Hivi ni CCM ndio inatumia dola kubaki madarakani au dola inatumia CCM kutawala?

Poa 2

JF-Expert Member
Jul 7, 2019
1,294
1,288
Habari za jioni wapendwa

Moja kwa moja kwenye mada.

Kuna KM mmoja wa CCM aliwahi kuropoka kwamba CCM itaitumia dola kubaki madarakani, sijui kauli hii ina ukweli kiasi gani labda wajuvi wa mambo mnitoe tongo tongo.

Ni kweli raisi wa nchi ambaye ni m/kiti wa Ccm ndiye anaye wateua wakuu wote wa vyombo vya usalama.
Lkn huyu raisi tuliye naye ni zao la katiba si wa kuchaguliwa na wananchi, na kuna tetesi kwamba baada ya kifo cha jiwe wana Ccm waliokuwa madarakani walitaka kupindua meza ili SSH asirithi kiti lkn kuna chombo kimojawapo cha usalama kiliamua kusimamia katiba.
Sasa swali ni kwamba ikiwa ccm ndiyo inayoitumia dola kwanini ilishindwa kupindua meza?.

Je? Kuna kakikundi kadogo ndani ya dola kilichojificha nyuma ccm na kanachoitumia kututawala au kuna kakikundi ndani ya CCM kanaitumia dola kututawala?.
 
Ukisikia vyombo vya dola ndio ccm wenyewe. Siku ikitokea vyombo vya dola(usalama, polisi, jeshi) wakakata kutumika kuiba kura ndio utakuwa mwisho wa CCM.
Kwa hiyo hapa unasema siku CCM ikakataa kukitumia yenyewe ndio itakuwa mwisho wake au mm ndio sijaelewa?
 
CCM siyo chama cha siasa bali ni chama dola. Dawa yake ni mapinduzi ya kijeshi tu
JamiiForums-979014263.jpg
 
Habari za jioni wapendwa

Moja kwa moja kwenye mada.

Kuna KM mmoja wa CCM aliwahi kuropoka kwamba CCM itaitumia dola kubaki madarakani, sijui kauli hii ina ukweli kiasi gani labda wajuvi wa mambo mnitoe tongo tongo.

Ni kweli raisi wa nchi ambaye ni m/kiti wa Ccm ndiye anaye wateua wakuu wote wa vyombo vya usalama.
Lkn huyu raisi tuliye naye ni zao la katiba si wa kuchaguliwa na wananchi, na kuna tetesi kwamba baada ya kifo cha jiwe wana Ccm waliokuwa madarakani walitaka kupindua meza ili SSH asirithi kiti lkn kuna chombo kimojawapo cha usalama kiliamua kusimamia katiba.
Sasa swali ni kwamba ikiwa ccm ndiyo inayoitumia dola kwanini ilishindwa kupindua meza?.

Je? Kuna kakikundi kadogo ndani ya dola kilichojificha nyuma ccm na kanachoitumia kututawala au kuna kakikundi ndani ya CCM kanaitumia dola kututawala?.
Swali makini ambalo linahitaji tafakuri pevu.
Ila wewe hatari, ume reveal fact ambayo wengi hatuifahamu. Pia umeanisha nadharia ya "kati ya kuku na yai kipi priority katika uendelevu wa generations ya kuku. Mimi nahisi vinategemeana kwani kila mmoja anafaidika kwa namna yake. siku wana mageuzi wakijua umuhimu wa kuyakumbatia mayai na namna kumwibia au kumwondolea kuku mayai yake, ndipo mambo yatakuwa mambo. ila kwa sasa bado wamelala usingizi wa pono.
 
Ukweli ni kwamba hata hicho chombo kwa sasa ndip kinaelewa kwanini,wale watu wachache ndani ya dola walitaka wafanye vile.

Kuna dola yenye vyombo vyake ambayo imevaa koti la kijani,maamuzi ya wengi ni maamuzi sahihi,hao wachache walikosa baraka za vyombo.
 
Swali makini ambalo linahitaji tafakuri pevu.
Ila wewe hatari, ume reveal fact ambayo wengi hatuifahamu. Pia umeanisha nadharia ya "kati ya kuku na yai kipi priority katika uendelevu wa generations ya kuku. Mimi nahisi vinategemeana kwani kila mmoja anafaidika kwa namna yake. siku wana mageuzi wakijua umuhimu wa kuyakumbatia mayai na namna kumwibia au kumwondolea kuku mayai yake, ndipo mambo yatakuwa mambo. ila kwa sasa bado wamelala usingizi wa pono.
Au pengine ccm nao wanasubiri mapinduzi kama walivyopindua wait Zanzibar? Maana Kwa box la kura tusahau kabisa
 
CCM ipo madarakani kwa ridhaa ya watanzania wanaoipigia kura na kuiunga mkono katika kila uchaguzi kutokana na kuwa na sera na ajenda zinazogusa maisha ya watu.
 
Mleta mada Yote mawili sahihi una swali lingine?
Hauwezi kukalia viti viwili Kwa Tako Moja lzm kuwe na kimoja ambacho ni sahihi hebu jaribu kufikiri saidi.
Halafu swli lingine mm Sina labda wewe uulize
 
Mleta mada kwani vyombo vya vya Dola sio Watanzania wenye Kadi wapiga kura kuwa wao hawaruhusiwi kupigia Chama wanakikibali?

Wao pia Wana vitambulisho vya mpiga kura na hupiga kura popote Kwa vitambulisho vya mpiga kura sio vya Jeshi
 
CCM ipo madarakani kwa ridhaa ya watanzania wanaoipigia kura na kuiunga mkono katika kila uchaguzi kutokana na kuwa na sera na ajenda zinazogusa maisha ya watu.
Kura Kwa tume ya uchaguzi ambayo mwenyekiti, mkurugenzi na wajumbe wote wanachaguliwa na mgombea wa chama Cha ccm? Au maisha ya wananchi yanayoguswa ni Kwa tozo, makodi, kupanda bei za bidhaa nk
 
Hauwezi kukalia viti viwili Kwa Tako Moja lzm kuwe na kimoja ambacho ni sahihi hebu jaribu kufikiri saidi.
Halafu swli lingine mm Sina labda wewe uulize
Kupiga kura hutakiwa kitambulisho Cha mpiga kura ambacho ni haki ya Kila mtanzania na hakionyeshi kazi yake Sasa kama wao Wana vitambulisho vya mpiga kura Wana Haki ya kupigia Chama chochote sababu kitambulisho Cha mpiga kura Wala hakionyeshi kazi ya mpiga kura awe na kazi au la mradi ana kitambulisho Cha mpiga kura anapiga
 
Mleta mada kwani vyombo vya vya Dola sio Watanzania wenye Kadi wapiga kura kuwa wao hawaruhusiwi kupigia Chama wanakikibali?

Wao pia Wana vitambulisho vya mpiga kura na hupiga kura popote Kwa vitambulisho vya mpiga kura sio vya Jeshi
Ukisoma hoja yangu kwa umakini utaelewa ila ukisoma kama gazeti la Lumumba naamini mchango wako hautavuka zaidi ya hichi ulichoandika
 
Kupiga kura hutakiwa kitambulisho Cha mpiga kura ambacho ni haki ya Kila mtanzania na hakionyeshi kazi yake Sasa kama wao Wana vitambulisho vya mpiga kura Wana Haki ya kupigia Chama chochote sababu kitambulisho Cha mpiga kura Wala hakionyeshi kazi ya mpiga kura awe na kazi au la mradi ana kitambulisho Cha mpiga kura anapiga
Kwa mfano uchaguzi wa 2020 unaweza kutuambia magufuli alipata kura ngapi na utupe reference na sisi tujiridhishe
 
Back
Top Bottom