) wako watano (5) lakini wanaowasindikiza Washiriki wako 12 You can Only find in Tanzania......

6. Sehemu Pekee ambaye Mtu uliyetaka Kumdhuru kwa Kukusumbua then unaomba Umlinde (refer to Ulimboka's Case)..Yaani Mbwa Mwitu anaomba kazi ya Kulinda Mbuzi......You Can Only find in Tanzania..

Yapo Maajabu Mengi sana Lipi nimesahau???
naomba nikujibu namba 4, waliofeli ni wale ambao walipata mimba kwa viherehere vyao na hawajui hata shule ilipo kwahiyo siku ya mtihani hawakwenda kufanya
 
Nchi pekee inayokata PAYE kwa watumishi wote pamoja na walimu lakini inakata tena take home za walimu kwa ajiri ya ujenzi wa maabara shule za kata. Only Tanzania
 
yapo tanzania tu, hiyo point ya tano ukiwauliza wanajijitetea kati ya nchi 54 zilizoshiriki mashindano, only 10 ndo wamepata kitu wengine wote hatujaambulia kitu, hatuko peke yetu. Ha ha ha ha,....you can only find such answers in tz

Mcba wa wengi ni haruc
 
ONLY IN TANZANIA....

Waziri Mkuu kila Alhamisi bungeni kwenye maswali ya papo kwa papo majibu yake huanzia na sentensi hizi:

Nadhani....
Nafikiri....
Tuliona tuliweke hivi...
Tumeliona hilo...
Sina hakika sana...
Tuliache kama lilivyo...
Hili jambo lipo mahakamani.....



Ha-ha-ha-haa-hah-hah!
 
Nchi ambayo wenye akili ndogo ndio wanachuguliwa kuongoza nchi na wenye nyingi hawachaguliwi
 
Nchi ambayo raisi anaenda kufungua wodi mahususi ya EBOLA na kuwasifu wahusika halafu kuwashauri wahakikishe maji yanatoka maana aliona maji hakuna. Usiulize gharama za hio wodi ilikua sh ngapi.

Nchi ambayo kiongozi wake anajisifu kwa kuomba na kupewa misaada kutoka nchi za nje! Kwakweli hili nitamshangaa mpaka kufa!
 
Back
Top Bottom