Wakati Catherine akipambana na Biashara kutoka Mtaji wa Milioni 1 hadi 100, wanawake wengine wanalalamika hawaolewi ili wapate Kitonga

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,115
49,838

1710919689127.png

Hongera sana Malkia wa Nguvu Catherine Kwa kuonesha mfano.

Tukiendelea kusheherekea Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani mwezi huu wa March, ambapo Dunia hutambua michango ya Wanawake Wapambanaji wanaotumia akili, ubunifu na vipaji walivyonavyo kufanya mambo makubwa na kubadilisha fikra, mitazamo na hata kukuza uchumi kwenye Jamii.

Leo nakukutanisha na Malkia wa Nguvu kutoka Mtandao mkubwa wa Africa Women Leaders Network Tanzania Catherine Shembilu kutoka Mkoani Tanga ambaye baada ya kuhitimu Chuo Mkoani Iringa aliiona fursa ya kuviongezea thamani vikapu na kuvifanya vyenye ubora utakaowezesha viuzwe kwa bei ya juu ndani na nje ya Nchi na kuwakomboa Wanawake.

Akiwa ameanza na Mtaji wa Tsh. Milioni 1 tu aliianzisha safari yake na sasa Catherine ni Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Vikapu Bomba ambayo inafanya kazi na Wanawake wa Vijijini zaidi ya 300 wa Mikoa ya Iringa na Njombe kwa kuwawezesha kutengeneza vikapu bomba vya kisasa na kuwatafutia masoko ndani na nje ya Nchi ambayo yanafanya wauze kwa bei nzuri inayowafanya waepukane na umasikini.

Kutoka mtaji wa Tsh. Milioni 1 sasa Catherine ana Mtaji wa Milioni zaidi ya 100, ametoa ajira kwa watu wengi huku akiwezesha Wanawake kubadili hali zao za kiuchumi ambapo kwa sasa wanauza vikapu hadi Tsh. Laki 1 na zaidi.

Mtandao wa wanawake wa Awlntz ni jitihada za kimapinduzi za viongozi wanawake wa Kiafrika. Inatekelezwa kwa msaada wa Ofisi ya Mjumbe Maalum wa African Union, kuhusu Wanawake, Amani na Usalama, na Shirika la Umoja wa Mataifa la Usawa wa Jinsia na Uwezeshaji wa Wanawake.

Mpango huo unalenga kuimarisha uongozi wa wanawake katika mabadiliko ya Afrika, kulingana na Ajenda ya Afrika 2063 na Malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2030. Aspiration 6 ya Ajenda ya Afrika 2063, "Afrika Tunayoitaka", inatazamia Afrika ambayo inazingatia watu, yenye usawa wa kijinsia, na ambapo wanawake wanawezeshwa na kutekeleza jukumu lao halali katika nyanja zote za maisha.

==========

My Take
Wanaume tuanze Kuwapiga Chini Wanawake Njaa ambao wako desperate wanaotaka kutufanya Chuma ulete.
1710919659789.png
 
To each their own....; Wewe Matamanio yako ni Tofauti na Mwingine...., Vipaumbele ni Tofauti sana.. Kwangu mimi yule Mama Single anayehangaika na kubangaiza asubuhi mpaka jioni angalau watoto wanywe uji ila kutokana na Sera mbovu za nchi yake mara nyingi anaishia kukopa au kujiuza ili tu watoto wasife ni Shujaa zaidi (Sababu huyu wala sio matamanio yake bali ni mzigo / wajibu wake)...

Tryin to make a dollar out of fifteen cents
It's hard to be legit and still pay tha rent
2Pac - Keep Ya Head Up.....​
 
Hongera sana Malkia wa Nguvu Catherine Kwa kuonesha mfano.

Tukiendelea kusheherekea Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani mwezi huu wa March, ambapo Dunia hutambua michango ya Wanawake Wapambanaji wanaotumia akili, ubunifu na vipaji walivyonavyo kufanya mambo makubwa na kubadilisha fikra, mitazamo na hata kukuza uchumi kwenye Jamii.

Leo nakukutanisha na Malkia wa Nguvu kutoka Mtandao mkubwa wa Africa Women Leaders Network Tanzania Catherine Shembilu kutoka Mkoani Tanga ambaye baada ya kuhitimu Chuo Mkoani Iringa aliiona fursa ya kuviongezea thamani vikapu na kuvifanya vyenye ubora utakaowezesha viuzwe kwa bei ya juu ndani na nje ya Nchi na kuwakomboa Wanawake.

Akiwa ameanza na Mtaji wa Tsh. Milioni 1 tu aliianzisha safari yake na sasa Catherine ni Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Vikapu Bomba ambayo inafanya kazi na Wanawake wa Vijijini zaidi ya 300 wa Mikoa ya Iringa na Njombe kwa kuwawezesha kutengeneza vikapu bomba vya kisasa na kuwatafutia masoko ndani na nje ya Nchi ambayo yanafanya wauze kwa bei nzuri inayowafanya waepukane na umasikini.

Kutoka mtaji wa Tsh. Milioni 1 sasa Catherine ana Mtaji wa Milioni zaidi ya 100, ametoa ajira kwa watu wengi huku akiwezesha Wanawake kubadili hali zao za kiuchumi ambapo kwa sasa wanauza vikapu hadi Tsh. Laki 1 na zaidi.

Mtandao wa wanawake wa Awlntz ni jitihada za kimapinduzi za viongozi wanawake wa Kiafrika. Inatekelezwa kwa msaada wa Ofisi ya Mjumbe Maalum wa African Union, kuhusu Wanawake, Amani na Usalama, na Shirika la Umoja wa Mataifa la Usawa wa Jinsia na Uwezeshaji wa Wanawake.

Mpango huo unalenga kuimarisha uongozi wa wanawake katika mabadiliko ya Afrika, kulingana na Ajenda ya Afrika 2063 na Malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2030. Aspiration 6 ya Ajenda ya Afrika 2063, "Afrika Tunayoitaka", inatazamia Afrika ambayo inazingatia watu, yenye usawa wa kijinsia, na ambapo wanawake wanawezeshwa na kutekeleza jukumu lao halali katika nyanja zote za maisha.

==========

My Take
Wanaume tuanze Kuwapiga Chini Wanawake Njaa ambao wako desperate wanaotaka kutufanya Chuma ulete.
alafu wakisha2ufanya chuma ulete wanabeba vitu wanasepa
 
Kuna Niffa wa yahaya muuza ngada nae muweke. Mwanamke kufanikiwa bila mwanaume sometimes ni kwa mbinde sana, hawasemi ukweli
 
Attachments

  • ddef8397-0e4b-4349-8369-8a8f060447c1.jpeg
    ddef8397-0e4b-4349-8369-8a8f060447c1.jpeg
    44.2 KB · Views: 6
Back
Top Bottom