nimepata kazi mkoani ...najishauri!!

Kama unaona karaha nyingi na starehe kidogo hapo mjini ni dili kwako baki lakini kama unataka utoke kimaisha nenda meatu,pamechoka yes nimewahi fika pale ila kuna opportunity kibao pale za kufanya kama unaweza kuzungusha mil 1 au 2 unaweza ukacheza dili za dhahabu na almasi zinapatikana maganzo pale dhahabu unaweza ukapata sehemu ya shy rural ambayo sio mbali,ni uamuzi wako mzee.
 
Mkuu nenda mikoani kuna fursa nyingi za kiuchumi mambo ya kuganda Dar ni ushuzii mtupu hakuna lolote la maana zaidi ya joto kali,foleni,starehe za kijinga,.

Hapo nakusapoti kabisa, kwani huko mikoani ni kweli fursa za kiuchumi ziko nyingi ukilinganisha na Dar. Ukijituma kidogo tu kwa kutumia akili yako ya kuzaliwa basi utashangaa maisha yatakavyokunyookea.

Na hasa maeneo ya kanda ya ziwa ambapo fedha za kilimo na mifugo zinatembea nje nje (nawacha za madini).
 
kila kitu mjini bwana...hizo laki 2 bado ukikaa dsm unaweza kuzipata..bora ungesema mikoa kama ya mwanza na arusha ningekwambia nenda lakini shamba..du unakwenda kuwa mstaafu kabla ya wakati..mie nilipiga kazi wilayani baadaye nikaona ushenzi huu nikabwaga manyanga chini..hakuna challenge wala nini na kujiendleza ni ngumu sana..kwa ushauri wangu kaa mjini..kila kitu bongo..
 
njoo mkoani,huyo mchumba ako anaejiliza hapo ukizipata noti atakusifu na kukupenda zaidi!
Afu mkuu,unasahau sana jambo muhimu...wanawake!
Marehemu babu yangu aliwah kuniambia,"mjukuu wangu the magnificient,ukiwaendekeza wanawake utakufa maskini"
huwa najitahd sana nisitoke nje ya maneno yake!
Kila la kheri mkuu,amua kwa busara!
 
Kombo usidanganye watu bwana, jina lako laonesha Dar es Salaam ni kwako au watoka jirani na hapo. Waache watu wakalete maendeleo nje ya Dar.


Jamaa kauliza kizembe ndo sababu na mie nimempa jibu hilo la kizembe. Mi nafanya kazi nje ya Dar na nina makazi rasmi Dar.
 
wewe unaenda mkoani kwa difference ya laki 2 tu! labda ingekuwa zaidi ya laki 7! itakugarimu huko mbeleni ukitaka kurudi town unaweza shindwa hata kuwahi interview ukipata kazi nzuri sehemu
 
ww kumbe unachagua pa kukaa mbn hata meatu utafanya kz na hko ndo utakapo make vzur chaguo lako bana
 
kivyangu naona ubaki bongo, bongo ni kila kitu, mkoa ukienda mkoa bana sijui manake wengi tumetoka huko kuja bongo.
 
Kaka akili kumkichwa hiyo hardbody meatu ni basi la abiria we jifanye mtoto wa daslam. Watu wanfanya kazi mkoani wanajenga dar wakati wa dar wanishia kubadili nyumba za kupanga
 
sasa kama hakufai unataka nani akafanye kazi huko,kama sio mm na ww,...kwani huko dar mbona kuna kero kibao,..foleni,joto,maji ya chunvi na bado shida etc,...kama ni mawe nipigeni bana mmezidi usharobaro usio na maana

Hivi Igwe tofauti ya mshahara wa Laki mbili ???? ...haya bana hata kama hela inatafutwa duu ..all the best ndugu .
Kila mtu na maamuzi yake na huyo aliyeuliza alitaka mitizamo ya watu tofauti huo ulikuwa ni mtizamo wangu sio lazima kila mtu akubaliane nao zaidi ya mhusika kufanya maamuzi sahihi
Igweeeeeeeeeeee.
 
acha mtazamo hasi wewe laki mbili hiyo ni mshahara wa mtu! kwani Dar ni mbinguni? kwanza kwa mtu anayejua hakuna mji mbaya saizi kama Dar hata uwe na gari lako ni sawa tu na aliye huko meatu kwani mifolen kero za kila namna

haya Bwana ni mtizamo tu..mie hiyo tofauti ya mshahara haikunivutia hata kidogo labda kama anaenda kuwa mdokozi wa mali ya umma
 
haya Bwana ni mtizamo tu..mie hiyo tofauti ya mshahara haikunivutia hata kidogo labda kama anaenda kuwa mdokozi wa mali ya umma

Mtu anayelipwa milioni moja Dar na anayelipwa milioni moja mkoani, nakuhakikishia wa mkoani baada ya miaka 2 ana nyumba na gari na maisha yake mazuri. Mkoani unakodisha nyumba nzima nzuri haizidi hata laki na nusu, gharama za vyakula n.k. zipo chini kulinganisha na Dar na isitoshe kule anapata na muda wa kufanya shughuli nyingine za kumuongezea kipato. Maana kazini unaenda saa 2 asubuhi na saa 9 tayari upo free, sio Dar uamke saa 11 kuwahi foleni na hata kama unatoka kazini saa 9 basi utafika nyumbani saa 12 jioni!!
 
Mtu anayelipwa milioni moja Dar na anayelipwa milioni moja mkoani, nakuhakikishia wa mkoani baada ya miaka 2 ana nyumba na gari na maisha yake mazuri. Mkoani unakodisha nyumba nzima nzuri haizidi hata laki na nusu, gharama za vyakula n.k. zipo chini kulinganisha na Dar na isitoshe kule anapata na muda wa kufanya shughuli nyingine za kumuongezea kipato. Maana kazini unaenda saa 2 asubuhi na saa 9 tayari upo free, sio Dar uamke saa 11 kuwahi foleni na hata kama unatoka kazini saa 9 basi utafika nyumbani saa 12 jioni!!

hata mie niko Mkoani ndugu Limbani ...anatakiwa kufanya maamuzi yake sahihi.
all the best mtoa mada . jaribu kufanya evaluation zako binafsi changanya na zetu utapata majibu
 
habarini JF

nipo dms nafanya kazi kampuni fulani ya simu.nimepata kibarua kingine kwenye kampuni nyingine ya simu kwa tofauti ya mshahara ya laki 2...i mean ya mkoani imezidi kwa laki 2 mshahara wa apa dar..........wananipa na gari ya kazi!!hardbody...lakini bado naona ugumu kuenda huko meatu...nishaurini niende au nibaki?

kwa nini uliapply kama hutaki kufanya kazi mahali popote?

wacha kutuzingua. tatizo mmesha kariri dar ndo sehemu nzuri ya kumake life, kiasi fulani ni ushamba
 
Tofauti ya mshahara ni ndogo sana kulingana na utavoenda kusota mkoani, baki dar

mme wako nini?

laki mbili mkoani ni nyingi sana ukilinganisha na dar. chakula huku bei nafuu kila kitu bei nzuri. hata hivyo anatuzingua tu huyu, kwani tulimtuma aaply? kwa nini aliapply wakati anajua ana kazi nyingine tena ileile?

si kuwaharibia vijana ambao wanatafuta kazi kwa mara ya kwanza?
huu nao ni ufisadi
 
kuna thread amefungua huyu jamaa.......kaamua kwenda meatu...safi sana
 
Back
Top Bottom