Nini mustakabali wa siasa za Tanzania na vikundi vya "Wanamgambo" wa Vyama?

Mimi napendekeza mpango wa kuimalisha ulinzi wa chadema ni sahihi kwani ccm tayali wana vijana wakakamavu kwanini wahofie upande mwingine kuimalisha kama wao,yaani uhalali kwao na halamu kwa wengine mh! Jamani kama nikuvunja, vivunjwe vyote nasio kuzungumzia upande mmoja wa chama kama kuimalisha ulinzi wao
 
Matokeo ya kuwepo kwa vikundi vya ulinzi katka vyama vya siasa ni HATARI SANA kwa mstakabali wa amani na usalama taifa hili. Hatari yake tunaweza jifunza toka uchaguzi wa Igunga hii ni picha ndogo tu nadhani tutegemee makubwa zaidi kama kila chama cha siasa kitakuwa na chombo chake cha ulinzi.

Sijajua kwa undani hasa kazi za vikundi hivi kama RED GUARD, GREEN GUARD, BLUE n.k kwa wenye vyama husika watufafanulie, nia na dhamira za vikundi hivi ni nini? na je, wanajitofautishaje na Jeshi la polisi hasa kwa swala la ulinzi na usalama wa raia? Je ni kwamba jeshi la polisi halitoshelezi au limeshindwa kazi lililopewa kisheria?
 
Wana jamii, tumezoea kusikia majina haya, Green, Blue, Guards na Sasa Red Brigade. Yakiwa ni majina ya vikozi vya ulinzi vilivyo undwa na vyama vya ccm, cuf na cdm respectively.

Enzi zile za zama za Mwl wakati mfumo wa siasa hapa nchini ulikuwa wa chama kimoja ilikuwa si tatizo chama kuwa na kikosi cha ulinzi. Kwani adui alijulikana kuwa ni kaburu, au yule anayetaka kuleta mfumo wa ubepari kwa mfano.

Sasa tuna mfumo wa vyama vingi. Tuliukubali wenyewe na umri wake sasa ni takribani miaka 23. Na tena tukasema siasa ya vyama vingi si uadui, ni kushindanisha sera na utumishi uliotukuka kwa wananchi.

Sasa vyama vina majeshi yake, hebu tujiulize ni majeshi dhidi ya adui nani, kama siasa si uadui?

Wakufunzi wa hivi vikosi wanapotoa mafunzo kwa wapiganaji wao, wana waambia mafunzo wanayo pewa ni dhidi ya adui yao nani?

Mimi na fikiri kama Taifa tuna kosea kuendesha mfumo wa vyama vingi vya siasa kwa staili hii.

Nani wa kusimama na kusema huko tunako peleka taifa hili siko? Kama ni kuto kuaminiana ndiko kumetufikisha hapa basi tutafute kuaminiana.
 
Hili ni janga kubwa sana linatunyemelea. . . . .mchezo wa ndama utaamsha madume. . .
 
hii ni ishara police wameshindwa wajibu wao kwa vile wanatumika na ccm ndio maana vyama vingine vimejitafutia ulinzi binafsi na mbaya zaidi ccm chama tawala mbali na kuwa na police jwtz ties back wameunda green guard nani afunge paka kengele??
 
Moja yà swali la kipuuzi linalopaswa kuingia kumi bora hapa JF ni hili ulilo uliza.
Kabla ya kutuuliza huo utumbo wako ulipaswa kutuambia adui wa kampuni za ulinzi kama ULTIMATE,GROUP 4,CHUI,na zinginezo.adui wao ukimpata na Red brigade watakutajia adui wao
 
Huko ni kuandaa vikosi vya uasi bila kujua tunachokifanya...hatuoni hatuoni kama tunakalia kuti kavu huku chini tumekoka moto wa mkaa....Eeeeh Mungu tuepushie kila baya tunakolipeleka taifa hili la masikini.
 
Moja yà swali la kipuuzi linalopaswa kuingia kumi bora hapa JF ni hili ulilo uliza.
Kabla ya kutuuliza huo utumbo wako ulipaswa kutuambia adui wa kampuni za ulinzi kama ULTIMATE,GROUP 4,CHUI,na zinginezo.adui wao ukimpata na Red brigade watakutajia adui wao
Hao uliowataja wanalinda mali binafsi na watu dhidi ya uharibifu wa mali, wizi, kusindikiza mizigo na pesa, wanafunga mitambo ya ulinzi,wana huduma za zimamoto pia!!!
 
