Nini iwe hatma ya Wapiganaji walio CCM, Warudishe kadi au?

Tatizo hata hao tunao waita "wapiganaji" kuna wengi tu kati yao ni wanafiki and they are just paying lip service. Kama wapiganaji wapo very serious waunganishe nguvu na kuunda chama kipya from the ground up. Ila hii ita hitaji kuji tolea kwa hali ya juu na kutambua kwamba wao wanaweza wasi faidi hayo matunda binafsi(kwa maana wasianzishe chama kipya kwa kila mmoja wao kuwa na dhana ya kupata cheo fulani). Tanzania ina hitaji chama walau kimoja cha upinzani chenye nguvu na hiyo inaweza kuwa ndoto ya wapiganaji hao.

- Sawa sawa mkuu, mawazo mazito sana na tupo pamoja hapo, ndio mambo ya Great Thinking haya na yatafikishwa kama yalivyo.

Respect.

Field Marshall Es!
 
CCM ni Chama cha Wakulima na Wafanyakazi! Mafisadi Ondokeni! Rev. Kishoka
user_offline.gif
Yesterday, 11:58 PM
Katika sehemu ya kwanza ya Katiba ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kifungu cha cha tatu, hitimisho la Azimio la kuunganisha TANU na ASP linasema hivi:

Quote:
12n2_01.png

Tumeamua kwa pamoja kuunda Chama kipya cha kuendeleza Mapinduzi ya Kijamaa nchini Tanzania na Mapambano ya Ukombozi wa Afrika juu ya misingi iliyojengwa na TANU na ASP.

Kisha katiba ya CCM inaendelea kwa kusema hili

Quote:
12n2_01.png

Chama tunachokiunda tunataka kiwe chombo madhubuti katika muundo wake na hasa katika fikra zake na vitendo vyake vya kimapinduzi vya kufutilia mbali aina zote za unyonyaji nchini, na kupambana na jaribio lolote lile la mtu kumuonea mtu au shirika au chombo c a nchi kuonea na kudhalilisha wananchi, kudhoofisha uchumi au kuzorotesha maendeleo ya Taifa; Chama tunachokiunda tunataka kishike barabara
hatamu za uongozi wa shughuli zote za umma kwa maslahi ya wafanyakazi na wakulima wa Taifa letu; Chama tunachokiunda tunataka kiwe kiungo kati ya
wanamapinduzi wa Tanzania na wanamapinduzi wenzetu kokote waliko.

Halafu katika kifungu cha nne kinachozungumzia Imani ya CCM, katiba ya CCM inasema

Quote:
12n2_01.png

4. Chama Cha Mapinduzi kinaamini kwamba:
(1) Binadamu wote ni sawa.
(2) Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake.
(3) Ujamaa na Kujitegemea ndiyo njia pekee ya kujenga jamii ya watu walio sawa na
huru.

Kisha ukiendelea nakifungu cha tano kinachogusia malengo ya CCM utakuana na maneno mazito na yenye nguvu kama yafuatayo:

Quote:
12n2_01.png

(2) Kulinda na kudumisha Uhuru wa Nchi yetu na raia wake.
(3) Kuhimiza ujenzi wa Ujamaa na Kujitegemea kwa mujibu wa Azimio la
Arusha.
(5) Kuona kwamba kila mtu anayo haki ya kupata kutoka katika Jamii hifadhi ya
maisha yake na mali yake kwa mujibu wa sheria.​
(6) Kuona kwamba katika Nchi yetu kila mtu aliye na uwezo wa kufanya kazi anafanya kazi; na kazi maana yake ni shughuli yoyote halali inayompatia mtu riziki yake.
(7) Kusimamia haki na maendeleo ya Wakulima, Wafanyakazi na Wananchi
wengine wenye shughuli halali za kujitegemea; na hasa kuona kwamba kila
mtu ana haki ya kupata malipo yanayostahili kutokana na kazi yake.​
(12) Kuona kwamba Dola inakuwa Mhimili wa Uchumi wa Taifa.
(13) Kuona kwamba Serikali na Vyombo vyote vya Umma vinasaidia kwa vitendo kuanzishwa na kuendeleza shughuli za Ushirika na za Ujamaa, na shughuli nyinginezo halali za wananchi za kujitegemea.
(14) Kuona kwamba matumizi ya utajiri wa Taifa yanatilia mkazo maendeleo ya Wananchi na hasa jitihada za kuondosha Umasikini, Ujinga na Maradhi.​
(16) Kuona kwamba katika nchi yetu hakuna aina yoyote ya dhuluma, vitisho, ubaguzi, rushwa, uonevu na/au upendeleo.
(17) Kuendelea kupiga vita Ukoloni Mamboleo,ubeberu na ubaguzi wa aina yoyote.

Ukimaliza malengo na imani ya chama, kinachofuatilia ni Uanachama na wajibu wa Mwanachama wa CCM

Quote:
12n2_01.png

(3) Kuwa mtu mwenye kuamini kuwa kazi ni kipimo cha Utu, na kuitekeleza imani hiyo kwa vitendo.
6) Kuwa wakati wote ni mfano wa tabia nzuri kwa vitendo vyake na kauli yake, kuwa mwaminifu na kutokuwa mlevi au mzururaji.
(7) Kuwa ama Mkulima, Mfanyakazi, au mwenye shughuli nyingine yoyote halali ya kujitegemea.
(2) Kutumikia nchi yake na watu wake wote kwa kutekeleza wajibu wake bila hofu, chuki wala upendeleo wa nafsi yake, rafiki au jamaa.
(3) Kujitolea nafsi yake kuondosha Umasikini, Ujinga, Maradhi na Dhuluma, na kwa jumla kushirikiana na wenzake wote katika kujenga Nchi yetu.​
(4) Kuwa wakati wote mkweli, mwaminifu na raia mwema wa Tanzania.​
(7) Kuwa tayari kujikosoa na kukosolewa ili kuweza kuwa na msimamo sahihi wa siasa ya CCM.

Mwishoni, Katba hii ya CCM toleo la mwaka 2001 linaweka Ahadi za Mwanachama wa CCM ambazo ni hizi

Quote:
12n2_01.png

AHADI ZA WANACHAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI
(1) Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja
(2) Nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote.
(3) Nitajitolea nafsi yangu kuondosha umaskini, ujinga, magonjwa na dhuluma.
(4) Rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa.
(5) Cheo ni dhamana, sitatumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu.
(6) Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na kuitumia elimu yangu kwa faida ya wote.
(7) Nitashirikiana na wenzangu wote kujenga nchi yetu.
(8) Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.
(9) Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa CCM na raia mwema wa Tanzania na Afrika.

Sasa ukishaisoma katiba ya CCM kisha ukasoma sehemu kadhaa za Muongozo wa CCM wa Mwaka 1981 hasa kifungu cha 36

Quote:
12n2_01.png

36. Aidha, kuna matatizo ya kijamii kama vile kuongezeka kwa rushwa, hujuma za
kiuchumi, wizi, ujambazi na uharibifu wa mali ya umma, mambo ambayo
yanatupunguzia nguvu zetu za kiuchumi na kudhoofisha dhamira ya umma ya
kujenga ujamaa. Haya yote yamo katika uwezo wa Chama, Serikali na wananchi
kuyapiga vita na kuyashinda.

utabaini kuwa Chama cha Mapinduzi kama Chama cha Kisiasa, kwa Miongozo yake na Katiba zake, si chama kibovu, bali hali halisi ya sasa hivi ni kuwa kuna genge ama kundi la watu fulani ambao wamejiingiza ndani ya Chama na kushikilia madaraka na mamlaka ndani ya Chama na Serikali ambao ndio wanaokiharibia sifa CCM, ndio wanaolihujumu Taifa letu na kutumia kisingizi kuwa anayepiga vita Ufisadi na Uhujumu ni mhaini!

Vikao viwili vikubwa vya CCM vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ambavyo vilanzia kule Butiama na hiki kilichoisha majuzi hapa Dodoma, vinaashiria wazi ni jinsi gani CCM iliyoundwa mwaka 1978 na malengo yake ya kimapinduzi katika kulijenga Taifa la Kijamaa na Kujitegemea, imetekwa nyara na kutumiwa kunufaisha wajanja wachache ambao ni watwana wa Wakoloni na Mabeberu, ni waroho, wavivu, wazembe, wasiowajibika na wanaojinufaisha kutumia hatamu ambazo CCM imepewa na Watanzania kuliongoza Taifa la Tanzania kwa manufaa yao binafsi.

CCM ni chama cha Wakulima na Wafanyakazi, si cha Wanafiki, Mafisadi au Wazembe!

CCM ni chama ambacho kilijijenga kwa Watanzania kwa ahadi za kulijenga Taifa letu liwe huru na lenye kujitegemea, liwe mfano wa kuigwa, na si Taifa dhaifu ambalo halina utashi wa kujiimarisha kwa kutumia Juhudi na Maarifa kupiga vita Ujinga, Umasikini na Maradhi!

Wanaoongoza CCM ni dhaifu na ndio wanaokidhoofisha Chama na kukipa taswira mbaya ambayo inanuka kama kidonda kilichooza.

Waliopewa dhamana ya kuongoza CCM katika ngazi zote anzia Mtaa, Kata, Kijiji, Tarafa, Wilaya, Mkoa na Taifa hawafai tena kuendelea kukiongoza Chama cha Mapinduzi au kunufaika kwa matunda ya Uimara wa CCM.

Uimara wa CCM umebakia kuwa nadharia na maneno na si vitendo na ndio sababu kauli za kipuuzi na kijinga zilizosikika Butiama na juzi Dodoma, zinadhihirisha wazi kuwa maneno ya Marehemu Kolimba kuwa CCM imepoteza dira kuwa ni maneno sahihi na ni lazima yapatiwe ufumbuzi.

Mimi nina jibu moja tena rahisi sana, nalo ni kuleta Mapinduzi ndani ya CCM kwa wale wote ambao wanasimama upande wa misingi ya awali na ya kweli ya kuundwa kwa CCM na wanaofuatilia masharti, wajibu, majukumu na dhamana ya kuwa Wana CCM, basi wao ndio walio warithi na wamiliki halisi wa CCM na si hawa wengine ambao wamegeuka na kuwa ndumilakuwili na kufikiria nafsi zao kwanza.

Walioko madarakani CCM wanatia AIBU!

Nasema tena kuwa CCM imetekwa nyara na mahaini na wahujumu ambao wanatumia kila nyenzo na nguvu za dola kujiimarisha kwa kutumia rushwa, wizi, uhujumu na kuvunja kabisa miiko ya uanachama na kupuuzia maagizo yote ya Chama ambayo bado hayajabadilika hata pamoja na kuwa tumeingia katika mfumo wa Vyama vingi na mfumo wa kiuchumi wa soko huria.

Hivyo basi, kauli ya Mchungaji kwa WanaCCM imara ni simameni kidete na msione haya Ufisadi ulioko ndani ya Chama! Msionee haya viongozi wabuvu na wazembe ambao wameendelea kushindwa kuleta maendeleo ya kweli kwa Tanzania!

Wapiganaji wa CCM, simameni imara msiyumbishwe na vitisho au mizenge. CCM ina wenyewe, na wenyewe ni Wakulima na Wafanyakazi na si Mafisadi na virabaka na makuwadi wao!

Asiwatishe mtu kwa kutumia kikao chochote kile cha Chama au hata vitisho vya kuvuliwa uanachama. Hakuna haja ya Walio CCM wa kweli ambao ni watiifu na waaminifu kwa Katiba na Miongozo ya CCM kuwa leo waondoke wakaunde Chama kingine cha Kisiasa au kuhamia chama kingine.

Jiungeni, mshikamane na mlete Mapinduzi ndani ya Chama, kwa maana wote hawa wanaotetea na kulinda ufisadi, wanaogopa kuondolewa madarakani na kuvuliwa uanachama, na hivyo wanaanza kuwatuhumu wale walio watiifu kwa Katiba ya CCM kuwa hawafuati maadili ya Chama na hawalindi maslahi ya Chama.

Maslahi ya CCM ni kuongoza Tanzania na kujenga Taifa imara linalotumia rasilimali zake kwa manufaa ya Wananchi wake.

Maslahi ya CCM ni kujenga Uongozi na kuwa na Siasa Safi ambazo lengo ni kumkomboa Mtanzania kutoka Unyonge wa kuwa Masikini, Mggonjwa na Mjinga.

Maslahi ya CCM ni kuhakikisha kuwa Tanzania inajitegemea na kujitosheleza.

Maslahi ya CCM ni kuhamasisha Uzalishaji mali, Utiifu wa Sheria, Haki, Utu na Uwajibikaji.

Haya ndio maslahi ya CCM ya kweli ya Wakulima na Wafanyakazi walioko pande zote za Muungano toka Wete, Vikokotoni, Malagarasi, Songea na Manyara.

Enyi mafisadi na vibaraka wenu, kiacheni CCM chama cha Wakulima na Wafanyakazi. Ondokeni mkaanzishe chama chenu kisicho na nidhamu wala dira!
 
But CCM spokesman John Chiligati denied reports claiming Speaker Sitta was at the centre of the subject during CC and NEC meetings. He blamed the press for reporting the case without conducting thorough investigation, a factor that distorts the truth.

“Among other things discussed, the meetings examined the situation in the party, including finding a better way to restore party discipline among our party members that now appears to be withering away,” he said.

Kama Chenge, Yona, Mramba na hata Lowassa, Karamagi na Msabaha walikiuka masharti ya Uongozi na kuvunja miiko ya Uongozi ambayo ndiyo misingi imara ya Nidhamu ya Chama, je Chama kimewachukulia hatua gani kwa Utovu wao wa nidhamu ambao umekiaibisha Chama na kukifanya kipakwe matope na kuwa na madoa yanayonukia Ufisadi, Hujuma na Rushwa?
 
- I understand, lakini tatizo hapa sio tafsiri yako na yangu, tatizo ni katiba au sheria ya Jamhuri, ni kwamba Spika na wapiganaji wameapa kulinda sheria na katiba ya jamhuri, na sio ilani ya CCM ndani ya bunge, sidhani kama unahitaji kua professor kuelewa hili, na it has nothing to na fikra zako au zangu!

- Spika na wabunge wote wapiganaji wanaangukia kwenye kikaango cha sheria ya jamhuri, na sio ilani za CCM walipochaguliwa kuwa wabunge as far as taifa is concerned waliapa kusimamia katiba ya jamhuri, ni kamati ya maadili ya bunge peke yake ndiyo yenye mamlaka kisheria kuwathibiti kama wanaleta upiganaji bungeni kinyume na sheria, ni simple politics ambazo hata huhitaji maadili ya ufisadi kutoka CCM, kuelewa!

- Hatuna sheria yoyote inayosema kwamba matatizo ya ndani ya CCM yahamishiwe kwenye bunge la taifa, kama kuna matatizo CCM basi yamaliziwe huko huko bila kugusa Bunge, bunge ni la Jamhuri sio la CCM, kikao cha NEC kuwashambulia wabunge wa jamhuri na Spika wake ni makosa sana kisheria, sisi Jamhuri we could careless kama hawa wabunge ameapa huko CCM au hawakuapa, what we care ni kwamba waliapa kwa Jamhuri, je wamevunja kiapo chao kwa Jamhuri? Wa kutuambia hayo sio NEC ya CCM, ila Attorney General au kamati ya maadili ya bunge!

- Spika kuwa na kundi lake ndani ya wabunge huko bungeni kama ni kuvunja sheria ya jamhuri basi tuambie ni kifungu gani kilichovunjwa, kama huko CCm mna matatizo yamalizeni huko huko msituletee kwenye Jamhuri.

- Wabunge wamezungumzia kukerwa na mafisadi ndani ya serikali, na sio huko kwenu CCM, tunachojali ni katiba ya jamhuri, sio ilani za kifisadi za CCM, kama mnataka kujiondoa jiondoeni huko CCM, lakini sio kushambulia Mhimili muhimu wa taifa letu kama Bunge.

- Ninarudia hivi, kama huko CCM mnataka kuondoana basi mmalizane huko huko msituingilie kwenye bunge!

Respect.

Field Marshall Es!
Hapa tupo pamoja mkuu. Real great thinking.
 
FMES hivi nini kilimfanya Nyerere kuwafukuza akina Seif Sharifu na wenzake ndani ya Chama...?

Kitu Kimoja Nyerere alikuwa hapendi ni Upinzani Ndani ya Chama...CCM ya sasa inafuata kanuni hiohio...!!! Wanachokifanya akina Sita na Wenzake japo wao wenyewe si Wasafi kwa Sura ya wananchi ni kizuri...ie kuonesha Maovu...lkn kwa Upande Mwingine kinakidhooficha CCM...!!!

Wasafi CCM hakuna...!!! Kama wao ni wasafi watoke "CCM" Kuwaambia wabakie CCM maana yake ni wao ni MAFISADI...!!! Nchi Kila Kona Imeoza..Haijaoza tu ktk mambo 2 au 3....!!!

.....Pia mnawatia Uwoga kuwa ukiwa Nje ya System ya CCM utakufa Njaa... Wapeni Ujasiri ya kuweza...Waacheni wafeel the real struggle Nje ya CCM...Kuwepo ndani ya CCM ni kuendelea Kuneeemeka na Manufaa ya UFISADI...!!!
 
Waheshimiwa,

Suala hili lina speculations za element ya RUSWA. Je TAKUKURU watachukua hatua au vikao vya vyama havihusiki katika kuchunguzwa?
 
Waheshimiwa,

Suala hili lina speculations za element ya RUSWA. Je TAKUKURU watachukua hatua au vikao vya vyama havihusiki katika kuchunguzwa?
Kesi ya nyani tuipeleke kwa ngedere aisimamie?!

Btw, habari za masiku Bibi Ntilie?!...Umepotea sana siku za hivi karibuni.
 
SteveD, Utu uzima unaleta shida lakini nimo katika kusoma michango yenu ninapopata nafasi.

Mie nadhani panapokuwepo shutuma za rushwa inabidi TAKUKURU wawajibike haraka sana katika kutafuta ukweli wa mambo ili haki itendeke kwanza kwa wale walioathirika kutokana na Rushwa hiyo. Pia wale wanaoshutumiwa kutoa ama kupokea rushwa wachukuliwe hatua kurejesha imani ya wananchi kwa CCM na Serikali yake.

Kama ni kweli wajumbe hao walipokea rushwa kwa madhumuni yaliyopangwa, ni aibu kubwa kwa wajumbe waliopewa heshima na wanachama wenzao ya wadhifa mkubwa wa ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama kuweza kupokea rushwa ili kumhujumu mwanachama/Mjumbe mwenzao! Ikibainika kama kweli wapo waliotoa na waliopokea hiyo rushwa ndio, hao ndio wanaopaswa kufukuzwa kwenye chama. Mambo ya aina hii yakiachwa kupita hivi hivi yatazidi kukiangamiza CCM.

SteveD, uko sahihi kabisa kesi ya ngedere haiwezi kupelekwa kwa nyani, lakini nyani wetu hakupaswa kujivika unyani; alipaswa kuwa chui/simba asiye na huruma na mhalifu wa aina yoyote.
 
Nikirejea kwenye mada, wapiganaji wala hawana sababu ya kurudisha kadi zao ukizingatia kwamba ni watu wachache ndio wanaokihujumu Chama chenye itikadi safi, katiba na miongozo iliyosheheni mambo mengi mazuri na ya msingi yenye manufaa kwa Chama chenyewe na Taifa kwa ujumla. Kinachotakiwa ni wapiganaji tunaowajua pamoja na watu wengine wasafi ndani ya Chama kuunganisha nguvu na kuweka mikakati madhubuti ya kuwadhibiti hao wachache wanaokiharibu chama badala ya kuwaachia waendelee na vitendo vyao vinavyoelekea kwenye kuangamiza Chama, Serikali na Taifa.

Naamini kwamba haikuwezekana Mzee Sitta kupokwa uanachama wake kutokana na busara za watu wenye msimamo ndani ya chama hicho walioelewa vyema kilichokuwa kikiendelea na kwamba endapo kundi la mahasimu wa Mzee Sitta lingeendekezwa, Chama kingeathirika vibaya.
 
Mkuu Kitila Mkumbo, mawazo yako ni mazuri sana tu. Ila mtazamo wangu ni kinyume na fikira zako.

Kwa mtazamo wangu, hatua yoyote ya kurudisha kadi, kujitoa au kuacha mapambano na ufisadi ni kusalimu amri (kitu ambacho ni cha hatari sana kwa Taifa, kwa sasa). Sababu za imani hiyo ni kama zifuatazo;
1. Mafisadi walio ndani ya chama wana sali sana wanachama wanaopingana nao wajitoe kwenye chama. Hii itawasaidia kupambana na kauli zao kwa kuzichukulia kuwa ni za wapinzani, wataweza kuwazulia kashfa za uongo n.k.
2. Wapambanaji hao bado wanaamini kuwa CCM ni chama chenye sera nzuri, wanakubaliana na itikadi na imani za chama hicho kwa kiasi kikubwa
3. Ni vigumu sana kuhama chama na kuweza kujiimarisha kwenye chama kingine ambacho si rahisi sana kujua sera na imani zake na kuweza kusimamia sera na imani hizo (uanachama hauishii kwenye kadi tu, bali ni lazima uendane na uelewa
kamili wa imani ya chama hicho)
4. Mapambano yanayofanyika ndani ya chama ndio yanayoweza kuleta mageuzi ya kweli. Naamini kuwa si rahisi kusafisha chumba ukiwa nje ya chumba hicho. Vile vile, wahenga walisema "fimbo ya mbali ..."
5. Wakosefu ndani ya chama si hao wanaitwa wapiganaji/wapambanaji na ufisadi. Wao wanalinda maslahi ya chama na taifa kwa kufuata kwa vitendo imani na sera za chama. Wanaoshindwa kutii ni mafisadi ambao wao hasa ndio wanaotakiwa waondoke kwa kushindwa kusimamia viapo vyao na imani na sera za chama chao.

Mkuu, sifahamu mwana mapinduzi aliejitoa kwenye chama (bila kuwa na madaraka makubwa) na kuweza kusimama kisiasa na kupambana na mahasimu wake. Mifano ya Mrema (ambae kwa mtazamo wangu hakufanikiwa kisiasa) ni mmoja wa mifano hai ya kushindwa pamoja na nguvu kubwa mtu anayoweza kupewa na baadhi ya waumini wake. Mbingu wa Mutharika alijitoa kwenye chama bila kupoteza madaraka yake ya uRais na hivyo kubaki kuwa na nguvu kubwa hata alipoamia/anzisha chama kingine.

Mapambano yote ni lazima yafanyikie ulingoni. Ulingo tulionao ni huo wa kuwa ndani ya chama. Mafisadi waondoke, waachie chama kabla hawajakimaliza na kumaliza nchi yetu kabisa. Hawana nia njema kwa Taifa hili hata kidogo. Wasiachiwe watawale kiurahisi. Njia pekee ni kwa wapiganaji kuendelea bila kurudi nyuma.
 
Kwa jinsi hali ilivyo ndani ya CCM ni vigumu sana kwa wapiganaji wetu kupata mafanikio katika vita hii kubwa dhidi ya ufisadi. Chama kimeshikwa na mafisadi wenye nguvu kubwa ya pesa walizowaibia Watanzania. Kama mlivyojionea kwenye vikao vya CC na NEC ni rahisi sana wawakilishi wetu kununuliwa na kufanya maamuzi ya ajabu ambayo yatazidi kuichimbia hii nchi kwenye lindi la umasikini. TUFANYE NINI? Sisi wachache ambao tumefumbuka macho tufanye jitihada za makusudi za kuwaelimisha watanzania wenzetu (kila mmoja mahali alipo) ili waanze kuachana na hiki chama cha mafisadi. Tuanze utaratibu, kwa kushauriana na wapiganaji wetu walioko ndani ya CCM, wa kuanzisha chama kikubwa chenye nguvu ya wananchi ambacho hatimaye ndicho kitakachosimamia UHURU wetu. Tunaweza kuchangia humu ni jinsi gani tunaweza kuanza mkakati huo. Hatujachelewa! Tuanze sasa!
 
FMES hivi nini kilimfanya Nyerere kuwafukuza akina Seif Sharifu na wenzake ndani ya Chama...?

Kitu Kimoja Nyerere alikuwa hapendi ni Upinzani Ndani ya Chama...CCM ya sasa inafuata kanuni hiohio...!!! Wanachokifanya akina Sita na Wenzake japo wao wenyewe si Wasafi kwa Sura ya wananchi ni kizuri...ie kuonesha Maovu...lkn kwa Upande Mwingine kinakidhooficha CCM...!!!

Wasafi CCM hakuna...!!! Kama wao ni wasafi watoke "CCM" Kuwaambia wabakie CCM maana yake ni wao ni MAFISADI...!!! Nchi Kila Kona Imeoza..Haijaoza tu ktk mambo 2 au 3....!!!

.....Pia mnawatia Uwoga kuwa ukiwa Nje ya System ya CCM utakufa Njaa... Wapeni Ujasiri ya kuweza...Waacheni wafeel the real struggle Nje ya CCM...Kuwepo ndani ya CCM ni kuendelea Kuneeemeka na Manufaa ya UFISADI...!!!
Mkuu Chuma, ni kweli kabisa upinzani usio na maana ndani ya chama haufai na unaweza kukiua chama. Nyerere alikuwa akipambana na watu waliokuwa wakifanya mambo kinyume na taratibu, itikadi na imani za chama. Hakuwa na mgogoro na mtu yeyote aliefanya mambo kwa mujibu wa kiapo alichokula.

Kwa upande mwingine, viongozi wanaoitwa mafisadi ndani ya chama ni wakiukaji wakubwa kabisa wa imani, sera na misingi ya chama. Ila wao wanajidai kuwa wengine ndio wanaokiuka misingi hiyo, na kwa bahati mbaya wanaungwa mkono na wale waliotakiwa kuwakanya.

CCM inauawa na wanaotuhumiwa kuwa mafisadi na wale wanaowaunga mkono. Kusingizia kuwa akina Sitta ndio wanaoiua CCM ni kujidanganya sana. Sifa za chama zilianza kuporomoka mara baada ya serikali kushindwa kuchukua hatua kwa mafisadi wote na kushindwa hata kutoa ufumbuzi (kama si kutekeleza) maazimio ya Bunge. Wanaopingana na Mafisadi wanachofanya kikubwa ni ku-echo tu kelele za wananchi ambazo zilianza zamani sana.
 
Tatizo wote hao unaotaka tuwashauri sio wapiganaji,wanaongea tu pale wanapona hakuna 10% zao mezani hakuna hata moja anasubutu kufanya kitendo hata kimoja tena hata kidogo maneno matupu hao.
We utaona now watakavyo watatisha watanzania tamaa.
Kama wapiganaji kweli wabaki humo humo washikamane mikono wapigane kwa vitendo now.
 
FMES hivi nini kilimfanya Nyerere kuwafukuza akina Seif Sharifu na wenzake ndani ya Chama...?

Kitu Kimoja Nyerere alikuwa hapendi ni Upinzani Ndani ya Chama...CCM ya sasa inafuata kanuni hiohio...!!! Wanachokifanya akina Sita na Wenzake japo wao wenyewe si Wasafi kwa Sura ya wananchi ni kizuri...ie kuonesha Maovu...lkn kwa Upande Mwingine kinakidhooficha CCM...!!!

Wasafi CCM hakuna...!!! Kama wao ni wasafi watoke "CCM" Kuwaambia wabakie CCM maana yake ni wao ni MAFISADI...!!! Nchi Kila Kona Imeoza..Haijaoza tu ktk mambo 2 au 3....!!!

.....Pia mnawatia Uwoga kuwa ukiwa Nje ya System ya CCM utakufa Njaa... Wapeni Ujasiri ya kuweza...Waacheni wafeel the real struggle Nje ya CCM...Kuwepo ndani ya CCM ni kuendelea Kuneeemeka na Manufaa ya UFISADI...!!!

- Mkuu Chuma, kwanza heshima yako mkuu na nimekusikia sana, watoke ndani ya CCM.

Respect.

FMEs!
 
Nikirejea kwenye mada, wapiganaji wala hawana sababu ya kurudisha kadi zao ukizingatia kwamba ni watu wachache ndio wanaokihujumu Chama chenye itikadi safi, katiba na miongozo iliyosheheni mambo mengi mazuri na ya msingi yenye manufaa kwa Chama chenyewe na Taifa kwa ujumla. Kinachotakiwa ni wapiganaji tunaowajua pamoja na watu wengine wasafi ndani ya Chama kuunganisha nguvu na kuweka mikakati madhubuti ya kuwadhibiti hao wachache wanaokiharibu chama badala ya kuwaachia waendelee na vitendo vyao vinavyoelekea kwenye kuangamiza Chama, Serikali na Taifa.

