Ni ushirikina mtupu, Anaongelewa nani hapa?

Kumbuka ni mbunge wa upinzani, mzee wa vijisenti hayuko upinzani

Ndugu Ndachuwa umeiona hii sentensi???

"MMOJA kati ya wabunge maarufu kutoka Kanda
ya Ziwa, Kambi ya Upinzani"

Huyo Hon. Vijisenti siku hizi yupo Kambi ya Upinzani??

Nilitegemea majibu yenu maana gazeti la Rai haliwezi kuandika mazuri ya upinzani. Hiyo ziara ya Dar - Ziwani - Mombasa nayo ilichukua siku ngapi? BTW Mwenyekiti wa kamati kuna anachofaidi kikubwa sana zaidi ya wajumbe wengine?
 
Ndugu Ndachuwa umeiona hii sentensi???

"MMOJA kati ya wabunge maarufu kutoka Kanda
ya Ziwa, Kambi ya Upinzani"

Huyo Hon. Vijisenti siku hizi yupo Kambi ya Upinzani??

No wonder mbunge wanayesema anatoka ziwa tanganyika akatutishia ataumaliza kama mapanya ,hivi ni yeye tuuu anayetaka kurogwa au yeye ukigagula wake umemfanya atapetape kama mwewe
 
Nataka niamini kuwa CCM imeandaa kikundi cha kufuatilia nyendo za wabunge wa upinzani kuwamaliza kwa kashafa baada ya ligwaride la majukwaani kuwashinda. Tukianzia na Rwakatare, then hili la Cheyo na ninajua wapo wengine wengi wanafuatiliwa ili kurekodiwa kwa lengo la kuwachafua na hivyo kunyongonyesha kasi ya upinzani.

Nawashauri wabunge wa upinzani wawe extra care kwa wanaye ongea naye, vitu wanavyoongea na mahali wanapoviongelea. Ikiwezekana mamabo ya siri waongee na watu wanaowaamini tu na si vinginevyo la sivyo inteligensia ya CCM imejipanga kwa kiasi kikubwa na wamebuni mbinu hii ya kigaidi kuwamaliza.
 
hizi ndumba zinazidiana, maana kuna za
a) Tanga (Mwambao wa pwani) hawa hutumia majini ya baharini
b) Za Sumbawanga hizi kaka ni hatari sana, zinatumia mizimu ya kale, hapa hata radi saa sita mchana jua kali inakurarua rarua.
c) Kuna za kigoma; hizi zina asili ya nchi jirani ya Burundi hizi ni noma pia
d) Za Shinyanga; hizi ni ndagu, zinatumia mizimu na fisi-watu; hapa kiboko ya matatizo, hufiki mbali umeshakudaka.

upo mzee; ila ile ya Tanga kiboko yao maana hizi zingine hazivuki bahari....

Kiboko yao woote ni Yesu maana ni zaidi ya wachawi na ni mganga wa waganga.
 
Huyo ni mzee wa mapesa ambapo 2010 alishinda kuongoza hiyo kamati ambayo sasa imechukuliwa na mwana wa lake tanganyika..95% ya watanzania wanaishi kwa kutegemea ushirikina.
 
Huyo mbunge atakuwa wa Chadema tu.
Hakuna Cham kingine kinaweza fanya madudu ya namna hiyo.
 
Mwanzo wa habari ilielekea kama ni Hon.Cheyo lakini mbela ya habari inabadilika na kuwa Hon. Vijisenti

Kwa hiyo ndo kusema hapa wewe inakuchanganya? Unashindwa kuelewa kama huyu ni Mapesa au Vijisenti? Duh!
 
Nataka niamini kuwa CCM imeandaa kikundi cha kufuatilia nyendo za wabunge wa upinzani kuwamaliza kwa kashafa baada ya ligwaride la majukwaani kuwashinda. Tukianzia na Rwakatare, then hili la Cheyo na ninajua wapo wengine wengi wanafuatiliwa ili kurekodiwa kwa lengo la kuwachafua na hivyo kunyongonyesha kasi ya upinzani.

