Niffer: Nilianza na mtaji wa elfu 40, sasa hivi nashika hadi milioni 150

Ila Mange kamchamba nifa kisa shoga zake kina Rest, kakosea sana angetakiwa kumpongeza na kusema wadada waige niffer anajipambania
 
Binafsi nilishawahi kuletewa simu ndogo kutoka Kenya,kipindi hicho 1000 ya Kenya ni 18,500-19,500 na nikiileta Tanzania nauza 45,000. Nikaaona iwe biashara Kila nikiletewa pesa yote naagizia mizigo. Mwisho wa siku nikakata passport ya east and central emergency travel document. Kwa week nilikuwa Nina uwezo wa kwenda Kenya Mara tatu,Dar-Nairobi,Hata majirani hawakuamini walijua natumia ndege lakini ilikuwa basi. Nairobi nilikuwa nakaa dk 45 tu nishafunga mizigo nageuza Tanzania. KABLA mwezi haujaisha nikawa Nina milioni sita. Ila short cut mbaya. Tauteni halali na mlipe Kodi kwa Kaisari au uwe unakula na kina Zakayo mkata ushuru Bila ya hivyo!!!!!!!!!!!!! Story ndefu na Mimi sio mwandishi MZURI
 
wakati mnalalamika yanga kaonewa....mamelod wamesonga, na ile tuu kufika nusu finale kuna mshiko mnono.... dunia ndivyo ilivyo....so mtaji wa 40sauzandi now ana 150m.....wacha tupige kellele ila matokeo ndio hayo.....Niffer kongole kwako.....maisha ni mbinu tuu......ukifuata mstari utafutika huko mbele....
 
Isingekuwa orodha yake ndefu ya waliopiga, unaweza kujizima Siku Moja ukaenda kupiga

Kuna mdau mmoja alinambia ukihitaji yeyote niambie nikusogezee ila muhimu uwe na cash 🙌

Nikamwambia umri huu siwezi maana tumezeeka sana 🤗

Mtu amepigwa na Mapeshee ya tangu 2006, Kuna kupona hapo kweli 🙌
Hadi Marehemu liyumba yule gavana wa benki . Pia dogo janja janjaro kafumua marinda.

King Kong III
 

Mlimbwende kunako kiwanda cha Utangazaji, Mjasiriamali na mwanamitandao maarufu Bongo, Niffer Jovin, maarufu kama "Niffer" amefunguka namna alivyohaha kujitafuta hadi kufikia mafanikio makubwa akiwa na umri mdogo.

Niffer ambaye ametimiza miaka 24 mwaka huu, amesema safari yake ya kuutwaa utajiri haikuwa rahisi kama watu wanavyodhani, amesema yeye ni miongoni mwa watu waliotokea katika familia za kimasikini ambazo asubuhi unalazimika kula maembe badala ya kunywa chai, mrembo huyo amesema amewahi kwenda shule bila viatu, amewahi kupigwa kisa tu kukosa sabuni ya kufulia sare zake za shule, lakini pia alikuwa akimuona mama yake namna alivyokuwa anawahangaikia ili wapate chochote kitu na wakati mwingine alikosa kabisa, amesema hiyo ndiyo ilimpa chachu ya kuyasaka mafanikio kwa udi na uvumba ili asipite walimopita familia yake.

Kama ulikuwa unadhani mtaji wa duka kubwa la Niffer "Niffer Outfitstore" lilianza na mtaji wa mamilioni kadhaa unajidanganya, mpambaji huyo amesema hakuanza na mtaji wa milioni, laki moja wala elfu 50, amesema alianza na elfu 40 pekee na haijamchukua muda mrefu tayari amekuwa tajiri kwa mtaji huo mdogo wa nyanya chungu na vitunguu.

Siri kubwa ya mafanikio ya Mwanaharakati huyo wa maisha amesema ni kuwa na nidhamu na pesa, kuwa na marafiki wa kukujenga, kumuomba Mungu huku ukifanya kazi, kwani yeye wakati anajitafuta alikuwa anafanya biashara hadi saa nane, saa tisa za usiku wa manane. Muhaya huyo wa Bukoba amesema watu wanamshangaa kwa kuwa na duka kubwa akiwa na miaka 24 kwasababu hawajui namna alivyopambana kwa bidii kuyasaka mafanikio.

Amemalizia kwa kuwashauri wasichana wenye umri mdogo na wanawake ambao umri umeenda na bado wanahaha kutafuta maisha kwamba wafanye kazi kwa bidii, waache kubwabwaja mitandaoni kufatilia maisha ya watu na badala yake wautumie huo muda wauze hata pilipiii mbuzi watafika alipofika yeye.
Hizi story za, wadada wa bongo, hazinaga uhalithia hata kidogo,
Kuna Yule mdsda alikuwa anahitisha mikutano anawakusanya wanawake, wasichana anawapa madini ya lo motivational jinsi ya kutengeneza pesa,akijitolea mfano jinsi ye ye alivyofanikiwa, kumbe, nyuma ya pazia ye ye na mumewe, wanauza, "unga" Cocaine, sasa hv ananyea debe lupango, Mali zote zilitaifishwa,
Watu wa kusikiliza ni wale wanaofanya biashara zinazoonekana, Lady jayd,shilole, au, Freddy vunja bei, ukisikia wanamiriki bilioni 500,wala, hushangai! Maana, biashara zao, zinaonekana, lakini hawa, ambao wanaibuka ghafra,mwaka mmoja alikuwa, hafahamiki, ghafla Leo Ana mijengo, mindinga nk! Hapo, utakuta ni danga la waziri,
 
Mim pia nilianza na nyoya la kuku saizi nina kuku 1700 bandani, naingiza zaidi ya million 30 Kwa mwezi...

Vijana tafuteni pesa, ajira hakuna ila kazi zipo ....
Kazi, si kazi, tu, inahitqjika, yenye kuingiza maokoto, na ndio ajira, hata kutembea kutoka bagamoyo au chalinze mpaka posta dar, au masasi mpaka nachingwea, au tinde mpaka kahama, ushirombo, kagongwa, ni kazi, lakini sio, ajira,
 
Back
Top Bottom