Kwa vitendo vya Polisi wetu na vyombo vya usalama dhidi ya upinzani angalieni isije ikawa wale vijana walioitwa Green Guard ndio hivi sasa wamejazwa huko.
  • Wale waliokuwa wa juu wamepewa Uwaziri
  • Waliofuatia wamepewa Ukuu wa Mikoa
  • Wakafuatia waliopewa Ukuu wa Wilaya
  • Wa chini yake wakapewa Ukurugenzi
  • Je wale wa chini kabisa ndio wamepewa Uafande?
uvccm5-jpg.700553

2012, wakiwa na Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete

Wengi bado kwa uchungu mkubwa tunakumbuka vitendo vya kikatili vilivyokuwa vikifanywa na hawa vijana wa Green Guard bila kuchukuliwa hatua yoyote na Jeshi letu la Polisi.


Je kuna yeyote amewahi kujiuliza hawa hapa chini hivi sasa wako wapi?

uvccm-jpg.700531

Kutoka CCM Chipukizi hadi CCM Green Guard...polisi? TISS? JW?
uvccm1-jpg.700532


Mwenye macho haambiwi ona! Hebu fikiria yule polisi mhuni aliyekuwa anafyatua risasi hovyo kwa lile tukio la Adam Malima...nina hakika kama IGP Simon Sirro angekuwa na uwezo angeagiza akamatwe pale pale na kuwekwa chini ya ulinzi. Lakini masikini Sirro alijikuta kama kiwete asiyeweza kufanya lolote kwa sababu hakuwa na mamlaka ya kumchukulia hatua.

uvccm2-jpg.700548



uvccm3-jpg.700550

Hawa si polisi, hawa ni waliokuwa vijana wa Green Guard!

uvccm4-jpg.700551

Miongoni mwa hawa washambuliaji waliobeba mawe na silaha zingine, wapo waliokuwa Wabunge na wengine ambao hivi leo ni mawaziri!

Hakika vitendo vya vyombo vyetu vya Usalama kwa wakati huu kama kutumia risasi za moto dhidi ya upinzani vinazua maswali kuliko majibu. Kama alivyowahi kuonya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, aliyeonja nyama ya mtu haachi.

Nadhani sote ni mashuhuda wa vitendo vya hovyo na unyama unaotendeka hivi sasa nchini kama wakuu wa wilaya kuwasweka ndani wabunge wawakilishi wa wananchi na vyombo vya usalama kuwateka, kuwatesa na kuwaua viongozi wa upinzani.

Taifa linaelekea kubaya na wenye jukumu la kutulinda wamelewa madaraka. Cry my beloved country, kichaa kapewa rungu.

mbuni-jpg.700555


Huyu ndege anaitwa mbuni na yasemekana anayo tabia ya kuficha kichwa chake mchangani akiamini kwa kufanya hivyo atabaki salama wakati wa hatari.

mbuni2-jpg.700557

Wengine wetu Watanzania tumeamua kuwa kama mbuni na tumeamua kuficha vichwa vyetu mchangani huku tukijiaminisha walioonja damu wataacha! Naomba tena niwakumbushe maneno ya Hayati Baba wa taifa...aliyeonja damu ya mtu haachi!


Wakiwamaliza wapinzani mkae mkijua damu yenu itakuwa halali yao!

Mambo ni hivi, mara kadhaa hata polisi wenyewe wameonekana wakishangaa vitendo vinavyodaiwa kufanywa na polisi wenzao na hili jambo nimeliwaza sana kwamba huenda tunalo shadow police force! Imefikia wakati watu wanajiuliza hawa polisi wanafuata maagizo ya nani?

Nakumbuka kwa mfano wale walioongozana na Bashite wakivamia ofisi ya Clouds FM au wale waliomtolea Nape Nnauye bastola. Kwa nini mwanzo Waziri husika alionekana kuwakana?


Kunakuwepo na utata mwingi sana na kutupiana mpira kwa maafande tukio linapotokea huku kila moja akionekana kukwepa kutoa ufafanuzi. Mathalan hii ya kuvamia makazi ya watu usiku kudai kufanya msako na mara nyingi bila warrant ni kitendo kinachotia shaka kwani taratibu na miongozo ipo ya namna ya kufanya msako.

Je tunalo Jeshi la Wasioonekana? Jeshi ambalo hata IPG Sirro hana mamlaka nalo? Jeshi linaloteka, kutesa na kuua wananchi wanaoikosoa serikali? Jeshi linaoanza majukumu yake jua linapozama? Jeshi linalowalazimisha walengwa kwa kuwapa an offer they cannot refuse?

Kwa kweli tunalo Jeshi la Polisi lisilo na maadili na lisilofuata kanuni wala taratibu za kikazi jambo linalotia shaka sana. Mara nyingi nimewashuhudia viongozi wa juu kabisa wa Polisi wakionekana kushangaa kwa yanayotokea. Ni kama vile hawajui wajibu wao kikazi.
 
Back
Top Bottom