Ni vita, Rage amvaa Mnyika

kuna mfano mbaya sana "ashakum si matusi" ... baba akiamua kujisaidia haja ndogo wkenye kona ya ukuta wa nyuma yake, ni chini ya mamlaka yake, lakini kamwe ile haiwezi kuwa sahihi... Rage asihalalishe kila mamlaka iliyo chini ya rais basi ni halal na yafaa kuliwa

Kinachosikitisha zaidi ni sisi watanzania, huyo jamaa ni convict, alifungwa kwa kosa la kisheria, sasa ni mwenyekiti wa wazazi tabora, mwenyekiti wa Simba, mbunge, anaendesha radio na anabwabwaja hovyo.............. THIS IS TOO SICK TO OUR NATION

HE SHOULD BE BARRED AS A CONVICT

Mkuu heshima kwako.Nadhani alichoaema Rage ni sahihi. Rais ameteua kwa mujibu wa katiba iliyopo sasa. Hapa tatizo si Rage wala Rais tatizo ni Katiba ambayo tunatakiwa tuijadili na kuiunda upya na madaraka kama ya kuteua watu kama hao yaondolewe kwa Rais. Iwe kama Kenya ambapo nafasi kama hizo zilitangazwa na watu kuomba na kuhojiwa hadharani. Ila sasa tatizo wanalolipata wakenya ni kwamb mchakato na nafasi zilichukuliwa na wanaharakati!
Mkuu Rage alitakaswa na mahakama kuu hivyo conviction yake ilifutwa.
 
Ruge ni Al shaabab nasikia, wana jf mnijuze katika hili.....!

Mbona kule Igunga hiyo ilikuwa ovious! Unajua Al Shababu ni wadau wakubwa wa kuilinda seroikali ya ccm. Maana wote ni waasi wa katiba ya nchi zao. Kama uamini muulize IGP Mwema au Jk mwenyewe atakuambia!!!
 
MBUNGE wa Jimbo la Tabora Mjini, Ismail Aden Rage (CCM) amemjia juu Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema) akimtaka kuacha kuubeza uteuzi wa Mwenyekiti na Mkurugenzi Mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), uliofanywa na Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni. Badala yake, amemtaka afahamu kuwa, yote yanayofanywa na Rais Kikwete yamo ndani ya mamlaka yake kikatiba.

“Jamani, mwambieni Mnyika aache kutafuta umaarufu wa kisiasa kwa kupinga kila kitu. Hivi Rais amekosea wapi Alichokifanya si kimo ndani ya katiba ya nchi ambayo ilimpa rais kuteua tume iliyosimamia uchaguzi mkuu uliopita na ambao Mnyika alishiriki na kushinda?” alihoji.

Rage, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoani Tabora, alisema Mnyika na viongozi wengine wa kambi ya upinzani wanatumia nguvu nyingi kubeza mchakato wa kuelekea kupatika kwa katiba mpya, badala ya kuhangaika kutatua kero za wananchi.

Alisema kiongozi wa kweli ni yule anayeguswa na matatizo ya mwananchi, na si anayetumia muda mwingi kupinga kila jambo, hata ambalo mwananchi wa kawaida halimgusi sana.

Chanzo: Jambo leo

Huyo RAGE ni mjinga tu!Hajui kwamba matatizo mengi ya wananchi yanazaliwa na mfumo uliotengenezwa na katiba!
 
Rage anaeleweka ni mtu wa majungu tu, hata historia yake toka mwenyekiti DRFA, katibu FAT mpaka mwenyekiti Simba ni migongano tu. Hata hivyo lazima asifie JK kwni ndiye aliyemtoa jela.
 
Mkuu heading yako ilinishitua sana nilidhani Rage kampiga kamanda Mnyika kwa ile bastola yake

Lugha za waandishi hizo.mimi nia yangu wengi muone watu wanavojikomba.jinsi wasivyo wazalendo.
Nadhani rage atapata anachokitakitaka.
 
Mkuu heshima kwako.Nadhani alichoaema Rage ni sahihi. Rais ameteua kwa mujibu wa katiba iliyopo sasa. Hapa tatizo si Rage wala Rais tatizo ni Katiba ambayo tunatakiwa tuijadili na kuiunda upya na madaraka kama ya kuteua watu kama hao yaondolewe kwa Rais. Iwe kama Kenya ambapo nafasi kama hizo zilitangazwa na watu kuomba na kuhojiwa hadharani. Ila sasa tatizo wanalolipata wakenya ni kwamb mchakato na nafasi zilichukuliwa na wanaharakati!
Mkuu Rage alitakaswa na mahakama kuu hivyo conviction yake ilifutwa.
nipe tatizo ni rage, amehalalisha uteuzi, hivyo kuhalalisha katiba hivyo kushundwa kuwa na wisdom ya kukaa kimya hasa kutokana na historia yake ya kifedhuli

hapa haikuzungumziwa mamlaka, bali product iliyotokana na mamlaka........... tusichanganye mambo
 
Rage anaeleweka ni mtu wa majungu tu, hata historia yake toka mwenyekiti DRFA, katibu FAT mpaka mwenyekiti Simba ni migongano tu. Hata hivyo lazima asifie JK kwni ndiye aliyemtoa jela.

Embu tukumbushe alipelekwa jela kwa kosa gani.
 
Mbona kule Igunga hiyo ilikuwa ovious! Unajua Al Shababu ni wadau wakubwa wa kuilinda seroikali ya ccm. Maana wote ni waasi wa katiba ya nchi zao. Kama uamini muulize IGP Mwema au Jk mwenyewe atakuambia!!!

Losomich,
nashukuru kunijuza hayo sasa nimepata uelewa mzuri zaidi,
 
Embu tukumbushe alipelekwa jela kwa kosa gani.
Duh! hujui? alighushi stakabadhi ya malipo ya sh. milioni mbili akahukumiwa miaka miwili jela akatoka kwa msamaha wa Rais(Kikwete) baada ya kutumikia mwaka mmoja hivyo iaonekana bado ana hangover ya segerea
 
nipe tatizo ni rage, amehalalisha uteuzi, hivyo kuhalalisha katiba hivyo kushundwa kuwa na wisdom ya kukaa kimya hasa kutokana na historia yake ya kifedhuli

hapa haikuzungumziwa mamlaka, bali product iliyotokana na mamlaka........... tusichanganye mambo
kwa hiyo mkuu unasema product ya mteule wa rais si mzuri? Kama si mzuri kwako kwa aliyemteua ni mzuri! Kwa hiyo mkuu ili mimi na wewe tupate product nzuri inabidi tushiriki kwa kupitia uwakilishi yaani mchakato uwe wa wazi na uteuzi ukifanywa basi wawakilishi wetu yaani wabunge waupitie n kuubariki/kuukataa. Hayo yote yanatakiwa yawepo kwenye katiba. Lakini kwa hali.ya sasa mtu mmoja kuamua si rahisi kukidhi matarajio yangu na yako! Kila mtu ni mbinafsi kwa hiho atakidhi matarajio yake kwanza! Tusipigie kelele product tupigie kelele process ya kupata hiyo product cause product is just an end result coming out of the process.
 
Unajua kiukweli huyu mzee mm sijajua bado kuwa kwenye siasa alifuata nn?huwa simuelewi kabisa katika mambo anayongea!
Na nina wasiwasi katika uwezo wake wa kuchambua mambo,yeye anamshangaa MNYIKA kupinga sasa na yeye anachopinga kwa MNYIKA ni kipi?
Anasema kiongozi ni yule anayeguswa na mataizo ya wananchi na hili la tume la uchaguzi halimgusi sana mwananchi wa kawaida!
mmmh!yaani huyu mzee ni zerro brain kweli!
 
huyu msomalia namchukia sana. Huyu na Manji wanafanya hata soka la bongo liwe bovu. Oovyo
 
nipe tatizo ni rage, amehalalisha uteuzi, hivyo kuhalalisha katiba hivyo kushundwa kuwa na wisdom ya kukaa kimya hasa kutokana na historia yake ya kifedhuli

hapa haikuzungumziwa mamlaka, bali product iliyotokana na mamlaka........... tusichanganye mambo

MTM,
Hivi mpaka saizi utakuwa umekunywa bia ngapi?
 
Back
Top Bottom