Nawashauri wabunge wa upinzani wawe extra care kwa wanaye ongea naye, vitu wanavyoongea na mahali wanapoviongelea. Ikiwezekana mamabo ya siri waongee na watu wanaowaamini tu na si vinginevyo la sivyo inteligensia ya CCM imejipanga kwa kiasi kikubwa na wamebuni mbinu hii ya kigaidi kuwamaliza.

Mkuu, kama kweli ni Cheyo wala usiwe na wasiwasi. CCM hata siku moja haiwezi kuhangaika nae. Baada ya kusoma hii habari nimekuja na theory hii: Mwandishi wa hiyo habari alinyaka sakata la huyo mbunge mshirikina. Baada ya kulinyaka (kama walivyo waandishi wengi wa Tz) akampigia simu mhusika kumwambia kuwa ushirikina aliofanya umegundulika na atamwanika mchana kweupe asipomshikisha kitu kidogo. Mbunge mshirikina akamwasa mwandishi wakutane bar wayamalize Siku ya siku ilipofika mwandishi na mbunge hawakuelewana na ndio yakaishia polisi (huenda ni mbunge aliwatonya polisi lakini mwandishi akashtukia. Labda niongezee hao waganga kwa asilimia kubwa watakuwa ni matapeli ambao:
1.walichukua fedha kwa mbunge mhusika kwa kujifanya kumgangia
2.Halafu wakapeleka dili kwa mwandishi ili mbunge atakapohonga mwandishi kumfichia siri, awakatie kitu kidogo
Vingenevyo unafikiri huyo mwandishi aliwezaje kupata karatasi ya aliyoondika huyo mbunge?
 
Huyo mbunge kwa hiyo alishindwa na bingwa mwenzake ambaye ni pro kwenye ushirikina ama aliyemshinda huyo mbunge ni bingwa wa maswala ya kiroho?Duh,wanasiasa wasomi!

You are so predictable! Huwezi kuacha vijembe kijana. Ha ha ha ha!
 
Huyo ni mzee wa mapesa ambapo 2010 alishinda kuongoza hiyo kamati ambayo sasa imechukuliwa na mwana wa lake tanganyika..95% ya watanzania wanaishi kwa kutegemea ushirikina.

Mkuu ukijua undani wa haya mambo wala hutashangaa sana (japokuwa ni ya kushangaza kwelikweli). Unajua siku hizi kuna mtandao wa matapeli unaoshirikiana na waandishi wa habari. Matapeli wanawafuatililia wanasiasa/viongozi wa dini/na watu maarufu katika jamii halafu wanapojua ma-skandali yao wanawapelekea waandishi wa habari, na waandishi nao wanamshtua mhusika na kutisha kumwanika uchi mbele ya dunia kama hatawapooza. Na wanapofanikiwa kupata kitu wanawagawia matapeli. Inaweza ikawa skandali yoyote, kuanzia ushirikina, ngono, rushwa n.k. Mfano hai ni ile kesi ya Muro. Ni kwavile mambo yanamalizwa kimya kimya tu lakini ni wengi wameshalizwa. Listi ni ndefu eg Mama Lwakatare, January na wengine wengi. Sasa hili la huyu mbunge naona kuna mahali walishindwana au hawakuaminiana. Wewe hebu fikiria huyo mwandishi anadai ana mpaka karatasi ambayo huyo mbunge aliandika ''ma-wishes'' yake. Huona atakuwa anafahamiana na hao ''waganga'' na wana ushirikiano wa karibu kabisa?
 
Mwanzo wa habari ilielekea kama ni Hon.Cheyo lakini mbela ya habari inabadilika na kuwa Hon. Vijisenti

Ingawaje wote ni wanyantuzu na washirikina kwa kwenda mbele; vijisenti amesoma mpaka Havard University lakini bado anaendekeza mambo ya nguvu za giza!!! Safari hii Vijisenti hajagombea uenyekiti bali ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa kamati mpya ya bajeti hivyo anabaki huyo bwana Mapesa kama ndio mlengwa wa thread hii!!
 
Ndo maana tuna maisha magumu na Mungu anazidi kutuenyesha wa Tz ,giza limeingia sana serikalini kuanza na ikulu
 
Back
Top Bottom