Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
20,721
45,129
Kuna wimbo mpya umetoka. Si mwingine ni kijana wetu, Roma Mkatoliki.

Wimbo unaitwa "Nipeni Maua Yangu" humo ndani kuna madini ya kutosha. Roma Mkatoliki kama kawaida yake katoa ya moyoni yanayoendelea katika utawala huu wa awamu ya 6. Kama kawaida kanyoosha maelezo hajapindapinda.

Hakika baada ya kuusikiliza nampa maua yake ayanuse angali akiwa hai.

Ni mstari upi umekuvutia zaidi? Tushirikishe hapa...



Maua yangu.png
 
1. Jeshi gani mpaka leo Mmeshindwa kumjua Kigogo
2. Mbona vyuma vimekaza halafu mama anaificha grisi
3. Tulihoji mkajibu kwa dharau tuhamie Burundi
4. Iringa tuna msitu lakini stick tunaagiza China
5. Mnatuambia tujiajiri mbona nyie hamkujiajiri? Ok nikupe boda yangu unipe uwaziri. Nikukabidhi vyeti vyangu hangaika navyo mwezi mmoja, niko pale nakungoja uje tuzungumze lugha moja😂😂
 
"Nchi gani raia akihoji mnasema anakosoa na akikosoa mnasema anatukana serikali"

"Mnatuambia tujiajiri mbona nyinyi hamkujiajiri nikupe boda yangu nawe unipe uwaziri? Nikukabidhi vyeti vyangu uangaike navyo mwezi mmoja niko pale nakungoja uje tuongee lugha moja."

Anakwambia "mi sio CCM sio Chadema, ila ukiweka CCM na andazi ntachgua andazi".

haya sikilizeni na nyinyi Ngoma


Roma ft Abiud Maua yangu.

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom