Mwanakili90
JF-Expert Member
- Nov 24, 2010
- 1,568
- 245
MBUNGE wa Jimbo la Tabora Mjini, Ismail Aden Rage (CCM) amemjia juu Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema) akimtaka kuacha kuubeza uteuzi wa Mwenyekiti na Mkurugenzi Mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), uliofanywa na Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni. Badala yake, amemtaka afahamu kuwa, yote yanayofanywa na Rais Kikwete yamo ndani ya mamlaka yake kikatiba.
Jamani, mwambieni Mnyika aache kutafuta umaarufu wa kisiasa kwa kupinga kila kitu. Hivi Rais amekosea wapi Alichokifanya si kimo ndani ya katiba ya nchi ambayo ilimpa rais kuteua tume iliyosimamia uchaguzi mkuu uliopita na ambao Mnyika alishiriki na kushinda? alihoji.
Rage, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoani Tabora, alisema Mnyika na viongozi wengine wa kambi ya upinzani wanatumia nguvu nyingi kubeza mchakato wa kuelekea kupatika kwa katiba mpya, badala ya kuhangaika kutatua kero za wananchi.
Alisema kiongozi wa kweli ni yule anayeguswa na matatizo ya mwananchi, na si anayetumia muda mwingi kupinga kila jambo, hata ambalo mwananchi wa kawaida halimgusi sana.
Chanzo: Jambo leo