Ni vita, Rage amvaa Mnyika

Mwanakili90

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
1,568
245
MBUNGE wa Jimbo la Tabora Mjini, Ismail Aden Rage (CCM) amemjia juu Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema) akimtaka kuacha kuubeza uteuzi wa Mwenyekiti na Mkurugenzi Mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), uliofanywa na Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni. Badala yake, amemtaka afahamu kuwa, yote yanayofanywa na Rais Kikwete yamo ndani ya mamlaka yake kikatiba.

“Jamani, mwambieni Mnyika aache kutafuta umaarufu wa kisiasa kwa kupinga kila kitu. Hivi Rais amekosea wapi Alichokifanya si kimo ndani ya katiba ya nchi ambayo ilimpa rais kuteua tume iliyosimamia uchaguzi mkuu uliopita na ambao Mnyika alishiriki na kushinda?” alihoji.

Rage, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoani Tabora, alisema Mnyika na viongozi wengine wa kambi ya upinzani wanatumia nguvu nyingi kubeza mchakato wa kuelekea kupatika kwa katiba mpya, badala ya kuhangaika kutatua kero za wananchi.

Alisema kiongozi wa kweli ni yule anayeguswa na matatizo ya mwananchi, na si anayetumia muda mwingi kupinga kila jambo, hata ambalo mwananchi wa kawaida halimgusi sana.

Chanzo: Jambo leo
 
MBUNGE wa Jimbo la Tabora
Mjini, Ismail Aden Rage
(CCM) amemjia juu
Mbunge wa Ubungo, John
Mnyika (Chadema) akimtaka
kuacha kuubeza uteuzi wa Mwenyekiti na Mkurugenzi
Mpya wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC), uliofanywa na
Rais Jakaya Kikwete
hivi karibuni. Badala yake, amemtaka
afahamu kuwa, yote
yanayofanywa na Rais
Kikwete yamo ndani ya
mamlaka yake kikatiba. “Jamani, mwambieni Mnyika
aache kutafuta umaarufu wa
kisiasa kwa kupinga kila kitu.
Hivi
Rais amekosea wapi? Alichokifanya si kimo ndani ya
katiba ya nchi ambayo ilimpa
rais kuteua tume iliyosimamia
uchaguzi mkuu uliopita na
ambao Mnyika alishiriki na
kushinda?” alihoji. Rage, ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Wazazi mkoani Tabora,
alisema Mnyika na viongozi
wengine wa kambi ya
upinzani wanatumia nguvu nyingi kubeza mchakato wa
kuelekea kupatika kwa katiba
mpya, badala ya kuhangaika
kutatua kero za wananchi. Alisema kiongozi wa kweli ni
yule anayeguswa na matatizo
ya mwananchi, na si
anayetumia
muda mwingi kupinga kila
jambo, hata ambalo mwananchi wa kawaida
halimgusi sana.

Chanzo:Jambo leo

Rage ni muwamba ngoma tu ivyo nilazima avutie kwake,ila kwenye maongezi yake sijaona mantiki yoyote,
mfano:-hapo chini{mwishoni} amesema kua mh.mnyika anapingaga ata" jamba ambalo mwananchi wa kawaida halimgusi sana".Je anaushaidi gani?
Nimjuavo mh.mnyika ni kiongozi makini na mwenye kutetea haki za wananchi tena kwa umakini na hayo yanaonekana wazi ubungo.
Hivyo Mh.rage ni lazima ajue tume ya uchaguzi ni kiungo nyeti na chenye impact kubwa kwa wananchi ,chombo hiko kinaposhikiliwa na viongozi dhaifu au wasio na sifa muhimu ni hatari kwani mwisho wa siku wananchi watatangaziwa matokeo ambayo si sahihi.
Mh.Rage asikurupuke akajipange sawa sawa!
 
Matatizo yaliyopo Tabora mjini na ambayo Rage ameshindwa kuyasimamia ni Mengi,miaka 50 ya uhuru maji Tabora ni issue kubwa' manispaa ya Tabora imezungukwa na barabara mbovu ajabu,aache kumjadili Mnyika ajadili matatizo ya jimbo lake!
 
kuna mfano mbaya sana "ashakum si matusi" ... baba akiamua kujisaidia haja ndogo wkenye kona ya ukuta wa nyuma yake, ni chini ya mamlaka yake, lakini kamwe ile haiwezi kuwa sahihi... Rage asihalalishe kila mamlaka iliyo chini ya rais basi ni halal na yafaa kuliwa

Kinachosikitisha zaidi ni sisi watanzania, huyo jamaa ni convict, alifungwa kwa kosa la kisheria, sasa ni mwenyekiti wa wazazi tabora, mwenyekiti wa Simba, mbunge, anaendesha radio na anabwabwaja hovyo.............. THIS IS TOO SICK TO OUR NATION

HE SHOULD BE BARRED AS A CONVICT
 
Mh.Ruge ni Al shaabab nasikia, wana jf mnijuze vizuri katika hili.....!
 
Wananchi wazalendo ni lazima watumie muda mwingi kuhakikisha kuwa mchakato wa kupata katiba mpya ya nchi yetu hauchakachuliwi, kuepuka kupata katiba ambayo haitakidhi matakwa ya wengi!! Katiba mpya ikipatikana kero nyingi za wananchi zitatatuliwa kirahisi; kwa mfano mamlaka ya Rais kuteua watu kwenye nafasi nyeti kumbe ni mafisadi ambao vitendo vyao vinaongeza umasikin kwa wananchi, mamlaka hayo ya uteuzi yakithibitiwa na bunge upuuzi wa kuwapa vyeo maswahiba wa rais wasiowaadilifu utakwisha na hivyo kuwapunguzia machungu wananchi.
 
na wewe na watawala wa chama tawala kazi yako kubwa ni kuwapinga wapinzani kwa kila kitu sasa what is the difference??

Unampinga anayekupinga so tumeishia kupingana 100%

what a myopic vision

sure mkuu!
 
sisi wananchi tunajua kuwa Mnyika yuko sahihi.Na Rage lazima asifie mambo ya chama chake.Wasubiri 2015 wataisoma namba.Nipo kijijini kabisa kila ninayeongea nae anasema amechoka na mambo ya CCM .
 
wapinzani wao kazi yao kubwa ni kupinga kila kitu.
yes ni kweli, kama ilivyokazi ya watawala ccm, kufanya ufisadi, pa kuandaa logistic za kujilinda na maovu na dhuluma walizofanya lazima kupinga, wewe vipi??? Kama unakuwa una la maana kuwasilisha janvini heri uwe unakaa kimya kuliko kutuchefua na pwenti zako shudu pia pumba
 
Hakuna mtu huwa simtilii maanani kama Rage but katika hili la Mh Rais kumteua Lubuva yuko sahihi na tunapaswa kukubali maana katiba/mamlaka iliyomuongoza Jk ni hii hii ambayo haijabadilishwa,sasa aache kuteua? Ni mpaka hapo katiba itakap[obadilishwa na kuelekeza tofauti katika jambo la tume ya uchaguzi na upatikanaji wa viongozi wake
 
Wapinzani wao kazi yao kubwa ni kupinga kila kitu.

Kama kila kitu anachofanya mkuu wa nchi kimekaa kisiem siem na siyo kimaslahi ya taifa wataachaje kupinga? Kama hawataki kupingwa waache usiem siem waanze kuwatumikia wenye nchi bila kujaki tabaka zao za kisiasa. Hapo wataelewana na vyama vya upinzi!!!
 
Hivi Rage nae na ubongo wa kubishana na Mnyika? Rais wako ni mchemfu siku zote na ataendelea kupingwa hata nyinyi wachumia tumbo akina Rage mumtetee mpaka povu ziwatoke.
kuchemka ni maumbile ya kibinadamu hata mnyika alichemka kusaini karatasi zile ikulu baada ya kupiga tea na juice za ikulu na kutuingiza choo cha stendi,lakini tumemsamehe,ndio tz yetu,ingekua kwa watani wa jadi hapo jirani sijui nini kingempata mnyika kwa "uzembe" ule
 
kuna mfano mbaya sana "ashakum si matusi" ... Baba akiamua kujisaidia haja ndogo wkenye kona ya ukuta wa nyuma yake, ni chini ya mamlaka yake, lakini kamwe ile haiwezi kuwa sahihi... Rage asihalalishe kila mamlaka iliyo chini ya rais basi ni halal na yafaa kuliwakinachosikitisha zaidi ni sisi watanzania, huyo jamaa ni convict, alifungwa kwa kosa la kisheria, sasa ni mwenyekiti wa wazazi tabora, mwenyekiti wa simba, mbunge, anaendesha radio na anabwabwaja hovyo.............. This is too sick to our nationhe should be barred as a convict
ni kweli mkuu mtm.. Hii ni hatari sana kwa nchi yetu ndo ata hakuna la maana linalofanyika maendeleo tuko nyuma kabisa, huyu alifungwa tena kwa kosa la wizi, mdokozi pia kibaka uyu, kama angefanya udokozi wake manzese wallahi tungemchoma moto, leo hii kaaminiwa na ccm wezi wenzake, watarajia ataongea nini, nawalaumu sana ata simba wanajua uyu ni kibaka wao wamempa madaraka lzm alikata mlungula, tabora pia watakuwa wanajua wamemchagua kiongozi mwizi pia mdokozi, kwa kuwa alifungwa kwa kosa la kukwapua ela pale fat sasa tff, lakini kuna siku mafisadi watashindwa....
 
Back
Top Bottom