Ni ripoti ya Kijinga: I really mean it...

Msingi wa haya yote ni dharau dhidi ya wananchi (contempt of the people). Watawala wanaamini wanaweza kusema lolote, vyovyote, kwa yeyote bila kujali matokeo yake. Hawataki kuulizwa na wakiulizwa wanaona unaleta vurugu.

Kwa hiyo unashauri nini kifanyike?
 
inasikitisha sana kusikiliza taarifa ile........ hizi tume za nchi hii zimeshindwakutoa taarifa za kweli hata kwa kitu kinachooneka aibu tupu
 
Kufuatia matunda na unyenyekevu alioounesha Teophil Makunga kwa genge la wauwaji, natalajia soon DPP kuiondoa kesi yake mahakamani pamoja na Samson Mwigamba kwa maelezo kwamba upande wa mashtaka hauna nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Usaliti wa namna hii kamwe haukubaliki ni heri ujitoe kwenye kamati na Dunia ingemuheshimu, mimi na Familia yangu tutafanya maombi ya Novena na kufunga kushitaki kwa Mwenyezi Mungu aishushe laana juu ya huyu Tophil Makunga. sababu yeye ndio mtu pekee aliyekuwa akitalajiwa asimamie kweli. Mungu huwa hadhiakiwi wait n see.
 
inasikitisha sana kusikiliza taarifa ile........ hizi tume za nchi hii zimeshindwakutoa taarifa za kweli hata kwa kitu kinachooneka aibu tupu
Ile siyo tume bali ni kamati, ndio maana msimamo wa Chadema ulikuwa very clear kwamba hawawezi kushirikiana na kamati ambayo haina tofauti na kamati ya harusi, kilichokuwa kinahitajika ni Tume huru ya kimahakama yenye nguvu za kisheria.
 
Msingi wa haya yote ni dharau dhidi ya wananchi (contempt of the people). Watawala wanaamini wanaweza kusema lolote, vyovyote, kwa yeyote bila kujali matokeo yake. Hawataki kuulizwa na wakiulizwa wanaona unaleta vurugu.
Nakubaliana kabisa na Mwanakijiji., Sasa inabidi walipe gharama zote za hii kazi sifuri. Halafu kwa hii dharau waliotuonyesha, Mungu awashughulikie. Inaniuma sana, Duhhhh.
 
Heshima kwako MM,

Wajinga ni wengi sana kuliko werevu katika jamii hii, na hata hivyo kwa fursa ambayo sijui ilitokea vipi, wengi wao wanapewa heshima kubwa na majina makubwa kama wasomi, wanasheria waliobobea, waheshimiwa mawaziri, majaji n,k.
Ripoti kama hizi hazitakosekana hadi hapo mfumo wa maisha katika jamii utakapobadilika na wajinga wasitukuzwe na kuheshimika tena.
Ni muhimu kujua kwamba wajinga hao wana mtandao mkubwa na mbinu zao za kijinga zinafanikiwa kwa sababu ya wingi na madaraka yao!
 
Nyerere aliwahi kusema "mtu mwenye akili akijua kuwa na wewe una akili akakushauri jambo la kipumbavu na wewe ukakubali atakudharau". Hili ni kweli pia kwenye suala hili. Mtu mwenye akili akijua na wewe una akili ahalafu akakuandikia jambo la kijinga na wewe ukalikubali atakudharau!

Hata hivyo kuna ujinga mwingine katika ripoti hii. Waziri wa Mambo ya Ndani Bw. Nchimbi akiokoa jahazi alisema kuwa kuna taarifa ambazo kamati yake (ya serikali) imeweka kibindoni kwa sababu za kimahakama. Ameeleza kuwa mambo hayo yamefichwa ili kuzuia mtu aliyeshtakiwa asije kuitumia kujinusuru. Kwa maneno yake amesema hivi:

Sasa mwenyewe Nchimbi hapa inawezekana aliamini kuwa amezungumza "pointi" sana. Katika mawazo yake haki ya adui yake siyo haki. Kumbe yule mtuhumiwa anayo haki ndio maana mahakamani kwenye kesi hizi wale wa upande wa mashtaka wanatakiwa waweke wazi ushahidi wote ambao wanao hata ule unaoweza kutumiwa kumtoa mtuhumiwa hatiani katika kile kinachoitwa "discovery" kabla ya kesi kuanza. Lengo ni kuhakikisha kuwa ushahidi wowote - wa kumtia mtu hatiani au kumtoa - unawekwa wazi kwa upande mwingine ili kuhakikisha kuwa mtuhumiwa anapewa nafasi ya haki.

Kwa maneno ya Nchimbi serikali inao ushahidi wenye kuonesha kuwa yule mtuhumiwa wa polisi inawezekana asiwe na hatia (hata kama picha zinaonesha kashika bunduki au kweli aliua) na serikali iko tayari kuficha ushahidi huo ili mtuhumiwa yule atiwe hatiani. Sijui wanasheria wetu wanaweza kusema vipi kuhusu haki ya yule mtuhumiwa kuweza kumuita Waziri Nchimbi, Mwenyekiti wa Kamati pamoja na ripoti kamili kama sehemu ya utetezi wake ili waweze kuona kama kuna ushahidi wowote wa kuweza kumsaidia. Haki ni haki hata kama ni ya adui yako. Si ndio wanasema "mnyonge mnyongeni haki yake mpeni"? Kama kuna ushahidi unaoweza kumtoa yule kijana Polisi hatiani kwanini Nchimbi na Kamati wauweke pembeni?

