Nimemfumania mke wangu, nimechanganyikiwa! Ushauri tafadhari...

Wana JF nimeoa na nina mtoto mmoja ana miaka minne,nimemfunia mke wangu anafanya mambo na kijana fulani wa mtaani hapa hapa.Nimemrudisha kwao ila naona kama adhabu haitoshi kuna muda natamani kama nimkatekate vipande vidogo vidogo vya nyama au hata niende kwa mganga amfanye chizi.Bado wazazi wamekutana wanasema nimsamehe.Naomba busara zenu wanaJF ila pia nawapeni somo msiwaamin wanawake anaweza kukugeuka siku yoyote,mm mke wangu nimetoka nae shule ya msingi mpaka mwaka huu ni zaidi ya miaka 13

ah ndio wajua leo kuwa usimuamini mwanamke? pole!!! hawa ni wakugegeda na kusepa mwana....wee utajipinda wenzio wanamega kiulainiiii.
 
Mkuu pole sana! Hili jambo ni gumu sana hivyo kuwa mvumilivu na huhitaji kuamua chochote zaidi ya kusubiri hasira zipungue (mwezi 1 au 2).
Hushauriwi kufanya maamuzi magumu ukiwa na hasira sana au furaha sana.
 
Ukumbuke vile vile tumeruhuciwa kutoa talaka kwa kosa la zinaa.. (Mathayo 5:32).. Kuzini nje ya ndoa ci tu kwamba ni kosa kuliko makosa mengine.. Ni kuvunja kitu kitakatifu kilichopata baraka machoni pake Baba Mungu.. Kibinaadamu ni betrayal ambayo itabaki kama jeraha ndani ya moyo..
Unakumbuka habari ya yule mwanamke mzinzi aliyepelekwa kwa YESU wakitaka wampige mawe? YESU alipowaambia asiye na dhambi awe wa kwanza kumpiga?
MUNGU wetu ni wa upendo na kusamehe mara saba sabini! Mwombe akuwezeshe kusamahe, msamaha utoke ndani yako! kama huwezi kusamehe fanya lile ambalo litakuacha na amani ndani yako
 
Pole sana maamuzi magumu unayo wewe suala la kuacha wala aliitaji ushauri mkuu.
 
Ushauri wangu mimi ni kuwa usijilazimishe kumsamehe. Kama moyo wako unakataa kumsamehe, basi na iwe hivyo... usimsamehe eti tu kwa sababu ya kutaka kuwaridhisha watu fulani, utakuja kufanya mambo mabaya sana huko mbele ya safari

pwenti
 
Pole sana mwanangu ila si vizuri kuwahukumu wanawake wote. Wapo waaminifu na wasio waaminifu sawa na wanaume. Suala la kumsamehe au la linatoka moyoni mwako . Ingawa kusamehe ni vizuri, hakuna anayeweza kukufundisha kuchukia wala kusamehe. Hivyo piga moyo konde uone ni lipi linakufaa. Na unapotoa uamuzi uhakikishe unatuliza mawazo na kuangalia faida na hasara za kufanya hivyo hasa wakati huu wa miwaya.
 
Pole sana mkuu,la msingi je ulihisi hali hiyo ilikwepo tangu mwanzo na mapenzi yalipungua?kama nafsi yako hairidhiki achana naye vuta ndani mwingine wa kutibu moyo
 
kuna jamaa mja alimfumania mke wake ,akataka kumpa talaka ila akasema ngoja akaongee na baba yake ili ampe ushauri zaidi.ok baba yake hakumjibu ila baba akapanga na jamaamja ajifanuye mganga siku moja kabla akawataarifu wanae wote na wake zao wafike pale yeye ni mgonjwa sana!basi wakafika mganga akawa bise na mambo yake baba amelela kama anatka kufa vile,yule mganga akasema anayetakiwa kumyesha baba hii dawa ni mtu ambaye hajawahi msaliti mume/mke wake haya chance ikatolewa wote kimya wakaulizwa wale wamamam wote kimya na akaitwa mke wa yule baba nae akakataa maana mganga alisema ukidanganya unakufa ikabidi wamwite mtto mdogo amnyweshe .sasa basi akamwambia yule aliyekuwa anataka kumtalaka mkewe si unaona hata mke wangu amenisaliti hajadhubutu ninywesha dawa wewe mwenyewe umemsalit nenda ukaish na mkeo kwa upendo na amani

Story ya kusadikika hii ... Lol
 
Humridhishi na hakupendi jitahidu mambo ya chumbani.usiwe mtakatifu chumbani , kuoa sio kitu Kama hujui mchochomeo( kuyarudi mavitu) .
 
Baba, kitanda usichokilalia hujui kunguni wake. Nina uhakika mkeo umemfundisha wewe mwenyewe na hata jinsi ya kukucheat. Nakuahidi, maumivu yake ni yale yale. Sema tu vile wewe hujawahi kuonjeshwa dawa yako mwenyewe. Ulishawahi kuona dokta ama nesi akiugua? Naye sindano inamuuma na huwa muoga, yale maneno ya 'jikaze bwana wewe mkubwa' huwa hawayakumbuki.

Mi nakushauri jipe muda, usikurupuke. Kama ambavyo nae alikuwa anakasirika akikubamba, ananuna na kulia na kukunyima unyumba, halafu anakuja kukupenda upya. Basi labda nawe ungefanya hivyo. Pole mwaya, na sie tunaumiaga hivyo hivyoooo.
nimetoka ila unajua kwa mwanaume kutoka sio kama mwanamke
 
Ukishakata hizo nyama unazila.? Ukimfanya awe chizi assume anatembea urchin barabarani akipita mtaani watu wanasema make wa Fulani yulee kawa chizi, au mwanao akikua anamuona mama hake chizi barabarani will that makes you happy? Mi naomi uamuzi aw kumrudisha Kwao ukupe muda aw kufikiria na kutafakari, usifate hasira unaweza jikuta unajisaidia kwenye ndoo keko halafu watu wanaendelea Kama kawa.
thenx hata mimi nimefikiri sana usiku nimeona hili la kumfanya chizi au kumuua sio zuri ila mkuu nimeumia sana hata nimfanyaje hawezi kupata maumivu kama haya,nakaribia wiki sipati hata usingizi
 
Pole sana mkuu,la msingi je ulihisi hali hiyo ilikwepo tangu mwanzo na mapenzi yalipungua?kama nafsi yako hairidhiki achana naye vuta ndani mwingine wa kutibu moyo
hapana hata kidogo,mm nilikuwa naona ananipenda sana hakukuwa na dalili zozote za usaliti,ni mzuri sana kwa kujipretend kama ananipenda
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom