Nini iwe hatma ya Wapiganaji walio CCM, Warudishe kadi au?

Mimi nimesema wabaki lakini uzi uwe ule ule - kutetea maslahi ya taifa, kutetea uhuru wa Bunge na kuisimamia na kuilinda Katiba. Sioni mtego hapa kwa sababu kama watasimamia wanachoamini ni sawa bila kutetereka na CCM ikaamua kuwatosa, watakuwa wameshinda awamu ya kwanza kwenye hii vita - watapokewa na wananchi kama mshujaa.
I am trying hard to believe that somebody, somewhere, somehow is not trying to pool the wool over our eyes !

- Another Great thinking, hapo tupo pamoja sana mkuu.

Respect.

Field Marshall Es!
 
- Mkuu wangu vipi unaita Ufisadi kwamba ni lengo la kuimarisha chama? Halafu bado hujaelewa the ishu ni kwamba Spika anatakiwa apindishe sheria za bunge ili kukumbatia sera za ufisadi, wabunge wapiganaji hawakuapa kiapo cha kutetea ufisadi bungeni,

- Wamelaaniwa kwa sababu wanawashambulia mafisadi bungeni so kwenye chama, jaribu kuelewa tofauti, Spika sio mkuu wa chama ni Spika wa bunge, wapiganaji walioshambuliwa hawakushambuliwa kwa sababu wameshambulia chama, ila kwa sababu wameshambulia serikali bungeni, kitu ambacho ni wajibu wao kwa mujibu wa katiba!

- Ninaheshimu sana mawazo yako na ningeshangaa kama hii thread ingefika mpaka mwisho hujajitokeza kwa njia moja au nyingine, lakini bado huelewi mkuu the real ishu hapa, Spika ametimiza kazi yake bungeni, kama amekosea basi atakuwa amekosea kisheria, yaani amevunja katiba, sasa kwa nini CCM isimfikishe kwenye sheria, badala yake inamuita kwenye vikao visivyohusu katiba ya Jamhuri na kumtishia kwa kazi yake bungeni that is a crime byitself, sisi wananchi tungekua makini na wenye uwezo sasa hivi tulitakiwa kuwafungulia mashitaka NEC ya CCM, kwa kuvuruga katiba ya jamhuri , that is what they did Dodoma juzi ni kuichafua katiba ya Jamhuri, ndio maana Karume akagoma kwenda kushiriki kwenye kuvuruga katiba ya Jamhuri ya Muungano.

- Hebu nenda mkuu usome tena, kama ilani na itikadi ya CCM kama inasema CCM inafuata ufisadi, kwa hiyo hoja zako hapo mkuu nafikiri ni clear kwamba ni batili, wapiganaji wameapa kiapo cha kusimamia taifa na Jamhuri sio sera na itikadi za kifisadi.

Respect.

Field Marshall Es!

FMES,
Tafsiri uliyokuwa nayo wewe katika mawazo yako si lazima iwe ndiyo ileile niliyokuwa na yo mimi. Ukomavu katika maono ndiyo msingi mkubwa wa kukuza fikra. Kisiasa unaweza kubadili jambo lolote na kuliweka kule ambako wewe unataka kuvuta hisia na mawazo ya wale unaotaka wakuunge mkono na hali kadhalika mimi ninajaribu kupima uhalali wa yale unayoyatetea. Hii ndiyo kawaida na hakuna ubishi juu ya hili.

Spika na "wapiganaji' wote wanaangukia katika kikaango cha CCM ambacho kinawataka wanachama wote wafuate taratibu zilizowekwa. Pia ikumbukwe kwamba as long as wao ni wanachama wa CCM basi wanafungwa na taratibu na maamuzi ya chama chao. CCM ndiyo yenye serikali iliyoko madarakani na ndiyo yenye wabunge wengi bungeni kwa maana hiyo huwezi kuwa na CCM mbili zinazotawala nchi moja. Kitendo chochote cha kwenda kinyume na maelekezo na maagizo ya mwisho na juu ni kitendo cha utovu wa nidhamu hata kama una hoja yenye nguvu bado.

Washauri 'wapiganaji' wako kuwa neno 'fisadi' si ajenda ya mtu binafsi au ajenda ya kukipaka matope chama tawala.

Vilevile haya yote yanayotokea hayana tija yeyote kwa wapinzani wa CCM kwani hizi power struggle within CCM kwa ajili ya kiti cha urais cha 2015. Kundi linaloitwa la 'wapiganaji' ni another mtandao unataka kushika madaraka ya urais 2015 na wanategemea CCM zaidi ya ridhaa ya wananchi. Tumeona hata baadhi ya wanaCCM wakirushiana makombora wenyewe kwa wenyewe huko nyuma na leo hii ndiyo unatutanabahisha kuwa Sitta kumbe ana kundi lake la 'mashujaa' ndani ya CCM, ni mashujaa wa kufanya nini kama si wapigania nafsi zao?

Ajenda ya ufisadi isitumike katika kuhadaa wananchi kwa malengo binafsi na kuzorotesha juhudi za upinzani kujijenga kikwelikweli.

Whoever ambaye anao CCM haikidhi matarajio yake Mzee Malecele alisema AJIONDOE!!!
 
Pundamilia,

Yote tisa, ila hata kama tutabadilisha jina, kama hili la wapiganaji linakuudhi, basi labda wan JF watafute jina lingine lakini, labda tuwaiite ''Raia wema wa Tanzania'' kwa kipindi kifupi, SITTA amewafurahisha watanzania walio wengi ndani na nje ya nchi, amewafanya watanzania kufurahia siasa zaidi, naami 2010, watu wengi watajitokeza kwenda kupiga kura maana wengi sasa wanajua cha kufanya, tofauti kabisa ni kile jamaa yetu alichotufanyia, eti maisha bora ka kila mtanzania, aibu tupu.
Yaani nikwambie, sasa hivi Sitta ana heshima kuliko Msanii. Just by comparison. Wewe endelea tu kutetea chama, ila tukirudi Dodoma, tunaibuka na jipya, si umeona mwenyewe jinsi ambavyo serikali ilivyotolewa baru, mbiombio kupitia mawaziri wake katika bunge lililopita,wanatulteate ripoti za kifisadi bungeni tena mbele ya Sitta, halafu usifikiri ni Sitta tu, pia watanzania wanamuomba na Mungu pia asaidiê, hivyo vita ni kali mno, utashangaa tu jamaa wanapeta, kwa mfano, angalia Dr. Slaa, akiwa chumbani akagundua kuwa ametegeshewa kinasa sauti, utasema uchawi, kumbe sio, angalia Dr. Mwakyembe, watu walijua sasa basi, tumemshau, kumbe licha ya kuwa ajari ilikuwa mbaya, lakini anapeta, hivi kwa hii mifano michache, naomba ujue kuwa sidhani kama JK atapita 2010, alikosea sana kutudanganya.
 
Zurich,
As long as wako kwenye kikaango cha CCM basi hawana budi kufanya yale ambayo vikao vya juu yao vimeelekeza. (kuna ubishi hapa?)

Endapo kama kweli hawakubaliani na Chama chao, basi warudishe kadi (kuna ubishi hapo?)

Vinginevyo ni drama tu za kupigania madaraka ndani ya chama na hayana manufaa yeyote nje ya hapo.
 
Pundamilia,

''Vilevile haya yote yanayotokea hayana tija yeyote kwa wapinzani wa CCM kwani hizi power struggle within CCM kwa ajili ya kiti cha urais cha 2015''

Naomba nilekebîshe usemi hapa, watanzania wanasubiri kwa hamu 2010, na sio 2015. Wewe fikiria, badala ya watu kupewa maisha bora, inafikia hatua watoto wetu wanapewa pipi.

Pia kuendelea kukikumbatia chama tawala(CCM), ni sawa na kusafiri ndani ya meli ambayo ndani wamo wamerakani na humuhumo wamo magaidi(terrorists), pengine yumo Osama, hapo usalama ni mdogo sana, na kwa bahati mbaya hiyo meli inapitia upande wa Somalia, ohoo, utakutana na maharamia(watu waliochoka maisha, njaa, hakuna elimu, watu ambao hawataki kusikia tena msamiati wa maisha bora kwa kila mtu). Labda niseme, kama wamerekani hawatailipua hiyo meli, basi magaidi wenyewe watajilipua, au maharamia(pirates), wataiteka. Nasema hivi, wapiganaji(anti-grand corruption,wanaopinga ufisadi) ni vizuri washuke kutoka katika hiyo meli maana, kama wapiganaji wenyewe hawatailipua ccm, basi sisi raia tutafanya kazi(2010), maana nia ipo, ushahidi upo, tena kwa kasi mpya kabisa, na ari mpya kabisa na nguvu mpya kabisa.
 
Mkuu FMES kurudisha kadi ni moja ya option, lakini sio sasa. Kama BOB alivyosema "when one door is closed, many more are open". Wametuonesha njia na wametufunulia kahwa sasa it is up to us kuwasadia. Midomo ya haki haiko kwa wapiganaji wa CCM tu wakko wengine opposition na wako wengine nje ya bunge. 2010 is just around the corner upepo kwa CCM si mzuri, na kuna mengi tu yatatokea kwa sasa ni kuangalia tu upepo utavuma vipi in two three months to come then tutajua bendera inanyayuliwa vipi.

Mzizi wa fitna sasa hivi uko Igunga, kuna dalili ya kuanza kuung'oa,let us wait and see first. Kurudisha kadi kwa sasa kunaweza kuwarahisishia sana kazi mafisadi, kunaweza kukaja automatically so again leets wait and see what time brings to us.
 
Pundamilia,

''Vilevile haya yote yanayotokea hayana tija yeyote kwa wapinzani wa CCM kwani hizi power struggle within CCM kwa ajili ya kiti cha urais cha 2015''

Naomba nilekebîshe usemi hapa, watanzania wanasubiri kwa hamu 2010, na sio 2015. Wewe fikiria, badala ya watu kupewa maisha bora, inafikia hatua watoto wetu wanapewa pipi.

Pia kuendelea kukikumbatia chama tawala(CCM), ni sawa na kusafiri ndani ya meli ambayo ndani wamo wamerakani na humuhumo wamo magaidi(terrorists), pengine yumo Osama, hapo usalama ni mdogo sana, na kwa bahati mbaya hiyo meli inapitia upande wa Somalia, ohoo, utakutana na maharamia(watu waliochoka maisha, njaa, hakuna elimu, watu ambao hawataki kusikia tena msamiati wa maisha bora kwa kila mtu). Labda niseme, kama wamerekani hawatailipua hiyo meli, basi magaidi wenyewe watajilipua, au maharamia(pirates), wataiteka. Nasema hivi, wapiganaji(anti-grand corruption,wanaopinga ufisadi) ni vizuri washuke kutoka katika hiyo meli maana, kama wapiganaji wenyewe hawatailipua ccm, basi sisi raia tutafanya kazi(2010), maana nia ipo, ushahidi upo, tena kwa kasi mpya kabisa, na ari mpya kabisa na nguvu mpya kabisa.

Verdict ya 2010 katika kiti cha Urais ilishapita, hizi ni race za 2015 ndugu yangu. Wanasiasa wanaangalia sasa wajipange vipi kwa ajili ya 2015. Atakayeweza kufanya vizuri kwenye 2010 atakuwa anaweka mazingira mazuri ya 2015. Lakini ukipigwa bao mapema maana yake unakuwa na kibarua kigumu huko mbele ya safari.

Huu ni mchezo wa karata ni lazima ujue kuzichanga na kutambua mzungu amelala wapi.
 
Mkuu ES,

Wapiganaji hawana options kwenye ili, THERE IS ONLY ONE WAY FORWARD.

Kuendelea na kupinga ufisadi na kuacha jukumu la kufukuzwa CCM kwenye hands za NEC.

Trust me, CCM CAN NOT AFFORD TO SACK THEM, NO WAY.

Kumbuka kuna hao wajinga wanaoongea kuhusu kuwafukuza, lakini wameshapata picha namna nchi na hata mataifa mengine yanavyowashangaa, na wameanza kuback pedal.

Yaani NEC itasema tunawafukuza CCM sababu wanapinga ufisadi?? Which then means CCM wanasupport Ufisadi!!!!

HAIWEZEKANI MKUU, waambie wapiganaji waendelee kama kawaida na hiyo martyrdom wakipewa na CCM kwa kufukuzwa, ndio itakuwa mtaji wao kwenye furure political life yao.
 
Pundamilia07;FMES,
Tafsiri uliyokuwa nayo wewe katika mawazo yako si lazima iwe ndiyo ileile niliyokuwa na yo mimi. Ukomavu katika maono ndiyo msingi mkubwa wa kukuza fikra. Kisiasa unaweza kubadili jambo lolote na kuliweka kule ambako wewe unataka kuvuta hisia na mawazo ya wale unaotaka wakuunge mkono na hali kadhalika mimi ninajaribu kupima uhalali wa yale unayoyatetea. Hii ndiyo kawaida na hakuna ubishi juu ya hili.

- I understand, lakini tatizo hapa sio tafsiri yako na yangu, tatizo ni katiba au sheria ya Jamhuri, ni kwamba Spika na wapiganaji wameapa kulinda sheria na katiba ya jamhuri, na sio ilani ya CCM ndani ya bunge, sidhani kama unahitaji kua professor kuelewa hili, na it has nothing to na fikra zako au zangu!

Spika na "wapiganaji' wote wanaangukia katika kikaango cha CCM ambacho kinawataka wanachama wote wafuate taratibu zilizowekwa. Pia ikumbukwe kwamba as long as wao ni wanachama wa CCM basi wanafungwa na taratibu na maamuzi ya chama chao. CCM ndiyo yenye serikali iliyoko madarakani na ndiyo yenye wabunge wengi bungeni kwa maana hiyo huwezi kuwa na CCM mbili zinazotawala nchi moja. Kitendo chochote cha kwenda kinyume na maelekezo na maagizo ya mwisho na juu ni kitendo cha utovu wa nidhamu hata kama una hoja yenye nguvu bado.
Washauri 'wapiganaji' wako kuwa neno 'fisadi' si ajenda ya mtu binafsi au ajenda ya kukipaka matope chama tawala.

- Spika na wabunge wote wapiganaji wanaangukia kwenye kikaango cha sheria ya jamhuri, na sio ilani za CCM walipochaguliwa kuwa wabunge as far as taifa is concerned waliapa kusimamia katiba ya jamhuri, ni kamati ya maadili ya bunge peke yake ndiyo yenye mamlaka kisheria kuwathibiti kama wanaleta upiganaji bungeni kinyume na sheria, ni simple politics ambazo hata huhitaji maadili ya ufisadi kutoka CCM, kuelewa!

Vilevile haya yote yanayotokea hayana tija yeyote kwa wapinzani wa CCM kwani hizi power struggle within CCM kwa ajili ya kiti cha urais cha 2015. Kundi linaloitwa la 'wapiganaji' ni another mtandao unataka kushika madaraka ya urais 2015 na wanategemea CCM zaidi ya ridhaa ya wananchi. Tumeona hata baadhi ya wanaCCM wakirushiana makombora wenyewe kwa wenyewe huko nyuma na leo hii ndiyo

- Hatuna sheria yoyote inayosema kwamba matatizo ya ndani ya CCM yahamishiwe kwenye bunge la taifa, kama kuna matatizo CCM basi yamaliziwe huko huko bila kugusa Bunge, bunge ni la Jamhuri sio la CCM, kikao cha NEC kuwashambulia wabunge wa jamhuri na Spika wake ni makosa sana kisheria, sisi Jamhuri we could careless kama hawa wabunge ameapa huko CCM au hawakuapa, what we care ni kwamba waliapa kwa Jamhuri, je wamevunja kiapo chao kwa Jamhuri? Wa kutuambia hayo sio NEC ya CCM, ila Attorney General au kamati ya maadili ya bunge!

unatutanabahisha kuwa Sitta kumbe ana kundi lake la 'mashujaa' ndani ya CCM, ni mashujaa wa kufanya nini kama si wapigania nafsi zao? Ajenda ya ufisadi isitumike katika kuhadaa wananchi kwa malengo binafsi na kuzorotesha juhudi za upinzani kujijenga kikwelikweli.

- Spika kuwa na kundi lake ndani ya wabunge huko bungeni kama ni kuvunja sheria ya jamhuri basi tuambie ni kifungu gani kilichovunjwa, kama huko CCm mna matatizo yamalizeni huko huko msituletee kwenye Jamhuri.

Whoever ambaye anao CCM haikidhi matarajio yake Mzee Malecele alisema AJIONDOE!!!

- Wabunge wamezungumzia kukerwa na mafisadi ndani ya serikali, na sio huko kwenu CCM, tunachojali ni katiba ya jamhuri, sio ilani za kifisadi za CCM, kama mnataka kujiondoa jiondoeni huko CCM, lakini sio kushambulia Mhimili muhimu wa taifa letu kama Bunge.

- Ninarudia hivi, kama huko CCM mnataka kuondoana basi mmalizane huko huko msituingilie kwenye bunge!

Respect.

Field Marshall Es!
 
Mada nzito hii.

Hapa tulipofikia, ni vigumu sana kusema unapingana na ufisadi bila kuipinga CCM. Hii ni kwa sababu viongozi wengi kupitia CCM waliingia madarakani kwa kufadhiliwa na hao tunaowaita mafisadi, na inaonekana wanaendelea kuwa watiifu kwao.

Sasa kama hivyo ndivyo, hawa tunaowaita mashujaa wa taifa ndani ya CCM wanachofanya ni kukata mti walioukalia, nao lazima wataanguka. Lakini kabla hawajamaliza kuukata huo mti waliopo nao huko juu hawatakubali waukate hadi uanguke; watawatupa wao chini na wao waendelee kubaki katika huo mti.

Kwa vikao vya juzi, ni wazi kwamba wana CCM katika NEC wanachukizwa sana na tabia za akina Sita na wenzake za kuwabana mafisadi. Hawa wanawaona kwamba wanaibana CCM, na hawatakubali na wameonyesha hivyo juzi. Mwenye macho hawaambiwa tazama.

Kwa hiyo, kwa maoni yangu, akina Sita wana options mbili.

Option 1: wakae kimya, wafanye kama alivyokuwa anafanya Spika aliyemtangulia Msekwa: ukada, ubabaishaji na kulinda wazembe katika serikali, n.k. Kwa kifupi ni kwamba wakubali yaishe, na waendelee kubaki CCM.

Option 2: Wavae ujasiri watoke katika CCM. Najua ni ngumu maana gharama zake sio kidogo, lakini kama kweli wameamua kupambana hiyo ndiyo option.

Kusema kwamba waendelee kupambana ndani ya CCM ni kujidanganya kwa sababu hawa jamaa watawafukuza. Sasa wana hiari ya kutoka CCM kwa kufukuzwa au kwa kuondoka wenyewe kwa hiari yao. Wakisubiri wafukuzwe watakuwa wamewanyang'anya silaa ya ujasiri, wataonekana ni 'reject' wa CCM.

Mwisho, hakuna mwanasiasa hapa Afrika aliyepambana ndani ya chama chake akafanikiwa kupigania yale aliyokuwa anayaamini. Yalimshinda Bingu wa Mutharika hadi akaamua kukikimbia chama chake, tena akiwa Rais wa nchi, nyie wenzangu ni kitu kinawaaminisha kwamba hawa wabunge wetu wataweza kushinda mafisadi wakiwa ndani ya tanuru la kupika mafisadi?

It is simple: they have to choose either to be with 'them' or with 'us'; double dealing will not take them any far. If they decide to continue to fight from within they will very soon shut up or be shut up by powers that we know. The choice is theirs, anyway!
 
naungana na mwanafalsafa1 moja kwa moja!
kama kweli wako serious watoke nje ya system waanzishe chama chao,WE WILL GIVE THEM SUPPORT IN ANY ASPECT
 
Kitila Mkumbo

THEY MUST COMPLY WITH OPTION TWO!....i repeat,THEY MUST!wapiganaji wote duniani they go for option two.i promise,wapiga kura tupo nyuma yao,tutawapa support kubwa tu
 
Last edited by a moderator:
Mada nzito hii.

Hapa tulipofikia, ni vigumu sana kusema unapingana na ufisadi bila kuipinga CCM. Hii ni kwa sababu viongozi wengi kupitia CCM waliingia madarakani kwa kufadhiliwa na hao tunaowaita mafisadi, na inaonekana wanaendelea kuwa watiifu kwao.

Sasa kama hivyo ndivyo, hawa tunaowaita mashujaa wa taifa ndani ya CCM wanachofanya ni kukata mti walioukalia, nao lazima wataanguka. Lakini kabla hawajamaliza kuukata huo mti waliopo nao huko juu hawatakubali waukate hadi uanguke; watawatupa wao chini na wao waendelee kubaki katika huo mti.

Kwa vikao vya juzi, ni wazi kwamba wana CCM katika NEC wanachukizwa sana na tabia za akina Sita na wenzake za kuwabana mafisadi. Hawa wanawaona kwamba wanaibana CCM, na hawatakubali na wameonyesha hivyo juzi. Mwenye macho hawaambiwa tazama.

Kwa hiyo, kwa maoni yangu, akina Sita wana options mbili.

Option 1: wakae kimya, wafanye kama alivyokuwa anafanya Spika aliyemtangulia Msekwa: ukada, ubabaishaji na kulinda wazembe katika serikali, n.k. Kwa kifupi ni kwamba wakubali yaishe, na waendelee kubaki CCM.

Option 2: Wavae ujasiri watoke katika CCM. Najua ni ngumu maana gharama zake sio kidogo, lakini kama kweli wameamua kupambana hiyo ndiyo option.

Kusema kwamba waendelee kupambana ndani ya CCM ni kujidanganya kwa sababu hawa jamaa watawafukuza. Sasa wana hiari ya kutoka CCM kwa kufukuzwa au kwa kuondoka wenyewe kwa hiari yao. Wakisubiri wafukuzwe watakuwa wamewanyang'anya silaa ya ujasiri, wataonekana ni 'reject' wa CCM.

Mwisho, hakuna mwanasiasa hapa Afrika aliyepambana ndani ya chama chake akafanikiwa kupigania yale aliyokuwa anayaamini. Yalimshinda Bingu wa Mutharika hadi akaamua kukikimbia chama chake, tena akiwa Rais wa nchi, nyie wenzangu ni kitu kinawaaminisha kwamba hawa wabunge wetu wataweza kushinda mafisadi wakiwa ndani ya tanuru la kupika mafisadi?

It is simple: they have to choose either to be with 'them' or with 'us'; double dealing will not take them any far. If they decide to continue to fight from within they will very soon shut up or be shut up by powers that we know. The choice is theirs, anyway!

- Mkuu Kitila, hii ni another Great Thinking na maneno ni mazito sana ila yatafika kama yalivyo.

Respect.

FMEs!
 
Wakuu naona NEC inasikitsha sana, na wajumbe wake wanasikitisha sana. I wonder who is the mother of Tanzanians, is it CCM or Tanzania. Kama hakutakuwa na stable Tanzania, ni obvious kuwa hakutakuwa na CCM, inaonekana kuwa NEC haitaki kuona prosperity na stability ya Tanzania.
Kuwafunga watu midomo hakuna maana kuwa unawafanya waache kufikiri au kuona. People see things and think about them. Na baada ya muda wata-act tu. It is so hard to fool people for a long time. The best way to shut them up is to adress the problem of mafisadi na kurudi kwenye basics za CCM.
 
Siasa is all about Timing.

Timing ilivyo kwa sasa ni bora wabakie CCM lakini waendelee kupambana kwa moyo mmoja.

Wapambane Bungeni kama Katiba inavyowataka, wafuate taratibu kwa maslahi ya Taifa.

Wakiwa kwenye vikao vya CCM wafuate katiba ya CCM, kwani hakuna kipendele kwenye katiba ya CCM kinachoruhusu ufisadi.

Wananchi watakuwa mbele yao, iwe ndani au nje ya CCM.
 
Siasa is all about Timing.

Timing ilivyo kwa sasa ni bora wabakie CCM lakini waendelee kupambana kwa moyo mmoja.

Wapambane Bungeni kama Katiba inavyowataka, wafuate taratibu kwa maslahi ya Taifa. Wananchi watakuwa mbele yao, iwe ndani au nje ya CCM.

- Sawa sawa mkuu, hii pia ni great thinking to ishu, kwamba wa-stick to Katiba.

Respect.

