Ni ushirikina mtupu, Anaongelewa nani hapa?

PhD

JF-Expert Member
Jul 15, 2009
4,599
3,673
Alhamisi, Machi 21, 2013 07:26 Na Mwandishi Wetu


UONGOZI KAMATI ZA BUNGE
*Mbunge maarufu akutana na waganga hoteli ya Lamada
*Aulizwa, akana, amkamatisha mwandishi polisi Oysterbay

MMOJA kati ya wabunge maarufu kutokana Kanda ya Ziwa, Kambi ya Upinzani, (jina tunalihifadhi kwa sasa), ametajwa kutumia njia za kishirikina katika kuwania uongozi wa moja ya kamati za Bunge.

Mbunge huyo ambaye hata hivyo juzi alibwagwa katika kinyang'anyiro hicho, anadaiwa kufanya kitendo hicho wakati wa uchaguzi wa kamati hizo mwaka 2010 jijini Dar es Salaam, na akashinda.

Mbali na kiongozi huyo, pia uchunguzi wa Rai kupitia vyanzo mbalimbali vya habari umebaini kuwa, wanasiasa wengi nchini pamoja na watendaji waandamizi serikalini wamekuwa wakijihusisha na masuala ya ushirikina katika kulinda na kutetea nyadhifa zao.

Kundi jingine ambalo linatajwa kujihusisha na vitendo vya kishirikina ni watendaji au wastaafu ambao kwa namna moja au nyingine wamejikuta wakiwa na kesi mahakamani, hivyo kukimbilia kwa waganga kutafuta kinga kutokana na kuchanganyikiwa kunakosababishwa na madhila yanayowakabili.

Taarifa za uhakika ambazo Rai inazo zimedai kuwa, baada ya kutambulishwa kwa waganga hao, Mbunge huyo alikwenda kukutana nao katika hoteli ya Lamada iliyopo Ilala jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kupata msaada ili ashinde.

Baada ya kukutana nao na kueleza ni nini alikuwa akihitaji kutoka kwa waganga hao, walikubaliana malipo na ndipo kazi ya ‘kumrekebeshia' mambo yake ikaanza.

Masharti aliyopewa:

Kwa mujibu wa uchunguzi wa Rai, Mbunge huyo alitakiwa na waganga hao achukue karatasi na kundika yale yote ambayo alitaka waganga wayafanye, ili kufanikisha azma yake.

Katika karatasi hiyo (nakala tunayo) ikiwa na sahihi yake, Mbunge huyo pamoja na mambo mengine alitaka asaidiwe kushinda uenyekiti wa moja ya kamati nyeti za Bunge, na kuwataka wamdhuru (Mbunge kijana) aliyekuwa tishio kwake, kwa kumuandika jina.

Baada ya hapo, alichukuliwa na kupelekwa Ziwa Victoria maeneo ya Musoma ambako alivuliwa nguo na kuogeshwa maji ziwani, akavikwa shuka jeusi, kisha akapelekwa Mombasa, Kenya, ambako pia aliogeshwa maji ya Bahari ya Hindi na kufanyiwa matambiko mengine.

Baada ya kurejea Dar es Salaam akiwa ‘mzito' kutokana na mchakato wa uganga, alishiriki uchaguzi na kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti, ingawaje hakuna uthibitisho kama alishinda kwa uwezo wa nguvu za giza 2010.

Pia kwa mujibu wa taarifa zilizopo, Mbunge huyo alitoa mamilioni ya shilingi kwa ajili ya shughuli hiyo, pamoja na kutoa fedha kuhakikisha taarifa hizo hazivuji, ambapo baadhi ya namba za akaunti alizotuma fedha Rai inazo.

Hatua alizochukua kukabiliana na Rai:

Jumapili iliyopita (Machi 17), kiongozi huyo alipigiwa simu na kuulizwa juu ya ushiriki wake katika vitendo vya ushirikina, lakini hakukubali wala kukataa, bali alimtaka mwandishi akakutane naye katika baa moja maarufu maeneo ya Masaki jijini Dar es Salaam saa 9:30 mchana, kwa ajili ya kutoa ufafanuzi.

Mwandishi alifika eneo la tukio saa 9:40 akiwa ameambatana na mtu mwingine, na dakika chache baadaye, Mbunge huyo alifika na kusaliamiana kisha kuketi pamoja.

Sekunde kadhaa baada ya mbunge huyo kukaa, walifika watu wawili ambao walikaa kwenye viti katika meza ya pembeni, na mwingine wa tatu akasimama nyuma ya mwandishi.

Baada ya watu wale wawili kuketi, mara moja walihamia kwenye meza aliyokuwapo kiongozi huyo na mwandishi, na wakajitambulisha kuwa wao ni askari polisi kutoka Kituo cha Oysterbay, na kwamba wanamuhitaji mwandishi kwa ajili ya mahojiano kituoni.

Mwandishi alitii sheria bila shuruti, na wakati wa kulipa ankara, wale polisi waligundua kuwa mwandishi hakuwa peke yake, bali aliambatana na mtu mwingine, hivyo wakasema na yule mtu mwingine pia anahitajika kwa mahojiano.

Baada ya malipo ya vinywaji kufanyika, askari watatu, mwandishi na mwenzake pamoja waliingia ndani ya gari la Mbunge huyo (namba za usajili tunazo) huku akiendesha yeye mwenyewe na kwenda kituoni Oysterbay.

Kituoni hapo, Mbunge huyo alipelekwa chumba tofauti na mwandishi, lakini polisi walipotaka kuchukua maelezo, mwandishi aligoma na kuwataka wasubiri hadi wakili wake atakapofika, jambo ambalo polisi walikubali.

Lakini muda mfupi baadaye, walikuja kumwambia mwandishi kuwa anaitwa ofisini kwa OC-CID, lakini kabla ya kumpeleka yeye na mwenzake, waliwakagua na hawakukuta chochote kile.

Baada ya kufika kwa OC-CID, mwandishi aliulizwa kwa nini amekataa kuandika maelezo, naye akajibu kuwa hajakataa, ila angependa aandike maelezo mbele ya wakili wake.

Lakini mwandishi aliwaomba polisi awape maelezo kwa mdomo ili wajue ni nini hasa kinaendelea, kwa sharti kuwa mbunge naye aitwe ili asikie nini mwandishi atawaeleza polisi.

Polisi bila ajizi, wakamwita mbunge huyo, na ndipo mwandishi akamueleza mbunge yote aliyoyafanya, jambo ambalo lilisababisha kiongozi huyo kusawajika kabisa, ilhali akikanusha kwamba hahusiki.

Baada ya hapo, akawaambia polisi kuwa yeye binafsi hana ugomvi na mwandishi, lakini alitaka mwandishi aisaidie polisi kwa kuwataja wabaya wake (waliotoa siri), ambapo baadaye mwandishi aligundua kwamba kitu kikubwa ambacho mbunge huyo alikuwa akikitaka, ni ile karatasi aliyoandikisha kwa waganga, na ndio sababu iliyofanya mwandishi na mwenzake kupekuliwa.
 
:scared: Dah! Kama mtu mzima anaweza kuonesha utupu wake wa kizee kwa mganga wa kienyeji ili apate cheo, akiambiwa akalete mkono wa kushoto wa albino pamoja na sehemu zake za siri atashindwa kweli? Hii inatisha kweli kweli. Kumbe ukiwavua baadhi ya watu nguo utawakuta na mahiriza makubwa makubwa. I thank God for I worship a living God and not the Devil and his agents who are deceivers on earth and tormentors in hell.
:msela:
 
Yaani hawa watendaji wa serikali ya nchi hii ni mafundi kwelikweli nyei waoneni hivyo hivyo na suti zao.
 
Huyo mbunge kwa hiyo alishindwa na bingwa mwenzake ambaye ni pro kwenye ushirikina ama aliyemshinda huyo mbunge ni bingwa wa maswala ya kiroho?Duh,wanasiasa wasomi!
hizi ndumba zinazidiana, maana kuna za
a) Tanga (Mwambao wa pwani) hawa hutumia majini ya baharini
b) Za Sumbawanga hizi kaka ni hatari sana, zinatumia mizimu ya kale, hapa hata radi saa sita mchana jua kali inakurarua rarua.
c) Kuna za kigoma; hizi zina asili ya nchi jirani ya Burundi hizi ni noma pia
d) Za Shinyanga; hizi ni ndagu, zinatumia mizimu na fisi-watu; hapa kiboko ya matatizo, hufiki mbali umeshakudaka.

upo mzee; ila ile ya Tanga kiboko yao maana hizi zingine hazivuki bahari....
 
Ben, wasomi wetu wana program za kujiwezesha kupitia weapons of mass destruction. We need a level play ground in political and social life wazee, maana kama mimi ninatumia akili kupambana na wengine wanatumia majini (halafu wanatumia kivuli cha Ujana na Usomi kuzuga haaaa!!!! give me a brake bro!

Huyo mbunge kwa hiyo alishindwa na bingwa mwenzake ambaye ni pro kwenye ushirikina ama aliyemshinda huyo mbunge ni bingwa wa maswala ya kiroho?Duh,wanasiasa wasomi!
 
:scared: Dah! Kama mtu mzima anaweza kuonesha utupu wake wa kizee kwa mganga wa kienyeji ili apate cheo, akiambiwa akalete mkono wa kushoto wa albino pamoja na sehemu zake za siri atashindwa kweli? Hii inatisha kweli kweli. Kumbe ukiwavua baadhi ya watu nguo utawakuta na mahiriza makubwa makubwa. I thank God for I worship a living God and not the Devil and his agents who are deceivers on earth and tormentors in hell.
:msela:

Nahofia maisha ya ndugu zetu Ma-Albino,kama wanasiasa hizo ndio zao ,sasa maisha ya hawa wenzetu yapo matatani.
 
Mwanzo wa habari ilielekea kama ni Hon.Cheyo lakini mbela ya habari inabadilika na kuwa Hon. Vijisenti

Ndugu Ndachuwa umeiona hii sentensi???

"MMOJA kati ya wabunge maarufu kutoka Kanda
ya Ziwa, Kambi ya Upinzani"

Huyo Hon. Vijisenti siku hizi yupo Kambi ya Upinzani??
 
Last edited by a moderator:
"...Mkinichagua kuwa Raisi nitawajaza mapesaa.." kumbe mapesa ya kishirikina!!
 
Back
Top Bottom