Naamini kwamba haikuwezekana Mzee Sitta kupokwa uanachama wake kutokana na busara za watu wenye msimamo ndani ya chama hicho walioelewa vyema kilichokuwa kikiendelea na kwamba endapo kundi la mahasimu wa Mzee Sitta lingeendekezwa, Chama kingeathirika vibaya.

- Bibi Ntilie hii yako ni katika zile zile za Great Thinking, nimekusikia sana, wabaki ndani ya CCM.

Respect.

FMEs!
 
Mkuu Kitila Mkumbo, mawazo yako ni mazuri sana tu. Ila mtazamo wangu ni kinyume na fikira zako.

Kwa mtazamo wangu, hatua yoyote ya kurudisha kadi, kujitoa au kuacha mapambano na ufisadi ni kusalimu amri (kitu ambacho ni cha hatari sana kwa Taifa, kwa sasa). Sababu za imani hiyo ni kama zifuatazo;
1. Mafisadi walio ndani ya chama wana sali sana wanachama wanaopingana nao wajitoe kwenye chama. Hii itawasaidia kupambana na kauli zao kwa kuzichukulia kuwa ni za wapinzani, wataweza kuwazulia kashfa za uongo n.k.
2. Wapambanaji hao bado wanaamini kuwa CCM ni chama chenye sera nzuri, wanakubaliana na itikadi na imani za chama hicho kwa kiasi kikubwa
3. Ni vigumu sana kuhama chama na kuweza kujiimarisha kwenye chama kingine ambacho si rahisi sana kujua sera na imani zake na kuweza kusimamia sera na imani hizo (uanachama hauishii kwenye kadi tu, bali ni lazima uendane na uelewa
kamili wa imani ya chama hicho)
4. Mapambano yanayofanyika ndani ya chama ndio yanayoweza kuleta mageuzi ya kweli. Naamini kuwa si rahisi kusafisha chumba ukiwa nje ya chumba hicho. Vile vile, wahenga walisema "fimbo ya mbali ..."
5. Wakosefu ndani ya chama si hao wanaitwa wapiganaji/wapambanaji na ufisadi. Wao wanalinda maslahi ya chama na taifa kwa kufuata kwa vitendo imani na sera za chama. Wanaoshindwa kutii ni mafisadi ambao wao hasa ndio wanaotakiwa waondoke kwa kushindwa kusimamia viapo vyao na imani na sera za chama chao.

Mkuu, sifahamu mwana mapinduzi aliejitoa kwenye chama (bila kuwa na madaraka makubwa) na kuweza kusimama kisiasa na kupambana na mahasimu wake. Mifano ya Mrema (ambae kwa mtazamo wangu hakufanikiwa kisiasa) ni mmoja wa mifano hai ya kushindwa pamoja na nguvu kubwa mtu anayoweza kupewa na baadhi ya waumini wake. Mbingu wa Mutharika alijitoa kwenye chama bila kupoteza madaraka yake ya uRais na hivyo kubaki kuwa na nguvu kubwa hata alipoamia/anzisha chama kingine.

Mapambano yote ni lazima yafanyikie ulingoni. Ulingo tulionao ni huo wa kuwa ndani ya chama. Mafisadi waondoke, waachie chama kabla hawajakimaliza na kumaliza nchi yetu kabisa. Hawana nia njema kwa Taifa hili hata kidogo. Wasiachiwe watawale kiurahisi. Njia pekee ni kwa wapiganaji kuendelea bila kurudi nyuma.

- Mkulu Recta kama kawaida yako, na Great Thinking sawa sawa na tupo pamoja sana hapo, wapiganaji wabaki ndani ya CCM.

Respect.

FMEs!
 
Kwa jinsi hali ilivyo ndani ya CCM ni vigumu sana kwa wapiganaji wetu kupata mafanikio katika vita hii kubwa dhidi ya ufisadi. Chama kimeshikwa na mafisadi wenye nguvu kubwa ya pesa walizowaibia Watanzania. Kama mlivyojionea kwenye vikao vya CC na NEC ni rahisi sana wawakilishi wetu kununuliwa na kufanya maamuzi ya ajabu ambayo yatazidi kuichimbia hii nchi kwenye lindi la umasikini. TUFANYE NINI? Sisi wachache ambao tumefumbuka macho tufanye jitihada za makusudi za kuwaelimisha watanzania wenzetu (kila mmoja mahali alipo) ili waanze kuachana na hiki chama cha mafisadi. Tuanze utaratibu, kwa kushauriana na wapiganaji wetu walioko ndani ya CCM, wa kuanzisha chama kikubwa chenye nguvu ya wananchi ambacho hatimaye ndicho kitakachosimamia UHURU wetu. Tunaweza kuchangia humu ni jinsi gani tunaweza kuanza mkakati huo. Hatujachelewa! Tuanze sasa!

- Mkulu Punch, heshima zaidi unajua maneno haya coming from you, ni very serious! Ninayachukulia haya maneno at your word mkuu ninaamini umeyafikiri sana kabla ya kuyasema, haya nimekusikia sana waondoke ndani ya CCM.

Respect.

FMEs!
 
Mkandara,

..Sitta alikuwa mwanamtandao. sasa ni kitu gani kimemkosanisha na wenzake? kwani hakuona uozo wote uliokuwa unaendelea?

..kama anataka imani yetu, the he has a lot of explanation to do.

..unajua hata mama ndani ya nyumba ukimkosea kuna kipindi cha mpito unabidi ufanye mambo fulani fulani kurudisha imani yake kwako. kwa mfano unaweza kulazimika kwamba ukitoka kazini moja kwa moja nyumbani hupitii tena vijiweni au kwenye wanzuki etc etc.

..tatizo letu wa-Tanzania kila analotutamkia mwanasiasa tunaliamini kwa wakati husika. hatuhoji kwamba mbona jana na juzi ulitoa kauli tofauti?
Nakubali kuwa Sitta alikuwa Mtandao, so was JK na wengine wengi tu. Ila nachelea kusema kwamba mtandao walianza kugawanyika wenyewe baada ya kifo cha Ditto.. sielewi kilichotokea haswa lakini nina hisia kubwa kuwa baada ya kifo cha Ditto, Mh. JK was done!...Haya ni mawazo yangu msiyachukulie kuwa ndio fact kwa sababu nashindwa kabisa kuelewa JK amekutwa na vitu gani kiasi kwamba hata kuongoza nchi anakwenda kama gari bovu tu..

Navyokumbuka mimi JK alianza kubadilika tu baada ya kifo cha Ditto..was it a concidence? sina uhakika ila nakumbuka vizuri jin Sitta , kina Mwakyembe na kundi lote la wabunge wa CCM walivyokuwa wakimshambulia Dr.Slaa na Zitto. Pale CCM mkali wetu alikuwa marehemu Amina Chifupa tu akiwa na ile list ya wauza Unga..lakini pamoja na yote hayo, tukiachana nayo ukweli unabakia kuwa JK alipochukua urais utengano ndani ya CCM ulikuwa baina ya CCM -Asilia na CCM Mtandao..baada ya kifo cha Ditto mambo yalibadilika kabisa within kundi hilo. Na nguvu ya wazee wa Asilia ikarudishwa..

Hivyo, kutokana na lawama za watu kwa JK na pengine hata baadhi ya watu kusema JK hakumlinda ndugu, mshikaji, na kipenzi chake ilimtibua JK na toka siku hiyo hakuwa na imani na kundi zima la Mtandao. Sina uhakika na habari hii lakini ni muhimu sote tukubali kwamba kuna sababu kubwa sana ambayo imemfanya JK kukaa mbali na wana Mtandao.
Haya yote yanayotokea leo ni matokeo ya mgawanyiko ktk kundi la Mtandao..
 
Haya yote yanayotokea leo ni matokeo ya mgawanyiko ktk kundi la Mtandao..

Nilidhani kugawanyika kwa mtandao kulitokana na UFISADI hivyo haya yote yanayotokea leo ni matokeo ya UFISADI na DHANA YA KULINDANA KATIKA KUSHUGHULIKIA MAFISADI ambao miongoni mwao ni vinara wa MTANDAO na walitumia kiasi fulani cha MAFAO YA UFISADI kujenga na kuimarisha MTANDAO?

Omarilyas
 
Hakuna haja ya kurudisha kadi pasipo ulazima, ulazima niuonao ni kwa hawa wapiganiji kulazimishwa kurudisha kadi zao ili wasiwenwanachama wa cahama A kwa lengo kwamba chama A kitabakia na nguvu kuliko vyama B, C, D n.k. Nadhani Tanzania ya kweli itajengwa na watanzania wa kweli pia, na watanzania wa kweli ni wale ambao daima hufikiria mstakabali wa nchi yao tofauti na maslahi ya vyama vyao.

Linapofika suala la maslahi ya Taifa itikadi zote za vyama yafaa ziwekwe kando na ndipo utaifa uendelee. Kigezo kwa mfano kwamba spika Sitta aliruhusu mno wabunge kuwa huru kuongea na kuibana serikali hakitoshi kumuachisha uanachama wake aliuchagua kwa demokrasia aliyoiona yeye(Sitta).

Pili kigezo kwamba wabunge wa ccm wanaibana serikali sana kama wabunge wa upinzani ni hoja nyepesi sana, kwani mbunge bungeni kazi yake ni nini?

Mwisho nadhana wapiganaji waendelee kupigania maslahi ya taifa hili na wote wapenda nchi tupo pamoja wasitishwe kupokwa kadi zao za vyama na kama wakipokwa kadi zao Tanzania ina vyama vingi na kwa kuwa wameshaonwa na watanzania wapenda nchi yao basi hawatakuwa natatizo la kuupata ubunge tena. Tuchoke sasa na tabia ya viongozi wapaswao kuwa wa watu(Umma ) kuwa viongozi wa kutafuta maslahi yao wenyewe.

"TANZANIA ITADUMU NA WENYE NIA NJEMA NAYO TU"
 
Back
Top Bottom