Hivi Magobe unaujua Ukatoliki vizuri au unafuata mkumbo tu ndugu yangu?
1. Je unajua ya kuwa amri kumi za MUNGU wakatoliki wamezibadilisha kwa kuondoa ile ihusuyo kuchonga sanamu na kuigawa mara mbili ile ya kumi ili ku-maintain namba kumi?
2. Unajua kuwa mafundisho ya wakatoliki ni kwamba Maria baada ya kumzaa YESU hakuzaa watoto wengine (uongo wa wazi)?
3. Unajua mafundisho ya wakatoliki ni kuwa hakuna kuokoka duniani (denial to what JESUS brought to humankind)?
4. Unajua wakatoliki hawakubaliani na matendo makuu ya miujiza ya MUNGU?
5. Unajua ya kuwa wakatoliki wanaamini kuwa pombe ni sakrament takatifu (quote from Pengo).
6. Unajua zinaa kwa wakatoliki ni halali tu na ndo maana tunaona vijana wanafungishwa ndoa huku mdada wa watu akiwa hoi na mimba ya miezi nane
etc.
Je bado utasema hii dini ni ya MUNGU kweli au inamfuata shetani kwa umbrella ya Ukristo?
etc.
Haya yote ni garbage!
1. Je unajua ya kuwa amri kumi za MUNGU wakatoliki wamezibadilisha kwa kuondoa ile ihusuyo kuchonga sanamu na kuigawa mara mbili ile ya kumi ili ku-maintain namba kumi?
Wakatoliki hawakuondoa Amri yoyote. Huo ni uongo mkubwa. Biblia ina Amri zote Kumi za Mungu. Kilichofanyika ni kuziandika kwa namna zinavyoweza kukumbukwa katika 'catechesis'. Mfano, unapomfundisha mwanafunzi ili aweze kukumbuka vizuri unatumia 'summary form' na kumpa 'refence' ili aweze kwenda kwenye chanzo mwenyewe.
Katika mafundisho, of course, Kanisa haliwezi ku'reproduce' Biblia nyingine. Ila inatumia 'summary' ili iwe rahisi kwa wale wanaofundishwa kuelewa. Kwa hiyo, Kwenye Katekismu (yaani, kitabu kinachotoa 'summary' ya mafundisho makuu ya imani na 'reference' zake) vitu vimeelezwa kwa kifupi lakini kama mtu anataka kujua uhalisia wake anasoma kwenye Biblia yenyewe.
2. Unajua kuwa mafundisho ya wakatoliki ni kwamba Maria baada ya kumzaa YESU hakuzaa watoto wengine (uongo wa wazi)?
Baada ya kumzaa Yesu, Maria hakuzaa watoto wengine kutokana na mapokeo (watu waliorithishwa maelezo kuhusu maisha ya Maria). Biblia imesema ndugu/jamaa zake Yesu - haikusema watoto wa Maria. Na katika jamii yao kaka/ndugu/jamaa ilikuwa inatumika pia katika maana jinsi tunavyoitumia sisi.
Mfano, mtu anasema "huyu ni dada yangu" na ukimwuliza ni dada tumbo moja na wewe? Anasema hapana, "ni mtoto mjoma, wa mama mkubwa/mdogo au wa baba mkubwa/mdogo. Kitu ambacho ungeweza kusema ni kwamba katika ku'interpret' baadhi ya vifungu vya maandiko matakatifu jumii moja ya watu inaweza kutofautiana na nyingine katika kile kinachoitwa 'schools of thought'.
Mfano, lugha zilizotumika katika tafsiri za Biblia mpaka tupate nakala tulizo nazo kwa Kiswahili leo ni Kiebrania na Kigriki, Kilatini, Kifaransa, Kiingereza na Kiswahili (na lugha zingine za kibantu kama Kihaya, Kisukuma, Kikerewe, nk walau kwa hapa Tanzania). Ukumbuke kuwa Yesu alitumia lugha ya Aramaic na waandishi wa mwanzo waliandika kwa Kiebrania na Kigriki kutegema 'adressees' wao.
