Nini iwe hatma ya Wapiganaji walio CCM, Warudishe kadi au?

Kwa kuwa wao pia ni kama kundi, wakae pomoja waunde kundi A na B,

Kundi A litoke CCM na kujiunga na wapambanaji wengine ili kuongeza nguvu na kuwahakikishia watanzania kuwa Tanzania isiyo na Mafisadi inawezekana

Kundi B libaki CCM na liendelee kupambana na mafisadi ndani kwa ndani, kundi hili litawanyima mafisadi kubuni baadhi ya mipango ndani ya CCM kwa kuwa watajua si wote wafuasi wao, kwa mfano kama CCM yote itabaki kuwa ya mafisadi ni rahisi kwao kupanga mpango wa kuwamaliza wapinzani wao (either political death or physical death ... utajaza mwenyewe), mfano mzuri ni kwamba, wakati kina Nyerere wanapigania uhuru walipata msaada kutoka kwa baadhi ya Waingereza ambao walikuwa wanawapa tip .... kwamba kimepangwa hiki na hiki.

Ikumbukwe kuwa Vita dhini ya mafisadi (tangu ilipoanza rasmi pale mwembe yanga) imekuja kwa kuwashitukiza (it has taken them by suprise) na mpaka sasa wemetumia pesa nyingi sana kujaribu kuizima, na wanatumia pesa nyingi sana kununua supporters na hawapati dili za pesa kama ilivyokuwa zamani,

kwa ufupi ni kwamba wanatumia pesa nyingi na hawaingizi chochote

Nini kosa la kuwaachia Mafisadi uhuru 100% ndani ya CCM?
Mafisadi wanahitaji Mwaka mmoja tu wa uhuru ndani ya chama/serikali ili waikamue vilivyo Tanzania kiasi kwamba watarudisha ghalama zao na kujilimbikizia utajiri mkubwa kwa ajili yao mpaka watoto wa wajukuu zao.

Tafadhali wasipewe hiyo nafasi.
 
?

hakuna dawa rahisi ya ufisadi zaidi ya kukaa mbali na mafisadi.

Mrema aliweza............

- Sawa sawa mkuu, unasema watoke lakini wengi so far wanasema wabaki, lakini point taken mkuu, in the end tutahesabu kama demokrasia inavyotaka kati ya wanaosema wabaki na wanaosema waondoke.

- Na my promise ni kwamba nitaufikisha huu mjadala kama ulivyo, kwa sababu by next week nitakuwa na ugeni wa mpiganaji mmoja, ambaye pamoja na kuwasukumia wapiganaji wengine kwa mtandao huu mjadala, huyu nitampatia print yote mkono kwa mkono ya huu mjadala ambao ninauchukulia kuwa a very serious one, kama mawazo yetu wananchi wengi hapa JF, kwa hiyo ninatoa heshima kwa wale wote ambao mmekuwa serious kwenye mawazo yenu on this ishu na ninaomba tuendele hivyo hivyo lakini nita-edit lugha zote zisizofaaa kabla ya kukabidhi, na pia tutaangalia uwezekano wa kumhoji huyu mpiganaji moja kwa moja live hapa JF on this ishu kwa hiyo stay tuned!,

- Na hasa maswali na majibu moja kwa moja kutoka kwa wananchi hapa na mdomoni mwa huyu mpiganaji.

Respect.

Field Marshall Es!
 
Mkuu, mimi kwa maoni yangu naona wapiganaji ni bora wabaki ndani ya CCM ili kupambana na ufisadi uliokithiri ndani ya CCM na Serikali badala ya kurudisha kadi na kupigana wakiwa je ya CCM.

Nasema hivyo kwa kuangalia historia ya watu mbali mbali ambao waliwahi kushika nafasi ndani ya CCM ikiwemo yule aliyeshika nafasi ya juu kama Mh. Mrema ambaye baada ya kutokubaliana na mambo mbali ndani ya chama hicho aliamua kujiengua.

Tukiangalia watu hawa akina Mrema na wengineo wengi ambao walijiengua CCM hatuoni mafanikio yoyote waliyoyapata baada ya kujiengua huko. Na wengine kama akina Kabouru, Tambwe Hizza na wengineo wengi baada ya kupibgwa na njaa kali waliamua kurudi tena CCM ili wakagange njaa zao.

Wakiamua kuondoka kwa maoni yangu vyama vya upinzani vilivyopo bado havina nguvu na havijajijenga sana katika sehemu mbali mbali nchini ili kuweza kupambana na CCM. Pamoja na ushawishi mkubwa unaofanywa na Watanzania ndani na nje ya nchi ya vyama hivyo kuungana na hivyo kuunda chama kimoja chenye nguvu cha kupambana na CCM katika kila kona ya nchi yetu, bado viongozi ndani ya vyama hivyo hawajaona umuhimu wa kuungana na kwa maoni yangu hili linasabishwa na ubinafsi mkubwa wa kuogopa kupoteza madaraka katika chama kipya kama wakiamua kuungana

Hivyo hawa wapiganaji ni bora tu waendelee kupambana ndani ya CCM badala ya kuamua kurudisha kadi na huku Watanzania wenye vyama na tusio na vyama tukiwaunga mkono kwa hali na mali ili kuhakikisha wanawashinda mafisadi ndani ya CCM.

Wakiamua kurudisha kadi watakuwa wamewapa mafisadi ndani ya CCM na Serikali ushindi mkubwa na hivyo kuathiri kwa kiasi kikubwa mapambano dhidi ya mafisadi ambayo yanaungwa mkono na Watanzania walio wengi.

Mkuu BAK, heshima mbele sana na hii ndio hasa tunayoita Great Thinking,

- Simple and very clear, uanjau hoja kama hizi zako ambazo hazina abusive language na point ziko very clear ninawajibika kuzifikisha kama zilivyo bila kupunguza anything, I wish post zote humu zingekwua hivyo, yaani kama hii yako.

Respect.

Field Marshall Es!
 
Kutoka kwa mzee Mkandara na waambia hivi... Kadi ya CCM ni mali ya wapiganaji, mali ya Wakulima na Wafanyakazi na sii vinginevyo kwani Ilani na katiba ya chama inajieleza wazi nini ibada za chama chenu CCM..hakuna nafasi kabisa ya kundi la Pili hao wanaodai mrudishe kadi za chama.

Hakika huu ni wakati wenu mnaojiita Wapiganaji (kama kweli mpo) kuhakikisha hao Mafisadi wanarudisha kadi wao, na mkishindwa kufanya hilo within the next 3 Month, basi nyie nyote matapeli. yaani chama na wanachama wake ni frame tupu, bango la display njia panda kufurahisha macho ya wananchi. Huu ni wakati wenu kutuonyesha mnaweza mapambano na sii kukimbia mkaacha misahafu yenu mikononi mwa shetani.

Na hakika mwaka 2010 mtakuwa watumwa wa chama chenu wenyewe..kwa mtumwa wa kujitakia, msije huko wala sikukaribishi nyumbani kwangu!

Kifupi mkuu wangu yaani uko tayari kunyang'anywa kiunga chako!.. upo tayari kurudisha hati ya kumiliki ardhi wakati unafahamu vizuri urithi huo wazazi wako walivyoutafuta kwa taabu, leo vikaragozi visivyojaa mkononi wakuondoe wewe ktk ardhi yako mwenyewe. Comeon bro, U must be kidding me!

Nooo!.. mkuu wangu hata kama ikibidi mmalizane, CCM ife kabisaaa kabla ya Uchaguzi basi na iwe hivyo kwa sababu kama mtashindwa kujikinga na watu hawa wawili mkakimbilia vyama vya Upinzani, sijui kama wananchi watawakubali. Kwani siku zote adui mkubwa wa Mpiganaji ni POLICY, itikadi iliyopo dhidi yake na wananchi wake na sio kupambana na kuogopa kichwa cha mtu.,Hii ndio kwanza naiona yaani mtu unaogopa mkono wa binadamu mwingine badala ya kuogopa kichwa..
Mkiwapisha chama basi mmeshindwa na hatuwezi kuwaachia dhamana ya National security watu kama hawa.

Mkulu Bob,

- Heshima mbele, hii ndio tunaita great thinking.

Respect.

FMEs!
 
Mkuu by next month itakuwa too late.. hawa mafisadi mnatakiwa kuwashughulikia haraka ipaswavyo kwa sababu hapo mlipo hakuna mtu anayejua Plan B ya mafisadi. Hawa jama wamejiandaa wamekwisha weka mikakati yao tayari kuhakikisha wanarudi ktk uongozi na mkikimbia mtakuwa mnawapa nguvu Mpya..

Hakika hakuna kati yenu aliyetegemea Ushindi Kisiasa baada ya kikao cha NEC lakini JK alicheza kama Pele, na sasa hivi Sitta anajibebea Umaarufu Mkubwa. Isipokuwa tu kinachotakiwa ni roho ya Kiyahudi yaani jicho kwa jicho, Mhanga ni kujitolea na kuwa mstari wa mbele ktk mapambano na sii haya maswala kina Mandela kuchukua adhabu, mateso ati shahidi wa Mungu!..

Siwaombie vita wala sitaki, sishabikii umwagaji damu lakini kama CCM wameweza kuyafanya machafu huko Pemba, Mwembechai, ktk chaguzi ndogo za majimbo hata wakaua mbwa alovaa jezi ya chama... nashndwa kuelewa mnashindwa nini kuwashikisha adabu hawa viumbe waliokiuka kabisa misingi ya utu..Kwa watu washenzi kama hawa mnashindwa kipi kufikisha mapambano yenu uwanjani kwao - WATU WAWILI ndio wanaisumbua nchi nzima VICHWA VIWILI!..
 
Wapiganaji ni lazima wabaki ccm tena kwa makini sana na wakilindana kwa umahiri zaidi.
Jambo muhimu sana ni kuangalia sana kwamba Wazee walioteuliwa kufanya uchunguzi wa mwenendo wa wanachama Mzee Mwinyi, Kinana na Msekwa hawafanyi vituko. Maana nina wasiwasi wanawafahamu wapiganaji wengi. Kunauwezekano kuwa hata wao ndani kabisa ya roho zao hawaupendi ufisadi. Lakini wanaweza kuwaita na kuwashauri kupooza kasi. Halafu kingine ambacho kinatakiwa kipewe fikra za uvumilivu ni kungoja kuona jinsi Bunge la Novemba litakavyokwenda, nadhani baada ya bhilo Bunge ndiyoi wengi tutaweza sana kutafakari nini CCM imeamua, kuwakumbatia au kuwadhoofisha mafisadi? Bunge la Novemba litakuwa kipima joto cha uhusiano wa ccm na mafisadi. Hakuna namna yote yataeleweka.
Wapiganaji baada ya hapo ndipo watabidi waanze fikra za kamili za kuikomboa nchi. Itabidi kianzishwe chama kingine madhubuti kwa utaratibu usiowezekana kuwa "infiltrated" by CCM this time around. Na wapiganaji wachache mahiri wabakie ili kuendeleza mapambano ya kweli.
 
FMES,

..hili somo la vita ya ufisadi bado halijawaingia wananchi kiasi cha kuwakosesha raha CCM.

..siku CCM wakiona kwamba wananchi wamechoshwa na ufisadi na hakuna njia ya kuwalaghai, na zaidi wanaweza kushindwa uchaguzi, basi huo ndiyo utakuwa wakati wa kuwatema mafisadi.

..hata Republicans walimtetea sana Mzee Richard Nixon, lakini walipoona mambo yamewachachia, walitokea wazee wakamfuata Nixon White na kumpa the bad news.

..kitendo cha wazee kumfuata Nixon White House ndicho kilichomlazimisha kuachia ngazi.

..kitu kingine wananchoweza kufanya kama imeshindikana kuondoka CCM basi wahakikishe ktk kila UCHAGUZI wa CCM wanakuwa na wagombea wao WASAFI.

..actually hicho hapo juu ndicho walichofanya wana mtandao. lakini waliudanya umma kwamba ni vijana wanaotaka kuwaondoa wazee CCM, wakati ukweli ni kwamba walikuwa ni kundi na vibaka na wezi wakubwa-wakubwa wenye uchu wa madaraka.

..sasa hawa wapinga ufisadi nao kweli ni wasafi hawa? hivi kweli Samwel Sitta huyu ni msafi au amejibanza tu akitegemea hakuna anayekumbuka uchafu wake aliokuwa akifanya wizara ya ujenzi na CDA?
 
Jokakuu,
sasa hawa wapinga ufisadi nao kweli ni wasafi hawa? hivi kweli Samwel Sitta huyu ni msafi au amejibanza tu akitegemea hakuna anayekumbuka uchafu wake aliokuwa akifanya wizara ya ujenzi na CDA?
Duh! mkuu wangu una maana tunayoyaona ni kugombea nyama ktk Palau la Maulidi..Mnnnnh. sikuwahi fikiria upande huo lakini kitu hii kweli inawezekana ikiwa tunaamini binadamu anaweza kutubu na akasameheka..Pengine Sitta kisha mrudia bwana iweje tufikirie mambo ya wizara ya Ujenzi na CDA kujibu Uadilifu wake leo hii..

Nina hakika Jokakuu nimjuaye enzi za Club (Mbowe) sii huyu ambaye ana mke na watoto, au sio?.. (usiogope wala sikujui)
 
Wakuu wote JF yaani Great Thinkers,

- Ninaamini kwamba kilichotokea majuzi Dodoma ni only a big set back lakini sio mwisho wa vita na mafisadi, sio siri kwamba wapiganaji wetu kwa sasa spirit ziko chini, sasa huu ni wakati wa Great Thinkers, kuwapa ushauri of what to do next.

- Ninaomba kutoa shukrani kwa wakuu wote wa JF waliotoa maoni yao mazito kule kwenye thread ya Kusila, yamesaidia sana kuwapa moyo baadhi ya wapiganaji, ambao nimewasukumia tayari.

- Ninaomba mawazo hapa ili niwafikishie kama yalivyo, binafsi ninaanza kuwaza kwamba huenda huu ni wakati muafaka kwa wapiganaji kurudisha kadi zao za CCM, kwa sababu sasa hawawezi tena kupiga kelele za kuikosoa serikali, wala CCM mbele ya public, wanatakiwa kuyafanya haya ndani tu ya vikao vya chama chao CCM, hapa nia na madhumuni pamoja mengine mengi ni ili sisi wananchi tusijue wala kusikia ya huko ndani ya vikao vyao, na vile vile kuwakimbia mafisadi kunaweza kuwapa mwanya wa kutumaliza kabisa sisi wananchi!

- Sasa hawa wapiganaji wafanye nini as we move forward na hii vita na haya manyang'au?, wabaki CCM au warudishe kadi, au what else? Tujadili wakuu ili tuwafikishie mawazo yetu wananchi!

Respect.

Field Marshall Es! - ni Sauti ya Umeme!

Mkuu,

Hii ya kurudisha kadi ni uamuzi mgumu na wa kishujaa na utawapa mwanga watanzania kwamba labda kunahitajika mabadiliko ya kisiasa na namna ya kuchagua viongozi kwa makini kwenye chaguzi zijazo.

Kuhusu kwamba kukosoa serikali mbele ya umma wa watanzania kwa ujumla wao, ni kwamba hicho ni kitendo cha kidemokrasia ya kweli na iloiva haswa, kwamba wanasiasa wapiganaji wa haki na usawa ni lazima waoneshe kwa umma jitihada zao na huenda zikasaidia kubadilisha fikra za wananchi wengine.

Hali hii inasaidia sana kuleta mabadiliko katika kuchagua viongozi na ndio njia muhimu ya kupata wapiganaji hodari wenye uchungu na nchi yao.

Kwa hio basi, njia ya pili ambayo mkuu Kitila amependekeza ndio njia pekee ya kurekebisha mfumo wa siasa Tanzania na baadae mifumo mingine kama vile wafanyakazi na wahangaikaji wote.

Kushiriki katika shughuli za serikali kwa kuwa mpinzani (tuchukulie wapiganaji wameunda chama chenye nguvu) ni njia muafaka pale tu ikiwa asilimia zaidi ya kumi katika bunge ni wapiganaji waliounda chama cha upinzani chenye nguvu na ambacho kitawakutanisha wabia wote wana JF, wana mazingira, wafanyakazi, wanasheria, wachumi na wataalam wengine.

Ila sina hakika kama wapiganaji hawa watakuwa tayari kukabiliana na hii "challenge" ya ufisadi na viota vyake vyote kama vile wafanyabiashara wakubwa, makampuni ya kigeni na NGOs za kutoka nje, maana hawa ni tatizo.
 
Mkandara,

..Sitta alikuwa mwanamtandao. sasa ni kitu gani kimemkosanisha na wenzake? kwani hakuona uozo wote uliokuwa unaendelea?

..kama anataka imani yetu, the he has a lot of explanation to do.

..unajua hata mama ndani ya nyumba ukimkosea kuna kipindi cha mpito unabidi ufanye mambo fulani fulani kurudisha imani yake kwako. kwa mfano unaweza kulazimika kwamba ukitoka kazini moja kwa moja nyumbani hupitii tena vijiweni au kwenye wanzuki etc etc.

..tatizo letu wa-Tanzania kila analotutamkia mwanasiasa tunaliamini kwa wakati husika. hatuhoji kwamba mbona jana na juzi ulitoa kauli tofauti?
 
- I understand, lakini tatizo hapa sio tafsiri yako na yangu, tatizo ni katiba au sheria ya Jamhuri, ni kwamba Spika na wapiganaji wameapa kulinda sheria na katiba ya jamhuri, na sio ilani ya CCM ndani ya bunge, sidhani kama unahitaji kua professor kuelewa hili, na it has nothing to na fikra zako au zangu!

- Spika na wabunge wote wapiganaji wanaangukia kwenye kikaango cha sheria ya jamhuri, na sio ilani za CCM walipochaguliwa kuwa wabunge as far as taifa is concerned waliapa kusimamia katiba ya jamhuri, ni kamati ya maadili ya bunge peke yake ndiyo yenye mamlaka kisheria kuwathibiti kama wanaleta upiganaji bungeni kinyume na sheria, ni simple politics ambazo hata huhitaji maadili ya ufisadi kutoka CCM, kuelewa!

- Hatuna sheria yoyote inayosema kwamba matatizo ya ndani ya CCM yahamishiwe kwenye bunge la taifa, kama kuna matatizo CCM basi yamaliziwe huko huko bila kugusa Bunge, bunge ni la Jamhuri sio la CCM, kikao cha NEC kuwashambulia wabunge wa jamhuri na Spika wake ni makosa sana kisheria, sisi Jamhuri we could careless kama hawa wabunge ameapa huko CCM au hawakuapa, what we care ni kwamba waliapa kwa Jamhuri, je wamevunja kiapo chao kwa Jamhuri? Wa kutuambia hayo sio NEC ya CCM, ila Attorney General au kamati ya maadili ya bunge!

- Spika kuwa na kundi lake ndani ya wabunge huko bungeni kama ni kuvunja sheria ya jamhuri basi tuambie ni kifungu gani kilichovunjwa, kama huko CCm mna matatizo yamalizeni huko huko msituletee kwenye Jamhuri.

- Wabunge wamezungumzia kukerwa na mafisadi ndani ya serikali, na sio huko kwenu CCM, tunachojali ni katiba ya jamhuri, sio ilani za kifisadi za CCM, kama mnataka kujiondoa jiondoeni huko CCM, lakini sio kushambulia Mhimili muhimu wa taifa letu kama Bunge.

- Ninarudia hivi, kama huko CCM mnataka kuondoana basi mmalizane huko huko msituingilie kwenye bunge!

Respect.

Field Marshall Es!

Mkuu FMES,
I respect your views lakini hata hivyo taarifa kamili ya nini kilichojiri katika kikao cha NEC ya CCM zimeshatolewa na mambo si kama hivyo ulivyokuwa unayaripoti. For that matter, I am no longer going to discuss anything on this thread kwa vile ukweli tayari umeshapatikana.
 
images

one, two, three....game over !

Mkuu FMES,
I respect your views lakini hata hivyo taarifa kamili ya nini kilichojiri katika kikao cha NEC ya CCM zimeshatolewa na mambo si kama hivyo ulivyokuwa unayaripoti. For that matter, I am no longer going to discuss anything on this thread kwa vile ukweli tayari umeshapatikana.

Pundamilia,

Ukweli gani? Tangu tamko rasmi la yaliyojiri kweli vile vikao lilipotolewa na Chiligati, kuna watu wangapi wamefafanua tamko hilo? Na kwa kadri wanavyozidi kufafanua ndivyo wanavyozidi kujikanyaga na kujichanganya.

Tatizo ni kwamba vile vita vilivyo ndani ya CCM vinapiganwa na watu wengine ambao hawako smart. Kuna baadhi ya wajumbe walio kwenye kambi ya RA na EL ambao waliamua kuwa-feed waandishi wao wa habari info zote kama zilivyo na magazeti yakaripotii kama walivyoambiwa. Wao walidhani kwamba wananchi watazipokea kwa furaha. Jamii imezipokea kwa mshangao na masikitiko makubwa na nina uhakika kuna watu wanajuta kwanini walioongea hivyo kwenye vikao maana ujinga waliousema tayari uko mitaani na wao tunawahesabu kwamba ni mafisadi tu.

Hivi CCM huwa hawajifunzi kutokana na makosa? Walipomfungia Zitto walishangilia sana Bungeni, kilichofuata wanakijua wao wenyewe, mawaziri ilibidi waanze kukwepa kutembea kwa kuogopa kuzomewa na kuitwa mafisadi na wakaanza kusema wanazunguka nchi nzima kuelezea bajeti, lakini hawakuwa wanaelezea bajeti walikuwa wanaficha ujinga walioufanya bungeni. Sasa naona NEC wamerudia tena na labda walirudia hayo kwa kuwa walijua wanafanya vikao vya siri na kumbe ni vikao vya wazi, maana wajumbe walikuwa wana rekodi kila kitu na hao hao mafisadi ndiyo walikuwa wa kwanza kwenda kuwapa waandishi habari details zote.

Ukisoma ile habari iliyoandikwa Tanzania Daima unakuta kuna sehemu nyingi tu wanam-refer RA kama source yao. Bado mnasema kwamba chama hakina nidhamu na wanaotoa siri za vikao ni hao hao mafisadi. Siku wajumbe wa upande wa pili wakitoa hizo siri za yaliyosemwa kwenye vikao ndipo mnakuja juu kama moto wa kifuu, lakini kama source ni RA ni sawa tu, maana anachokisema kina maslahi kwa chama kwa kuwa kinatetea maslahi ya mafisadi.

Kilichoandikwa kwenye magazeti yote kinatofautiana kwa kiasi kikubwa sana na tamko la Chiligati. Tamko haliko wazi limefunika funika mambo. Tamko limejaa unafiki mtupu, hawataki kuwa wazi kwamba wanatetea ufisadi na badala yake wanakuja na uongo kwamba Bunge limegeuzwa kuwa Ze Comedy na kufanya malumbano. Hoja ya kutetea maslahi ya mafisadi imejadiliwa kwa masaa zaidi ya 10, lakini serious issues za kupanga mikakati ya kuendeleza wananchi zinajadiliwa kwa nusu saa na hakuna hata wachangiaji. Impliedly, mafisadi ni muhimu sana kuliko wananchi zaidi ya milioni 40. Bado unasema kwamba CCM ni nambari one? Hicho chama ni mkusanyiko wa mafisadi ambao wameamua kuifilisi hii nchi kwa kutumia kila aina ya mbinu chafu.
 
- Mkuu Pundamilia, tulikuwa tunajadili hoja, sasa imekuwaje tena umeamua kwenda nje ya hoja? Now naomba nikuambie hivi hii chini ndiyo the most trusted version ya yaliyojiri ndani ya kikao, na imeandikwa na the most trusted paper ya bongo, yaani IPP Media kwa Mzee Mengi, sasa nakuomba uichambue halafu uiambie hii forums ni wapi wamesema ambacho sikukiripoti, na pia ninakuwekea wekundu kwenye yote niliyoyasema! infact kama kawaida yetu JF, again this time tumeliongoza taifa na facts za yaliyojiri huko ndani, taifa zima na media zote za bongo zilikuwa zinafuatia the leader, yaani hapa JF mkuu.

- Halafu kumbuka mimi sijadai hata mara moja kwamba nilikuwemo ndani ya kikao, kama wewe ulivyodai na hoja yako ya Sitta hakuomba radhi, sasa what are you saying kwamba hilo tu ndilo lililozungumzwa huko ndani yaani Sitta kutoomba au kuomba msamaha?

- You can't have it both ways mkuu, sio wote hapa JF ni wajinga na ni kwamba unajidanganya wewe mwenyewe, kama huwezi kujadili hoja wapo ambao wapo tayari kujadili hoja mkuu, jiheshimu ili uheshimiwe kama huna hoja basi waachie wenye nazo wajadili hoja, lakini hatuwezi kuharibu mjadala kwa sababu you can't get your way! Hebu soma hapa hawa wanalipwa kufanya hii kazi, mimi ninajitolea tu mkuu:-

Urambositta.jpg

Speaker Samuel Sitta addressing a rally at Urambo yesterday. (PHOTO: Edwin Mjwahuzi)

Source: Guardian Sunday.

Speaker Samuel Sitta has vowed to maintain his principled approach, and declared that he is still very strong.He has furthermore called on his well-wishers to pray for him, so that he may have better health and remain steadfast in his patriotism-driven activities.

The sentiments were among the highlights of a nearly 25-minute address Sitta gave to a huge crowd that had earlier given him a tumultuous welcome after arriving in Urambo Constituency in Tabora.

He told the audience comprising mainly people in his constituency, that his record as MP over the past four years was impressive, one of its manifestations being facilitating a Sh60billion road construction.

However Sitta didn't directly speak about what transpired during the just ended NEC meeting in Dodoma.
"I am still strong…just pray for me so that God gives me better health, to enable me work for you and our country," Sitta told hundreds of cheering supporters yesterday evening. Earlier, Urambo residents led by a traditional leader, Lameck Kabuda, presented a shield and spear to Speaker Sitta as a symbolic acknowledgement of his unrelenting resolve to fight grand corruption.

At Tabora airport, Speaker Sitta was received by four priests who drove from his Urambo constituency to welcome him in the region. Conspicuously absent were government and ruling party officials.

A failed mission

They secretly planned a mission to oust him, triggering sharp criticism from the public, opposition and the some religious leaders. Putting their hopes on the money's deceit, the group of three prominent politicians believed to be behind the failed mission had at least 90 percent assurance that the end of their political enemy Samuel Sitta has arrived.

Banking their hopes on how Maalim Seif Shariff Hamad and Abdul Jumbe were cornered by top party's organs before being forced to resign from their positions, anti-Sitta's group failed to understand one thing that the political environment of two decades ago is quite different from the current situation.

Although the group used an example of how South Africa's ruling party ANC kicked out Thabo Mbeki, and still scored a landslide victory in this year's general election, to cement their motion the events that have followed this week after the conclusion of NEC meeting have proved that ‘their mission was ill-conceived."

Though at the short-run the group might has emerged as a winner in the long standing political battle, at the long-run Speaker of the National Assembly is gaining momentum politically sending an alarming message that ‘their botched mission was nothing but just a ladder to promote Sitta politically'.

Two top CCM leaders, Yusuf Makamba and Tambwe Hiza, have strongly tried this week to calm what they described as negative and distorted media reports about what transpired.
However, their move has totally failed to change the political wind as Sitta continues to enjoy a very strong support from the people.

While Makamba made it clear that the party has the full authority to discuss as well as to question the way Sitta was managing the Parliament, Hiza on his side cried foul, insisting that the media has totally distorted what transpired.

But their clarifications didn't make any difference as the political wind continues to blow in favour of Sitta.
In his constituency, the Speaker received a heroic welcome, as thousands of his supporters came out in multitudes to receive on Saturday.

As Sitta a lawyer turned politician continues to enjoy the massive support, to his opponents, the wind has changed dramatically as news about a fifty million shillings mission continue to unfold this week.

While first, it was thought that the move to crucify Sitta was a strong agenda planned by the ruling party, the fresh versions of majority of NEC members who attended the just ended meeting show that ‘it was just a an attempt by a small faction of members' who attempted to use the authorized meeting to oust the Speaker.

According to media reports quoting some NEC officials, about 30 NEC members mainly from Zanzibar were paid up to Sh2million per person to execute the deal with a promise of being paid another amount after successfully completing the mission.

Although it failed to takeoff as expected, Sitta and his group were taken by surprise when their rivals launched massive attacks, calling for his resignation as well as surrendering of his membership card.
Just few hours before the meeting, The Guardian on Sunday team contacted Mr Speaker asking him whether he was aware about the mission, but the man seemed very clearly that ‘he wasn't aware."

"This cant be true…I should have known earlier" Sitta told The Guardian on Sunday few hours before the series of Central Committee and National Executive Committee meetings in Dodoma last week. With nearly 14 months before the 2010 general election, the battle for the control of the key political groups within the ruling party is expected to widen , as every faction attempts to ‘install' a leader of their choice starting with the election of lawmakers.

Never apologized

The Speaker of the National Assembly Samuel Sitta never apologized as reported by some section of the media this week, The Guardian on Sunday has learnt.
Contrary to media reports quoting inside sources within National Executive Committee, Sita told his accusers, "I have heard you; let us forgive each other…I am a matured person and have heard you all."

"I was in the meeting and witnessed everything that transpired…but I was shocked to read on the newspapers next day that Mr. Speaker apologized," one NEC member from Lake zone regions told the Guardian on Sunday yesterday.

The NEC member who declined to be named citing the sensitivity of the subject queried, "Is this an apology or just misinterpretation of what Sitta said?""Some of us where shocked to hear what the Speaker was being accused of; that he wanted to overthrow the president…but finally at the end we were able to understand the growing rift within our party." The NEC member added.

Another member of NEC told The Guardian on Sunday this week that some ‘planted' members from Zanzibar went beyond the mark accusing Sitta of muzzling the presidential powers, under the umbrella of managing the parliament in a modern way.

"There is nothing else bad and dangerous in politics than being accused of grabbing control of the State through Parliament. This is equal to treason whose punishment is either death or life imprisonment," the source said
. Inside information had it that it seemed NEC members from Zanzibar were planted by some individuals with ill-mission against the speaker since it was the ones who spearheaded the agenda.

"First the agenda on speaker was not on the list, but it was suddenly brought by some members; what was even surprising is that NEC members from Zanzibar appeared to spearhead the matter during the meeting, something that hinted the possibility that they were prepared by those seeing Sitta as their political enemy." He said

But CCM spokesman John Chiligati denied reports claiming Speaker Sitta was at the centre of the subject during CC and NEC meetings. He blamed the press for reporting the case without conducting thorough investigation, a factor that distorts the truth.

"Among other things discussed, the meetings examined the situation in the party, including finding a better way to restore party discipline among our party members that now appears to be withering away," he said.

He added: "People should understand that our meetings were not centered on speaker because he was not part of the agenda meetings. What transpired is that Speaker Sitta was discussed as a CCM member just like any other CCM members in relation to the conduct of CCM legislators within the Parliament and in the House of Representatives,"

He said of relate a strange behavior has emerged within with the party whereby every party member has turned out to be a spokesman despite the presence of special people with such responsibilities.
 
Wapiganaji ni lazima wabaki ccm tena kwa makini sana na wakilindana kwa umahiri zaidi.
Jambo muhimu sana ni kuangalia sana kwamba Wazee walioteuliwa kufanya uchunguzi wa mwenendo wa wanachama Mzee Mwinyi, Kinana na Msekwa hawafanyi vituko. Maana nina wasiwasi wanawafahamu wapiganaji wengi. Kunauwezekano kuwa hata wao ndani kabisa ya roho zao hawaupendi ufisadi. Lakini wanaweza kuwaita na kuwashauri kupooza kasi. Halafu kingine ambacho kinatakiwa kipewe fikra za uvumilivu ni kungoja kuona jinsi Bunge la Novemba litakavyokwenda, nadhani baada ya bhilo Bunge ndiyoi wengi tutaweza sana kutafakari nini CCM imeamua, kuwakumbatia au kuwadhoofisha mafisadi? Bunge la Novemba litakuwa kipima joto cha uhusiano wa ccm na mafisadi. Hakuna namna yote yataeleweka.
Wapiganaji baada ya hapo ndipo watabidi waanze fikra za kamili za kuikomboa nchi. Itabidi kianzishwe chama kingine madhubuti kwa utaratibu usiowezekana kuwa "infiltrated" by CCM this time around. Na wapiganaji wachache mahiri wabakie ili kuendeleza mapambano ya kweli.

- Mkuu mpendaTZ, heshima mbele sana hizi ndio zile zile tunazoita Great Thinking na itafika kama ilivyo bila kupunguza anything.

Respect.

Field Marshall Es!
 
Mkuu,

Hii ya kurudisha kadi ni uamuzi mgumu na wa kishujaa na utawapa mwanga watanzania kwamba labda kunahitajika mabadiliko ya kisiasa na namna ya kuchagua viongozi kwa makini kwenye chaguzi zijazo.

Kuhusu kwamba kukosoa serikali mbele ya umma wa watanzania kwa ujumla wao, ni kwamba hicho ni kitendo cha kidemokrasia ya kweli na iloiva haswa, kwamba wanasiasa wapiganaji wa haki na usawa ni lazima waoneshe kwa umma jitihada zao na huenda zikasaidia kubadilisha fikra za wananchi wengine.

Hali hii inasaidia sana kuleta mabadiliko katika kuchagua viongozi na ndio njia muhimu ya kupata wapiganaji hodari wenye uchungu na nchi yao.

Kwa hio basi, njia ya pili ambayo mkuu Kitila amependekeza ndio njia pekee ya kurekebisha mfumo wa siasa Tanzania na baadae mifumo mingine kama vile wafanyakazi na wahangaikaji wote.

Kushiriki katika shughuli za serikali kwa kuwa mpinzani (tuchukulie wapiganaji wameunda chama chenye nguvu) ni njia muafaka pale tu ikiwa asilimia zaidi ya kumi katika bunge ni wapiganaji waliounda chama cha upinzani chenye nguvu na ambacho kitawakutanisha wabia wote wana JF, wana mazingira, wafanyakazi, wanasheria, wachumi na wataalam wengine.

Ila sina hakika kama wapiganaji hawa watakuwa tayari kukabiliana na hii "challenge" ya ufisadi na viota vyake vyote kama vile wafanyabiashara wakubwa, makampuni ya kigeni na NGOs za kutoka nje, maana hawa ni tatizo.

- Mkulu Richard, sawa sawa another Great Thinking haya ya kwako pia ni maneno mazito sana, yamefika.

Respect.

Field Marshall Es!
 
- Mkuu Pundamilia, tulikuwa tunajadili hoja, sasa imekuwaje tena umeamua kwenda nje ya hoja? Now naomba nikuambie hivi hii chini ndiyo the most trusted version ya yaliyojiri ndani ya kikao, na imeandikwa na the most trusted paper ya bongo, yaani IPP Media kwa Mzee Mengi, sasa nakuomba uichambue halafu uiambie hii forums ni wapi wamesema ambacho sikukiripoti, na pia ninakuwekea wekundu kwenye yote niliyoyasema!

- Halafu kumbuka mimi sijadai hata mara moja kwamba nilikuwemo ndani ya kikao, kama wewe ulivyodai na hoja yako ya Sitta hakuomba radhi, sasa what are you saying kwamba hilo tu ndilo lililozungumzwa huko ndani yaani Sitta kutoomba au kuomba msamaha?

- You can't have it both ways mkuu, sio wote hapa JF ni wajinga kwamba unajidanganya wewe mwenyewe, kama huwezi kujadili hoja wapo ambao wapo tayari kujadili hoja mkuu, jiheshimu ili uheshimiwe kama huna hoja basi waachie wenye nazo wajadili hoja, lakini hatuwezi kuharibu mjadala kwa sababu you can't get your way! Hebu soma hapa hawa wanalipwa kufanya hii kazi, mimi ninajitolea tu mkuu:-

Urambositta.jpg

Speaker Samuel Sitta addressing a rally at Urambo yesterday. (PHOTO: Edwin Mjwahuzi)

Mkuu FMES,
I respect your views lakini hata hivyo taarifa kamili ya nini kilichojiri katika kikao cha NEC ya CCM zimeshatolewa na mambo si kama hivyo ulivyokuwa unayaripoti. For that matter, I am no longer going to discuss anything on this thread kwa vile ukweli tayari umeshapatikana.
 
Pundamilia,

Ukweli gani? Tangu tamko rasmi la yaliyojiri kweli vile vikao lilipotolewa na Chiligati, kuna watu wangapi wamefafanua tamko hilo? Na kwa kadri wanavyozidi kufafanua ndivyo wanavyozidi kujikanyaga na kujichanganya.

Tatizo ni kwamba vile vita vilivyo ndani ya CCM vinapiganwa na watu wengine ambao hawako smart. Kuna baadhi ya wajumbe walio kwenye kambi ya RA na EL ambao waliamua kuwa-feed waandishi wao wa habari info zote kama zilivyo na magazeti yakaripotii kama walivyoambiwa. Wao walidhani kwamba wananchi watazipokea kwa furaha. Jamii imezipokea kwa mshangao na masikitiko makubwa na nina uhakika kuna watu wanajuta kwanini walioongea hivyo kwenye vikao maana ujinga waliousema tayari uko mitaani na wao tunawahesabu kwamba ni mafisadi tu.

Hivi CCM huwa hawajifunzi kutokana na makosa? Walipomfungia Zitto walishangilia sana Bungeni, kilichofuata wanakijua wao wenyewe, mawaziri ilibidi waanze kukwepa kutembea kwa kuogopa kuzomewa na kuitwa mafisadi na wakaanza kusema wanazunguka nchi nzima kuelezea bajeti, lakini hawakuwa wanaelezea bajeti walikuwa wanaficha ujinga walioufanya bungeni. Sasa naona NEC wamerudia tena na labda walirudia hayo kwa kuwa walijua wanafanya vikao vya siri na kumbe ni vikao vya wazi, maana wajumbe walikuwa wana rekodi kila kitu na hao hao mafisadi ndiyo walikuwa wa kwanza kwenda kuwapa waandishi habari details zote.

Ukisoma ile habari iliyoandikwa Tanzania Daima unakuta kuna sehemu nyingi tu wanam-refer RA kama source yao. Bado mnasema kwamba chama hakina nidhamu na wanaotoa siri za vikao ni hao hao mafisadi. Siku wajumbe wa upande wa pili wakitoa hizo siri za yaliyosemwa kwenye vikao ndipo mnakuja juu kama moto wa kifuu, lakini kama source ni RA ni sawa tu, maana anachokisema kina maslahi kwa chama kwa kuwa kinatetea maslahi ya mafisadi.

Kilichoandikwa kwenye magazeti yote kinatofautiana kwa kiasi kikubwa sana na tamko la Chiligati. Tamko haliko wazi limefunika funika mambo. Tamko limejaa unafiki mtupu, hawataki kuwa wazi kwamba wanatetea ufisadi na badala yake wanakuja na uongo kwamba Bunge limegeuzwa kuwa Ze Comedy na kufanya malumbano. Hoja ya kutetea maslahi ya mafisadi imejadiliwa kwa masaa zaidi ya 10, lakini serious issues za kupanga mikakati ya kuendeleza wananchi zinajadiliwa kwa nusu saa na hakuna hata wachangiaji. Impliedly, mafisadi ni muhimu sana kuliko wananchi zaidi ya milioni 40. Bado unasema kwamba CCM ni nambari one? Hicho chama ni mkusanyiko wa mafisadi ambao wameamua kuifilisi hii nchi kwa kutumia kila aina ya mbinu chafu.

- Mkuu Keil, sawa sawa yaani hii ni ile ile ya line za Great Thinking.

Respect.

Field Marshall Es!
 
Kwa kuwa wao pia ni kama kundi, wakae pomoja waunde kundi A na B,

Kundi A litoke CCM na kujiunga na wapambanaji wengine ili kuongeza nguvu na kuwahakikishia watanzania kuwa Tanzania isiyo na Mafisadi inawezekana

Kundi B libaki CCM na liendelee kupambana na mafisadi ndani kwa ndani, kundi hili litawanyima mafisadi kubuni baadhi ya mipango ndani ya CCM kwa kuwa watajua si wote wafuasi wao, kwa mfano kama CCM yote itabaki kuwa ya mafisadi ni rahisi kwao kupanga mpango wa kuwamaliza wapinzani wao (either political death or physical death ... utajaza mwenyewe), mfano mzuri ni kwamba, wakati kina Nyerere wanapigania uhuru walipata msaada kutoka kwa baadhi ya Waingereza ambao walikuwa wanawapa tip .... kwamba kimepangwa hiki na hiki.

Ikumbukwe kuwa Vita dhini ya mafisadi (tangu ilipoanza rasmi pale mwembe yanga) imekuja kwa kuwashitukiza (it has taken them by suprise) na mpaka sasa wemetumia pesa nyingi sana kujaribu kuizima, na wanatumia pesa nyingi sana kununua supporters na hawapati dili za pesa kama ilivyokuwa zamani,

kwa ufupi ni kwamba wanatumia pesa nyingi na hawaingizi chochote

Nini kosa la kuwaachia Mafisadi uhuru 100% ndani ya CCM?
Mafisadi wanahitaji Mwaka mmoja tu wa uhuru ndani ya chama/serikali ili waikamue vilivyo Tanzania kiasi kwamba watarudisha ghalama zao na kujilimbikizia utajiri mkubwa kwa ajili yao mpaka watoto wa wajukuu zao.

Tafadhali wasipewe hiyo nafasi.

- Mkuu MC, umesikika sana na haya ni yale yale ya Great thinking, saafi sana na ni mawazo yaliyotulia.

Respect.

Field Marshall Es!
 
Back
Top Bottom