Nisaidieni wazazi wangu hawataki nimwoe mmachame

Ndugu zangu wana jf naomba ushauri kwani nilikuwa na mahusiano na mrembo wa kichaga nilimpenda nae alinipenda sana
sasa niliamua kwenda kumtambulisha kwa wazazi. wazazi wanasema kamwe hawakubaliani kumuoa mchaga wa machame
eti baada ya mwanaume kuwa na mali huwa wanauwa waname. Je hoja hii ina ukweli kwa wale wanao wafahamu vizuri?
Hayo ni mambo ya kizamani sana mkuu, waeleweshe wazazi, zamani zile mambo sio kama ya sasa hivi, nina marafiki zangu wamachame na majirani wako vizuri tu na waume zao na wanaishi kwa amani naupendo, wifi yangu pia mmachame yuko fresh tu na bro wangu miaka mingi tu....usiwe na wasiwasi wala papara kaa nao chini waambie huyo ndiye uliyepangiwa na Mungu watakuelewa tu
 
Wamachamee! Twapataje tabu na hayo maswali ya kuua na kuchukua mali? Kweli km hujapata mchumba iko kazi ktk kumpata, kuolewa na kuishi! Anyway...am proud to be Mmachame!

Kila mtu lazima awe proud na alivyoumbwa na alichoumbiwa..............am proud......very very proud to be CHAGGA,uniite wa marangu,machame,kibosho,uru,rombo nk. the truth remain kwamba mimi ni Mchaga bana!.......

Unajua huwa inaanza...sisi wamarangu,wao wakibosho,alafu inafuata...sisi wachaga,wao wahaya.......kisha inakuja......sisi wa.....................

TUACHE UBAGUZI!

Ndugu zangu wana jf naomba ushauri kwani nilikuwa na mahusiano na mrembo wa kichaga nilimpenda nae alinipenda sana
sasa niliamua kwenda kumtambulisha kwa wazazi. wazazi wanasema kamwe hawakubaliani kumuoa mchaga wa machame
eti baada ya mwanaume kuwa na mali huwa wanauwa waname. Je hoja hii ina ukweli kwa wale wanao wafahamu vizuri?
Inawezekana ikawa ni imani za kizamani tu ndugu yangu. Siku hizi mali haziwi kwa mwanaume peke yake. Tena inawezekana huyo mwanamke akawa na mali nyingi kukuzidi wewe. For that case, akuuwe kwa sababu ipi?
 
Fanya uchunguzi kabla ya kuchukua uwamuzi wowote ukiona hakuna ukweli wwote kaa chini na wazazi wako washawishi kwa hoja madhubuti mwisho utapata uamuzi sahihi
 
Fanya uchunguzi kabla ya kuchukua uwamuzi wowote ukiona hakuna ukweli wwote kaa chini na wazazi wako washawishi kwa hoja madhubuti mwisho utapata uamuzi sahihi

Jamani kuna user name zingine..mh! ...Mkuu mtu ukimshauri na hiyo user name yako si anaweza ogopa kusoma tena thread..
 
Kama unapenda maisha yako na unapenda ndoa yenye amani sikiliza maneno anayokuambia mama yako wamachame noma
 
Kama unapenda maisha yako na unapenda ndoa yenye amani sikiliza maneno anayokuambia mama yako wamachame noma

Toa takwimu inayoonyesha kuwa ndoa zote zenye matatizo zina wake wamachame
Toa takwimu zinazoonyesha kuwa ndoa zote ambazo waume wamefariki,wake zao ni wamachame
 
wewe unaishi dunia ipi? ungewauliza wana data zinazonyesha ni wanawake wangapi wakimachame wameuwa waume zao baada ya kufanikiwa? Hakuna hata chembe ya ukweli katika hilo,

unachotakiwa utambue anayeoa ni wewe na sio wazazi wako, walipokuambia hivyo ilikuwa ni fursa pekee ya kuwaelimisha kuhusu huo mtizamo wao mbaya.

kale kamsamiati ketu mkuu...lisemwalo lipo...
 
Ndugu zangu wana jf naomba ushauri kwani nilikuwa na mahusiano na mrembo wa kichaga nilimpenda nae alinipenda sana
sasa niliamua kwenda kumtambulisha kwa wazazi. wazazi wanasema kamwe hawakubaliani kumuoa mchaga wa machame
eti baada ya mwanaume kuwa na mali huwa wanauwa waname. Je hoja hii ina ukweli kwa wale wanao wafahamu vizuri?

Kamuulize mzee Ben inakuwaje? atakupa ushauri mzuri tu...
 
Haya ni maneno tu,pesa tunazo kwa nini tuue kwa ajili ya pesa?kwa hyo wewe watu wanavyosema wamakonde wanakula watu unaamini?waambie wazazi wako waache mitizamo ya ajabu haya mambo hayapo,issue sio umachame ni tabia ya m2 je huyo dada unavyomuona ana tamaa ya mali?alishakufanyia ukatili wowote?
 
Vipi kaka wewe ni kabila gani? Hizi kasumba zipo sana kwani kuna jamaa alipata mchumba wa kichaga, watu wakamuuliza "unataka kuoa mchaga?", kilichofuatia alibwaga manyanga, baadaye alimpata mpare, akaambiwa nao ni walewale, jamaa alisonga mbele na akaja akapata binti wa tanga, bado walimwambia tanga ipo karibu na k'njaro. Lakini baadaye wakaja kumwambia kwamba mabinti wote huku huwaoni?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom