Hatuna utawala wa sheria tuna watawala wa sheria

joseph2

Senior Member
May 31, 2015
126
251
WAKILI mahiri na msomi kweli kweli. Pia shangazi wa taifa, Bi Fatma Karume, amesema kuwa hatuna utawala wa sheria Bali tuna watawala wa sheria.
Hii inamaana gani kwamba nchi inaendeshwa kwa matakwa ya watu na sio kwa majibu wa sheria. Kwa maneno mepesi ni kwamba watawala au watu wenye mamraka badala ya kufuwata matakwa ya katiba wao waamuwa ni sheria ipi ifuwate na ni sheria ipi isifuwatwe.

Kudhibitisha hayo Bi Fatma katowa mfano huu. Kasema mwaka 2016 mwendazake alipiga marufuku mikutano ya hadhara ambayo ilikuwa inaruhusiwa kisheria na kikatiba lakini msajiri wa vyama vya siasa hakukemea wala kusema chochote. Akaongezea kwa kusema sheria ya vyama vya siasa imempa mamraka msajiri wa vyama vya siasa kufuta Chama cha siasa kinacho kiuka matakwa ya kisheria, ambayo yanavitaka vyama vya kisiasa kuendeleza demokrasia.

Na hapa akauriza swali la kizushi. Je mwenyekiti wa Chama tawala alipo kataza mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa kwa miaka saba ya utawala wake alikuwa anajenga demokrasia au alikuwa na ibomowa. Na kama alikuwa anaibomowa mbona sheria hazi kuchukuwa mkondo wake?
 

Attachments

  • IMG-20240311-WA0015.jpg
    IMG-20240311-WA0015.jpg
    58.1 KB · Views: 2
  • IMG-20240311-WA0014.jpg
    IMG-20240311-WA0014.jpg
    132.1 KB · Views: 1

Fatma Karume: Hatuna Utawala Wa Sheria, Tuna Watawala wa Sheria



View: https://m.youtube.com/watch?v=PukvbrQZ048
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kwa kushirikiana na taasisi ya TWCP - Ulingo wameandaa tukio kuwakutanisha wanawake na wadau wengine kutoka maeneo mbalimbali ya nchi kwa ajili ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani IWD leo Machi 8, 2024.

Fatma Karume ahoji Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa kutochukua hatua pale Mwenyekiti wa CCM taifa alipopiga marufuku mikutano ya kisiasa, tamko lililokuwa kinyume na sheria ya vyama vya siasa kuwa lazima vyama vya siasa vikuze demokrasia ama sivyo vitafutiwa usajili.

Lakini cha kushangaza anaongeza wakili Fatma Karume , kuwa msajili akaufyata mkia kwa kutotoa kauli au karipio na kukiwajibisha chama cha CCM kuenda kinyume na sheria kwa kufuta mikutano siyo tu ya vyama vingine bali hata ya CCM kwa miaka 6 kinyume na sheria ya vyama vingi ambayo msimamizi wa vyama yaani Msajili wa Vyama vya Siasa anatakiwa kuhakikisha vyama vinakuza demokrasia ama sivyo anaweza kuvifuta kama sheria inavyotamka....
 
Fatma Karume : Wakurugenzi kukwepa kupokea fomu za wagombea au kuengeua wagombea


View: https://m.youtube.com/watch?v=Jw024916q1Y

Fatma Karume aibua mifano ya kuengua wagombea au mkurugenzi wa uchaguzi kujifungia na kutofungua mlango kwa wagombea wa upinzani kurudisha fomu ni mifano ya kukosekana utawala wa sheria kwa kuwa tuna watawala wa sheria badala ya utawala wa sheria
 
Back
Top Bottom