Si ndio uvunjaji mkubwa zaidi wa haki kwenda kumhukumu mtu kwa sababu hatutaki aachiwe hata kama sababu ya kumwachia ipo?

Simply put, Ni ripoti ya kijinga.
kwa taarifa nilizonazo ni kuwa huyu Nchimbi ana PhD. Tena nasikia ya kwake ni ya kusomea kabisa darasani kama Dr. Magufuli na wala sio kama za mkulu na mwenzake.
Pia nasikia mkuu wa hiyo tume naye ni jaji mstaafu.

Sasa labda kuna haja ya kuulizana maswali ya kitoto lakini tusameheane: Kwani PhD holder ana tofauti gani na bibi yangu hapa kijijini!??

Sijui ni kishindo gani kitaweza kutuamsha Watanzania na kuwaondoa madarakani hawa jamaa ambao hata Malawi inataka kutumia opportunity hii kutunyanganya Ziwa letu

 
Kamati ya Nchimbi ni FAKE sawa na ile ya Mwakyembe iliyohusu Richmond. Kamati inatoa Taarifa robo kwa kisingizio kuwa suala lipo mahakamani (kwanini waliunda kamati wakati walijua ni suala la mahakama?). Na Mwakyembe naye kwenye sakata la Richmond alisema hawezi kuweka mambo yote wazi kwasababu serikali itaumbuka!
 
Mambo mengine yanayofanyika katika nchi hii ni ya kusikitisha sana, nautilia shaka sana uwezo wa kufikiri wa Watanzania, ripoti ya kijinga namna ile huwezi kuileta kwa watu mpaka uwe una uhakika kwamba uwezo wao wa kufikiri ni duni sana, nawapeni pole sana Watanzania, poleni sana ndugu zangu Watanzania.

100% Agreed with you!....Viongozi walishajiaminisha kuwa Watanzania wote ni mazuzu tu, 'isipokuwa wao wenyewe', jambo ambalo linahitaji watanzania wenyewe kudhihirisha hivyo au la! What is the next level?? ONLY CDM to educate the mass of this 'mental-wash'! NO ANY OTHER WAY OUT OF THIS CATASTROPHIC situation we live in!!
 
Well said MM Mwanakijiji!! Ni ripoti ya KIJINGA sana, wamegeuza maisha ya watu usanii,na bado wanaendelea kuua! Ni dhahiri sasa hivi Taifa letu linaongozwa na tuliowapa mamlaka kuelekea shimoni,gizani..Tatizo kubwa viongozi wetu wengi tuliowapa madaraka ni wale wenye akili hizi ndogo za akina Nchimbi..Wakati mwingine ni bora kutokuongea kabisa kuliko kuongea upuuzi! Kuna wakati ukitathmini baadhi ya viongozi wetu na mambo wanayofanya au kuyasema,utaona hawafai hata kuongoza kikiundi cha ngoma sembuse nchi? ANYWAY mimi na wewe kwa namna moja ama nyingine tuliwezesha "AKILI HIZI NDOGO KUTAWALA AKILI KUBWA" Tafakari,Chukua hatua 2015 haiko mbali!
 
Inaonyesha jinsi gani watawala wanavyo walazimisha wananchi kucheza ngoma yao
 
.
.
Kaka inakera!! Hata ripoti ya mwakyembe ya richmond, Mwakyembe mwenyewe amekiri kuwa kuna vitu vilifichwa!!!

Ripoti nzima... hakuna sehemu ilipozungumzia kitu kinachoitwa HAKI!!!

Ni ***** tu!! *****!!!


Mkuu this is the point, no body cares about HAKI, the definition of the word justice in today's Tanzania is only understood by very few people, those with money and power. Si mara ya kwanza au mara ya pili kwa hili kutokea, na ni wazi kabisa si mara ya mwisho. Lakini kinachokasirisha ni kuona kuwa baadhi ya watu wanajidai kuona hili zaidi na kuonesha kuchukizwa, kuliko mengine mengine yaliyopita.

Mtu kama makunga anahongwa tu au anatishiwa halafu...atasema analotaka waseme.

Richmond iko wapi? Dowans iko wapi? EPA iko wapi....ukiwa na nguvu unaiba unaua na mambo yanaendelea.......
 
Sio ya kijinga tu! Bali huu ni upumbavu na matumizi mabaya ya kodi za wananchi, wakati nachangia kwenye huu ukurasa baada ya Nchimbi kutangaza sijui ni kamati au tume, nilisema wazi kwamba huu ni wizi wa kodi zetu na ujinga usio kubalika. Naipongeza sana Cdm kukataa kutoa ushirikiano hii kamati mfu. Pia naomba kutangaza kumuunga mkono 100% Mh Lisu kwani alisema mapema mapungufu ya mwenyekiti wa tume. Hili nilikubaliana nalo wakati akijieleza kwa waandishi. Yaani hafai hata kuwa mzee wa baraza la mahakama ya mwanzo.
Nalaani matumizi mabaya ya kodi zetu. Nchimbi anatakiwa ajiuzulu mara moja. Hebu ona ripoti ya MCT ilivyo nzuri. Na wamefanya kazi siku saba tuu! Na wakaonyesha kasoro zilipokuwa. Ifike mahali sasa ccm na viongozi wake wajue Watanzania wa leo sio wale wa elimu ya watu wazima.
 
sasa nani wa kumfunga paka kengele? hata wale tunaowaamini wanamtumikia kaisari!
 
Back
Top Bottom