Nisaidieni wazazi wangu hawataki nimwoe mmachame

damashizo

Member
Jan 20, 2011
61
15
Ndugu zangu wana jf naomba ushauri kwani nilikuwa na mahusiano na mrembo wa kichaga nilimpenda nae alinipenda sana
sasa niliamua kwenda kumtambulisha kwa wazazi. wazazi wanasema kamwe hawakubaliani kumuoa mchaga wa machame
eti baada ya mwanaume kuwa na mali huwa wanauwa waname. Je hoja hii ina ukweli kwa wale wanao wafahamu vizuri?
 
wewe unaishi dunia ipi? ungewauliza wana data zinazonyesha ni wanawake wangapi wakimachame wameuwa waume zao baada ya kufanikiwa? Hakuna hata chembe ya ukweli katika hilo,

unachotakiwa utambue anayeoa ni wewe na sio wazazi wako, walipokuambia hivyo ilikuwa ni fursa pekee ya kuwaelimisha kuhusu huo mtizamo wao mbaya.
 
Jamani hakuna ukweli hata kidogo wamachame wanatiwa doa2, kweli wazazi wanatakiwa kushirikishwa kwenye ndoa na wana haki yakukata ikiwa wana sababu za msingi sio kama hizo.
 
Mkuu, kila mtu atakufa, lakini hili suala hapo mbele litaleta matatizo makubwa kama wewe utatangulia kufa. Hapo patatokea mgawanyiko mkubwa ktk familia haswa kama utakuwa na watoto. Mapenzi nimaamuzi binafsi lakini tuangalie hapo mbele itakuaje, jaribu kuwaelewesha wazazi kama watakubali itakuwa vizuri zaidi ikishindikana basi wasikilize wazazi mkuu.
 
hapo mkuu uwamuzi ni wako but jitahidi kupata radhi toka kwa bi mkubwa (mama yako ) ... mara nyingi kina mama wanakuwa na moyo mwepesi kubadillishwa mawazo na watoto wa kiume sansana katika jambo la kheri kama ndoa.. kuwa karibu sana na mama! baba itakuwa ngumu kubadili msimamo

ikishindikana nenda kwa kiongozi wa dini ajaribu kuongea na wazazi wako!

jitahidi kuangalia kama tabia zenu weye na huyo binti kama zinaendana ... wajuwa waswahili tuna ule usemi ( TULIMWAMBIAA HAKUTUSIKILIZA)

Good luck!
 
wazazi wanasema kamwe hawakubaliani kumuoa mchaga wa machame
eti baada ya mwanaume kuwa na mali huwa wanauwa waname.

Duh....kwani wanaoa wazazi au wewe... hebu jiulize mwenyewe..kwa bahati mbaya wazazi wakiondoka kesho utaoa huyo bint au utaendelea kuweweseka na usia na wosia uliopitwa na wakati..

..Ngo ngo ngo..Zinduka!
 
Ndugu zangu wana jf naomba ushauri kwani nilikuwa na mahusiano na mrembo wa kichaga nilimpenda nae alinipenda sana
sasa niliamua kwenda kumtambulisha kwa wazazi. wazazi wanasema kamwe hawakubaliani kumuoa mchaga wa machame
eti baada ya mwanaume kuwa na mali huwa wanauwa waname. Je hoja hii ina ukweli kwa wale wanao wafahamu vizuri?

Hizi ni hisia tuu na sidhani kama kuna ukweli katika hili
Mbona wapo wanawake wengi sana wa kimachame wameolewa na wanaume mbalimbali na ndoa zao zinadumu na hao wanaume wao hawajafa
Nina kaka yangu ameoa mmachame na sasa ni mwaka wa 25 wako pamoja na wamechuma mali kibao
Jaribu kukaa na wazazi wako uwaeleweshe maana wewe ndiye muoaji na sio hao wazazi wako na waambie hiyo ni imani na kitu ambacho watu wanajaribu kukizusha
Unaweza kupata mke labda ametokea sumbawanga ukaambiwa Sumbawanga kule wachawi sana ila ukweli halisi sio huo. Kitu ambacho kimefanywa na mtu mmoja kisiwe ndio tabia ya kabila au ukoo mzima
 
Kaka hao watu manatisha, ushaidi ninao, usije ukajuta siku za mbele. Chukua hatia. Asiyesikia la mkuu...........!
 
Hamna ukweli wowote! Hizo zamani zilikuwa propaganda za wakibosho dhidi ya wamachame kutokana na ugomvi uliokuwepo baina yao!Siku hizi Wanaoana vizuri na ndoa zinadumu!Kwa hiyo ukimpata mmachame oa tu, ni wachapa kazi na wanapenda maendeleo!
 
Ukimuacha huyo utaregreat 4 the rest of ur miserable life hakuna wanawake mafighter katika maendeleo kama wamachame na mfano mzuri kati ya wanaume wote wenye mafanikio hapa nchini wameoa wamachame Mengi reginald mkewe mmachame nadhani huhitaji kujiumiza kichwa kujua mafanikio yake Mbowe wa Chadema mkewe mmachame unaona alipo sasa bora ugombane na wazazi kuliko kwenda kuoa mwanamke asiye chaguo lako kumbuka wazazi kazi yao walishamaliza na wataondoka utabaki wewe na maisha yako kuna mshlj wangu ilikuwa kama wewe akamuacha dada wa watu akaenda kuoa mchaga wa kibosho kiruu chaaa anajuuta saa hizi kazi yao kubwa ni kuachana na kurudiana yaani mara 3 kwa mwaka wanaachana kila siku kesi haziishi na hata bajaji hajanunua kikorola alikuwa nacho kabla alikiuza na hajui hela iliishia wapi fikiria chukua hatu!!!
 
Si wako bize na kuendesha kesi zao kila siku badala ya kupanga maendeleo ya familia,sasa maendeleo yatatoka wapi ndugu yangu.
Hapo simuhukumu mkibosho,namtazama kama mwanamke yeyeyote na kama binadamu mwingine lazima ana mapungufu yake.
Kumbuka jamaa alio ASIYEMPENDA,chaweza kuwa chanzo cha ugomvi pia.
 
wamachameeeee!!!

Tupooooooooo!!!..............Tena ningekuwa mimi natafuta mwenye pesa kabisa,nikishampata tu ......wanazika......sitaki tabu za dunia eti mpaka nikaishi naye weeee,mpaka apate mali ni leo?...(ukizingatia mi nitakuwa nimekaa tu nyumbani)nasubiri azitafute ili nimuue.Hii itanipotezea muda.
 
hahaha Kekuu!
 
Kaka hao watu manatisha, ushaidi ninao, usije ukajuta siku za mbele. Chukua hatia. Asiyesikia la mkuu...........!
acha ushabiki wa ki......! Huo ushahidi unaosema aliuawa babako au wewe mwenyewe? Mxx!!
 
Nenda mahakama ya hai-kilmanjaro uliza kesi za mauwaji zilizopo mbele ya hakimu au mtafute mama ANANILEA NKYA muulize kwasababu nayeye ni waukouko kwa wanawake wapiganaji.jibu utapata acha kusumbua wa2 na ao wazaz wako vilaza
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom