nimepata kazi mkoani ...najishauri!!

Hivi miaka hii bado kuna watu wanajiuliza mara mbili mbili ni wapi kwa kufanya kazi!
What matters ni kiasi benefit inayopatikana kwa kufanya kazi mahali!
Nenda mkoani ukafanye kazi, kwanza opportunities ni nyingi kuliko dar, pia
maisha ni rahisi sana kwa maana ya gharama za kuishi, mfano nyumba,
vyakula n,k.
Nenda mkoa!
 
Je umewekeza au una vitega uchumi vingine mbali na kazi yako huko Dar? Kama huna nenda tu huko Meatu kaanze maisha mapya kwa amani zote.

Wengi wenu hampendi kuja huku mikoani ingawa kuna opportunities nzuri zaidi ya huko Dar. Mimi ni mfano wa kama wewe, nimeishi Dar na elimu yangu yote nimeipata huko na Kazi nimefanya huko kwa mwaka na nusu ( Sikufanikiwa kupata mali zangu za maana) ndo nikaajiriwa huku Morogoro, lakini maisha ya huku nimeyaona ni mazuri sana kuliko kuishi Dar. Kwa kipato kidogo ninacholipwa mimeweza kupata Kiwanja na shamba baada ya kufanya kazi kwa muda wa miezi mitatu na nategemea sasa hivi kuanza kujenga nyumba na life lipo shwari tu.

Hata hivyo maamuzi yote yapo mikononi mwako mkuu. Huo ni ushauri tu
 
Mkonowapaka,nilipata uhamisho kikazi bila kuongezewa mshahara mwaka 2008 kuja mwanza.Nilitaka kuresign but after experience ya kutokuwa na kazi for 8month nikaja Mwanza.Siku za mwanzo nilipata shida sana.But kwa sasa sidhani kama naichukia sehemu yoyote ya mkoa wa Tanzania kuacha Dar.Mikoani utatengeneza hela mpaka uchoke.Dar wajanja walikuwepo so you need to be "extra smart to be rich" Nakushauri nenda Meatu!!Hutasahau watu waliokushauri kwenda bara!!!!
Nimekulia Dar na kufanya kazi hapo btn 2003-2007 so najua mazingira ya Dar!!!
 
acha utoto, watu wanasaka pesa mikoani wana-invest Dar ndio maana hata Ben Mkapa anapumzika Lushoto anapata hewa safiiiiiiiiii.
 
Bora ubaki tu hapa hapa, huko meatu porini hata ukiwa na gari utatembea nalo wapi.
 
Wenye akili mgando, wasiojiamini, washamba, waendekeza starehe za kulala club, na wasiokuwa na malengo katika maisha yao ndio wanang'ang'ania kufanya kazi Dar es salaam. Utakuta mtu anapata kipato kidogo, ila kwa kuwa yupo tu Dar anaridhika ile mbaya, utadhani mwanamuziki wa Bongo Flavour au akina Majuto wasiokuwa na profession ya kuwalipa mikoani.
Nani kakwambia mshahara utakuletea maisha bora? Hata ukawe Mkurugenzi wa TANROAD mshahara haukutoi ng'o. Hiyo ni mbegu unayotakiwa uipande. Lakini utaipandaje mbegu Dar es Salaam ambapo kama wataka kufungua biashara bei ya pango la frame ni sawa na mshahara wako? Kaangalie watu waliotengeneza pesa wametokea wapi kabla hawajafika Dar es Salaam. Wengi wametoka mikoani, tena sio makao makuu ya mikoa bali mawilayani kabisa. Nimesikia kuna watu wakienda Mbarali au huko Kamsamba Sumbawanga yaani hawarudi wakilikamata jembe. Dsm ina wenyewe, kama akina Manji. Akina sisi tukikaa Dar tutaishia kutamani tu wenzetu mafisadi wanapo invest na pia kufurahia foleni na mataa ya usiku.
 
kama kule kuna san siro,maisha club,bahari na mihuri ya mifukoni nenda na kama foleni za magari,ukosefu wa maji,umeme na mazingira machafu ya dsm havikuathili baki.mia
 
nimekaa mjini nikafanikiwa kias....then nikajaribu kwenda mkoani......aiseeeee asikwambie mtu.....nilijilaumu kwa nini sikuja mapema...mkoani panalipa sana kama utatumia akili lakini kama unategema mshahara na hiyo gari ya ofc wafwa na hautapiga move.....mwakani mwanzoni nategema kuachana nakazi za kuajiliwa...

fanya maamuzi sahihi kijana...chanzo cha tatizo kwako sisi wengine ndo chanzo cha suluhisho...yatumie mazingira vizuri kijana..
 
meatu? Sikushauri! Difference ndogo, unless kama utajishughulisha kama kilimo, au usafirishaji, kupo isolated sana ingawa kupo well planned kimtindo
 
kazi nzuri ni ipi???????

we unaangalia mshahara tu?

je mkeo hafanyi kazi?watoto shule?
ndugu?

maelewano ofisini? future ya kampuni??
 
