Ni ripoti ya Kijinga: I really mean it...

Wakulaumiwa ni Watanzania,tunatukanwa wazi wazi tupo kimya,hakuna anayejali.nimechukia sana jana mpaka najiuliza tuna vyombo makini na viaminifu vya ulinzi na usalama kweli?
Tunashikwa Mat.ako hadharani alafu tunajichekesha tu!!!!:smash:
 
Hawa wametuchoka kifuatacho ni sisi kutumia akili zetu maana haiwezekani wakatufool kama watoto hata mtoto akiangalia ile picha alipowekwa chini na atatoa maelezo bora kuliko haya ya kamati.
Kingine kwanini sisi tusubirie haya yote yqendelee kutokea? We need change in these three years laa sivyo tutajuta kuishi Tanzania.
Raisi yuko angani muda wote wananchi tunateseka na rasilimali zote hizi kweli naendelea kuamini kuwa Penye miti hapakosi wajenzi ila kwetu wajenzi hakuna.
Wananchi tuache kununuliwa kwa kuprotect mtu fulani huku tukiendelea kuumia

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Ripoti ya MCT imeeleza kile kilichofichwa na ripoti ya Jaji Ihema. Ninachotarajia mimi ndani ya saa 24 zijazo ni RPC Kamuhanda kuwajibika na hatimaye afikishwe mahakamani kwa matumizi mabaya ya madaraka yake.
 
Kuitoa CCM madarakani iwe ni kampeni zaidi ya kisiasa,Pia wanasiasa wa upinzani watakaokuwa wana compromise na wanaCCM kwa jambo lolote nao watakuwa maadui zangu rasmi

Lazima tuwatoe CCM madarakani kwa namna yoyote hata bila Chadema!!!
 
Kwanini wasiendelee kudharau iwapo wanajua cha mwisho wasomaji wanachoweza kufanyi ni uchambuzi tu! Kama matokea ya msomaji yanatabirika kwa mwandishi, kwanini apate hofu! Labda katika hili tume huru/binafsi/wakereketwa ndio zinapaswa kuibuka kuandika kwa kina!
 
Nyerere aliwahi kusema "mtu mwenye akili akijua kuwa na wewe una akili akakushauri jambo la kipumbavu na wewe ukakubali atakudharau". Hili ni kweli pia kwenye suala hili. Mtu mwenye akili akijua na wewe una akili ahalafu akakuandikia jambo la kijinga na wewe ukalikubali atakudharau!

Hii ripoti ni ushahidi wa kile ambacho wengine tunaamini ni kweli; CCM na serikali yake ni lazima waondolewe madarakani sooner kwa sababu wanatudharau! Ni dharau ya ajabu sana hii. Fikiria mtu anaandika hivi kwenye ripoti:

Kwa minajili hii basi Kamati imeshindwa kubaini baada ya kumalizika operesheni na askari Polisi kuanza kuondoka, kwa nini Mwangosi alishambuliwa kwa kipigo kabla ya kulipuliwa na bomu la kishindo?


Hili swali ni la msingi sana katika tukio zima.

Lakini Kamati imeshindwa kujibu swali ambalo kwa walioona iile video ya mauaji wanalikumbuka sana yaani linalohusiana na kukatazwa kufanyika kwa mikutano ya ndani ya chama. Kamati inatuambia kuwa barua ya zuio hilo inasema hivi:


Kumbe zuio lilihusu "mikutano na maandamano". Kwamba inaweza kujengwa hoja ya kuwa "mikutano" ilimaanisha "mikutano yote" ni vigumu kutetea hasa kwa vile wakati huo huo mikutano mingine ya kisiasa ilikuwa ikifanyika sehemu mbalimbali nchini bila kuzuiwa. Kamati ili kuonesha ulinganifu ingejaribu kutafuta maelezo ya Polisi Zanzibar kwanini waliruhusu CCM kufanya mkutano wake kule wakati kuna zuio. Lakini vile vile ni vigumu kusema kuwa mikutano yote ya kisiasa ya ndani haikuwa imeruhusiwa! Ni vyama vingapi ambavyo vilikuwa na mikutano ya ndani ya kamati zake mbalimbali kati ya August 26-Septemba 8?

Kamati ingeweza ili kulinganisha "utii wa sheria" kwa vyama vingine kuelezea kuwa vyama vingine havikufanya mikutano yoyote kati ya tarehe hizo na ni CHADEMA tu ambao walikuwa na mkutano Iringa. Hoja kuwa CDM hawakuwa watii ingekuwa na nguvu! Nje ya hapo ni kutuandikia ujinga.

Lakini kuthibitisha upuuzi wa kamati hii imeshindwa kuelezea kuwa kwanini katazo hilo liwe halali Iringa lakini Zanzibar lisiwe halali wakati CCM walipofanya uzinduzi wa kampeni yao ya Bububu? Hiki ndio kipimo cha upuuzi wa ripoti hii. Kama amri ambazo zilitolewa zilihusu vyama vyote kwanini Zanzibar waliendelea na mikutano ya kisiasa? Au wao hawakutakiwa kutiia sheria hiyo au kwa vile hakukutokea machafuko yoyote (na hayajawahi kutokea yakisababishwa na polisi!) huko Zanzibar?

Ikumbukwe kuwa uhalali wote wa polisi kutumia nguvu kuwatanya CHADEMA pale Nyololo unatokana na ukweli kuwa mkutano ule ulikuwa haramu. Lakini kama mkutano ulikuwa halali (kwa maana ya mkutano wa ndani ambao haukukatazwa) uhalali wa kutumia polisi unatoka wapi?

Ili kuthibitisha kuwa ilikuwa ni ripoti ya kijinga ni kuwa Kamati haikuwahoji wale polisi waliokuwa wamemzunguka Mwangosi na haijamhoji yule mtuhumiwa ili aelezee ilikuwaje yeye na wenzake wamshambulie Mwangosi na kwanini atumie nguvu zaidi. Inashangaza tu kuwa ripoti inataka wachukuliwe hatua za kisheria. Na kamati inaonekana haikuchukua muda kuangalia ile video au hata kuitisha watu waliokuwepo kuwapatia picha za video za tukio hilo zima. Na cha kushangaza Kamati hii iliyofanya mambo mengi ya uchunguzi imeshindwa kutoa jibu au hata dokezo la vilikopotelea vifaa vya kazi vya Mwangosi (kamera na laptop)!!

Lakini vile vile ripoti hii ambayo nina uhakika imetumia fedha ya kutosha tu (sijui nani atauliza Bungeni tuambiwe) imeshindwa kumhoji au hata kutuambia maoni ya shahidi muhimu sana katika sakata hili. Ripoti inatutajia kitu muhimu kumhusu:



Huyu Godrey Mushi ni mzima? kwanini alipigwa? Kwanini alikamatwa baada ya kupigwa? Hivi hawa watu hawakuona kuwa kulikuwa na kashfa mbili pale? ile ya Mwangosi na ile ya Mushi? Hivi ingekuwa Mwangosi hajafa pale hii kamati ingechunguza nini kama siyo kupigwa na polisi kwa Mushi?

Hata hivyo kuna ujinga mwingine katika ripoti hii. Waziri wa Mambo ya Ndani Bw. Nchimbi akiokoa jahazi alisema kuwa kuna taarifa ambazo kamati yake (ya serikali) imeweka kibindoni kwa sababu za kimahakama. Ameeleza kuwa mambo hayo yamefichwa ili kuzuia mtu aliyeshtakiwa asije kuitumia kujinusuru. Kwa maneno yake amesema hivi:



Sasa mwenyewe Nchimbi hapa inawezekana aliamini kuwa amezungumza "pointi" sana. Katika mawazo yake haki ya adui yake siyo haki. Kumbe yule mtuhumiwa anayo haki ndio maana mahakamani kwenye kesi hizi wale wa upande wa mashtaka wanatakiwa waweke wazi ushahidi wote ambao wanao hata ule unaoweza kutumiwa kumtoa mtuhumiwa hatiani katika kile kinachoitwa "discovery" kabla ya kesi kuanza. Lengo ni kuhakikisha kuwa ushahidi wowote - wa kumtia mtu hatiani au kumtoa - unawekwa wazi kwa upande mwingine ili kuhakikisha kuwa mtuhumiwa anapewa nafasi ya haki.

Kwa maneno ya Nchimbi serikali inao ushahidi wenye kuonesha kuwa yule mtuhumiwa wa polisi inawezekana asiwe na hatia (hata kama picha zinaonesha kashika bunduki au kweli aliua) na serikali iko tayari kuficha ushahidi huo ili mtuhumiwa yule atiwe hatiani. Sijui wanasheria wetu wanaweza kusema vipi kuhusu haki ya yule mtuhumiwa kuweza kumuita Waziri Nchimbi, Mwenyekiti wa Kamati pamoja na ripoti kamili kama sehemu ya utetezi wake ili waweze kuona kama kuna ushahidi wowote wa kuweza kumsaidia. Haki ni haki hata kama ni ya adui yako. Si ndio wanasema "mnyonge mnyongeni haki yake mpeni"? Kama kuna ushahidi unaoweza kumtoa yule kijana Polisi hatiani kwanini Nchimbi na Kamati wauweke pembeni?

