Niffer: Nilianza na mtaji wa elfu 40, sasa hivi nashika hadi milioni 150

Nesi mkunga

JF-Expert Member
Nov 28, 2022
701
1,842
Screenshot 2023-06-30 113146.png

Mlimbwende kunako kiwanda cha Utangazaji, Mjasiriamali na mwanamitandao maarufu Bongo, Niffer Jovin, maarufu kama "Niffer" amefunguka namna alivyohaha kujitafuta hadi kufikia mafanikio makubwa akiwa na umri mdogo.

Niffer ambaye ametimiza miaka 24 mwaka huu, amesema safari yake ya kuutwaa utajiri haikuwa rahisi kama watu wanavyodhani, amesema yeye ni miongoni mwa watu waliotokea katika familia za kimasikini ambazo asubuhi unalazimika kula maembe badala ya kunywa chai, mrembo huyo amesema amewahi kwenda shule bila viatu, amewahi kupigwa kisa tu kukosa sabuni ya kufulia sare zake za shule, lakini pia alikuwa akimuona mama yake namna alivyokuwa anawahangaikia ili wapate chochote kitu na wakati mwingine alikosa kabisa, amesema hiyo ndiyo ilimpa chachu ya kuyasaka mafanikio kwa udi na uvumba ili asipite walimopita familia yake.

Kama ulikuwa unadhani mtaji wa duka kubwa la Niffer "Niffer Outfitstore" lilianza na mtaji wa mamilioni kadhaa unajidanganya, mpambaji huyo amesema hakuanza na mtaji wa milioni, laki moja wala elfu 50, amesema alianza na elfu 40 pekee na haijamchukua muda mrefu tayari amekuwa tajiri kwa mtaji huo mdogo wa nyanya chungu na vitunguu.

Siri kubwa ya mafanikio ya Mwanaharakati huyo wa maisha amesema ni kuwa na nidhamu na pesa, kuwa na marafiki wa kukujenga, kumuomba Mungu huku ukifanya kazi, kwani yeye wakati anajitafuta alikuwa anafanya biashara hadi saa nane, saa tisa za usiku wa manane. Muhaya huyo wa Bukoba amesema watu wanamshangaa kwa kuwa na duka kubwa akiwa na miaka 24 kwasababu hawajui namna alivyopambana kwa bidii kuyasaka mafanikio.

Amemalizia kwa kuwashauri wasichana wenye umri mdogo na wanawake ambao umri umeenda na bado wanahaha kutafuta maisha kwamba wafanye kazi kwa bidii, waache kubwabwaja mitandaoni kufatilia maisha ya watu na badala yake wautumie huo muda wauze hata pilipiii mbuzi watafika alipofika yeye.
 
Mim pia nilianza na nyoya la kuku saizi Nina kuku 1700 bandani ,naingiza zaidi ya million 30 Kwa mwezi...

Vijana tafuten pesa ,ajira hakuna ila kazi zipo ....
Biashara ukiwa na juhudi lazima ufanikiwe, wanaolalamika biashara ngumu hao wazembe.

Me nilikuwa tu na wazo la biashara, sikuwa hata na mia lakini nikaweka juhudi hatimaye namiliki biashara kadhaa za mamilioni hapa mjini.
 
Back
Top Bottom