Wenye akili mgando, wasiojiamini, washamba, waendekeza starehe za kulala club, na wasiokuwa na malengo katika maisha yao ndio wanang'ang'ania kufanya kazi Dar es salaam. Utakuta mtu anapata kipato kidogo, ila kwa kuwa yupo tu Dar anaridhika ile mbaya, utadhani mwanamuziki wa Bongo Flavour au akina Majuto wasiokuwa na profession ya kuwalipa mikoani.
Nani kakwambia mshahara utakuletea maisha bora? Hata ukawe Mkurugenzi wa TANROAD mshahara haukutoi ng'o. Hiyo ni mbegu unayotakiwa uipande. Lakini utaipandaje mbegu Dar es Salaam ambapo kama wataka kufungua biashara bei ya pango la frame ni sawa na mshahara wako? Kaangalie watu waliotengeneza pesa wametokea wapi kabla hawajafika Dar es Salaam. Wengi wametoka mikoani, tena sio makao makuu ya mikoa bali mawilayani kabisa. Nimesikia kuna watu wakienda Mbarali au huko Kamsamba Sumbawanga yaani hawarudi wakilikamata jembe. Dsm ina wenyewe, kama akina Manji. Akina sisi tukikaa Dar tutaishia kutamani tu wenzetu mafisadi wanapo invest na pia kufurahia foleni na mataa ya usiku.


nadhani amekuelewa...yaani dar bwana ni ketro tupu....na huyu anaonyesha maisha yake yanategema mshahara wake...ila hajui kutumia mazingira yanayomzunguka katika kuboesha mazingira hayo....ndio maana wengien wanamwambia abaki dar maana akienda kule hakuna hata mahali pa kuendeshea gari...!!!
 
Ukienda mkoani wala huatatamani kurudi tena dar.


kweli kabisa......dar unarudi kupumzika kwa mda unakula bata na kujenga kama inawezakana then unarudi pori unafanya maisha...
 
Mkuu nenda mikoani kuna fursa nyingi za kiuchumi mambo ya kuganda Dar ni ushuzii mtupu hakuna lolote la maana zaidi ya joto kali,foleni,starehe za kijinga,.


nadhani ametuelewa....labda kama anapenda hizo starehe za kijinga, hana future, anategemea mshahara ile asonge mbele.....
 
tatizo nashindwa kuelewa kwa nn moyo wangu umekua mzito..........sijafanya maamuz nna siku 3 sasa..sina sababu za msingi saana zaidi ya mchumba ambaye yy analia tu mda wte akiskia naondoka,halinipi shida sana......sasa nitaufahamu vp huo mji?nitakua pia hadi maswa...nahitaji kufahamishwa na wenyej plz
watu kama nyie ndio huwa nawashangaa sana...nenda kapige kazi huko pia ni tanzania. hivi unadhani kila mtu akikataa kwenda kufanya kazi ma-wilayani ni nani atakaye wasaidia wananchi wa sehemu hizo? halafu ukienda huko ni namna nyingine ya kujifunza na kufahamu nchi yako ilivyo hasa maisha ya mikoani. sidhani kama ni busara kwa kila mtu kung'ang'ania hapa dsm.
Kwa ushauri wangu na kwa kuwa unasema bado hujawa na familia, nenda kapige kazi. hata huko utapata opportunities za kuongeza kipato chako kama ukiwa mbunifu. unaweza ukawa hapa dar lkn kama siyo mbunifu ukashindwa hata kuongeza kipato kwenye salary yako.
Kitakachokufanya uende huko siyo ongezeko la laki 2, ni uzalendo wako kuwasaidia watz wenzako ambao wanahitaji sana utaalamu wako ili na wao waweze kujikomboa.
Nenda kijana...nenda ukaijenge nchi na kwa kuwasaidia watu wa meatu na maswa!
 
Nenda wilayani mkuu ukafanye kazi, usinga'ang'anie Dar. Hakikisha unakuwa na laptop na modem kwa ajili ya mawasiliano ya Internet, na pia lazima ufunge DSTV nyumbani basi mambo mengine ni mteremko tu!! Bia zipo tena zimewiva vizuri na nyama choma, kuku n.k. safi tu tena wa kienyeji!!! Ukirudi Dar wanakuona umetoka NYC...
 
Back
Top Bottom