omarilyas
JF-Expert Member
- Jan 24, 2007
- 2,130
- 145
- Sasa hawa wapiganaji wafanye nini as we move forward na hii vita na haya manyang'au?, wabaki CCM au warudishe kadi, au what else? Tujadili wakuu ili tuwafikishie mawazo yetu wananchi!
Respect.
Field Marshall Es! - ni Sauti ya Umeme!
Kwanza hii dhana ya WAPIGANAJI inanikumbusha zile zama za WAPAMBANAJI wakati wa mchakato wa 2005 na baada ya ushindi wa MTANDAO. Je hii ina maana WAPIGANAJI ni maadui wa WAPAMBANAJI (ambao baadhi yao wapo wanaojiita wapiganaji hivi sasa)?Jee UPIGANAJI hautatuzalia yale yaliyoletwa na WAPAMBANAJI?
Pia nawashauri "WAPIGANAJI" waendelee kujibana hukohuko kwenye MADHABAHU yao kama wadau wakuu wa MFUMO FISADI waliotujengea, kuulinda na hata hivi sasa wakiwa mapiganoni bado wanaendelea kuutetea. Siamini kama wao kujitoa CCM watakuwa wakiwafanyia mema watanzania ambao ukweli HOPE yao ya kuondokana na madhila wanayokumbana nayo haiwezi kufanikishwa na WALIOZIKOSA MBICHI hizi.
Pia kwa kuwa hawa "WAPIGANAJI" wakitoka CCM kamwe hawawezi kuanzisha chama chao na hivyo kulazimika kujiunga na vyama vingine vilivyopo. Kwa muono wangu ni kuwa wataathiri NATURAL GROWTH TREND inayoendelea miongoni mwa baadhi ya vyama vya UPINZANI kitu ambacho kitatishia mustakabali wa watanzania kupata MBADALA MAKINI wa CCM hapo mbeleni.
Lakini pia siamini kama AJENDA ya UFISADI ambayo baadhi ya WAPIGANAJI wanakosa MORAL AUTHORITY ya kuisimamia kwani nao ni MAFISADI wa ama enzi za RUKSA, enzi za UWAZI NA UKWELI ama wengine hata enzi za ARI MPYA, inatosheleza kwa wao kujitoa katika KUNDI LAO na kwenda katika kundi lingine. Naamini inahitaji zaidi ya ajenda muda mfupi kama ya UFISADI kwa mtu ama kundi la watu kuhama chama. Kama wangekuwa na tofauti za KISERA, KIIMANI ama KIITIKADI, hapo ningesema kuwa kuondoka kwao CCM kunaweza kuwa na manufaa kwa mtanzania na sio kama hali ilivyo sasa.
Vilevile wakati nawafeel wanapopiga kelele kuhusu ufisadi, kwa muono wangu THIS IS THE GREAT SPIN OF ALL TIME YENYE LENGO LA KUJENGA IMANI KWA WADANGANYIKA KUWA "THERE IS HOPE IN CCM". Matamshi ya KILANGO kuwa hawapaswi kumuacha Zitto aongelee UFISADI na Mwakyembe kuwa JK awashukuru wao kwa kuweza kuwaondolea adha ya mawaziri wake kuzomewa huko mitaani yanadhihirisha hilo.
Naamini maoni yangu ambayo yanaweza yasiwe ya "GREAT THINKERS" lakini yapoyapo na yatawafikia "WAPIGANAJI" wetu...
omarilyas