Na pia kumbuka siku moja mama na "jamaa zake Yesu" walikuwa wanamtafuta na wakati huo alikuwa hekaluni akiwafundisha watu. Mara wakampekelea ujumbe kuwa anahitajika na mama yake na ndugu zake. Yeye akawauliza "Mama yangu na ndugu zangu ni nani? Ni wale wanaolisikia Neno la Mungu na kulishika. Hao ndio mama yangu, ndugu zangu..."
Je, unataka kwa kusema hivyo, kila anayelishika Neno la Mungu alimzaa Yesu au ni ndugu wa damu kabisa na Yesu au ni 'metaphor'? My friend, when reading the Bible don't be lost in the morphology of the narrative but what is behid it - the meaning of it.
3. Unajua mafundisho ya wakatoliki ni kuwa hakuna kuokoka duniani (denial to what JESUS brought to humankind)?
Understanding ya Wakatoliki na siyo denial ni kwamba Mungu ndiye anayewaokoa watu. Na huyo Mungu anawakoa hao watu muda wowote (wanapotubu na kutenda mema anyotaka) hapa duniani na pia hata baadaye watakapoenda Mbinguni. Kanisa linapinga wanaojifanya wameokoka na hali matendo yao ni ya kibaguzi, kudharau wengine, kudhani kuwa ni wao tu wanaomjua Mungu na kumtumikia kama Mungu anavyotaka.
Hawa hawajaokoka chochote! Waliookoka wanaonekana kwa matendo yao na hawahitaji mapaka waseme wameokoka. Hawa wana upendo wa kweli, ni wanyenyekevu na kweli Mungu yu pamoja nao. Wanaweza wakawa baadhi ya Walokole au dhehebu jingine lolote. Cha muhimi hapa ni neema ya Mungu ndani ya mtu na siyo 'lebal' (kuokoka au Ulokole). No one acan monopolise or domesticate God! God is for all and blesses anyone who accepts his Word and live by it.
4. Unajua wakatoliki hawakubaliani na matendo makuu ya miujiza ya MUNGU?
Siyo kweli pia! Wakatoliki wanaamiini miujiza inatendeka na kwa namna nyingi! Ila Kanisa Katoliki haliamini miujiza inayouzwa, inayotumiwa kuwarubuni watu na mtu kujifanya Mungu mdogo au kuwa fulani anaupendeleo na anaongea na Mungu 'direct'. Kitu ambacho Kanisa linafanya ni 'caution' - kuwa mwangalifu la sivyo mtu anaweza kuamini hata garbage.
Kuponywa ni matakwa ya Mungu na siyo mpaka fulani aseme 'pona'. Kama miujiza tunayosikia ni ya kweli, basi hapa duniani kusingekuwapo na haja ya kuwa na hospitali na ukimwi usingemaliza ndugu zetu kiasi hicho. Hata tusingeishi kwenye umaskini wa kupindukia kiasi hiki.
Maana watu wangeenda tu kwa hao watenda miujiza na kuponywa mara moja. Sasa hospitali zinajengwa kwa nini? Kanisa Katoliki linaaamini Mungu amewaumba binadamu na kuwashirikisha katika uumbaji wake (kupitia 'marriage institution') na pia katika matendo mema na vipaji vya watu (wengine waponyaji wa kweli).
Ndiyo maana kuliko kuamini tu fulani ana kipaji cha uponyaji, Kanisa lina namna yake ya kuthibitisha - mfano, unyenyekevu na imani ya huyo mponyaji na upendo wake na maisha yake kwa ujumla. Lakini kama mponyaji anaanza kutumia uponyaji wake kama nguvu yake mwenyewe na kuanza tabia za ajabu ajabu (kama kichaa), Kanisa haliamini uponyaji huo unatoka kwa Mungu hata kidogo!