Si ndio uvunjaji mkubwa zaidi wa haki kwenda kumhukumu mtu kwa sababu hatutaki aachiwe hata kama sababu ya kumwachia ipo?

Simply put, Ni ripoti ya kijinga.

Mzee Mwanakijiji I greet you!
nakubaliana nawe kwa mengi ila we are not doing justice to the late DM (R.I.P), hii ni kwa sababu badala ya ku-seek justice, some of us tuna mtumia for political gains! this is unfair! as we all know in politcs all means are as good provided inakupeleka Ikulu sote tualijua hilo ila are we doing justice to DM and his family? hapo kwenye red, do we have to wait mpaka kijana mmoja afe tutamke hayo? and kama ni kuiondoa ccm na serikali madarakani, how? tunapindua nchi, tuitisha uchaguzi au tunafanyaje? kwa upande mwingine hili suala la DM (R.I.P) lina pande mbili wazungu wanasema "it takes two to tango" kwanini CDM hawakubali kwa wana role japo kidogo katika hili? well Dr. Slaa nafsi imemsuta hadi kaamua kuwasomesha watoto wa marehemu nampongeza kwa hilo ila CDM wanatumia nguvu nyingi saana kujisafisha ila doa la damu halisafishiki kirahisi hivyo itachukua muda sana! all in all lets not use kifo cha DM for political gains! afterall CDM itself now ni household brand, wala hawahitaji kutumia mbinu za chini ki hivyo kupata popularity, what CDM needs ni stability and confidance period! the rest tutajua 2015 Bhaaaaas!
 
Wote tunajua ni namna gani hawa watala (wanaoshinda ulaya wakivutwa na farasi) wanavyotudharau, kitu ambapo naona ni kigumu kwetu na labda wengi hatujui na hata kama tunajua hatuchukui hatua ni 'nini nafasi ya mwananchi wa kawaida, wewe na mimi tufanye ili kukomesha uhuni huu'
 
hapa msishangae wanatoka na hukumu ya kwamba yule polisi aliuwa bila kukusudia ni ripot ya kijinga iliyoandaliwa na wajinga na kwa nia ya kupotosha umma kwa imani ya kuwa watanzania bado ni wajinga kama system inavyoamini
 
Tusubiri bunge mwakani (February au April), Mwanasheria mkuu anaweza kupeleka marekebisho ya sheria kuhusu uendeshaji wa shughuli za vyama vya siasa.

Lakini wakae wakijua, kamati ni batili (kisheria), na pili imechukua michango toka upande mmoja. CHADEMA walitoa tamko rasmi la kukataa kuongea na kamati-batili. Waliyokuwa wachovu hawa watu, walishindwa hata kuongea na familia ya marehemu Mwangosi ili kujua kama alikuwa anahofia usalama wake?
 
Hii ni kashfa pia waziri Nchimbi anatakiwa kujiuzuru kwa kuadaa wa TZ .
Na kutumia kodi ya wa TZ bila tija wakati ushahidi wa picha umeonyesha askali wake akifanya vitu vyake juu ya mwangosi.

Hatari sana anawaona wa TZ wajinga kwelikweli!
 
Mambo mengine yanayofanyika katika nchi hii ni ya kusikitisha sana, nautilia shaka sana uwezo wa kufikiri wa Watanzania, ripoti ya kijinga namna ile huwezi kuileta kwa watu mpaka uwe una uhakika kwamba uwezo wao wa kufikiri ni duni sana, nawapeni pole sana Watanzania, poleni sana ndugu zangu Watanzania.

Wewe mwenye uwezo mzuri wa kufikiri umefanya nini mpaka sasa? au wewe sio miongoni mwa watanzania! kuandika hapa JF haikufanyi uwe tofauti na watanzania wengine walioshikwa pabaya.

 
Ripoti haihusishi moja kwa moja jeshi la Polisi!!. Wakati huohuo Polisi anayehusiswa na mauaji ya mwangosi yupo Mahakamani!!!!?

Haya. Ripoti haijui kwanini Mwangosi kauliwa sasa ilikuwa na maana gani kuunda kamati? Hela zilizotumika ni kiasi gani? Jamani tuamke toeni hili li CCM pale 2015 jamani tutakwishaaaaa.
 
Hii ni dharau kubwa sana kwa wananchi wa nchi hii waliostaarabika, wenye uelewa. Tume imedhamiria kuonyesha dharau hata kwa wale walioshuhudia tukio live.

It is my impression that Judge Ihema and his team has never went to the scene of the incident
 
Back
Top Bottom