FMEs!
 
Najiuliza nani CCM mwenye ubavu huu wa kutaka kuwaza kurudisha kadi?

Jamani ebu tuacheni unafiki na umbumbumu hakuna dawa rahisi ya ufisadi zaidi ya kukaa mbali na mafisadi.

Mawazo ya wengi kuwa wabaki humohumo ni ya KITANZANIA na KWA UJINGA HUU tupo hapa, eti kuwa 'wastaarabu' as Kitila depicts only two option wa comply nao hao mafisadi au waondoke.

Hakuna msafi CCM kwa sasa hakuna!!!!!!!!!!!

CCM ni dampo ati!

Mrema aliweza............
 
FMES,

..waondoke CCM ili wananchi tuelewe kwamba CCM imebakia kuwa chama cha Mafisadi.

..wanakosea sana wanavyoendelea kubaki CCM na kuwalaghai wananchi kwamba hoja ya kupinga ufisadi ni ya CCM wakati ktk vikao rasmi vya CCM wapinga ufisadi wananyanyaswa.

..kama wana uhakika ndani ya nafsi zao kwamba wao ni wasafi, basi wajiondoe mara moja huko CCM. kinyume cha hivyo waendelee kubaki humohumo CCM bcuz that is where they belong or deserve to be.

NB:

..naomba kuwauliza hawa wanachama wa CCM wapinga ufisadi.

..kwanini walikaa kimya wakati wanamtandao wananunua waandishi wa habari?

..kwanini walikaa kimya wakati wanamtandao wanawachafua wana-CCM wenzao kama Salim Salim kwa mambo ya uongo na uzandiki?

.kwanini walikaa kimya wakati vitendo vya kugawa bahasha vikifanyika waziwazi ktk mikutano ya CCM?

..sasa labda hayo hapo juu yalitokea wakati bado hawajapata mwanga wa nini haswa kilikuwa kinaendelea.

..nina maswali zaidi:

..uchaguzi wa Mwenyekiti wa UWT ulifanyika wakati tayari vita ya ufisadi imepamba moto.

..kwanini wapinga ufisadi wa CCM mpaka dakika hii hawakukemea jinsi uchaguzi wa Mwenyekiti wa UWT-CCM ulivyotawaliwa na vitendo vya rushwa ya waziwazi?
 
Wakuu wote JF yaani Great Thinkers,

- Ninaamini kwamba kilichotokea majuzi Dodoma ni only a big set back lakini sio mwisho wa vita na mafisadi, sio siri kwamba wapiganaji wetu kwa sasa spirit ziko chini, sasa huu ni wakati wa Great Thinkers, kuwapa ushauri of what to do next.

- Ninaomba kutoa shukrani kwa wakuu wote wa JF waliotoa maoni yao mazito kule kwenye thread ya Kusila, yamesaidia sana kuwapa moyo baadhi ya wapiganaji, ambao nimewasukumia tayari.

- Ninaomba mawazo hapa ili niwafikishie kama yalivyo, binafsi ninaanza kuwaza kwamba huenda huu ni wakati muafaka kwa wapiganaji kurudisha kadi zao za CCM, kwa sababu sasa hawawezi tena kupiga kelele za kuikosoa serikali, wala CCM mbele ya public, wanatakiwa kuyafanya haya ndani tu ya vikao vya chama chao CCM, hapa nia na madhumuni pamoja mengine mengi ni ili sisi wananchi tusijue wala kusikia ya huko ndani ya vikao vyao, na vile vile kuwakimbia mafisadi kunaweza kuwapa mwanya wa kutumaliza kabisa sisi wananchi!

- Sasa hawa wapiganaji wafanye nini as we move forward na hii vita na haya manyang'au?, wabaki CCM au warudishe kadi, au what else? Tujadili wakuu ili tuwafikishie mawazo yetu wananchi!

Respect.

Field Marshall Es! - Sauti ya Umeme!

Mkuu, mimi kwa maoni yangu naona wapiganaji ni bora wabaki ndani ya CCM ili kupambana na ufisadi uliokithiri ndani ya CCM na Serikali badala ya kurudisha kadi na kupigana wakiwa je ya CCM.

Nasema hivyo kwa kuangalia historia ya watu mbali mbali ambao waliwahi kushika nafasi ndani ya CCM ikiwemo yule aliyeshika nafasi ya juu kama Mh. Mrema ambaye baada ya kutokubaliana na mambo mbali ndani ya chama hicho aliamua kujiengua.

Tukiangalia watu hawa akina Mrema na wengineo wengi ambao walijiengua CCM hatuoni mafanikio yoyote waliyoyapata baada ya kujiengua huko. Na wengine kama akina Kabouru, Tambwe Hizza na wengineo wengi baada ya kupibgwa na njaa kali waliamua kurudi tena CCM ili wakagange njaa zao.

Wakiamua kuondoka kwa maoni yangu vyama vya upinzani vilivyopo bado havina nguvu na havijajijenga sana katika sehemu mbali mbali nchini ili kuweza kupambana na CCM. Pamoja na ushawishi mkubwa unaofanywa na Watanzania ndani na nje ya nchi ya vyama hivyo kuungana na hivyo kuunda chama kimoja chenye nguvu cha kupambana na CCM katika kila kona ya nchi yetu, bado viongozi ndani ya vyama hivyo hawajaona umuhimu wa kuungana na kwa maoni yangu hili linasabishwa na ubinafsi mkubwa wa kuogopa kupoteza madaraka katika chama kipya kama wakiamua kuungana

Hivyo hawa wapiganaji ni bora tu waendelee kupambana ndani ya CCM badala ya kuamua kurudisha kadi na huku Watanzania wenye vyama na tusio na vyama tukiwaunga mkono kwa hali na mali ili kuhakikisha wanawashinda mafisadi ndani ya CCM.

Wakiamua kurudisha kadi watakuwa wamewapa mafisadi ndani ya CCM na Serikali ushindi mkubwa na hivyo kuathiri kwa kiasi kikubwa mapambano dhidi ya mafisadi ambayo yanaungwa mkono na Watanzania walio wengi.
 
Kutoka kwa mzee Mkandara na waambia hivi... Kadi ya CCM ni mali ya wapiganaji, mali ya Wakulima na Wafanyakazi na sii vinginevyo kwani Ilani na katiba ya chama inajieleza wazi nini ibada za chama chenu CCM..hakuna nafasi kabisa ya kundi la Pili hao wanaodai mrudishe kadi za chama.

Hakika huu ni wakati wenu mnaojiita Wapiganaji (kama kweli mpo) kuhakikisha hao Mafisadi wanarudisha kadi wao, na mkishindwa kufanya hilo within the next 3 Month, basi nyie nyote matapeli. yaani chama na wanachama wake ni frame tupu, bango la display njia panda kufurahisha macho ya wananchi. Huu ni wakati wenu kutuonyesha mnaweza mapambano na sii kukimbia mkaacha misahafu yenu mikononi mwa shetani.

Na hakika mwaka 2010 mtakuwa watumwa wa chama chenu wenyewe..kwa mtumwa wa kujitakia, msije huko wala sikukaribishi nyumbani kwangu!

Kifupi mkuu wangu yaani uko tayari kunyang'anywa kiunga chako!.. upo tayari kurudisha hati ya kumiliki ardhi wakati unafahamu vizuri urithi huo wazazi wako walivyoutafuta kwa taabu, leo vikaragozi visivyojaa mkononi wakuondoe wewe ktk ardhi yako mwenyewe. Comeon bro, U must be kidding me!

Nooo!.. mkuu wangu hata kama ikibidi mmalizane, CCM ife kabisaaa kabla ya Uchaguzi basi na iwe hivyo kwa sababu kama mtashindwa kujikinga na watu hawa wawili mkakimbilia vyama vya Upinzani, sijui kama wananchi watawakubali. Kwani siku zote adui mkubwa wa Mpiganaji ni POLICY, itikadi iliyopo dhidi yake na wananchi wake na sio kupambana na kuogopa kichwa cha mtu.,Hii ndio kwanza naiona yaani mtu unaogopa mkono wa binadamu mwingine badala ya kuogopa kichwa..
Mkiwapisha chama basi mmeshindwa na hatuwezi kuwaachia dhamana ya National security watu kama hawa.
 
Last edited:
Back
Top Bottom