5. Unajua ya kuwa wakatoliki wanaamini kuwa pombe ni sakrament takatifu (quote from Pengo).
Katika Biblia kitu ambacho hakikukatazwa directly, Kanisa linatoa msimamo wake na kuwaacha waamini wachague wao wenyewe kipi kinafaa. Mfano, ndani ya Kanisa katoliki kuna jumuia za Wakristo hawanywi pombe wala kuvuta sigara.
Ni vizuri. Lakini kuna wanaokunywa pombe na kuvuta sigara ila kwa hawa Kanisa linawataka waangalie pombe na sigara zisiwafanye watende dhambi, waharibu afya zao au wawe maskini na kushindwa kutunza familia zao. Kwa mtu anaykunywa pombe au kuvuta sigara hata kula chakula Kanisa linasema lazima kuwe na kiasi (moderation). Kwa hiyo, siyo kweli kwamba Kanisa linaamini pombe ni sakramenti. Hiyo ni 'formulation' yako tu.
6. Unajua zinaa kwa wakatoliki ni halali tu na ndo maana tunaona vijana wanafungishwa ndoa huku mdada wa watu akiwa hoi na mimba ya miezi nane etc.
Haya sasa ni mawazo yako. Kanisa liko 'strict' katika ndoa. Wanaofungishwa ndoa wakiwa wajawazito mara nyingi huwa ni wale walioficha kama mdada ni mjamzito au Kanisa limeona pamoja na kwamba mdada ni mjamzito wahusika wamekiri hivyo na wameomba waoane. Kwa sababu kinachomfanya mtu kuwa mdhambi siyo ujauzito bali ni tendo baya linaloharibu uhisiano kati yake na Mungu na watu wenzake.
Lakini pia kuna kujirekebisha. Tuchukue mtu amezini halafu akatubu na akasema amekosa na anaomba asamehewe. Mungu atamsamehe huyo mtu. Lakini je kama mtu amezini na kutubu na kama baadaye akagundua ni mjamzito kwani mimba huwa inatoka? Hapana!
Ndiyo maaana hata kama huyo mdada kutokana na uzinzi wake amepata ujauzito na kama ametubu na kulihakikishia Kanisa ametubu litamruhusu aendelee na imani yake. Kwani hao wanapjiita wameokoka huwa wameokaka kutoka nini kama hawajakosa? Je, mdada mjamzito akiokoka huwa mnamkataa? Na lini mnaamini mtu huokolewa muda wowote au ni baada ya kujifungua?
Je bado utasema hii dini ni ya MUNGU kweli au inamfuata shetani kwa umbrella ya Ukristo? etc
Hata kuwahukumu wengine ni dhambi tayari - ni kumfuata shetani! Kwa hiyo, kusema tu hayo uliyosema hakuwezi kulifanya Kanisa Katoliki (Wakatoliki wote duniani au Tanzania wawe wanamfuata shetani na eti Walokole kama na wewe ni mmojawapo) wawe tu ndio wanaomfuta Mungu wa kweli. Imani ni zaidi tu ya kufikiri na kusema. Imani maana yake ni nguvu ya Mungu na namna Mungu mwenyewe anavyowaongoza binadamu kama anavyotaka yeye.
Hivyo, kipimo chako cha wokovu siyo kipimo cha Mungu na mtazamo wako kwa Kanisa Katoliki siyo mtazamo wa Mungu. Ninachoweza kusema ni kwamba: we are all striving to serve God in truth. Certainly, we'll differ in many things but as long as it is God who serves no one can judge others as unworthy while he or she is also to be judged by God whether he or she has honestly served Him in truth.
Kwa hiyo, mheshimiwa: imani siyo tu unayoweza kusema kuhusu dini au dhehebu la wengine bali jinsi wewe mwenyewe unvyoishi na kumpendeza Mungu katika haki na ukweli.